Kikwete hajui bei ya CT scan kwa sababu serikali yake haijawahi kununua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete hajui bei ya CT scan kwa sababu serikali yake haijawahi kununua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Determine, Aug 8, 2012.

 1. D

  Determine JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Viongozi wa Serikali imesemekana kuwa wanashindwa kusema ukweli kwamba mashine ya CT Scan iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili haikunuliliwa na serikali bali ni msaada kutoka kampuni ya Philips ya nchini Uholanzi. Taarifa hizi zimekuja siku chache baada ya hotuba ya Rais wa Jamhuri wa Muungano kuhutubia na kufafanua kuwa si kweli kwamba bei ya CT Scan moja ni sawa na gari moja aina ya VX ,maarufu hapa nchini kama mashangingi.

  Katika hotuba ya Rais ya mwisho wa mwezi wa Julai,Rais alitaja bei ya halisi ya CT Scan bila kuelezea kwa kina ili umma wa watanzania ufahamu kuwa hata CT Scan mashine hii tuliyonayo tulipewa msaada tu na serikali bado haijapata uwezo wa kununua CT Scan kwa pesa zake yenyewe.

  Habari kutoka vyanzo vyetu vya habari vinavyoaminika zinasema kuwa msaada huo wa mashine ya CT scan kwa Tanzania kutoka kampuni ya Philips ulitolewa baada ya Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuipa kampuni hiyo tenda kubwa ya kufunga X-ray mashine za kisasa katika hospitali za wilaya,mkoa na Taifa zipatazo 98 nchini kote. Mradi ulikua na lengo la kufunga X-ray mashine,ultrasound,vifaa vya uchunguzi wa magonjwa ya meno,vifaa vya maabara na upasuaji ulitekelezwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi na Serikali ya Tanzania kama sehemu ya mradi wa ORET kwa nchi za Afrika ambapo hapa nchini ulianza 1996 na kukamilika 2004.

  "Hivyo utagundua kuwa aikuwa lengo la mradi uliokuwa ukitekelezwa kwa ushirikiano wa nchi kati ya Philips ya Uholanzi na Tanzania kufunga CT Scan lakini mashine hii ilikuja kama msaada na sio kama mashine nyingine ambazo Serikali ya Tanzania ilipewa kwa njia ya mkopo wenye masharti nafuu ya riba"kilisema chanzo hicho.

  Tenda hiyo iliyosimamiwa na wakala wa kampuni ya Philips aliyepo hapa nchini anayejulikana kama Mokasi Medical Systems mwenye makao yake makao upanga jijini Dar es salam kwa kuratibu shughuli za ufungaji wa mashine hizo nchi nzima. Mradi huu ulianza kwa kufanya upembuzi yakinifu kwa nchi nzima kuanzia mwaka wa 1996 ambapo Hospitali 21 zilitembelewa ili kujua utendaji wa vifaa vya X-ray,maabara,upasuaji,meno na ultrasound na ripoti ya matokeo ilitolewa mwaka huo huo ikionyesha pamoja na mambo mengine kuwa hali ya X-ray mashine nchini kwa wakati huo ilikua ni mbaya kwani nyingi zilikua ama zimekufa kabisa au zilikua zinaharibika mara kwa mara.

  Mwaka 1997 maombi ya Tanzania yalitumwa kwa nchi mbalimbali kuomba msaada wa kuokoa hali ya huduma za afya nchini lakini ilishindikana kupata msaada wa kutekeleza mradi huo kwa njia ya msaada baada ya nchi nyingi kuonyesha nia ya kutoa msaada katika afya ya msingi kama afya ya mama na mtoto na sio X-ray mashine. Ndipo maombi ya mkopo wenye riba nafuu ulipoombwa na Serikali ya Uholanzi ndiyo iliyokubali kutoa mkopo huo huku ikisemekana kuwa jambo ili liliwezekana baada ya Mokasi wakala wa Philips nchini kuzungumza na Philips makao makuu na mwisho maombi yalifikishwa katika serikali ya Uholanzi kupitia Philips,kama sio hivyo mradi huu ulishakosa wafadhili kilisema chanzo chetu.

  Mwaka 1999 taarifa zilikusanywa na itaji halisi ya aina ya vifaa vinavyoitajika katika mkopo huo vilitajwa lakini CT Scan mashine aikuwepo katika orodha ya vitu vinavyoitajika na ndipo kuanzia mwaka 2000 hadi 2004 mashine za X-ray zilifungwa katika hospitali za Wilaya,Mkoa na Taifa 98 baada ya kukamilika kwa taratibu za manunuzi na logistiki zengine.

