Kikwete, benno, shigela, zitto, halima mdee, lissu, mimi hatujalipa mikopo yetu udsm?

kanda ya kaskazini bodi ya mikopo ilitoa tenda kwa kampuni moja ya udalali in ayomilikiwa na aliyekuwa kamanda wa ufisadi kwenye bunge lililopita , Aloyce Kimaro ambao waliniletea barua ofisini kwangu lakini haikuwa na mantiki kwani ilinitaka kuorodhesha majina ya wafanyakazi waliokop:roll:eshwa na bodi ya mikopo ili waweze kuwadai
ilishindikana kwa kuwa wakati wa kuajiri mfanyakazi hakuna kipengele kinachohoji chuo kikuu ulikopeshwa na bodi hivyo kwa kweli kila niliyemuonyesha barua aliishia kucheka na kudai alisomeshwa na wazazi wake
hivyo sijui kwa makampuni mengine kama walifanikiwa lakini kwa inavyoelekea kufanikiwa kwa style hiyo si rahisi
 
I can forgive all, lakini sio
The Gaffer, The Main Man, The President....,
Hili halina mjadala sijui ni excuse gani anaweza akaja nayo
 
mimi walipaswa kunidai laki nne na thelathini. Nilipoenda kuzilipa hawakuona kumbukumbu zangu, wakanambia nilipe tu watarekebisha wakiziona. Nikawakatalia, nikaamua kuondoka bila kulipa kwani hawakuonesha umakini. Hata hivyo nasubiri invoice toka kwao wakinitumia ndo ntalipa
 
kanda ya kaskazini bodi ya mikopo ilitoa tenda kwa kampuni moja ya udalali in ayomilikiwa na aliyekuwa kamanda wa ufisadi kwenye bunge lililopita , Aloyce Kimaro ambao waliniletea barua ofisini kwangu lakini haikuwa na mantiki kwani ilinitaka kuorodhesha majina ya wafanyakazi waliokop:roll:eshwa na bodi ya mikopo ili waweze kuwadai
ilishindikana kwa kuwa wakati wa kuajiri mfanyakazi hakuna kipengele kinachohoji chuo kikuu ulikopeshwa na bodi hivyo kwa kweli kila niliyemuonyesha barua aliishia kucheka na kudai alisomeshwa na wazazi wake
hivyo sijui kwa makampuni mengine kama walifanikiwa lakini kwa inavyoelekea kufanikiwa kwa style hiyo si rahisi

Superfisadi, ahsante kwa taarifa hii. At least tuna pakuanzia! We must take action at least to show we care mimi nitajitolea kutafuta ukweli, ngoja bodi wanikatalie ndio tutajua tatizo liko wapi

S
 
mimi walipaswa kunidai laki nne na thelathini. Nilipoenda kuzilipa hawakuona kumbukumbu zangu, wakanambia nilipe tu watarekebisha wakiziona. Nikawakatalia, nikaamua kuondoka bila kulipa kwani hawakuonesha umakini. Hata hivyo nasubiri invoice toka kwao wakinitumia ndo ntalipa

Sasa hebu jamani angalieni haya mambo? Hii nchi inaendeshwa kienyeji. Kuna mwanafunzi St. Augustine amefukuzwa ada sh laki 7, huku kuna mtanzania yuko tayari kulipa mkopo wafanyakazi wa bodi hawana kumbukumbu!
 
Nakuunga mkono mkuu ni dhambi kwa yanayotokea na kuna sababu ya kila mmoja wetu kulipa deni tulilokopeshwa na bodi . Hii pesa inatakiwa iwe ya kuzunguka (revolving fund) sasa hivi inakuwa kama mzunguko huo umesimama mahali flani ni wazo zuri kuamsha watu ili huo mzunguko uendelee.

Kuhusu deni la serikali kuongezeka siiti hilo ni tatizo bali ni kashfa kubwa kwenye uhuru wetu wa mwaka 61.kumbe bado hatujapata uhuru kamili bado tunaitajika kupiga magoti au kuchoka kutangatanga dunia nzima kuomba msaada.Na tukipata msaada tunapiga makofi badili ya kusikitisha.

Wakati wa mkakati huu nawashauri wote tulioko jamvini tuache tabia ya uoga.Wengi hapa wanajiita mdudu,sijui mwingine atajiita fasaha n.k kana kwamba hapa Tanzania sio nyumbani kwake anadhani amepanga.Tutumie majina yetu asili ili swala kama hili au tukijikusanya watu kadhaa tukadhamiria kuanza kulipa kwa vitendo litaamsha dhamira ya wengi.litajenga ujasiri na wizara na bodi tutaprove kwamba hawajajishuhulisha vya kutosha kukusanya madeni.
 
