Kikwete fanya maamuzi magumu sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete fanya maamuzi magumu sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Desteo, Aug 4, 2011.

 1. Desteo

  Desteo JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Najua ewe rais wetu unashindwa kufanya maamuzi magumu kutokana na utata wa chaka lenyewe. Tunajua umeshika kiberiti ukitaka kulipua hilo chaka lililolowa wese kumbe na wewe umelowa wese. Ni rahisi. Kaa mbali kabisa kisha mpe mtoto wa mkulima hicho kiberiti. Hakika ukifanya hivyo na tukajua, hatia juu yako itapungua.

  Watz ni wepesi wa kusamehe pindi wakifanyiwa wema. Hilo chaka lina epa, richmond, meremeta, uda, rada, shimbo (huyu ni taasisi kabisa), n.k. Unajua fika hili chaka linatugharimu kwa uwepo wake. Pinda yu tayari kufanya utakalomwagiza. Nadhani ulipata hansard ya lile tukio la jairo. Ulimsikia kwa maneno yake. Kikwazo kikubwa kilikuwa wewe.

  Watz tumechoshwa na haya. Usione tuko kimya juu ya hii hali mbaya ya maisha. Nikwambie tu, watz wanakuchukia mpaka basi. Ila watakupenda mpaka basi ukiwapatia 'kichwa cha Yohana' Ni ngumu kweli ila ufanyeje? Fanya kujaribu tu.

  Hutaamini. Chukua hela za hiyo 'taasisi' ukatujengee stiegler's gorge-ahadi ya enzi na enzi. Unayo miaka minne ya kujipoteza ama kujisimika mioyoni mwa watz. Ila pia ukumbuke na ahadi ya babu. Hatakufa hadi kieleweke.

  You can prove him wrong by doing it right.
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  We! Hadhubutu!! Labda uamuzi atowe akiwa nje ya nchi! Na awe na makazi ya hapo atakapotoa kauli hiyo. Lakini tupige kimya tu maana iko siku isiyo rasmi NGUVU YA UMMA itatoa maamuzi yenye mwelekeo. Aluta Continue!!
   
 3. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kwa faida ya nani,??? Jk akwenda ikulu kuishi maisha ya tambu, Nafiki Rais wetu unge kuwepo usafi wa kwenda mbinguni mbinguni angeishafika.?
   
 4. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  Mnapoteza muda wenu, mwenzenu kalala na wala hana time ya kusoma comedy zenu hapa, unadhan hayaoni yanayoendelea hapa nchini?
   
 5. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Yeye Kikwete mwenyewe yuko behind all these dubious deals, akifanya maamuzi magumu na yeye atakwenda na maji. Mwizi hawezi kumshtaki mwizi mwenzie
   
 6. Desteo

  Desteo JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Msimuogopeshe hivyo wajameni. Tumpeni second chance ili abwage maukweli hapa. Najua hata kama hasomi yeye, wapambe wake humsomea
   
 7. m

  mtanzania1989 JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2011
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 2,140
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  hivi huyu jamaa (mkuu wa kaya) hata kuudanganya umma kisayansa anashindwa ?
  si amkamate Shimbo tu halafu asema anapigana na ufisadi tena mkubwa mkubwa
  mbona atawapa watz wengi tu na MAVUVUZELA wao watapata hata pa kuanzia
   
 8. regam

  regam JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama riz1 ameshindwa kuwakilisha ujumbe atathubutu kukusikiliza wee. kwani we nani bana?
  subiri muda wake uishe tumpe mwingine. Hivi unajua staili ya mbwa koko au unasikia tuu? mbwa koko linalala muda wote, kubweka wakati mwingine haliwezi. linakula chochote ikiwemo hata vinyesi (aaaaagh!)
   
 9. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,595
  Likes Received: 4,710
  Trophy Points: 280
  Huo sasa muhali, kumtaka JK achukuwe maamuzi magumu ni sawa na kumtaka ng'ombe dume atoe maziwa.Jamani JK ni rais dhaifu kuliko wote tuliowahi kuwa nao.HAWEZI!!!!!!!!!!!!
   
 10. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  lada ajitoe mhanga, lakini kwa logic ya kawaida hawezi.hyo petrol ye ndo kalowa kuliko wenzake.akiwashatru kiberiti hata kunusurika hakuna, lazima ateketee.
   
 11. m

  mtanzania1989 JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2011
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 2,140
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  inamaanisha yeye hana hata vibonde wake
  :disapointed:
   
 12. MGAWARIZIKI

  MGAWARIZIKI JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 306
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kujitia kitanzi inataka moyo angekuwa Mhehe wa IRINGA angeweza lakini si ******
   
 13. Desteo

  Desteo JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hivi wakuu kumbe yawezekana asili ya mtu inahusika katika kufanya maamuzi? Hivi ni asili au mazingira? Asili ya jk ni bagamoyo lakini kakulia mazingira tofauti
   
 14. m

  mwananchit Senior Member

  #14
  Aug 5, 2011
  Joined: Oct 13, 2008
  Messages: 145
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Hivi jamani tunataka JK afanye maamuzi yapi magumu kuliko haya yafuatayo ambayo alishayafanya?

  1. Alimsamehe Mkapa huku akitutaka tumwache apumzike (juu ya makaa yetu ya Kiwira, rada, NBC, EPA, MEREMETA, DEEP GREEN, NET
  GROUP SOLUTION, TTCL, nk, nk, nk)

  2. Aliwasamehe wezi wa EPA kabla hawajahukumiwa na mahakama kinyume na katiba yetu tena mbele ya Bunge, mkuu wa majeshi, IGP,
  TAKUKURU nk.

