Kikwete/CCM Kuigeuza Kigoma Dubai ya Afrika. Mmh!

SHERRIF ARPAIO

JF-Expert Member
Aug 25, 2010
9,539
5,903
As campaign heats up, candidates sling pledges

By Richard Mgamba
5th September 2010


Just two weeks since the campaign for the presidency kicked off, the three front-running candidates are already making a number of pledges that seem infeasible or poorly thought out in their efforts to court votes.

Incumbent Jakaya Kikwete of Chama Cha Mapinduzi has made questionable promises as to what they can accomplish if they are elected on October 31

International airports for everyone?
That wasn't the only promise made by the ruling party's presidential candidate last weekend, though. Kikwete also vowed that he would make Kigoma town the next 'Dubai of Africa' by constructing a modern international airport.

But how do you make Kigoma the next 'Dubai' when Dar es Salaam, the commercial capital, is itself still battling outrageous traffic, caused not by the number of vehicles on the road but by poor planning?

Dar es Salaam has only 170,000 vehicles with a population of 4 million, while a city like Johannesburg has 600,000 vehicles and a population of about 7 million, and yet Johannesburg has the capacity to accommodate its commuters while Dar es Salaam's workers spend up to 5 hours just getting to and coming from their offices.

Furthermore, is it even feasible to be targeting Kigoma in this way? Between Kigoma and Dar es Salaam or Bagamoyo, which one would be most effective as a duty free city? Obviously it's Dar or Bagamoyo because of their strategic coastal locations, but for over five decades, Tanzania has failed to utilise the potential for these two cities to act as a transport hub connecting passengers and cargo in the SADC region.

With the Tanzania Railways Corporation in the 'intensive care unit', is it possible to make Kigoma another Dubai? At the end of the day, importers and exporters from DRC, Zambia, Burundi and Rwanda need a reliable railway to transport their goods to Kigoma.

Railway is still the cheapest way to transport cargo within a short period, after seaways, and air freight is largely unrealistic. Speaking of which, Air Tanzania has all but died a natural death, and is now known as ‘Any Time Cancellation'(ATC).

The airline needed just $250 million to cover the down payment on four new Airbus A320s to enable the national carrier to resume its full role. This is because to order new commercial aircrafts, the buyer should at least pay 25 percent as down payments, while the rest would be paid after delivery pending on the agreements entered by the two parties.

But the company, and the government who is still the majority shareholder, does not have the money, and it's another example of failed corporate governance…Kikwete's promises to build Kigoma an international airport seem all the more unlikely when looking at his past similar promises to other regions especially in Mwanza.

This is the same president who promised in 2006 at Kirumba stadium that he would make Mwanza the next 'Amsterdam' by building an international airport there and bringing in modern infrastructure.

Five years down the line, there is no international airport, and Mwanza continues to struggle with horrendous traffic due to poor planning in infrastructure.

Over half of the city's 1 million inhabitants live in squatters or non-surveyed land. Its lucrative fishing sector is battling the global recession, stiff competition on the global market and rampant piracy on the world's second largest freshwater lake.

Speaking of piracy, in 2005, while addressing the residents of Ukerewe in Nansio Town, President Kikwete promised to make Lake Victoria a safer place for all fishermen by ending piracy if elected.

Today, piracy is worse than ever, making fishing business in Lake Victoria a fruitless and dangerous endeavour for thousands of fishermen. Confronted by the worsening piracy in the area, Kikwete promised last week at a campaign rally in Buchosa constituency, in Mwanza region, that he would make piracy history if elected for a second term.

SOURCE: GUARDIAN ON SUNDAY
 
Watanzania tuna matatizo ya akili. JK aahidi kuigeuza Kigoma kuwa Dubai ya Africa na Mwanza kuwa Amsterdam ya Africa! MMMnnnnnhhh
Kazi kweli kweli:confused2::confused2::confused2::confused2:
 
Five years ago he promised to revive the ailing Tanzania Railway coop. Today the TRL has been moved from ICU to mortuary,No one has questioned!!. The railway was constructed by the Germany masters a century ago! The same government has failed to put gravels and new engines 50 years post independence.
He could not revive the ATC,yet he want to construct an international airport!how many people in kigoma can afford a bus fare the least to say.white elephant!!
I don't know who suffers from amnesia! the wananchi who are not questioning the previous promise or the candidate who promised.
I wonder if the opposition party can seize the gaffe and turn it into their fortune. It remain to be seen
 
Watanzania tuna matatizo ya akili. JK aahidi kuigeuza Kigoma kuwa Dubai ya Africa na Mwanza kuwa Amsterdam ya Africa! MMMnnnnnhhh
Kazi kweli kweli:confused2::confused2::confused2::confused2:

Very dangerous kuwa na viongozi wanao "copy and Paste". Ina maana nchi nzima itakuwa Ulaya/Asia? maana mji huu utakuwa kama mji fulani wa nchi fulani nk. kwani hizi cities wenzake wameziotesha kila jimbo/Mkoa?

