Kikwete hafanyi tena kampeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete hafanyi tena kampeni

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by QUALITY, Sep 29, 2010.

 1. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu, jana ilikuwa siku yangu ya nne nikiwangalia JK katika mikutano yake ya hadhara "ya kampeni" lakini ukimsikiliza haongei kama mgombea bali Rais. Kwa mfano jana katika ITV alisema "wanaoiba hati punguzo za pembejeo watashughulikiwa kama wahujumu uchumi"!! Hii si kauli ya mgombea bali ya yule aliyeishapewa madaraka.

  Akasema, tutajenga barabara ya rami kupitia mbuga za wanyama, Serengeti. Hizi zote ni orders. Mbaya zaidi, wandishi wa habari humnukuu "Serikali imesema...." Siyo JK amesema akipewa ridhaa tena ata....

  Je hii ni kusema kuwa Hakuna haja ya kufanya uchaguzi sababu anayetaka kushinda ameishajitangazia ushindi? Je hapo kutakuwa na uchaguzi huru na haki? wale wenye maoni ya mtizamo wa kidini kama Ami wasichangie hapa.

  Karibuni kuchangia.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ana kihererehere (sorry to use his own word) ya kurudi mjengoni!!! Na ninawasikitikia Watz kwani akirudi, na kwa kuwa ndiyo miaka yake 5 ya mwisho, basi hatafanya chochote -- akakua anapiga anasa tu. Mwaka 2015 hatakuwapo yeye kujibu maswali iwapo katimiza ahadi zake au la.

  Watz -- hebu tujitutumue kidogo asirudi huyu mjengoni ili kutopoteza miaka mingine 5 ya maktaimu katika maendeleo. I know you can!
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Siku za JK Ikulu zinahesabikaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 4. E

  Edu Member

  #4
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naamini hiyo ni mikakati hasi zaidi ya uchaguzi ambayo inahusisha mambo yafuatayo:

  1. Mgombea kutoa matamko ya kiserikali yanayotekelezeka baada ya uchaguzi.
  2. Mgombea kuzungukwa na maofisa wa serikali wasio wanasiasa.
  3. Mgombea kusomewa risala hewa za mahitaji muhimu ya wananchi na kuombwa kumalizia au kukabili matatizo yaliyobaki
  4. Mgombea kupewa fursa ya kwaza kwenye media za serikali bila kujali wagombea wengine wamefanya/kuongea nini siku hiyo.
  5. Mgombea kuingia kwenye ugomzi/ lawama siziso za lazima na taasisi za nje na ndani kwa mambo yanayohitaji utaalamu kuliko utashi wa kisiasa.
  6. Mgombea kutumia rasilimali za serikali katika kampeni zake.

  Na mambo mengine mengi yafananayo na hayo. Sasa kwa mwananchi wa kawaida si rahisi kutofautisha mgombea wa nanma hii na kiongozi kamili wa nchi, hivyo anaishia kuamini kuwa huyu mgombea ndiye anayestahili kupewa kura (kwani tayari ni raisi wa nchi kwa matendo au muonekano).

  Naamini haya ni mambo yanayochochea mabadiliko kwenye katiba yetu.
   
 5. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hehehehe. Mbona kurudi mjengoni ni kama kawa tu? :becky:

  Wale wanaotoa kila aina ya ahadi, kuanzia kufuta kodi zote, kuongeza mishahara, elimu bure, afya bure, treni ya umeme kutoka Mwz Dar kujengwa mwaka mmoja baada ya kuingia Ikulu, huyo hana kiherere. Anawashwa na kuingia mjengoni. :becky:
   
 6. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hata mi nimemsikia. Anaongea kama rais. Ni kwa vile hana jipya. Wajiandae kwa serikali ya mseto bara pia
   
 7. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kwa nchii hii hata sishangai.
   
 8. Charles Mtekateka

  Charles Mtekateka Verified User

  #8
  Sep 29, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 310
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Tawile kaka!
   
 9. t

  truth Member

  #9
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani unasahau kuwa JK bado ni Rais wa nchi, unaweza kudhani ana additional privileges lakini ukweli ni kuwa pia yuko disadvantaged kwa sababu anapimwa kwa issues ambazo tayari zimeshafanyika tofauti na kidogo na asiye madarakani anapimwa kwa vitu ambavyo tunadhani vinaweza kufanyika.Hivyo that is a win win situation.
   
 10. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Mwenye kiherehere ni yule anayemtumia Yahay kutishia watu maisha!!!!!
   
 11. S

  SUWI JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kama ameshasambaza maofisa usalama kuhakikisha ushindi nchi nzima na kuandika nyaraka kwa wakuu wa mikoa, wilaya na uchafu mwingine kwa nini asiwe na uhakika wa kubaki kula vya wavuja jasho!!? Mi naona hapo anatamani siku ziende mambo ya uchaguzi yaishe aaze kutanua kama kawaida yake, leo marekani, kesho jamaika kupembea nk.... Lakini ajue sote twarudi mavumbini na ikifika siku hakuna cha afisa usalam, hakuna cha wakuu wa wilaya na hata akibadilisha hiyo damu ten times per day havitasaidia maana Mungu si mwanadamu. Sihukumu maana mimi si Mungu ila namuasa tu yeye na mafisadi wenzake wasijisahau wakadhani wataishi milele.
  Mungu Ibariki Tanzania!
   
 12. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Afanye kwa oda kama rais asifanye... yeye kwenye moyo wake anjua fika magogoni atapasikia tu!!!:becky:
   
 13. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,422
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  JK hajawahi kuwa rais, rais ni Rostam Aziz...eebo!
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaani ukisikia timu beki hazikabi ndo timu ya JK..yaani dakikak zinakwenda mipira inagonga besela kila dakika....hahaaaa hapagawa mzee wa watu yeye alidhani urais ni kuuza sura na kujipaka carolite lotion analo mwaka huu
   
 15. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #15
  Sep 29, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda kisharidhika na mkakati wa kufanya ujambazi wa kuiba kura ndiyo maana anaongea kama kishachaguliwa.
   
 16. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nashangaa unauliza makofi polisi!Wewe hujuhi kuwa JK ndiye rais?Kama hutaki saga chupa unywe taratibu,na mwaka huu mtalia vilio vya vyura wa kiansi!
   
 17. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwani mambo ya kusomewa risala katika kampeni yameanza lini? Mbona hata maswali hayaruhusiw? Anasomewa risala kama Rais badala ya mgombea. Kinachouma zaidi ni kuwa anawadharau watz wote. ndiyo maana anaongea kama raisi.
  1. Amwisha fanya mikakati ya kuiba kura kupitia kwa wakurugenzi wa Halmashauri ambao ndio wasimamizi. Ambaye mbunge wa CCM atashindwa katika Halmashauri yake, kazi hana
  2. Anajua watz hawana uwezo wa kuchambua baya na zuri hivyo watampa tu
  3. Amewekeza kaika vitu vinavyoonekana kama darasa n.k Ubora si muhimu na watz wachache wanaweza kuona hilo
  4. Familia nzima (badala ya chama na viongozi wastaafu) wako nyuma yake.
  Aibu tupu
   
 18. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hili ni muhimu kukumbuka na kuzingatia. Nadhani kama akirudi tena, hali itakuwa mbaya zaidi kwa sababu anajua ndio term yake ya mwisho.
   
 19. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chadema.jpg
  :becky: :becky: :becky: :becky: :becky: :becky: :becky:
   
 20. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280

  Tukaandikishiane nae MAHAKAMANI KUWA ATAYATIMIZA
   
Loading...