Elections 2010 Kikwete: Bila safari za nje tungekufa njaa

Sasa kila kitu tunafanya kwa kutumia misaada! Hivi hatuwezi kujitegemea kwa kutumia resources zetu kweli? Ndugu Mkapa alifanya mabaya fulani lakini alijaribu kutaka kuitemeza nchi, na mifano mizuri ni hii miradi ya maji ya ziwa victoria na mabarabara kadhaa ambayo yalijengwa kwa kutumia fedha zetu wenyewe. Lakini huyu the comedy wetu sidhani kama kuna mradi wowote aliouanza yeye ambao umetumia fedha yetu wenyewe.
 
kwa nini asingejisifu kwa kusimamia vizuri rasilimali zetu na kusema zimesaidia kwenye maendeleo pamoja na elimu bure, afya bure bila ya kwenda kuwapigia magoti wazungu huko kwao? None Sense
 
jana nilikukwa naongea na baba yangu juu ya hii habari

baba yangu akasema hivi hajawahi kuona Rais ''mp-------------u---mbavu kama huyu.''
 
"Kuna wakati nilikwenda Marekani nikakutana na rafiki yangu akasema wewe kwako si unatatizo la malaria, nikamweleza ndiyo akasema atanikutanisha na mtu atakayenisaidi na kumaliza tatizo ... kweli akanikutanisha naye na akanunua vyandarua vyenye thamani ya Dola milioni 78," alisema.

Ni aibu kwa raisi wa nchi kusema ujinga kama huo. Kwani hii nchi haiwezi kununua vyandarua? Kwanza anasema kuna wakati alienda, hajasema alienda kufanya nini, au anafika mitaa ya DC au NY na kuanza kuomba hivi "do you spare a change to buy mosquito nets" au "starving, need money to buy food for Kaliuas" or "my dogs need food, i am homeless, need money for my dogs back home"

Gharama ya ndege yake kuwa angani wa lisaa limoja tu ingetosha kununua vyandarua milioni 1. Ukiweka na gharama za malazi Per diem, shopping etc ni anaother 3 million mosquito nets. Na je net zitamaliza tatizo la maleria? Net hiyo itafungwa wapi wakati watu hawana nyumba?

It was very wrong kwa Mkapa kumuweka huyu jamaa foreign affairs, kwa sababu hakujifunza local administration, na ndio maana anafikiri kuongoza ni kwenda nje kuomba misaada wakati unaishi kwenyeey hoteli ya doal 8000 kwa siku moja. Na nshaona huo ujinga unaanza hata kwa Membe, ameshaona kuwa yeye ndio anafaa kuwa raisi, sijui huo ujinga wa foreign affairs minsters kudhani kuwa wanastahili kuwa maraisi umetoka wapi, uchizi tu
 
Sasa nimeelewa kwanini walikataa MDAHALO.Kauli hiyo angeitoa katika mdahalo Jahanamu ingemwangukia.Korea kaskazini kiongozi wake ameenda nje mara ngapi,wana hali gani,Thailand viongozi wao wanasafiri mara ngapi??
Mheshimiwa ni lazima aelewe ya kuwa safari yake moja ya nje inakamua hazina.

Nini Thailand, Kibaki hapo Kenya umemsikia mara ngapi anavinjari USA? au Jamaica kubembea. Mbona hajasema Jamaica alituletea nini, au bange, manake mtu anayeongea hivi lazima awe amekolea. Je kule Turkey na Cuba alituletea nini huko. Ile ahadi ya kuwa atasaidia Cuba kuongea na marekani ili wawaondolee vikwazo kwa kuwa yeye ni rafiki wa Obama (sijui huo urafiki ulianza lini) imeshatekelezwa. JK anadhani angepewa tena second time ya kukutana na Obama kama first time aliongea upupu, lol
 