Yote haya anajinadi kujenga International Airports kwenye viwanja ambavyo wameshindwa kujenga run ways kwa miaka nenda rudi japo kila siku wanatudanganya watajenga. International airport kwa ajili ya precisionair? Connection ya ndege tu hawajafanikiwa hadi uende nairobi sasa wataweza kufanya connection kila mkoa?

CCM mna kichaa!!!!!!!!!
 
Hawa wanaotutawala sasa wamekuwa na AMANA YA UONGOZI kwa miaka 50. Matokeo yake hatuna hata shirika la reli au la ndege la kuaminika. Kwenye upatikanaji wa umeme, maji na usafiri bora tuko nyuma kuliko hata nchi kama Uganda na Burundi ambazo zimepigana vita.

What do we have to show for fifty years of rule by CCM and its predecessor? Nothing but woe after woe of economic mismanagement.

It is enough. We must start the next 50 years with another team. Mwaka 1974 Mwalimu alisema tusipolima tutakufa. Na sisi tunasema leo Tusipobadilisha chama tawala tutakufa.
 
Hawa wanaotutawala sasa wamekuwa na AMANA YA UONGOZI kwa miaka 50. Matokeo yake hatuna hata shirika la reli au la ndege la kuaminika. Kwenye upatikanaji wa umeme, maji na usafiri bora tuko nyuma kuliko hata nchi kama Uganda na Burundi ambazo zimepigana vita.

What do we have to show for fifty years of rule by CCM and its predecessor? Nothing but woe after woe of economic mismanagement.

They can showcase AMANI, UTULIVU NA MSHIKAMANO. They have christened our country KISIWA CHA AMANI.
 
bagamoyo Hollywood.


JK anaweza kweli kufanya hayo, wala hakuna linaloshindikana. Uliza ni kwa namna gani?

1) Kuwapa walowezi sehemu nyeti kama fukwe, sehemu zenye madini, sehemu zenye mali nk
2) kuwekeza na jamaa zake wa huko ulaya na marekani kwa kuwa anajua muda si mrefu atakuwa anachuma tu bila jasho.
3) Kwa kuhakikisha tuchanga michango mingi bila kuelewa tunamchangia nani.

4) Atahakikisha anauza hadi kuta za nyumba zetu ili watu wajue nini maana ya ufisadi.
 
I wish this article could be translated into a brochures and distributed to all regions of Tanzania, so everyone could read and see this fuckin' promises of CCM.
I'm truly agreed with the writter on how come the ruling party continues to make promises while those promised in 2005 have not yet accomplished? Every where the president promised a morden infrastructure, where was this government before? didnt they see these problems to the community before? why today? for my layman knowladge I can call this also a corruption, if TAKUKURU couldn't be under the umbrella of the govt, they could sue these people. Mh Rais, why don't you think on improving our currency instead of making huge promises, don't you c our shilling falling daily?
Hey people wake up.. why don't we try to make some changes by selecting other parties so that we can see differences???

Kazi yao kula kodi zetu tu, na kwa ahadi tutaona watakavyokuja kutubana kwenye mbinu nyingine za kupatia kodi...
 
yea is just matter of time, love it or hate it

Time!? unahitaji muda gani kama miaka 45 wameshindwa yeye ataweza kweli
okey kwa msaada wa nchi gani kama anaenda kuomba net na anadai nchi haiwezi kuendelea bila kuomba!!
 
Matatizo ya Ilani ya CHadema hayo.. sasa japo waige na kilichoandikwa..

Mbona tayari walishaiga ndani ya "Kutoka hapa Mpaka Kule" pale uliposema Chadema wana makosa ya kuandika sera nyingine zinazofanana na CCM, JK akainyaka hiyo na kuirusha hewani kwenye kampeni zake kwamba Chadema wana Copy na Ku-paste hivyo akawaomba waTz wasitumie sera za copy and paste wakati sera original zipo kwenye CCM
 
JK: Ahadi mpya za nini? Ondoa kero hii



amka2.gif
BAADA ya kupotea kwa wiki kadhaa, napenda kuwaambia wasomaji wangu kwamba nimerudi kwa kishindo.
Kupotea huko kulitokana na matatizo yaliyokuwa nje ya uwezo wangu, lakini kuanzia sasa tuko pamoja kwa ajili ya kuendeleza mapambano haya.

Leo tunapokutana kila mmoja wetu anaelewa kitu kinachoendelea ndani ya taifa, nacho ni kampeni za Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani.

