Kikwete Hana Namna. Lazima Aachie Ngazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete Hana Namna. Lazima Aachie Ngazi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ng'wanangwa, Oct 4, 2010.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Naomba siku ikifika muikumbuke thread hii.

  Kikwete hafai na amekata tamaa. Sababu ni nyingi lakini sababu kubwa sitaitaja. Kamtu kadogo kama mimi siwezi kukubali kuleta taharuki ya taifa. Lakini ndiyo ukweli. Yatatokea.

  Kwa hiyo nitataja sababu zilizo wazi tu kwa nini Kikwete hawezi kuwa Rais wa 5:


  1. Kuanguka Jukwaani Siku ya Uzinduzi wa Kampeni
  2. Kuwapigia kampeni mafisadi wanaojulikana hata na watoto wa chekechea
  3. Kuahidi ahadi za uongo na nyingi kupita kiasi
  4. Kulifanya "Suala la Urais ni la Kifamilia"(hayo ni matusi kwa JWTZ na Usalama wa Taifa)
  5. Kutamka hadharani atashinda kwa kishindo "hata kama hamtaichagua CCM" (alikuwa Bukombe)
  6. Kutuma baadhi ya wanajeshi watiifu kwake kuzungumza pumba na waandishi wa habari. Hii imeligawa jeshi.
  7. Kushindwa kumkemea mtu wa majini Yahaya Husein
  8. Kuwaambia Watanzania kuwa asipozurura ughaibuni tutakufa njaa (huyu si Rais mbunifu).
  9. Kuutaka urais kwa ajili ya ufahari tu na si kuwatumikia Watanzania.
  Watanzania tukapige kura Oktoba 31. Tusimchague Kikwete.
   
Loading...