Kikwete, benno, shigela, zitto, halima mdee, lissu, mimi hatujalipa mikopo yetu udsm? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete, benno, shigela, zitto, halima mdee, lissu, mimi hatujalipa mikopo yetu udsm?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Feb 5, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa JK,

  Nakusalim!

  Hii ni taarifa ambayo nategemea utaifanyia kazi haraka iwezekanavyo!

  Nategemea utachukua hatua. Sitaki kuwa mnafiki na nafsi yangu imenisukuma kuwa mkweli. Nakulaumu kwa mengi lakini mengine mimi binafsi nimeyachangia. Wapo wengi humu jamvini wamechangia!

  Usipochukua hatua utathibitishia wananchi kwamba wewe huna maamuzi, ni muoga na huwajali wananchi masikini. Utaonyesha wazi kwamba taabu na shida za wanavyuo hazikukoseshi usingizi!

  Majina ya hawa wafuatao hawajarudisha mikopo yao na uwezo wa kurudisha wanao!! Kama wangerudisha UVCCM wasingepiga kelele kwamba bodi ya mikopo ivunjwe badala yake wangesimamia tuliokopa turudishe.

  1. Mh. Jakaya Mrisho Kikwete - Raisi (sheria haikulazimishi kulipa ila kumbuka ulisomeshwa bure na hali ya maisha haikuwa ngumu kama sasa. Kuna watoto wa masikini wengi hawana uwezo wa kusomeshwa hata kwa kuchangia kidogo sio bure kama wewe. Kama kiongozi kuwa mfano uchangie au urudishe kile ulichosaidiwa ukasoma ili na wengine wasome. Hii itatoa changamoto kwa waliosoma bure na wasiolazimishwa na sheria warudishe hizo 'grants' mlizofaidika nazo! Huo ni uzalendo).

  2. Mh. Zitto Kabwe - Mbunge

  3. Mh. Halima Mdee - Mbunge

  4. Mh. Benno Malisa - Kaimu M/Kiti UVCCM

  5. Mh. Martin Shigela - Katibu UVCCM

  6. Mh. Ridhiwani Kikwete - Mjumbe UVCCM

  7. Mh. Cyril Chami - Waziri (fuata ushauri/mawazo yangu kwa Mh. Raisi wako).

  8. Mh. Mhonga Ruhanya - Mbunge

  9. Wah. WanaJF wengi tu - Wanaharakati.

  10. Mh. Francis Kiwanga - Mkurugenzi LHRC

  11. Mh. Mwigulu Nchemba - Mbunge.

  12. Wah. Mawakili wote waliosajiliwa Tanzania.(Waliopewa mikopo)

  13. Wah. Madaktari wote Tanzania (waliopewa mikopo)

  14. Wah. Mahakimu wote waliopewa mikopo.

  15. Wah. Majaji wote waliopewa mikopo

  16. Wah. Watendaji wote wa serikali waliopewa mikopo

  Mheshimiwa Jakaya Kikwete, mimi na wewe na watanzania wengine lazima tuwaambie wanavyuo ukweli! Tulikopa hatujarudisha! Hao UVCCM wote hakuna hata mmoja aliyerejesha mkopo wake!!

  Bodi inatoa wapi hela za kukopesha sasa hivi? Au ndio nchi na yenyewe inaenda kukopa??

  Fedha ambazo tungerudisha mikopo tunajengea nyumba za kifahari, magari mazuri na kuendea safari dubai etc!

  Kwa watakaochukia wachukie, ila niliowataja wote wanaweza kulipa hata kesho! Haiwezekani wote tusingizie kukosa ajira!! Niliowataja wote wana ajira na wanaweza kulipa. Wale ambao hawajapata ajira basi itamkwe kwamba wamesamehewa au watalipa pindi wakipata ajira!!

  Kama wanaharakati wameenda mahakamani Dowans isilipwe na mimi nitaenda mahakamani hela za wananchi zilizokusomesha wewe na wengine zirudi ili wengine wazitumie!

  Kama mwanaJF tutaungana wote humu jamvini kufungua kesi mikopo irudishwe kwa wale wenye kazi na biashara zinazojulikana!

  Huo ni uamuzi mgumu, uchukue na uikoe elimu ya juu na taifa kwa ujumla!

  Usafi na uadilifu uwe wa vitendo!! Sio unafiki!
   
 2. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Bodi ya mikopo ndio wazembe,at this time wanadai over 58 Billions,majina ya wanaodaiwa wanayo,lakini ni wapuuzi hao bodi kwani awapo makini ktk ukusanyaji wa madeni hayo.
  hazina aikutakiwa kupewa lawama na bodi ,iwapo bodi ingekuwa makini kenye kukusanya madeni.Kwani hela ingekuwa inazunguka,wanakusanya wanakopesha wanakusanya....Sasa wao wanachota hazina hela kila mwaka,lakini awakusanyi madeni kisawasawa.
  So ni kweli bodi hivyunjwe.
  JK atakiwa kutupiwa lawama.
   
 3. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Chipukizi, mchango mzuri! Lazima Bodi iwajibike. Lakini unadhani tatizo ni bodi au viongozi wa bodi? Wakuchukuliwa hatua ni nani?
   
 4. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mkuu kwani tatizo ni bodi kukosa fedha?au ni mchakato mzima wa utoaji mkopo.mafedha yapo mengi ambayo yangeweza kuwasomesha bure wanafunzi wanaopata div one mpaka div 3.
   