Hivi sasa wagombea wote hawalali usingizi mnono, wanalala usingizi wa mang'amung'amu mithili ya sungura anayewindwa porini.

Wakati kila kona kukiwa na hali hiyo, wagombea wameanza kuzunguka mikoani kutafuta mitaji ya kisiasa (kura) za wananchi ili Oktoba 31 mambo yawe sawia

Wagombea hivi sasa wanapigana vikumbo vya kutoa ahadi zinazozidiana ili kuwajengea mazingira mazuri ya kuukwaa uongozi.

Si siri, kazi ya siasa ni ahadi na ‘uongo' ambao utekelezaji wake wakati mwingine huwa mbinde, hali ambayo inadhihirisha kuwa siasa ni mchezo mchafu.

Leo wasomaji wangu nimeguswa na ahadi nyingi zilizotolewa na mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete, katika mikoa aliyopita. Amekuwa akitoa ahadi nyingi ambazo zinaonekana kuwagusa wananchi wenye matatizo makubwa kama wale ambao usafiri wao hutegemea meli au vivuko.

Leo tunajadiliana katika hili, Kikwete ameahidi kama akichaguliwa atanunua meli kubwa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa mikoa ya Kagera na Mwanza ambao huo ndio usafiri wao mkuu kila kukicha.

Wananchi wa mikoa hii, wamekuwa na shida nyingi sana baada ya kuzama kwa meli ya mv Bukoba ambayo iliua mamia ya Watanzania.

Nimepata mshutuko mkubwa pale niliposikia eti anasema wakimchagua ndiyo atanunua, sikuamini kauli hii kwa sababu wakati meli hii inazama na kuua ndugu zetu, Kikwete alikuwa kwenye Serikali ya Awamu ya Tatu.

Mwaka 2005 Watanzania bila ajizi walimchagua kwa kishindo, amekaa madarakani kwa miaka mitano, ina maana hiyo shida ya wananchi kukosa meli alikuwa haioni?

Pili, hii inaonyesha wazi jinsi viongozi wa nchi za Afrika walivyo na udhaifu katika utendaji wao wa kazi, niliamini kiongozi mwenye uchungu na watu wake katika miaka mitano iliyopita angekuwa amefanya maamuzi mengine.

Tatu, kwa nini Kikwete atumie muda huu ambao anajua ana shida na kura za wananchi ndiyo atoe ahadi nono kama hizi? Hapa tunahitaji majibu.

Lakini si kwa wananchi Mwanza na Kagera, mgombea huyu ametoa ahadi kama hiyo mkoani Kigoma na kule Ziwa Nyasa, kwamba nako wakimchagua atahakikisha anapeleka meli na kivuko.

Nne, hivi wananchi hao wasipomchagua ina maana kwamba hawatapelekewa maendeleo mpaka CCM ichaguliwe?

Haiingii akilini kabisa katika hili, kwa nini tuwe na viongozi wa kujaza wananchi ahadi, wakati utekelezaji au ueletaji wa maendeleo ni jukumu la serikali na wananchi wake.

Moja ya kero kubwa ambayo imenigusa leo kuandika waraka huu ni ahadi ya Kikwete juu ya ujenzi wa viwanja vya ndege ambavyo ameahidi kama akichaguliwa tena.

Kwa bahati nzuri nimetembelea mikoa mingi ya Tanzania kwa usafiri wa angani na nchi kavu, ambapo nimeona ubovu wa viwanja vya ndege, tangu taifa hili limepata uhuru.

Nilisikitika sana kusikia Kikwete anasema kama akichagulia atahakikisha anajenga kiwanja kizuri cha ndege pale Sumbawanga na maeneo mengine.

Napenda kuchukua fursa hii kumtaka Kikwete kwa nia njema kabisa kwamba asianze kazi ya kujenga viwanja vipya, badala yake aidhinishe fedha za kuvijenga vilivyopo.

Msomaji wangu, nimebahatika kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Singida, uwanja huu unatia aibu ambayo haina kifani.

Nilipokuwa angani naelekea kutua pale, nilifikiri kwamba ni njia ya kupitishia mifugo, rubani niliyekuwa naye alishikwa na bumbuwazi.

Hebu Kikwete fikiria uwanja ule ni mkoa ambao wewe na viongozi wenzako mnaufahamu vizuri sana, umeshika nyadhifa serikalini, umeutumia, kwa nini usitenge fungu la kuukarabati?

Uwanja huu hauna gari la zimamoto, hauna michoro ambayo inaweza kumsaidia rubani wakati wa kutua na kuruka! Hili nalo linahitaji ahadi kweli?

Hebu Kikwete fikiria uwanja una jengo dogo la wageni maalumu (VIP), choo cha wageni kiko nje, hakina maji ya bomba wala nini, nasema katika ahadi sikubaliani na wewe kabisa.

