Kikwete hakuwa mwizi, Ila mfumo uliachwa na Mkapa ulimzidi nguvu

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,058
2,000
Aliye na ushaidi juu ya wizi wa Jakaya Mrisho Kikwete auweke hapa. Jk alikuwa mwasiasa mbobezi, alijua nchi inahitaji nini iendelee, aliujua uchumi vizuri.

Hana Mali au miradi binafsi, aliyoiacha kwake au kwa familia yake katika utawala wake. Kama unaushaidi weka hapa. Zaidi ya kijumba msoga. Tena chini ya mapato halali ya kwake.

Watu wengi hawajui ukubwa wa viongozi hasa maraisi wastafu wa Afrika. Ukidili na kiongozi aliyekutangulia siku zako zitahesabika.
JK na Luwasa walianza kwa Kasi ya ajabu. Walitaka kupitia mikataba yote ya madini ya awali, Walimuyang'anya Hadi Mkapa Mgodi wa makaa ya mawe aliojimilikisha akiwa Raisi. Lakini baada ya kuona mtu anayetaka kumshugulikia ndie aliyewaweka walinzi wake, usalama, uongozi wa Chama hakuwa na jinsi.

Kashfa zote zilizotokea, Zilijadiliwa kwa Uhuru na live bungeni na hatua zilichukuliwa.

Mfumo wa Mkapa ulijaa ufisadi na bado ulikuwepo na alishindwa kuudhibiti. Kuna wakati Jk alipiga kijembe waliposema kashfa Fulani hachomoi. Akauliza kwani alichomeka wapi? Alijua hausiki na hatohusika Katu.

Mkapa ndie Raisi aliyeunda mfumo wake mwenyewe na kuusimamia. Kwani aliyekuwa na nguvu kwenye mfumo alikuwa NI Nyerere na alipinga Sana Sera zake za ubinafsishaji wa hasara. Ila baada ya kuondoka mwaka 1999 Mkapa aliongoza kwa jinsi alivyotaka.

Kuna kasfa JK aliondoka na kuliacha bunge kujadili.

Tuwekane sawa, hapa licha ya Mkapa kuingiza wafanyabiashara kwenye siasa, Yeye mwenyewe kuanza biashara, Mke wake kuhusishwa kumiliki taasisi kubwa za kukopesha fedha kama Beypot. IliyoumizA Sana watumishi. Ila aliongoza nchi kuingia kwenye uchumi na mfumo wa kisasa wa uongozi.

Anayesema J K alikuwa mwizi alete ushaidi hapa.

Magufuli kwenye wizi alipambana Sana na mfumo uliachwa na Mkapa. Na baada ya Mkapa kuondoka gafla inaonekana wazi mfumo mzima ungezimwa kabisa. Mikataba ya iptl sijui Songas na Tanesco kwenda kuwa huru ndio hofu mpya ya wezi ndani ya mfumo wa Jpm. Ila bahati mbaya jpm alitutoka punde.

Timu Magufuli tusimchanganye Mama. Magufuli ameweza kuharibu kwa kiasi kikubwa mfumo wa wizi. Sasa NI wakati wa mama kujenga mfumo Bora wa KIUCHUMI. Kwani mfumo wa Jpm ulikuwa unawapeleka wananci kwenye umasikini wa kutupa.

Maraisi waliojaribu kubadili mifumo gafla au kuwashugulikia watangulizi wao Afika wengi walipotea gafla.
Zungumzia Bingwa mutarika au Revy Mwanawasa. Au Tomas Sankara.
 

Jamalm335

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
2,502
2,000
Kama hiki ni kijumba basi sitojali na mimi kukimiliki.
1618057837958.png
 

drilling

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
2,395
2,000
kuna siku makufuli alisema anafukua kaburi moja tu maana akifukua yote mtashindwa kuyafukia alisema alifungua faili moja tu pesa za umeme bilion za dolla za misaanda kutoka nje iliisha lipwa kwa ajili ya umeme kusini pesa haionekani na umeme hakuna jaribu kutafuta speech hii ya makufuli
 

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,058
2,000
kuna siku makufuli alisema anafukua kaburi moja tu maana akifukua yote mtashindwa kuyafukia alisema alifungua faili moja tu pesa za umeme bilion za dolla za misaanda kutoka nje iliisha lipwa kwa ajili ya umeme kusini pesa haionekani na umeme hakuna jaribu kutafuta speech hii ya makufuli
Je hizo fedha alizichukua Jk? Naamini pia Jk alihitaji busara Sana ili aendelee kuwepo na aongoze mabadiliko ata nje ya mfumo.
Uhuru wa kumchafua ulifanya watu wamtungie story. Ila hakuna uhusika wake unaothibitika ata kidogo.
 

Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
52,764
2,000
Siasa ndivyo zilivyo aliyekuwepo anaweka mifumo yake, akitoka anataka bado iendelee kulindwa na kuheshimwa shida inaanzia hapo...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom