Kikwete eti umesema kuishi ni nini vile? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete eti umesema kuishi ni nini vile?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jogi, Mar 13, 2012.

 1. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Nimezinduka leo, wakuu nilikuwa nimezimia!

  naamini masikio yangu yamemsikia sahihi kikwete anawaambia wanaoitwa "wazee wa darisalam" kuwa "kuishi ni haki ya kwanza ya binadamu" si tu tanzania bali duniani kote, jk, jk, jk hivi ni lini uliijua haki hii!!!!! jk ungemalizia kwa kusema "na hakuna mwenye mamlaka ya kumnyang'anya mtu haki hii"

  ewe jk,

  kule arusha askari polisi waliwanyang'anya haki hii ya kuishi raia wawili wa tanzania na mmoja wa Kibaki katika harakati za kudai haki RIP. umekaa kimyaaaaa, mbeya nako askari tena "buyaka buyaka" hadi mwisho watanzania kadhaa weshanyang'anywa haki ya kuishi RIP. Wewe jk kimyaaaaaaa, madaktari wakipigania maslahi na haki ya kutoa tiba sahihi (kumbuka hawana vifaa vya kutosha) unawapandikizia kosa la warugaruga!!! na wauzaji wa mali zetu (nasaco, uda. . . . .) eti "tunakushukuru sana mishimiwa rwais"

  Kama hukusoma hata mama mwanaasha akiandaa masomo hukuona methali 'tandauma mlango wa chuma ukiufungulia hauna huruma???????

  nisimuongelee zombe, nitawaliza wanaulanga(mnisamehe)
  Ningeandika mengi naanza kujisikia vibaya, kama kizunguzungu hivi, isije ikawa ni dalili za kuzimia tena,

  Lakini jk tuambie, hivii!!!! zile smg na ak47 unazowabebeshaga warugaruga a.k.a askari polisi wa mstari wa mbele kwenye mpambano na raia wasio na silaha huwa umeambiwa hizo ni powersafe, adrenalin inj. ppf au tetanus injection?

  yaani unajua ya kuwa ni haki yetu kuishi lakini unatu. . . . . . . . .
  endeleeni kumjadilini kikwete kama hamtamkuta na shitaka la kuua kwa kukusudia (mada kesi) au atujibu hapa hapa jf.

  Kizunguzungu kimenizidi madokta, lakini tumeambiwa na kikwete mnatuua nifanyeje sasa!!!!!!

  someone help!!!!!
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Msiwe na shaka sasa naweza kujadili, no kizunguzungu angalau kwa sasa!!!
   
 3. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mi sishangai kwa sababu nafahamu kuwa viongozi wengi wa Afrika wanaamini kile wasichokitekeleza na wanatekeleza kile wasichoamini.
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Mkuu, hapa ni ufahamu, kama anajua bunduki ya malima si zeze ama gitaa kusema umpe mlinzi wa amani akalinde nayo amani?
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Umekumbuka mkong'oto wa Arusha? wahuni wachache wakasababishe hasara na uvunjifu wa amani na kuwakosesha raha ya kuishi walio wengi halafu waachiwe wakiwa katika harakati za kuvamia kituo cha polisi kilicho sheheni silaha?
   
 6. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  miongoni mwa walio na haki ya kuishi ni hao unaowaita "wahuni" hii ni haki ya kwanza ya mtu 'ku-ekzist'
   
 7. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,006
  Likes Received: 2,659
  Trophy Points: 280
  Kunyanyaswa,kuteswa,kuporwa,kuuwawa ni haki ya kila Mtanzania mnyonge,upende usipende.
   
 8. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Umesemaje?
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hao wahuni wachache walipoanzisha fujo walikuwa hawajui kuwa kuna wenye haki ya kuishi pia? walipotaka kuvamia kituo cha polisi chenye silaha walikuwa hawajui hayo? au walikuwa wana nia ya kuweka rehani haki ya wengine ya kuishi kwa amani?
   
 10. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  walimpora na haki hiyo ya kuishi, nakumbuka walikuwa wanawafuata kuwatoa mahabusu wananchi waliowekwa ndani kibabe. nani kakutuma kudhani? pia hakutoi kibali cha kupora haki ya kuishi.
   
 11. The Listener

  The Listener JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 977
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35


  Na kule Songea wananchi walipigwa live tena za moto wakidai mauaji ya ajabu yakomeshwe.
   
