Kikwete Daima Nitakukumbuka Kama Shujaa Uliyejenga Mazingira ya Kuiua CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete Daima Nitakukumbuka Kama Shujaa Uliyejenga Mazingira ya Kuiua CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NdasheneMbandu, Apr 29, 2012.

 1. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wadau wanaJF,

  Dalili zipo wazi na kama kuna Mtanzania asiyeziona basi ana matatizo yake kwamba sasa ccm inaelekea kuzimu. Kwa mwenendo wa kisiasa ulivyo, sasa ni dhahiri kabisa kwamba miaka michache ijayo ccm itajiunga na kambi ya upinzani. Jana kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku kupitia kituo cha ITV tulihabarishwa kwamba mbunge wa Geita aliahirisha mkutano na wananchi baada ya zomeazomea kutoka kwa wananchi wachache waliohudhuria mkutano huo. Lilikuwa ni tukio la aibu ambalo siku za nyuma lisingeweza kutokea. Nimeambiwa na mdau mmoja kwamba hali kama hiyo, ilijitokeza pia Shinyanga baada ya mbunge wa Shinyanga Mjini Mhe. Masele kukosa kabisa watu kwenye mkutano alioitisha. Matokeo yake, aliamua kuahirisha mkutano.

  Kwa ujumla, ccm haina mvuto. Imechokwa na sasa inaishi kwa kupumulia mdomoni badala ya puani. Najua baadhi ya wadau watatofautiana nami katika hili lakini niseme tu kwamba uhai wa ccm unatoweka taratibu kama barafu inavyoyeyuka baada ya kutolewa kwenye freezer. Vijana wengi nchini ambao ndiyo nguvu ya chama wanaendelea mmoja baada ya mwingine kujiengua na kujiunga na cdm.

  Hivi karibuni tumeshuhudia kupitia vyombo vya habari jinsi wanachama wa ccm maeneo ya Geita, Sengerema, Babati, n.k. wanavyorejesha kwa hasira kadi, kofia na TShirt za ccm na kujiunga na cdm. Kwa hali hiyo, kwa nini nipate shida kutabiri mwelekeo wa kisiasa hapa nchini!! Hakika kwa sasa hakuna ubishi kwamba ccm itakufa, itazikwa na itapotelea mbali. Itabaki kuwa historia kuwa hapo zamani kulikuwa na dude libaitwa ccm lilitamba na kutamalaki kwa muda wa nusu karne laini baadaye lilijisahau likapotea mwelekeo na kuangushwa na wapinzani wake. Ni nani asiyejua kwamba Engineer na Archtect wa yote hayo ni Mhe. Dr. Dr. Dr. (Heshima-UDOM) Kikwete? KWA MANTIKI HIYO, KWA NINI NISIMKUMBUKE KIKWETE KUWA MIONGONI MWA VIONGOZI MASHUJAA WA UKOMBOZI WA NCHI HII?
   
 2. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Well said. Come 2015 ccm kwishney!! Hongera mkwerre kwa kusanifu na kusimamia ujenzi wa barabara ya kuelekea kaburi la ccm. Binafsi nitakuita BABA WA PILI WA TAIFA LA TANZANIA.
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  CCm kwishney lichama lililowanufaisha vigogo na kutusahau sie wapigikaji! lichama lililojiona kama Mungu flani hivi, lichama lililoleta umaskini mkubwa bongo, lichama lililozaa miungu watu, lichama linalotaka kuteka uandikwaji wa katiba mpya lichama lisilojua linafuata itikadi ipi, ujamaa, ubepari, ukomunisti yaani lipolipo tu halina sera, lichama linalojithamini lenyewe kuliko maslahi ya nchi!! tena life KIBUDU kabsaaaa!!
   
 4. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mi Kikwete ananiacha hoi anavyokaa kimya kwa swala la Zanzibar, kule Watanganyika wanaonewa kama si binadamu, bora hata Wakenya au raia wa nchi zingine wana ka heshima kadogo, Znz inawabagua na kwa matusi nje nje, bora hata wangekuwa wakimbizi wangeenda Unhcr, lakini kwa miaka mingi wakinyimwa haki hukimbilia huku bara na hawapati msaada wowote, je umma wa Tanganyika ujibu kivyake?
   
 5. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Enzi za kidumu chama chama cha mapinduzi kwishney! Kikwete hovy..o, aaahh samahani hoyeeeeee!
   
 6. I

  Imurumunyungu Senior Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama mpango wake wa kukiua chama cha CCM utafanikiwa hadi kufikia 2015 na akaweza kuikabidhi nchi hii kwa CDM katika hali ya Amani! Basi heshima ya JK itakuwa cyo ya hadhi ya DR tena ila atastahili kuitwa PROF..Mungu amusaidie JK aweze kulikomboa taifa hili kutoka kwa wakoloni CCM.
   
 7. k

  kiruavunjo Senior Member

  #7
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sina cha kuchangia ila natambua kwamba ccm mbali na kufa ilianza kuoza ikiwa bado hai.
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Apr 29, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mkuu uko sahihi kabisa! CCM itakufa kifo cha aibu. Pongezi kwa Dr. Dr. Dr. Kikwete kwa kuipeleka CCM Mortuary.
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  wapo nao wanaosema kuwa ccm kimeimarika. Hawa kina Al sahaf wako wengi sana. Ccm ndio kwa heri wandugu
   
 10. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Haya yote sijui bado ni upepo.
   
 11. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,116
  Trophy Points: 280
  Subirini hiyo 2015 muone jinsi Ccm kitakavyo peta katika uchaguzi, ndipo mtajua kama kimeisha au kipo. Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
  .
  "WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
   
 12. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Magamba yameshapukutika yote kwa moto hata kabla ya 2015!
   
 13. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,778
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  Bravo DR DR DR JK without you cdhani km huu umaskini wa watanzania ulioasisiwa na CCM ungeisha...Baba fanya uwezalo kuichanachana CCM vipande 72 ili iwe mwisho wa umaskini wetu loh
   
 14. kikokwe

  kikokwe Member

  #14
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 15
  HAKUNA CHAMA KITAKACHOSHIKA MADARAKA YA NCHI NA KUGAWA VIPANDE VYA DHAHABU, ALMASI, TANZANITE NA FEDHA KWA WANANCHI/WENYENCHI ILI UMASIKINI UWAISHE. UVIVU ULIONAO KAMA UTAENDELEA NAO UMASKIN KWAKO UTAKUWA NDO NYUMBANI KWAKE. Acha uvivu jishughulishe
   
 15. Prince Nadheem

  Prince Nadheem JF-Expert Member

  #15
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 1,026
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  Post mortem 2015! coroner will be CDM.
   
Loading...