  3. Amewaamuru wageni wachimbe na kuondoka na madini yote hata yale yaliyo ndani ya hifadhi ya Taifa ili wapiga kula wake wale jeuri yao kwa
  kumchagua kama kweli walimchagua au alijichagua mwenyewe. Kule Geita, Geita Gold Mine (GGM) inajichimbia Dhahabu popote wanapoiona
  hata nje ya eneo la mkataba na hakuna anayewauliza.

  4. Ameruhuhusu ufisadi usitawi na hivyo kuwafanya wenye pesa waidharau serikali yake sasa wanafanya wapendavyo utadhani hatuna serikali

  5. Ameruhusu wageni ambao hawakujaliwa kuwa na mbuga za wanyama waje wajuchukulie wanyama ili wakaanzishe mbuga zao wasiendeleee
  kusumbuka kuja huku mbali kuwaona.

  6. Ameruhusu ukame wa mipango thabiti na uthubutu utawale na kutuacha gizani tukiwa pia na njaa huku akidai kuwa ni ukame wa mvua wakati
  Mungu ametupa mito mingi, maziwa na maji mengi sana chini ya ardhi lakini yeye anangojea kukinga ya mvua tu!

  7. Amefanya maamuzi ya kihistoria kwa kusafiri nje ya nchi na mamlaka yote huku akiwaacha makamu wake na waziri wake mkuu wakiwa
  wanaangaliana wasijue cha kufanya hata kwenye tatizo dogo. Hatujui siku tukivamiwa na maadui wa nje JK akiwa ndani ya pipa itakuwaje!

  8. Amewaruhusu watoto wake wajichukulie kila wanachoona kinawavutia ndani ya hii miaka 6 tu huku watoto wa Nyerere aliyekaa ikulu zaidi ya
  miaka 25 wakiwa ni wanachi wa kawaida wasiotofautiana na watanzania wengine.

  9. Alithubutu kuwachafua watu safi na sasa sasa anachafuka yeye. Amefanikiwa pia kuwasaka watu wenye roho mbaya na chuki ya dhati dhidi ya
  watanzania na kuwapa uongozi na yeye yuko busy akiongoza nchi huku wananchi wakilia na wasijue wamlilie nani. mahakamani rushwa, polisi
  rushwa, ardhi rushwa, hospitali rushwa, nk, nk.

  10.Na mwisho, ameshabadilisha baraza lote la mawaziri, kamati kuu na sekretarieti nzima y achama chake lakini mambo yanakuwa bora jana.

  HIVI TUKIAMUA KUWA WAKWELI JAPO KUWA SIYO JADI YETU, TATIZO NI HAO WANAOBADILISHWA, AU HUYO ANAYEWABADILISHA?

  TATAFAKARI
   
 15. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  YOHANA?? Mbona kama ni kukabidhi kina yohana, serikali yake ndio imewakabidhi na wamechinjwa sana? Maana kina yohana ni wahanga wote waliopoteza haki zao ikiwa ni pamoja na ya kuishi, kwa sababu ya ufisadi wa kina BARABA.
  Jk anapaswa kutukabidhi ni kina BARABA, na sii kina YOHANA. Maana yohana ni alama inayowakilisha wenye haki bali baraba ni alama inayowakilisha wasio haki.

  .
   
 16. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jk siku hizi ana raha kwani analala anaota magamba yanamkaba usiku........msishangae akajilipua siku moja kwani nchi sasa hivi ni tete,
   
 17. Elinasi

  Elinasi Member

  #17
  Aug 5, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 64
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  and still more madudu to come,nafikiri ni serekali dhaifu kuliko zote duniani kwa sasa
   
 18. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #18
  Aug 5, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Jamaa hawezi kabisa kutoa maamuzi,huyo pinda mwenyewe ni mtu wa msimu hana msimamo kabisa,kama alikuwa anamsubili raisi mbona amerudi na hajatoa maamuzi ya jairo wakati yeye mwenyewe ndiye alituahidi kuwa akirudi tu atatupa jibu,hizo ni siasa.
   
 19. Desteo

  Desteo JF-Expert Member

  #19
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  dah! una utani na jkwewe. ulichosema nakifananisha na yule bwana aliyempiga mwizi kwa maganda yamayai. hakika yule mwizi alienda kufilia mbali. ila ugonjwa wenyewe uko hapo na ndio maana nikamshauri ampe Pinda hilo rungu. ikiwezekana achukue tena leave aende Oman sasa kisha huku nyuma Pinda aanze kupindua meza za walanguzi humu HEKLUNI

  Mkuu tukienda kimaandiko, jk hatasita kutupa huyo BARABA maana anajua lengo letu si kumhukumu BARABA bali kumuweka huru. japo YOHANA 'anauma' kutolewa haina jinsi. just pata picha ni jinsi gani mfalme alivyopata wakati mgumu baada ya bintie kuomba kuchwa. naye jkapate wakati mgumu pia kufanya maamuzi
   
 20. Desteo

  Desteo JF-Expert Member

  #20
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  tatizo hapa jk hakushaurika. kamaulimsikia Pinda vizuri alisema kuwa atajaribu kumweleza mheshimiwa rais halihalisina aone uzito wa jambo lenuewe ili achukue maamuzi sahihi (hope ni kumtimua). tatizo jk alichukulia simpo
   
Loading...