Tusiandike vitu bila ya kufanya Research, kipindi alichosoma Rais JK walikuwa hawapewi mikopo bali ilikuwa ni grants;kwa hiyo, hawakutakiwa kulipa. JK anaweza kufanya hivyo kama courtesy tuu but he is not mandated by law to do so. Mimi nadhani hii hoja ni nzuri sana kama hii bodi inataka kuendelea kuwepo, wale waliopata mikopo wanatakiwa kulipa. Tukiendelea kutoa fedha bila ya watu kulipa madeni basi hiki kitu hakitakuwa sustainable, lakini kama tunataka watoto na wajukuu wetu wafaidi matunda ya kupata elimu ni lazima tulipe.

Mimi napendekeza Serikali ipitishe sheria kali itakayolazimisha waajiri wawakate wale wote waliochukua hii mikopo juu kwa juu mishahara yao kama wanavyokatwa katika malipo ya NSSF.

Pia kama kuna mtu ana contact ya hii bodi ningependa nizipate ili nami nianze kulipa nilipie langu la UDSM. Ingawaje niko nje ya nchi, naona ni wajibu wangu kurudisha fadhila kwa watu walionikopesha. It's about time to start practising what we have been preaching.
Mimi sikubaliani mambo mengi tu na Kikwete, lakini katika hili la kukopa siliafiki kwani enzi alizosoma yeye kina Seif, Lipumba na wengineo wakati wa urais wa Nyerere hakukuwa na utaratibu wa mikopo bali grants. Kwa hiyo Kikwete hahusiki kulipa mkopo wowote ila mtoto wake Ridhwani anadaiwa na bado hajalipa hata senti. Naamini hali ni hiyo kwa watoto wa vigogo wote.
Laiti kama Bodi ya mikopo ingepewa nguvu za kisheriaa kuwabana waliokopeshwa kurejesha mikopo, leokusingekuwa na lawama na mivutanoyote hii. Hebu great thinkers tujiulize hapa wa kulaumiwa ni nani?
 
mimi mwenyewe nimekopa lakini silipi....kwani nimemaliza University halafu kazi sikupata.... nimetafuta msingi wangu kwa jasho langu mwenyewe.... nikaanza biashara na nimeshakua mjasiriamali sasa....... bila kutumia hata taaluma...huo mkopo haujanisaidia kitu...... nasema silipi n'goooo

Kwa mitazamo hii Tanzania kamwe hatutaendelea. Kwani ulipokopa uliahidiwa ajira??? Ulitaka huo msingi utafutiwe na na jasho la nani??? jirani yako??? Unasema mkopo haujakusaidia kitu na shule umemaliza??? Kama umemaliza shule na hujaelimika hiyo ni shauri yako na upeo wako. Sisi tunataka ulipe. Ni kodi zetu hizo tunazokatwa kwa jasho letu!
 
Mheshimiwa JK,

Nakusalim!

Hii ni taarifa ambayo nategemea utaifanyia kazi haraka iwezekanavyo!

Nategemea utachukua hatua. Sitaki kuwa mnafiki na nafsi yangu imenisukuma kuwa mkweli. Nakulaumu kwa mengi lakini mengine mimi binafsi nimeyachangia. Wapo wengi humu jamvini wamechangia!

Usipochukua hatua utathibitishia wananchi kwamba wewe huna maamuzi, ni muoga na huwajali wananchi masikini. Utaonyesha wazi kwamba taabu na shida za wanavyuo hazikukoseshi usingizi!

Majina ya hawa wafuatao hawajarudisha mikopo yao na uwezo wa kurudisha wanao!! Kama wangerudisha UVCCM wasingepiga kelele kwamba bodi ya mikopo ivunjwe badala yake wangesimamia tuliokopa turudishe.

1. Mh. Jakaya Mrisho Kikwete - Raisi

2. Mh. Zitto Kabwe - Mbunge

3. Mh. Halima Mdee - Mbunge

4. Mh. Benno Malisa - Kaimu M/Kiti UVCCM

5. Mh. Martin Shigela - Katibu UVCCM

6. Mh. Ridhiwani Kikwete - Mjumbe UVCCM

7. Mh. Cyril Chami - Waziri

8. Mh. Mhonga Ruhanya - Mbunge

9. Wah. WanaJF wengi tu - Wanaharakati.

10. Mh. Francis Kiwanga - Mkurugenzi LHRC

11. Mh. Mwigulu Nchemba - Mbunge.

12. Wah. Mawakili wote waliosajiliwa Tanzania.(Waliopewa mikopo)

13. Wah. Madaktari wote Tanzania (waliopewa mikopo)

14. Wah. Mahakimu wote waliopewa mikopo.

15. Wah. Majaji wote waliopewa mikopo

16. Wah. Watendaji wote wa serikali waliopewa mikopo

Mheshimiwa Jakaya Kikwete, mimi na wewe na watanzania wengine lazima tuwaambie wanavyuo ukweli! Tulikopa hatujarudisha! Hao UVCCM wote hakuna hata mmoja aliyerejesha mkopo wake!!