  Katika kipindi chote hicho Mokasi Medical systems iliyoanzishwa hapa nchini 1982 ilifanya kazi bega kwa bega kama kiungo kati ya serikali na kampuni ya Philips ya Uholanzi iliyopata tenda ya kusambaza na kufunga mashine za X-ray katika maeneo yote 98 nchini.
  Baada ya kupata kwa tenda hiyo kubwa na kumaliza kufunga mashine zote za X-ray ndipo Philips Medical System walipoamua kuizawadia Tanzania msaada wa CT Scan mashine aina ya Philips Brilliance 64 slice CT scanner ambayo licha ya mashine hii kusaidia wagonjwa kwa muda mrefu kwa muda wa miezi saba sasa haifanyi kazi.

  Chanzo hicho kilisema hii ni aibu kwa nchi kwamba toka uhuru atujaweza kununua mashine hata moja ya CT Scan na hata inapoalibika bado inashindikana kupata wataalam waliobobea kuitengeneza?.

  Chanzo hicho kilisema hata kama serikali inasema kuwa mashine ya CT Scan ni bei kubwa sio sawa na bei ya gari aina ya Shangingi maoja lakini serikali aiwezi kushindwa kununua mashine Kama hizo tano kwa nchi nzima ili zikahudumie kikanda kama kanda ya mashariki,kanda ya kati,kanda ya kaskazini,kanda ya kusini na kanda ya ziwa ili kuondoa usumbufu kwa wagonjwa kufuata kipimo cha CT Scan Muhimbili,ili ni suala la mipango na sio suala la pesa au umaskini kilisema chanzo hicho....

  source..DOCTORS...


   
 2. B

  Bijou JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kama ni mkopo, Ina Maana serikali NDIYO imenunua, MNYONGE MNYONGENI, HAKI YAKE MPENI
   
 3. m

  mang'ang'a JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  [h=1]How much does CT Scan machine cost?[/h] In: Medical Insurance, CT Scanning, Pulmonary Health [Edit categories]

  Ads
  Answer:
  the compute tomography machine costs depends upon the technology systems
  siemens ------------------200000 usd approx
  toshiba -------------------180000 usd approx
  beckam coulter------------250000 usd approx
  sharp------------------------200000 usd approx
  ge----------------------------300000 usd approx
  phillips ----------------------140000 usd approx

  Read more: http://wiki.answers.com/Q/How_much_does_CT_Scan_machine_cost#ixzz22wyO8oeV
   
 4. Titans

  Titans JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 867
  Likes Received: 1,073
  Trophy Points: 180
  read between lines sio kukimbilia ku-click keyboard

  "Hivyo utagundua kuwa aikuwa lengo la mradi uliokuwa ukitekelezwa kwa ushirikiano wa nchi kati ya Philips ya Uholanzi na Tanzania kufunga CT Scan lakini mashine hii ilikuja kama msaada na sio kama mashine nyingine ambazo Serikali ya Tanzania ilipewa kwa njia ya mkopo wenye masharti nafuu ya riba"kilisema chanzo hicho.
   
 5. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mkuu kuna uzi nyingine zinaletwa humu mtu unakosa kujuwa madhumuni zake ni nini hasa! Je zinatokana na itikadi za vyama, chuki binafsi au Uzalendo wa kweli unao jali atma ya TAIFA letu?

  Hivi tukitulizana akili tukajihuliza hivi: Wizara ya afya hiko chini ya Serikali ya chama gani tawala? kama ni misaada au mikopo ya kununulia hizo scanner nani muhusika mkuu wa kuomba misaada au mikopo?
   
 6. Mkaguzi

  Mkaguzi JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Unajua Kusoma? Mkopo na Zawadi (msaada) ni sawa? Hebu kasome tena habari hiyo. Mashine walisaidiwa kama ahsante
   
 7. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 521
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Inaletwa kwenu kwa msaada wa watu wa marekani
   
 8. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 521
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Tangazo hili limeletwa kwenu kwa msaada wa watu wa marekani
  kisima hiki kimechimbwa kwa msaada wa watu wa marekani
  darasa hili limejengwa kwa hisani ya watu wa marekani
   
 9. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 521
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  wewee acha hizo yaani asijuwe bei ya ct scan wakati ni daktari, DR.KIKWETE, 5YRS AT LUMUMBA + 1YR INTERNSHIP AT JANJA JANJA HOSPITAL
   
 10. m

  massai JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  anasubiri CT scan kama msaada alafu kutoka kwa watu wa marekeni.nakaribia kujuta kuwa mtanzania.
   
 11. d

  danizzo JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada wewe kina kuuma nini?
   
Loading...