 5. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Tatizo ni Viongozi wa bodi,so inabidi wawajibishwe.
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Majembe Auction Mart ..... anza kazi yako...... kamata wote waliokopa unsecured loans,mkishapata pesa hizo nitawapa A/C no. ya AKIBA Commercial Bank zitumbukize humo halafu mtanipa copy ya diposit slips


  mimi mwenyewe nimekopa lakini silipi....kwani nimemaliza University halafu kazi sikupata.... nimetafuta msingi wangu kwa jasho langu mwenyewe.... nikaanza biashara na nimeshakua mjasiriamali sasa....... bila kutumia hata taaluma...huo mkopo haujanisaidia kitu...... nasema silipi n'goooo
   
 7. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,030
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  hapo namba 16. kwa watendaji wote si kweli watu tunakatwa vimishahara vyetu vya laki 2 kila mwezi
   
 8. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hapo patamu, najaribu kuvuta kumbukumbu zinaonyesha hata mimi ninadaiwa:clap2:
   
 9. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  JB, serikali yetu ina tatizo katika ukusanyaji mapato, matumizi na kulinda rasilimali za taifa!

  Mgomo wa walimu arusha ulisababishwa na serikali kuchelewa kulipa fedha zao badala yake wakaielekeza halmashauri ya manispaa iikopeshe! Unaweza kuona tatizo!

  Lakini, kama fedha zipo kwa nini tunakopa? Kwa nini deni la taifa limeongezeka?
   
 10. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Kweli wangekuwa mfano wa kurudisha hizo hela hata nchi nyingine kama marekani ni utaratibu kukopeshwa na kurudishwa....tatizo hakuna utaratibu wa kurudisha hizo hela na uwepo wa bodi mbovu yenye uongozi mbovu wa serikali mbovu na inayoleta siasa kwenye kila kitu inaongeza tatizo juu ya tatizo.......serikali iwajibike,imetosha jamani,maisha ya wanafunzi ni magumu mno kutokana na kukosekana kwa utaratibu mzuri......:A S 20::A S 20:
   
 11. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ezan, tulipe haraka tuwe huru! Nashukuru umejitokeza na kukubali unadaiwa! Dawa ya deni ni kulipa!
   
 12. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mfarisayo, iweje wanakata kamshahara ka laki 2 halafu wale wenye mishahara na kipato kikubwa hawalipi? Mheshimiwa JK na viongozi wengine wote waje mbele ya wananchi na risiti zao za malipo!
   
 13. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hapo ndipo kiongozi wa nchi na waziri wake wanaonyesha uwezo wao! Naamini tukianzisha hii movement watachukua hatua!
   
 14. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #14
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh kumbe kuna wengine hawalipi wakati na mishahara yetu midogo bado tunakatwa kila mwezi. Bongo noma kweli.

  Serikali mbovu mbovu inafanya kitu kitu kibovu bovu.
   
 15. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2011
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Tusiandike vitu bila ya kufanya Research, kipindi alichosoma Rais JK walikuwa hawapewi mikopo bali ilikuwa ni grants;kwa hiyo, hawakutakiwa kulipa. JK anaweza kufanya hivyo kama courtesy tuu but he is not mandated by law to do so. Mimi nadhani hii hoja ni nzuri sana kama hii bodi inataka kuendelea kuwepo, wale waliopata mikopo wanatakiwa kulipa. Tukiendelea kutoa fedha bila ya watu kulipa madeni basi hiki kitu hakitakuwa sustainable, lakini kama tunataka watoto na wajukuu wetu wafaidi matunda ya kupata elimu ni lazima tulipe.

  Mimi napendekeza Serikali ipitishe sheria kali itakayolazimisha waajiri wawakate wale wote waliochukua hii mikopo juu kwa juu mishahara yao kama wanavyokatwa katika malipo ya NSSF.

  Pia kama kuna mtu ana contact ya hii bodi ningependa nizipate ili nami nianze kulipa nilipie langu la UDSM. Ingawaje niko nje ya nchi, naona ni wajibu wangu kurudisha fadhila kwa watu walionikopesha. It's about time to start practising what we have been preaching.
   
 16. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #16
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naamini kwamba ukibrowse utapata anuani ya bodi ya mikopo!

  Nashukuru kwa angalizo lako kuhusu grants vs loan! Natumaini kwamba JK atatumia busara pia kurudisha alichopewa kama grants ili na watoto wetu wafaidike pia!
   
 17. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #17
  Feb 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Usinambie wabunge hao wa upinzani wenye kujali sana maslahi ya taifa hawajalipa madeni yao.
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Feb 5, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145

  Gaijin,

  Hii hoja sio ya kuijadili kwa itikadi za kisiasa,
  kinachotakiwa hapa ni kwa wanufaika wote wa mikopo walipe ili wadogo zetu waweze kukopeshwa.

  Hiyo list ukiisoma unaona wapo watu mchanganyiko hata wasio wanasiasa, ametaja wanasiasa na watumishi wengine wa umma na hata wafanya biashara ama wenye shughuli zingine.

  tuweke pembeni siasa zetu za ccm vs cuf, ccm vs cdm na cuf vs cdm ili tuweze kuwa focused.
   
 19. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #19
  Feb 5, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,639
  Likes Received: 1,428
  Trophy Points: 280
  tatizo sio kulipa.. tatizo ni watavyozitumia hela zangu baada ya kulipa

  bora nikanywe bia kuliko kulipa then wanaenda kumlipa Rost tamu na kamuni zake
   
 20. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #20
  Feb 5, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Alberto,
  Kabla ya kuanza kukusanya hii mikopo ili watu wale wa bodi ya mikopo wakaitafune, ni lazima bodi ifanyiwe mabadiliko ya haraka. Kwa bahati mbaya kitu cha kutekeleza muda mfupi, tunafanya ni project ya muda mrefu...bodi ya mikopo inashahili kuvunjwa haraka iwezekanavyo ili mambo yaende sawasawa na wawekwe watu wenye uwezo wa kuifanya kazi ili kwa mafanikio.
   
Loading...