Kikwete chonde: Usitie sahihi mswada wa mfuko wa Jimbo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete chonde: Usitie sahihi mswada wa mfuko wa Jimbo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 11, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 11, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hilo ombi la kwanza; ombi la pili, naomba mwenye nakala ya sheria hii anitumie nakala kwenye email yangu ya mwanakijiji hapa jamiiforums.com ASAP. Ombi la tatu, tuache kusikiliza na kutukuza masuluhisho yanayopendekezwa na wazungu tukifikiria kwamba yote yana nia njema kwa sababu ni ya wazungu!
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Aug 11, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu mbona umenishtukiza! kuna hitilafu gani ktk mfuko wa Jimbo ambao umekupa kiamsho hicho!
  Itakuwa vizuri kama ukituelimisha sote manake wengine hatuna hata habari ya mfuko huo ukoje na unalenga vitu gani...
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Huo mfuko hautakuwa na maana yoyote kwenye maendeleo na badala yake utatumika kuendeleza rushwa.

  Pia nimeambiwa ni milioni 16 kwa mwaka ( sina uhakika asilimia 100) ambazo kwenye jimbo haziwezi kufanya mambo ya maana lakini zikipangiwa kazi nyingine kitaifa zinaweza kusaidia.

  Itakuwa vizuri JK akikataa kuweka sahihi yake. Pamoja na credit crunch hii wao wanaendelea kuongeza gharama kwenye serikali.
   
 4. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  JK amekuwa Rais mwenye maono mafupi kweli, yeye kila mara anafikiria kugawa hela.

  - Mabilioni ya JK (tathmini ya mafanikio au vikwazo hakuna anayejua)

  - Mil 500 kwa kila mkoa (tathmini ya mafanikio au vikwazo hakuna anayejua)

  - Na sasa mfuko wa jimbo. (sijui anatumia vigezo gani kuleta tena mfuko huu)

  Nchi inaendeshwa na "Vibwagizo"...
   
 5. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  MMkjj,

  Hii itakuwa ngumu kuungwa mkono, wapiganaji wetu wa upinzani ndio wanaomba kwa nguvu zao zote huo mfuko uwepo, na watawala wamewawekea chambo kama zilivyokuja pesa za ruzuku.
   
 6. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2009
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Lazima atasaini, hana jipya, CCM wote hakuna msafi, wote Majambazi, dawa ni kuwang'oa tu kama KANU Kenya.
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Jamaa atasign tu kama alipoulizwa na wale waandishi wa habari wa Ufaransa, JK akitokea kwenye mkutano wa umoja wa mataifa kwanini Tanzania ni masikini na jamaa akajibu "We are poor because we don't know why were poor" Unategemea nini kama head wa state yuko hivyo kwenye uelewa wake?
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Aug 11, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Bunge lina uwezo wa kutunga sheria tu, Rais halazimi kukubali na ndiyo sababu ya kuweka checks and balances. Sheria hii ni mojawapo ya sheria za kipuuzi ambazo zimewahi kuja kutoka Bungeni na kuungwa mkono kwa asilimia 100 wakati sheria ya madini ambayo ingesaidia sana jamii haijapitiwa kwa miaka 12 na sasa wanairusha rusha kama mpira wa dana dana.

  Kama Kikwete atatia sahihi mswada huu kama ulivyo sasa basi atakuwa kwa mara nyingine tena kuchagua upande wa maslahi ya watu wachache kuliko yale ya taifa na ataendelea kuonesha kile ambacho tumekiandika kwenye Cheche kuwa ni "kushindwa kuongoza". !
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Aug 11, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mkandara kuna vitu kama vitatu hivi ambavyo wabunge wetu hawakujadili huko Bungeni kuhusu huu mfuko. Vitu hivyo ndiyo kiini cha mimi kupinga mfuko huu na natarajia kuonesha siku chache zijazo.

  Kama nilivyosema huko nyuma kuna kitu kimoja tu mbele ya macho yangu nayo ni Tanzania. Yeyote anayesimama kinyume na maslahi ya Tanzania ni adui yangu.
   
 10. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2009
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkjj, JK ni lazima asaini huu muswada sababu ni wa kuwaendeleza wananchi vijijini.
  Kila wakati ambao kuna uwezekano wa pesa za serikali kupelekwa moja kwa moja kwa asilimia kubwa vijijini ni lazima wapenda maendeleo wote wawe mstari wa mbele kushabikia hilo suala.

  Kinachofuata hapa ni kuhakikisha kuwa hizo hela zitumike vizuri.

  Serikali yetu ukiwaachia hela zitatumia kwenye semina ngurdoto, kempinski na kwenye five star hotels huko europe.

  Ningekuona una msimamo kama ungekuja juu vitafunio vya 19bilion vifutwe ASAP na waheshimiwa wale majumbani kwao na wageni wote kwenye ofisi za serikali waambiwe wale makwao kabla ya kwenda huko maofisini.

  MKJJ, kwenye hili umekosea na tafakari Pros na Cons, utaona kwa wanavijiji kama sisi hili litatusaidia, issue ni kumake sure tu hizo hela zitumike vizuri.
   
 11. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  No no no huu ni ufisadi mwingine ati pesa zitaenda vijijini , vijiji gani hivyo. Kama vyama vya ushirika vilishindwa kumkomboa mkulima pesa hizi za kugawana bila malengo zitasaidiaje? Ubadhirifu wa fedha za umma ndio wimbo wetu wa taifa. Kinachokufanya uamini kwamba hizi wataogopa kuzitafuna ni nini?
  Kukuonyesha kwambahizi ni porojo tu hebu msome hapo chini huyu jamaa wa j(angwani, YANGA) Yebo Yebo

   
 12. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mimi sijaelewa kabisa kuhusu huu mfuko na nilimuona Dr. Slaa anautetea kuliko maelezo na hata Mzee Cheyo alitaka kupigana na yule jamaa wa policy forums.