Bodi inatoa wapi hela za kukopesha sasa hivi? Au ndio nchi na yenyewe inaenda kukopa??

Fedha ambazo tungerudisha mikopo tunajengea nyumba za kifahari, magari mazuri na kuendea safari dubai etc!

Kwa watakaochukia wachukie, ila niliowataja wote wanaweza kulipa hata kesho! Haiwezekani wote tusingizie kukosa ajira!! Niliowataja wote wana ajira na wanaweza kulipa. Wale ambao hawajapata ajira basi itamkwe kwamba wamesamehewa au watalipa pindi wakipata ajira!!

Kama wanaharakati wameenda mahakamani Dowans isilipwe na mimi nitaenda mahakamani hela za wananchi zilizokusomesha wewe na wengine zirudi ili wengine wazitumie!

Kama mwanaJF tutaungana wote humu jamvini kufungua kesi mikopo irudishwe kwa wale wenye kazi na biashara zinazojulikana!

Huo ni uamuzi mgumu, uchukue na uikoe elimu ya juu na taifa kwa ujumla!

Usafi na uadilifu uwe wa vitendo!! Sio unafiki!

Ktk hiyo orodha muongeze na Hizza Tambwe...
 
Hiyo list ina kila aina ya watu lakini mimi nimeamua kuwaangalia wanasiasa hasa waupinzani kwa sababu hao ndio role models wetu kwa sasa.

Iwapo wao wataonyesha vitendo vya kujali taifa, wapo katika nafasi nzuri sana ya kushamirisha na wengine.

Hii dhana ya kudharau mikataba wanayoifanya serikali sasa kumbe tunawakosoa bure kama hao wakosoaji wakuu bungeni nao walidharau mikataba waliyoingia.

Ni aibu kwa wahubiri wakubwa Wa mabadiliko wa upinzani kuwemo kwenye list kama hiyo awe anatoka CDM, CUF, TLP. Awe Zitto, Mtariro au Kafulila.

Gaijin,

Hii hoja sio ya kuijadili kwa itikadi za kisiasa,
kinachotakiwa hapa ni kwa wanufaika wote wa mikopo walipe ili wadogo zetu waweze kukopeshwa.

Hiyo list ukiisoma unaona wapo watu mchanganyiko hata wasio wanasiasa, ametaja wanasiasa na watumishi wengine wa umma na hata wafanya biashara ama wenye shughuli zingine.

tuweke pembeni siasa zetu za ccm vs cuf, ccm vs cdm na cuf vs cdm ili tuweze kuwa focused.
 
Wao (kikwete na wenzie) walijitoa katika kulipa mikopo ya bodi ya Bodi.

Sheria inasema watakao guswa na sheria hii ya mikopo kwa ajili ya kusoma ni kuanzia mwaka 1994.

Waliomaliza chuo kabla ya hapo sheria hii haiwagusi...! Someni hio sheria ili mfumbuke macho...!
 
Tatizo tulilonalo hapo kwetu ni namna ya kuweka sheria/ taratibu na kuzifuata!!!! Hilo ni tatizo linalohitajiwa ufumbuzi wa haraka. Mapendekezo yangu ni kama ifuatavyo.

1. Kwanza kabisa iundwe bodi ya madeni (This is very common in the developed world). In such a way ukikopa jina lako na details zako na kiasi cha mkopo kinakuwa registered huko. Hawa kazi yao ni kutunza taarifa za wadeni as such mfano unapotaka kukopa benki, benki wanafuatilia huko kwenye hiyo boadi na ikigundulika wewe ni mdaiwa sugu basi hawakupi mkopo. The same ukitaka say kuchukua mortgage, kupanga nyumba etc.

2. Mkopaji anatakiwa apewe muda say two years after graduation, awe tayari ameshaanza kulilipa hilo deni regardless ameajiriwa au la. Kwa sababu kusoma ni kuelimika na ukishaelimika si lazima uajiriwe ili uwe na kipato. Otherwise hata maana ya kuelimika inapotea.

3. Kuwe na incentive kwa wanaojipeleka wenyewe kulipa madeni ya zamani.

4. Kutengenezwe database ya waliokopeshwa woote na waajiri wawe na access na hiyo DB ili kujua status ya waajiriwa wao! - If these guys are serious this can be done in a month.

5. Bodi ya mikopo ivunjwe na shughuli za ukopeshaji zihamishiwe benki (Interest zidhibitiwe - na ziwe special)
 
hapo kwenye red..umenena ... yaani grace period
 
Mheshimiwa JK,

Nakusalim!