Kikwete, najua pale Morogoro wewe ni mwenyeji sana kwa sababu naelewa umekwishatembelea maeneo mengi ya mkoa huo, je uliwahi kufika kwenye uwanja wa ndege?

Hebu fikiria mkoa huu hauna uwanja wa ndege wa serikali, kwani uliopo ni uwanja wa Mamlaka ya Tumbaku.
Hebu fikiria aibu hii, ambayo mkoa umekuwa nao kwa zaidi miaka karibu 50 ya uhuru wa Tanzania. Niliposhuka na ndege pale sikuamini hata chembe uchakavu ule.

Uwanja ule hauna jengo lolote zaidi ya banda la kuhifadhia tumbaku, hauna gari la zima moto, hauna kituo cha polisi, hakuna michoro, umejaa majani ambayo wakati ndege inaruka rubani anatumia uwezo wake binafsi.

Mikoa hii yote ina viongozi kama vile mkuu wa mkoa, ofisa tawala na mkuu wa wilaya, ndiyo kusema hawaoni aibu hii? JK hapa nisaidie nipate jibu.

Mkoa huu ulipachikwa jina la utani la ‘Mji Kasoro bahari' niliamini kuwa ungekuwa mfano wa kuigwa katika suala zima la miundombinu.

Mbali ya mikoa hiyo, aibu hii iko kwenye viwanja vya Shinyaga, Kigoma na Musoma lakini pale Mpanda niliona shirika moja la Umoja wa Mataifa limeamua kuondoa aibu kwa kujenga ule uwanja.

Sijui ni kwa sababu anatoka waziri mkuu? Sina uhakika lakini majibu niliyoambiwa ni kwamba shirika hilo linalipa fadhila baada ya eneo hilo kukaliwa na wakimbizi kwa muda mrefu.

Viwanja hivi Kikwete amekwishatua na ndege mara nyingi na amejionea hali halisi, nilitegemea ahadi zake angesema sasa anaelekeza nguvu kwa ajili ya kuvijenga ili vifikie kiwango kinachotakiwa.

Uwanja kama ule wa Kigoma, Shinyanga na Musoma siamini kabisa kama serikali imeshindwa kutenga bajeti tu ya kuweka lami sehemu ya ndege kutua (Run way) au ndiyo ule msemo wa taifa letu bado changa?

Sikubaliani na hilo hata chembe, kama Mkuu wa mkoa mmoja anatumia gari la sh mil. 200 na tunao zaidi ya 21, hatuwezi kushindwa kutenga fedha za kujengwa viwanja hivi.

Huu ni uvivu wa wataalamu wetu ambao unaendelea kushamiri kila kukicha, au hili nalo linahitaji lifungiwe safari ya kwenda kwa wahisani kama vile Marekani na Ulaya?

Ni aibu, umefika muda wa kutumia rasilimali zetu kwa ajili ya manufaa ya kizazi kijacho.

Natumaini Kikwete leo anasoma waraka huu, ningependa walau katika yote niliyosema hapo juu ili tuondokane na aibu hii, kila mwaka bajeti za Wizara ya Miundombinu zitengwe pia zikigusa viwanja hivi.

Kwa mfano, pale Shinyanga serikali ya Kikwete ingesema inatenga kodi inayopatikana kutoka kwenye mgodi wa Mwadui, naamini ingeweza kujenga uwanja huu bila ubishi wowote ule.

Nimekuwa nikiusikia mgodi huu tangu nikiwa mdogo mpaka hapo nilipofikia, naelewa wazi pamoja na kubinafishwa unalipa kodi ama halmashauri au kwenye mamlaka nyingine, hapa tatizo ni mipango butu iliyozooeleka kwa watawala wetu.

Leo namalizia kwa kusema, Kikwete naomba majibu ya kuhusu viwanja hivi ili sisi Watanzania wanyonge tuendelee kuwa na imani na watawala wetu.

Tuachane na tabia ya kila kitu mpaka tupewe fungu na wakubwa wa nje (wahisani), hivi siku wakikataa tutakimbilia wapi? Tutakuwa wageni wa nani? Imetosha.

Tutumie utajiri wa madini, mbunga za wanyama, samaki, vivutio vya watalii na bahari kulijenga taifa kuliko kila kukicha kutembeza bakuli kwa wakubwa.

Mheshimiwa Kikwete nisaidie majibu haya nayasubiri kwa hamu.



JK: Ahadi mpya za nini? Ondoa kero hii
 
hayo yote yanawezekana.ni swala la kujipanga na wote mkaendelea kuikumbusha seriklai itakayoingia madarakni kutimiza hayo yaliyosemwa hata kwa kijikongoja jamani.tutafika tu,keep on making them accountable thu ur representatives.
 
Back
Top Bottom