Elections 2010 Kikwete hajui Peramiho imeshapandishwa hadhi?

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,213
JK kwenye kampeni zake leo Songea, kwa kujisahau au makusudi kwa kujua watanzania ni majuha, amezidi kutoa ahadi kwa mambo ambayo bunge limeshayapitisha. Leo anasema akiwa rais ataipandisha hadhi hospitali ya Peramiho- Songea. Hospitali hii imeshapandishwa hadhi na ilitangazwa na waziri wa afya na ustawi wa jamii katika bunge lililopita (Hospitali za jiji Dar zapandishwa hadhi).(Hii link pia inataja hospitali za mikoani zilizopandishwa hadhi toka July mwaka huu - Peramiho ikiwa mojawapo)

Hii inakuwaje tena ni ahadi? Hii kama si kuwahadaa wananchi na kutufanya majuha ni nini? Ili aje aseme tuliahidi na tumetimiza.

Tumuogope mtu huyu kama ukoma, yeye mwenyewe amesema ukimuona mtu mzima anasema uongo, kuna mawili, either yeye mwenyewe ana matatizo au anawaona majuha wale anaowaongopea, kwa hiyo JK labda ana matatizo au anatufanya sisi majuha. Tukatae kuwa majuha ndugu zangu nawaomba sana. Mungu awabariki.
 
Amechanganyikiwa hajui aseme nini na aache nini. Wamuulize kwani hizo hospital za rufaa wanakwenda kutibiwa bure? tena wamuulize Riz 1 akiumwa atakwenda kutibiwa hospital hiyo ya Peramiho?
Chadema mbali na kuwa na hospital nyingi huduma ni bure kabisaaaaaaaaa. chaguo ni lao.
Mwaka huu hatudnganyiki
 
JK kwenye kampeni zake leo Songea, kwa kujisahau au makusudi kwa kujua watanzania ni majuha, amezidi kutoa ahadi kwa mambo ambayo bunge limeshayapitisha. Leo anasema akiwa rais ataipandisha hadhi hospitali ya Peramiho- Songea. Hospitali hii imeshapandishwa hadhi na ilitangazwa na waziri wa afya na ustawi wa jamii katika bunge lililopita (Hospitali za jiji Dar zapandishwa hadhi).(Hii link pia inataja hospitali za mikoani zilizopandishwa hadhi toka July mwaka huu - Peramiho ikiwa mojawapo)

Hii inakuwaje tena ni ahadi? Hii kama si kuwahadaa wananchi na kutufanya majuha ni nini? Ili aje aseme tuliahidi na tumetimiza.

Tumuogope mtu huyu kama ukoma, yeye mwenyewe amesema ukimuona mtu mzima anasema uongo, kuna mawili, either yeye mwenyewe ana matatizo au anawaona majuha wale anaowaongopea, kwa hiyo JK labda ana matatizo au anatufanya sisi majuha. Tukatae kuwa majuha ndugu zangu nawaomba sana. Mungu awabariki.
"In politics, stupidity is not a handicap."
 
Tumsamehe bure, ugonjwa anougua unasababisha kupoteza kumbukumbu ndiyo maana wasaidizi wake wanamdanganya kila siku.KIFAFA SI MCHEZO.
 
hehehe hehhe
kinachompa msukumo jk kufikiria kuchakachua kura ni kukosa safari za nje maana zinalipa sana kwa upande wake huku sisi tukipata masimulizi tu
 
Kwa hali ya mambo ilivyo nchini ni mtu asiye na akili timamu tu atayekua anaishabikia serikali ya JK..laa basi huyu atakua msaliti kwa wenzake simply kwa kua kuna leakage anaipata kwa kutokana na vingozi wa serikali ya CCM kukosa maadili ya kiuongozi
 
JK kwenye kampeni zake leo Songea, kwa kujisahau au makusudi kwa kujua watanzania ni majuha, amezidi kutoa ahadi kwa mambo ambayo bunge limeshayapitisha. Leo anasema akiwa rais ataipandisha hadhi hospitali ya Peramiho- Songea. Hospitali hii imeshapandishwa hadhi na ilitangazwa na waziri wa afya na ustawi wa jamii katika bunge lililopita (Hospitali za jiji Dar zapandishwa hadhi).(Hii link pia inataja hospitali za mikoani zilizopandishwa hadhi toka July mwaka huu - Peramiho ikiwa mojawapo)

Hii inakuwaje tena ni ahadi? Hii kama si kuwahadaa wananchi na kutufanya majuha ni nini? Ili aje aseme tuliahidi na tumetimiza.

Tumuogope mtu huyu kama ukoma, yeye mwenyewe amesema ukimuona mtu mzima anasema uongo, kuna mawili, either yeye mwenyewe ana matatizo au anawaona majuha wale anaowaongopea, kwa hiyo JK labda ana matatizo au anatufanya sisi majuha. Tukatae kuwa majuha ndugu zangu nawaomba sana. Mungu awabariki.

Ni kawaida yake kuahidi vitu ambavyovimefanyika au viko kwenye mchakato wa kufanyika, mfano dodoma aliahidi kuikarabati Ikulu ndogo akiingia madarakani, wakati ukweli ni kuwa Ikulu ndogo inakarabatiwa sasa! sijui huyu mtu vipi!
 
huo ndo ujinga wa viongozi wa ccm! Wanaona watu wote ni wapuuzi na sio waelewa milele!

late bob marley said "you can fool some people some times but you can't all the all the time"!
 
JK wetu we acha tu! Mara asaini Sheria ambayo ina walakini, mara afungue jengo kesho yake uzio wa jengo hilo unabomolewa, nk! Sasa hivi nako anapandisha hosp kuwa ya rufaa huku ilishapandishwa tayari! Anyway, labda alikuwa "anatania" au "wasaidizi wake ndio wanamwangusha!"
 
Credibility ya president ni pamoja na kuwa makini kwa jambo analosema na kutenda. Huyu hayuko serious kwa jambo lolote hata hao wake zao wanajua. He is a caricature type of a president , who has turned the high office into kijiwe cha wezi na wapumbavu ndani ya bonge la nchi ya maziwa na asali tupu. TANZANIA . Ee mola tusamehe dhambi tuliyotenda ya kumwingiza unwise king in the white house kinyume na maandiko matakatifu 2005.
 
Tunaongea treni ya masaa 3 kutoka Mwanza mpaka Dar itakayojengwa ndani ya mwaka mmoja. Kama siyo nyeto za fikra basi sijui ni kitu gani.
 
Nimecheka mpaka basi.....asante mdau kwa kunichekesha siku ya leo!!

Kitu kimoja ninachompendea Rais Kikwete ni being "so easy going"!!
 
JK mbona unajichanganya wewe?????? Ahadi zote hizi za nini kwani wewe umekuja kugundua leo kwamba wananchi wako hawana maendeleo.
CCM ahadi zenu zimekuwa ni hizi kwa miaka 50 sasa acheni bla bla zenu. Oh kitakuwa chuo kikuu mara oh itakuwa hospitali ya rufaaa oh nitajenga barabara ya lami ulikuwa wapi miaka mitano iliyopita????uliahidi haya haya acha kutulaghai bana.. Kitaeleweka tu mwaka huu.
 
Bandari na meli kubwa Ziwa Nyasa - Mbambabay
 
Back
Top Bottom