Hii ni taarifa ambayo nategemea utaifanyia kazi haraka iwezekanavyo!

Nategemea utachukua hatua. Sitaki kuwa mnafiki na nafsi yangu imenisukuma kuwa mkweli. Nakulaumu kwa mengi lakini mengine mimi binafsi nimeyachangia. Wapo wengi humu jamvini wamechangia!

Usipochukua hatua utathibitishia wananchi kwamba wewe huna maamuzi, ni muoga na huwajali wananchi masikini. Utaonyesha wazi kwamba taabu na shida za wanavyuo hazikukoseshi usingizi!

Majina ya hawa wafuatao hawajarudisha mikopo yao na uwezo wa kurudisha wanao!! Kama wangerudisha UVCCM wasingepiga kelele kwamba bodi ya mikopo ivunjwe badala yake wangesimamia tuliokopa turudishe.

1. Mh. Jakaya Mrisho Kikwete - Raisi

2. Mh. Zitto Kabwe - Mbunge

3. Mh. Halima Mdee - Mbunge

4. Mh. Benno Malisa - Kaimu M/Kiti UVCCM

5. Mh. Martin Shigela - Katibu UVCCM

6. Mh. Ridhiwani Kikwete - Mjumbe UVCCM

7. Mh. Cyril Chami - Waziri

8. Mh. Mhonga Ruhanya - Mbunge

9. Wah. WanaJF wengi tu - Wanaharakati.

10. Mh. Francis Kiwanga - Mkurugenzi LHRC

11. Mh. Mwigulu Nchemba - Mbunge.

12. Wah. Mawakili wote waliosajiliwa Tanzania.(Waliopewa mikopo)

13. Wah. Madaktari wote Tanzania (waliopewa mikopo)

14. Wah. Mahakimu wote waliopewa mikopo.

15. Wah. Majaji wote waliopewa mikopo

16. Wah. Watendaji wote wa serikali waliopewa mikopo

Mheshimiwa Jakaya Kikwete, mimi na wewe na watanzania wengine lazima tuwaambie wanavyuo ukweli! Tulikopa hatujarudisha! Hao UVCCM wote hakuna hata mmoja aliyerejesha mkopo wake!!

Bodi inatoa wapi hela za kukopesha sasa hivi? Au ndio nchi na yenyewe inaenda kukopa??

Fedha ambazo tungerudisha mikopo tunajengea nyumba za kifahari, magari mazuri na kuendea safari dubai etc!

Kwa watakaochukia wachukie, ila niliowataja wote wanaweza kulipa hata kesho! Haiwezekani wote tusingizie kukosa ajira!! Niliowataja wote wana ajira na wanaweza kulipa. Wale ambao hawajapata ajira basi itamkwe kwamba wamesamehewa au watalipa pindi wakipata ajira!!

Kama wanaharakati wameenda mahakamani Dowans isilipwe na mimi nitaenda mahakamani hela za wananchi zilizokusomesha wewe na wengine zirudi ili wengine wazitumie!

Kama mwanaJF tutaungana wote humu jamvini kufungua kesi mikopo irudishwe kwa wale wenye kazi na biashara zinazojulikana!

Huo ni uamuzi mgumu, uchukue na uikoe elimu ya juu na taifa kwa ujumla!

Usafi na uadilifu uwe wa vitendo!! Sio unafiki!

Mmmh! huu msumari kaka umepiga katikati ya kichwa, watu huwa wanajifanya wana uchungu sana

na nchi humu JF, sasa tuone watakaojitokeza kulipa. Huwa ni rahisi sana kusema Lowassa na

Rostam mafisadi bila kuangalia kuwa hata sisi wenyewe tunaweza kuwa mafisadi kwa namna moja

au nyingine (kulingana na tafsiri pana ya ufisadi aliyoitoa Dr. Slaa). Nchi watu wengi mafisadi na

wengi wanalalamika mara nyingi ni kwakuwa wao hawakupata fursa (opportunity) ya kufisadi.

Haya basi wana JF, kama sisi tunachukia ufisadi tuanze na hili la kulipa mikopo yetu, tuishinikize bodi

ikusanye madeni na sisi tuwe wa kwanza kulipa. Kama vile tunavyoshinikiza Dowans isilipwe basi na

hili pia tulishikie bango.
 
Kikwete hakupata mkopo, alisoma Bureeeeeeeeeee pamoja na wengine wote waliomaliza tangu 1994 kurudi nyuma!...unampandisha hadhi!
 
Sasa huyu Mkuu aliyetuletea hii habari kumbe ametu-misslead :angry:, hebu afanyie masahihisho post yake...

VOC, nimerekebisha kwa kutoa wazo/ushauri kwa JK na wengine wote ambao sheria haiwalazimishi kurudisha! Natumaini watakuwa wazalendo!
 
Back
Top Bottom