  Hivi ni kwanini hizi pesa wasizipeleke kwenye halmashauri kuongezea budget za maendeleo?
   
 13. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Pesa sio mbaya, watu ndio wabaya.
  Usiichukie nyumba kwa sababu majambazi wanakaa humo, bali wachukie majambazi wanaokaa mle.

  Tafuta njia bora ya kumfukuza nyoka aliyebana ndani ya chungu, kamwe usipende kukibomoa chungu kwa kuwa nyoka ameingia mle.

  Hata EPA haikuwa mbaya, lakini mafisadi walioifisadi EPA ndio wabaya na hatujasikia EPA imepelekwa mahakamani bali walioifisadi EPA.

  Leka
   
 14. W

  WildCard JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kwa tuliomo humu ndani ya Nchi ni bora mfuko huu uanze ili tuone kama unaweza kuwa mbadala wa mapesa ya aina hii yanayopelekwa kwenye Halmashauri zetu. Yanatafunwa kwelikweli. SHIDA KUBWA ya Nchi hii ni UHASIBU na KANUNI zake. Hakuna anayezijali, hakuna anayezifuata, NBAA ipo kwa ajili ya MITIHANI tu. Mbaya zaidi ni pale tunapomtumia CAG ambaye pia ni muajiriwa wa serikali kufanya ukaguzi wa mahesabu ya TAASISI na ASASI za UMMA!
   
 15. M

  Mzee Mzima Senior Member

  #15
  Aug 12, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hivi kweli tunafikiri hizo pesa zitaenda kwa wananchi? unahisi kwa nini wabunge wameamua kupitisha sasa? nahisi ni kwa sababu ya campaigns, wabunge wetu vinara wa upinzani wamekubali haraka kwani wao hawamo katika sectors zinazowasaidia kuwa mafisadi hivyo hawana pesa kwa kampeni, ndo maana wamepigania huu mfuko. pia bwana mkubwa JK lazima appitishe kwani anajua kuwa akiwawezesha vizuri wabunge wake watatoa rushwa nzuri in the name of mfuko wa majimbo, so hata kama unataka kuweka pingamizi la rushwa unashindwa kwani mbunge anasaidia jimbo lake... hahahaha

  kweli wanatuona sisi vilaza... kwa kuwa statistics zinasema bado JK anapendwa basi atuonyeshe kweli ni wa wananchi na akatae kusign at lease mpaka uchaguzi mkuu uishe then bunge lijalo wajadili tena ndo apitishe.
   
 16. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2009
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mfuko huu unawaongezea nguvu wabunge. Wabunge wanataka wawe kama masultani. Wanataka wanyenyekewe na kuombwa ombwa. Chochote kinachowaongezea uwezekano wa kufika huko, wabunge hawewezi kukipinga. Huu mfuko ni mojawapo ya vikolombwezo vinavyowaongezea uwezo wabunge wa kuwa masultani.

  Kimsingi, ikiwa mfuko huu umekubaliwa na wabunge, ni vigumu kuupinga. Hakuna mwenye ridhaa ya wananchi, mwenye uwezo wa kukataa wanachokitaka wawakilishi wao. Hatuna ujanja hapa!

  Lakini mfuko huu ukisimamiwa inaweza kuwa kisu cha kuwachinjia wabunge wengi. Subirini mtaona yatakayotokea.

  Huu mfuko vile vile unaiongezea serikali nguvu dhidi ya wabunge. Kimsingi mfuko huo, unaifanya serikali ipate nguvu ya kuwashughulikia wabunge; mmoja mmoja au kama kundi. Kimsingi mfuko huo unawafanya wabunge wawe karibu zaidi na utawala (serikali); serikali kwa hivyo haiwezi kuukataa. Ni mojawapo ya vyambo vya kuwakamatia wabunge.

  Tusubiri na tuone, kupinga haiwezekani tena; serikali wana maslahi, wabunge wana maslahi. Njia pekee ya kupinga huu mfuko ni kutowachagua hao wanaoushabikia katika uchaguzi ujao. Tunaweza??
   
 17. Companero

  Companero Platinum Member

  #17
  Aug 12, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji rejea hotuba yake ya masaa takribani 4 Bungeni Agosti mwaka jana. Jibu la ombi lako liko humo. Kama huna nakala ya hotuba ile sema nikutumie. Muswada ushaupata, kama bado sema pia nikutumie.
   
  Last edited: Aug 12, 2009
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wamesema wanaipeleka bunge lijalo, lakini hawataki kuuweka muswada wazi ili ijulikane kama unajibu maswali na hoja zilizoibuliwa
   
 19. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Jk atasign kwani hakuna historia ya kukataliwa mswada na Raisi Tanzania!!!

  Hivi wabunge wetu ni mbumbumbu au vioja kwani sijawahi kusikia achilia mbali G55 wakija na mswada wao unaohusu masilahi ya umma na kuteteaa kwa nguvu zotee..wao wanapokea tuu miswada na kuijadili kwa shangwee...

  jamani ni kwamba intelligence zao zipo chini au hawajui wajibu wao??? wengi watapenda mbwembwee kwenye media oh nakuja na hoja binafsi gafla inayeyukaaa...ndivyo tulivyoo au??
   
 20. W

  WildCard JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Baadhi yetu hatukufatilia vizuri jinsi Mfuko ule utakavyokuwa managed.
   
Loading...