Kikwete: Bila safari za nje tungekufa njaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete: Bila safari za nje tungekufa njaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Oct 1, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  JK: Bila safari za nje tungekufa njaa

  Na Joseph Mwendapole


  * Asema hawezi kubakia Ikulu akimtazama Salma
  * Anataka akumbukwe kwa kujenga barabara, maji

  Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, akiwasalimia wananchi baada ya kuwasili katika Jimbo la Sikonge, mkoani Tabora kuhutubia mkutano wa kampeni jana.(Picha: Khalfan Said).

  Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amewashangaa watu wanaobeza safari zake za nje na kusema kuwa bila kwenda nje kuomba kwa wahisani huenda Watanzania wengi wangekufa kwa njaa.

  Aliyasema hayo katika jimbo la Urambo Magharibi na Mashariki akiwanadi wagombea wa ubunge katika majimbo hayo, Samuel Sitta na Profesa Juma Kapuya.

  “Ninapokwenda nje nakwenda kwa malengo. Siende tu. Siwezi kukaa Ikulu jijini Dar es Salaam, kuangalia uzuri wa mke wangu Salma … hapana lazima nikutane na watu huko huko waliko,” alisema na kuongeza:

  “Ziara zangu zina manufaa makubwa sana, hivi nikikaa pale Ikulu nikamwambia mke wangu 'Mama Salma umependeza sana' huenda wengine mngeshakufa kwa njaa, mimi bila kwenda nje Wajapani wangeijuaje wilaya ya Kaliua?” alihoji.

  Katika mikutano hiyo iliyofurika watu, alisema anapokwenda nje ya nchi anakutana na watu mbalimbali mashuhuri na matajiri ambao wamekuwa wakiisaidia Tanzania katika nyanja mbalimbali kama elimu, afya na miundombinu.

  “Kuna wakati nilikwenda Marekani nikakutana na rafiki yangu akasema wewe kwako si unatatizo la malaria, nikamweleza ndiyo akasema atanikutanisha na mtu atakayenisaidi na kumaliza tatizo ... kweli akanikutanisha naye na akanunua vyandarua vyenye thamani ya Dola milioni 78,” alisema.

  Alisema vyandarua hivyo, milioni 14 vitaanza kugawiwa na hadi Desemba mwaka huu zoezi la kuvigawa litakamilika.

  Alisema hata vyandarua vilivyotolewa bure kwa watoto ilikuwa ahadi ya Rais mstaafu wa Marekani, George W. Bush, ahadi iliyotekelezwa na Rais wa sasa wa nchi hiyo, Barrack Obama.

  Kwa upande wake Sitta alimwomba Rais Kikwete fedha zilizotengwa kwa ajili ya barabara za Urambo zisihamishwe ombi ambalo Kikwete alilikubali.

  Sitta alimmwagia sifa Kikwete kuwa alilelewa vyama na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, na kwamba kila aliyemwona alijua angefika hapo alipofika na kuwataka wananchi kumpa ushindi wa kishindo.

  Sitta alijisifu kuwa ni chuma cha pua na kwamba anakaribia kustaafu siasa na kuwataka wananchi kumchagua pamoja na madiwani.

  Katika hatua nyingine, Kikwete, amesema iwapo atachaguliwa tena kwa miaka mitano ijayo, anataka atakapostaafu Watanzania wamkumbuke kwa kutatua kero ya maji, elimu na barabara.

  Kadhalika, alisema Watanzania wasitishwe na wanasiasa wanaohubiri kuwa damu itamwagika.

  Aliyasema hayo katika tarafa ya Kaliua jimbo la Urambo Magharibi, mkoani Tabora.

  Alisema katika miaka mitano ijayo ataelekeza nguvu kubwa kutatua kero ya maji maeneo mbalimbali nchini ili atakapostaafu akumbukwe kwa hilo.

  Rais Kikwete alisema serikali imejitahidi kufanya mambo makubwa katika elimu kwa miaka mitano iliyopita na kwamba zamu hii miaka mitano nguvu kubwa itakuwa kuwapatia wananchi maji ya uhakika.

  “Kama ambavyo Watanzania watakavyoikumbuka serikali yangu ya miaka mitano iliyopita katika elimu nataka awamu hii wanikumbuke kwa kuwapa maji …watu waseme tulikuwa na tatizo la maji, lakini Rais Kikwete alitutatulia,” alisema.

  Alifafanua kwamba serikali imechimba visima, lakini havitoshi hivyo itachimba vingine 15 kwa kuanzia wilaya ya Urambo na vingine vitaendelea kuchimbwa hadi kero ya maji iishe. Pia, alisema serikali ya Japan imeahidi kufikisha maji katika wilaya mbalimbali mkoani Tabora.