Atakumbukwa kwa kuwakumbatia mafisadi, kwa matumizi mabovu ya fedha za walipa kodi, kupiga picha na Drogba, na hotuba zake zisizokua na mbele wala nyuma..kwa kifupi ni msanii
 
Naomba jamani tuelimishe umma juu ya kujitegemea mana hao wenzetu waliokuwepo enzi za mwalimu labda hawakumuelewa..........Juu ya kauli ya kufanya ili ukumbukwe hapana si sahihi ila wajue wanayofanya kuleta maji namengineyo ni haki na lazima kwa wananchi sio watumie ndege namashangingi bure wakati wananchi wanatembea umbali mrefu kufuata asprini kwenye vituo vya afya.
 
JK: Bila safari za nje tungekufa njaa

Na Joseph Mwendapole


* Asema hawezi kubakia Ikulu akimtazama Salma
* Anataka akumbukwe kwa kujenga barabara, maji

Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, akiwasalimia wananchi baada ya kuwasili katika Jimbo la Sikonge, mkoani Tabora kuhutubia mkutano wa kampeni jana.(Picha: Khalfan Said).

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amewashangaa watu wanaobeza safari zake za nje na kusema kuwa bila kwenda nje kuomba kwa wahisani huenda Watanzania wengi wangekufa kwa njaa.

Aliyasema hayo katika jimbo la Urambo Magharibi na Mashariki akiwanadi wagombea wa ubunge katika majimbo hayo, Samuel Sitta na Profesa Juma Kapuya.

“Ninapokwenda nje nakwenda kwa malengo. Siende tu. Siwezi kukaa Ikulu jijini Dar es Salaam, kuangalia uzuri wa mke wangu Salma … hapana lazima nikutane na watu huko huko waliko,” alisema na kuongeza:

“Ziara zangu zina manufaa makubwa sana, hivi nikikaa pale Ikulu nikamwambia mke wangu 'Mama Salma umependeza sana' huenda wengine mngeshakufa kwa njaa, mimi bila kwenda nje Wajapani wangeijuaje wilaya ya Kaliua?” alihoji.

Katika mikutano hiyo iliyofurika watu, alisema anapokwenda nje ya nchi anakutana na watu mbalimbali mashuhuri na matajiri ambao wamekuwa wakiisaidia Tanzania katika nyanja mbalimbali kama elimu, afya na miundombinu.

“Kuna wakati nilikwenda Marekani nikakutana na rafiki yangu akasema wewe kwako si unatatizo la malaria, nikamweleza ndiyo akasema atanikutanisha na mtu atakayenisaidi na kumaliza tatizo ... kweli akanikutanisha naye na akanunua vyandarua vyenye thamani ya Dola milioni 78,” alisema.

Alisema vyandarua hivyo, milioni 14 vitaanza kugawiwa na hadi Desemba mwaka huu zoezi la kuvigawa litakamilika.

Alisema hata vyandarua vilivyotolewa bure kwa watoto ilikuwa ahadi ya Rais mstaafu wa Marekani, George W. Bush, ahadi iliyotekelezwa na Rais wa sasa wa nchi hiyo, Barrack Obama.

Kwa upande wake Sitta alimwomba Rais Kikwete fedha zilizotengwa kwa ajili ya barabara za Urambo zisihamishwe ombi ambalo Kikwete alilikubali.

Sitta alimmwagia sifa Kikwete kuwa alilelewa vyama na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, na kwamba kila aliyemwona alijua angefika hapo alipofika na kuwataka wananchi kumpa ushindi wa kishindo.

Sitta alijisifu kuwa ni chuma cha pua na kwamba anakaribia kustaafu siasa na kuwataka wananchi kumchagua pamoja na madiwani.

Katika hatua nyingine, Kikwete, amesema iwapo atachaguliwa tena kwa miaka mitano ijayo, anataka atakapostaafu Watanzania wamkumbuke kwa kutatua kero ya maji, elimu na barabara.