 12. M

  MCHUMIPESA JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 2,095
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  inaonekana wewe unaunga mkono mauaji ya raia ole wako sijui utasema nini siku ya hukumu..............una element za magamba,subiri nguvu ya umma yan pipooooooooooooooooooooooooooz pawaaaaaaaaaaaaaa iwanyolee chupa na 2015 kazi mnayo,mtaua wawili watawakamateni mamalioni na kuwatafuna wazima wazima mnafikiri mtatawala milele?we subiri tu time will tell,nawasilisha kwako.
   
 13. B

  Benaire JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 1,947
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kumbe waliuawa kwenye kituo cha polisi...na kumbe na wao walikuwa na silaha...waliouawa ndio waliokuwa wanavamia kituo..mbona wachache sana ila Asante kwa Taarifa..Polisi walikuwa sawa kabisa kwani mtuhumiwa uhukumiwa papo hapo bila ushahidi.
   
 14. M

  MCHUMIPESA JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 2,095
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  umelaaniwa nini?rudia tena!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 15. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Watanzania walionyanganywa haki ya kuishi na polisi ni wengi na kila wakati polisi watasema "walitaka kuvamia kituo cha polisi au ghala la siraha. Lakini ukweli ni kuwa si kweli, Arusha hakukuwa na harakati hizo za kuvamia kituo, watu waliuawa maeneo mbalimbali ya mji wala siyo kituponi wala karibu na hapo. Songea juzi juzi watu waliouawa na nukyang'anywa haki ya kuishi walivaamia kituo? Zanzibar? Tunduma? Acha hizo iko siku hata wewe mwenye damu ya kijani yatakugeukia.

  Quality
   
 16. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Binadamu anaweza kufa ikibidi kuokoa watu wengi.

  Kumuua mtu kwa ajili ya kuokoa watu wengi ni haki isiyopingana na haki ya kuishi.


  kuua mtu anayeleta uvunjifu wa amani kwa ajili ya kuokoa walio wengi ni haki ya msingi ya viongozi kulinda walio wengi dhidi ya wachache.

  suala la msingi uuaji huo usiwe wa makusudi. kwa mfano, kwa Marekani kumuua Osama bin Laden ilikuwa ni haki ya msingi ili kuokoa wamarekani wengi.
   
 17. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kama Jk, polisi au serikali yake tunadhani imeua na kukiuka haki ya msingi ya kuishi ya mtu tuzingatie haki ya kuua mtu mmoja ili kuokoa wengi kama ilizingatiwa kwenye mauaji hayo lakini hilo ni jambo la kawaida kote duniani.
   
 18. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #18
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,006
  Likes Received: 2,659
  Trophy Points: 280
  Sija laaniwa ila kwa ubabe wa CCM ndivyo ilivyo.
   
 19. c

  chuwaalbert JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 3,062
  Likes Received: 1,449
  Trophy Points: 280
  Ndugu, kuhusu hii ishu si JMK alishaomba msamaha na kuonesha masikitiko yake kwa kitendo kile?
   
 20. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #20
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Kama ni kesi ya mauaji JK na timu yake ya watendaji wote wanapaswa kuozea Jela. Kwani ni wauaji wakubwa.

  Ukiorodhesha matukio ya kuwakatisha Raia haki ya Kuishi iliyofanywa na watendaji wa Kikwete, na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya wauaji.

  (1) Mauaji ya Askari Polisi kwa wale Wafanyabiashara wa Mahenge. (NI SAWA HAWAKUWA NA HAKI YA KUISHI WALE WAPOGOLO).

  (2) Mauaji ya Arusha (NI SAWA HAWAKUWA NA HAKI YA KUISHI WALE WA-IRAQ).

  (2) Mauaji ya Raia kule Songea (NI SAWA HAWAKUWA NA HAKI YA KUISHI WALE WANGONI).

  (3) Mauaji ya Mwanafunzi wa Chuo Mbeya (NI SAWA HAKUWA NA HAKI YA KUISHI YULE MNYAKYUSA).

  (4) .........................

  NASHIDWA KUIELEWA HAKI YA KUISHI ALIYOIONGELEA KIKWETE KATIKA KUWAPUMBAZA AIOWAITA ETI NI WAZEE WA DSM.


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
Loading...