Kikwete haeshimiki tena!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete haeshimiki tena!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Nov 20, 2010.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2010
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  Nimefuatilia kwa ukaribu kuhusu raisi kikwetwe na kwa mtazamo wangu ni raisi ambaye haishimiki na wana CCM na hata Watanzania. Kikwete atakuwa na wakati mgumu kipindi hiki kwasababu mawaziri wengine watu wanawaheshimu kuliko yeye. Hii inatokana na kikwete kushidwa kusimama kidete kwa mawaziri wa zamani wenye kashfa za ufisadi. Hivyo nasikitika Tanzania tutakuwa na raisi kwa miaka mitano ambaye haishimiki kabisa.
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Nov 20, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Ni kweli kwamba haheshimiki kwa kuwa amejipotezea nafasi ya kuheshimika, hata hivyo nimegundua kuwa Kikwete hahitaji kuheshimiwa zaidi ya kutaka kutimiza malengo yake ya kuiba rasilimali za wananchi kupitia kwa mafisadi, Kujaza ndg kwenye serikali yake, na kaharufu ka udini unaochipua kwenye serikali yake.
   
 3. n

  ngurdoto Member

  #3
  Nov 21, 2010
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hivi inawezekana vipi akaamini mbele ya jamii na Watanzania wakati yeye mwenyewe anasema mambo asiyoyajua. Eti nyufa za udini jamani huko mnapokaa hizo nyufa za udini kwa watanzania mmeziona?Anasimama na kuliambia taifa upuuzi kama huo hajui kama ndio anachochea ilijadiliwe. na iwe vichwani mwa watu.

  Na hili tatizo limeanzia kwa Makamba siku alipozungumza mbele ya vyombo vya habari kuwa Dk. Slaa eti ameacha upadri akaenda kwenye siasa. Kwa lugha nyepesi alikuwa anaingiza udini ili kumtenga Dk. Slaa asigombee.
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MWANADIPLOMASIA 'KUBAKA' DEMOKRASIA SI AIBU NDOGO HUKO NG'AMBO

  Kwa mtu aliyejitambilisha kama MWADIPLOMASIA anapogeuka na KUBAKA DEMOKRASIA, machoni mwa Umma wa Kimataifa hana tofauti na Askofu Mkuu au Imamu kusadikiwa KUMBAKA KICHANGA kwenye nyumba ya ibada!!!!!!!!!!!

  Kwa bahati zuri analifahamu hilo sana kuliko mtu mwingine yeyote yule hapa Tanzania. Akienda huko majuu wengi watakua wanamgwaya kama ukoma au kumpa pongezi za kejeli kusha dola tena.

  Ningekua yeye nisingeendelea kulisakama CHADEMA bali kufanya nao kazi kwa karibu ili aweze kuacha KUMBUKUMBU ya kuleta Mabadiliko ya KATIBA MPYA Tanzania kama ambavyo Mzee Kibaki kafanya kule Kenya. Laa sivyo, Kikwete LEGACY itakua ngumu sana kulizungumza katika historia siku zijazo.

  Hata hivyo, tushukuru kwa kila jambo kwani hawa jama wasingeiba kura kwa njia ya aibu kiasi hiki wenzenu tungepata wapi wazo la KUTAKA MABADILIKO YA KATIBA. Isitoshe, kama taifa tutapunguza sana GHALAMA kwenye kodi zetu kwa jinsi aibu itakavyomzuia kwenda Ma-Ughaibuni huko.
   
Loading...