  Aliwaomba wananchi wa Urambo Magharibi wamchague Profesa Kapuya, kwani amekuwa na msaada mkubwa kwake tangu mwaka 2005.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Our Preident is depended mind person; kwa yeye ili kuondokana na tatizo lazima aombe misaada, haoni fursa zilizoko nchini mwake ambazo zinawanufaisha hao ambao anawategemea kwa misaada.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyu mjamaa anavyoniboa mimi! Anaona ni bora atumie rasilimali za nchi kujenga viwanja vya ndege vya kimataifa kila mkoa huku akitembeza bakuli nje ya nchi kulisha wananchi wake! Anatakiwa akapimwe akili! This is TOO MUCH!!!!
   
 4. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Ni kweli JK, hatujafa njaa ila tumekopa stanbic ili tusife njaa. pathetic!!!
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Wanaotakiwa kupimwa akili ni wale Wadanganyika ambao wako tayari kumpa kura!!!
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Yeah, joker kweli tunaye.
   
 7. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #7
  Oct 1, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Hizi kauli zinaudhi sana, kawadharau sana Watanzania.
   
 8. s

  sadique Member

  #8
  Oct 1, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  sijui nimtukane??? Hivi kweli kuombaomba makombo kwa wazungu yeye anaona ujanja? eti kapewa neti za mbu! hii kweli ndiyo tiba ya malaria? badala ya kushughulikia chanzo cha malaria yeye anashughulikia symptoms??? Inatia kichefuchefu!!
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hapo ndo ananishangaza huyu jamaa, kama tungetumia vyema resource zetu mambo ya misaada tusingeomba.
   
 10. w

  wela masonga Member

  #10
  Oct 1, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 33
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Kama uelewa wake ndo huo basi watanzania walikosea kumpa urais mwaka 2005 na watakosea zaidi kumpa urais mwaka huu. Awaachie nchi wanaoamini kuwa ukiwa na rasilmali kama tulizonazo Tanzania, siyo lazima utegemee misaada. Uzembe wa kufikiri siyo sifa anayotakiwa kuwa nayo rais. Babu zetu wangekuwa hivyo Tanzania ingekuwepo?
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  anastahili either leave without pay or redundancy kuanzia 31st Oktoba 2010
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Rais dhaifu kutoka kwa chama chenye fikra dhaifu na wananchi dhaifu
   
 13. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #13
  Oct 1, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Akakomba kila kilichokuwa kwenye Hazina, akaenda kuomba misaada, kumbe huku nyuma watu wafa njaa, Hazina haina kitu!

  Akili hizi za Mbayuwayu.... LOL

  Sasa alichokifanya ni nini? Wako wapi hao wawekezaji? Iko wapi hiyo misaada?

  Mpaka leo watu wanaishi kwenye nyumba za udongo na nyasi, usiombe moto uwake, majivu kila pahala!

  Nenda bwana... nenda... ONDOKA IKULU, kwa amani! Ondokaaaaa!
   
 14. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Matonya at his highest level!
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hata mi namshangaa..
  Hivi muhimu ni kumpa mtu chandarua au kumwezesha yule mwananchi awe na kipato ambacho ni predictable kitakachomwezesha kununua chandarua huko mbeleni baada ya kuweza kujitegemea? Hivo vyandarua anavyoomba vikiharibika nani atanunua vingine?

  Kweli rahisi tunaye..
   
 16. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Salaam,
  Nimesoma hii taarifa Kwa masikitiko, Nashindwa Kuelewa, Tafadhali nisaidieni WanaJamii;
  Mbali na Elimu, Umri wa Mgombea Uraisi, akili timamu nk: Ni sifa zipi au elimu kiwango gani zingeongezwa kwa mgombea nafasi hii ya Juu ya kuongoza, kuwawakilisha Watanzania katika maswala tofauti ndani na nnje ya Nnchi yetu.

  Nina wasiwasi na upeo wa upembuzi wa maswala muhimu na mikakati yakinifu ya utatuzi wa matatizo makubwa ya nnchi yetu, siwezi kuainisha yote hapa, but niko interersted na;
  1. Tatizo la kutokujua tatizo
  2. Kirusi cha Akili tegemezi for now,

  1: Tatizo la kutokujua tatizo matatizo mengi yanatukabili, Mtanzania mmoja mmoja, na
  kwa ujumla, Najua hatua
  ya kwanza ktk utatuaji wa tatizo ni kulielewa vizuri tatizo, causes etc........