Kadhalika, alisema Watanzania wasitishwe na wanasiasa wanaohubiri kuwa damu itamwagika.

Aliyasema hayo katika tarafa ya Kaliua jimbo la Urambo Magharibi, mkoani Tabora.

Alisema katika miaka mitano ijayo ataelekeza nguvu kubwa kutatua kero ya maji maeneo mbalimbali nchini ili atakapostaafu akumbukwe kwa hilo.

Rais Kikwete alisema serikali imejitahidi kufanya mambo makubwa katika elimu kwa miaka mitano iliyopita na kwamba zamu hii miaka mitano nguvu kubwa itakuwa kuwapatia wananchi maji ya uhakika.

“Kama ambavyo Watanzania watakavyoikumbuka serikali yangu ya miaka mitano iliyopita katika elimu nataka awamu hii wanikumbuke kwa kuwapa maji …watu waseme tulikuwa na tatizo la maji, lakini Rais Kikwete alitutatulia,” alisema.

Alifafanua kwamba serikali imechimba visima, lakini havitoshi hivyo itachimba vingine 15 kwa kuanzia wilaya ya Urambo na vingine vitaendelea kuchimbwa hadi kero ya maji iishe. Pia, alisema serikali ya Japan imeahidi kufikisha maji katika wilaya mbalimbali mkoani Tabora.

Aliwaomba wananchi wa Urambo Magharibi wamchague Profesa Kapuya, kwani amekuwa na msaada mkubwa kwake tangu mwaka 2005.


CHANZO: NIPASHE

Hawa watu wanaoitwa sijui wahisani ndiyo leo wametufikisha kwenye umaskini wa kutupwa.Maana kama wasingekuwa wakitoa hivi vimisaada vyao huenda huyu ombaomba wetu angepata akili ya uongozi.Lakini sasa hata kufikiri hawezi tena yeye kila siku kuomba tu.Kwake yeye umaskini utaondoka kwa kuombaomba.Angalia wenzetu kenya bajeti yao sasa haita senti ya misaada ,sisi sijui tunakwenda wapi.
 
Oh My God, inabidi sasa hivi tuwe hata na code of ethics ya kuongea, sidhani kama ni sifa kusema nilienda kuomba. Kama nchi zote alizotembelea JK zingetoa ahadi na kutekeleza basi nadhani tungekuwa mbali sana. Lakini angesema ni gharama kiasi gani huwa anatumia kwa safari moja na tujue tija ya safari hizo ni nini. Otherwise tutakuwa tunafanywa wajinga tu.

Mbona Mkapa alikuwa hasafiri na hatukulala njaa, tulikuwa na neema zaidi kuliko sasa? mbona viongozi wa Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda hawasafiri ovyo na hawajalala njaa? Does he mean that we are not working tunakula kwa kuombaomba? wengine kwetu kuwa ombaomba ni jambo la aibu sana. Isitoshe katika kipindi chote cha miaka mitano tuymekuwa tunakula jasho letu bila msaada, na jasho letu ndio limekuwa linalipia safari za Rais na wasaidizi wake nje ya nchi.
 
Huyu jamaa naona ngao ya malaria awe anakunywa maana imemzidi sana kila akiumwa na mbu hata asiye wa malaria ana kuja na jipya. Madini anayogawa bure hayawezi kututosha mpaka akawe MATONYA. shame!! Sisi na salima au mwarabu hatuhusu! hana jipya. Sio mbunifu he is routine man. anachojua ni kukopa tu ulaya. CHAGUA Dr. Slaa kwa ubunifu na umakini.
 
Brainwashed Matonya.... Hivi huyu jamaa alisomea chuo gani, kozi gani na alipata GPA ngapi ili tumpime IQ yake!!
Ila ajue cku hizi hali ni mbaya, ukiwa baba wa familia halafu unategemea kuomba msaada au kuhemea ili watoto wale mijamaa lazima itakuchukulia mkeo tu....
 
Back
Top Bottom