  Nanukuu haya maneno na Mwakilishi wa sasa wa Jamuhuri
  "“Kuna wakati nilikwenda Marekani nikakutana na rafiki yangu akasema wewe kwako si unatatizo la malaria, nikamweleza ndiyo akasema atanikutanisha na mtu atakayenisaidi na kumaliza tatizo ... kweli akanikutanisha naye na akanunua vyandarua vyenye thamani ya Dola milioni 78,” alisema." Nimemaliza kunukuu.
  Niliwahi kufundishwa @primary school causes za malaria na tiba yake ni kutokomeza vyanzo vyake (madimbwi, vichaka na kadhalika); Nisaidieni, Tunatokomeza malaria kwa Kuweka chandarua? Fikiri mtaa unaoishi kuna vianzilishi vya aina gani na vingapi? je vinatokomezeka? Vinahitaji msaada kutoka jamuhuri fulani jirANI? wazungu au?

  Kiwanda cha Neti Arusha kimeajiri watu wengi, yes (GOOD)kwa ajira, mabasi mapya kabisa n.k. But hii ni genuine SOLN? I don think so!

  2. Kirusi cha Akili tegemezi
  Hili ni tatizo kubwa zaidi ya yote uliowahi kusikia, Naamini hata katika ufundishaji wa shule zetu, Wazungu wanafundishana kusaidia, sisi kusaidiwa, Ni aibu sasa mambi tunayoomba msaada kwayo, Tunadharaulika sana, Mh JK apokea misaada kadhalika, ukiangalia vizuri unaona neti, pikipiki, na bidhaa fulani fulani za kichina, ambazo naweza sema ni Aibu. Naamini uwezo tunao tukiamua kuachana na dhana hii ya Utegemezi (Yes we need them, bt kuna mambo twaweza fanya...for now,

  Kwenye hili "
  “Ninapokwenda nje nakwenda kwa malengo. Siende tu. Siwezi kukaa Ikulu jijini Dar es Salaam, kuangalia uzuri wa mke wangu Salma … hapana lazima nikutane na watu huko huko waliko,” alisema na kuongeza:" Nukuu
  Naamini kuna mengi ya maana JK angefanya akiwa hapahapa Kwenye nyumba yetu (IKULU) zaidi ya kuangalia Uzuri wa 1st Lady, Kuuangalia Uzuri huu Ikulu pia ni Mismanagement of resources, bse Anatakiwa awe pale kwa maslahi ya taifa (primary Objective) and not otherwise.

  Nyerere miaka fulani hakuwahi kabisa kwenda uko 1st world, kipindi ambacho unaweza fikiri tulihitaji misaada zaidi. ( alikataa mialiko mingi sana) akabaki nyumbani kufanya kazi za taifa and not kuuangalia uzuri wa Maria......

  I stop here 4 now.

  Quotes: Gezeti Nipashe.
  Na Joseph Mwendapole
   
 17. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Namshauli raisi kikwete ateue washauli wazuri na awasikilize labda itasaidia!
   
 18. MANI

  MANI Platinum Member

  #18
  Oct 1, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Haingii akilini kujisifu kwenda kuomba msaada hivi kwa nini tusaidiwe na tusifanye wenyewe mbona hapo nyuma kama ulivyosema mkuu mwalimu alikuwa anakaa hapa hapa na tulifanya makubwa sasa hili la kujisifu kuomba kweli lina walakini.
   
 19. 255Texter

  255Texter Senior Member

  #19
  Oct 1, 2010
  Joined: Aug 31, 2007
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa sababu huyu kidampa tunayemuita presidenti hataki kufanya midahalo, ingefaa sana kama Dr. Slaa angepita kila sehemu anayopita huyu kikwete na kutoa ufafanuzi na maelezo mbadala ili kuwaweka watu sawa. Na haswa kuhusu hili swala la safari za nje, Dr. Slaa aeleze gharama kubwa ambayo serikali inaingia katika hiyo misafara kulinganisha na tija inayopatikana. Na pia, endapo tutawabana wawekezaji katika migodi na sekta nyinginezo na kutowapa misamaha ya kodi, serikali ingekuwa na fedha za kulipia hivyo vyandarua na kununulia chakula watu wenye njaa. Nia akili tu za kuzaliwa ambazo huyu mkwere amekosa.
   
 20. STREET SMART

  STREET SMART JF-Expert Member

  #20
  Oct 1, 2010
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 667
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  Mi nadhani hawa watu na timu yao hawako commited kuliinua taifa hili, labda zaidi ni maslahi binafsi na ya chama tu.
   
Loading...