Kikwete bado apeta kwa umaarufu kuzidi wanasiasa wengine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete bado apeta kwa umaarufu kuzidi wanasiasa wengine

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kachero, Aug 11, 2009.

 1. K

  Kachero JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kuangalia umaarufu wa viongozi wa kisiasa, utafiti huo uliofanywa nchi nzima ukiwashirikisha watu 2,000, unaonyesha kuwa Rais Jakaya Kikwete anaongoza kwa asilimia 66 akifuatiwa kwa mbali na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ambaye amepata asilimia 11.

  Mwenyekiti huyo wa Chadema amempiku kwa umaarufu mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba, ambaye katika Uchaguzi Mkuu uliopita alishika nafasi ya pili.

  Prof Lipumba, ambaye atakuwa akigombea urais kwa mara ya tatu iwapo atapitishwa na chama chake, ameshika nafasi ya tatu kwa umaarufu akiwa amepata asilimia tisa, huku mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema akiambulia asilimia moja sawa na mwenyekiti wa UDP, John Cheyo.

  Utafiti huo umebaini kuwa kiwango cha demokrasia nchini kimeongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na Watanzania kujua majimbo yao ya uchaguzi na wawakilishi wao bungeni, huku CCM ikiongoza vyama vingine kwa kufahamika zaidi kwa wananchi.

  “Asilimia 67 wanaifahamu na kuipenda CCM kutokana na sera, uongozi wake na imani kwamba ni chama cha kidemokrasia,” alisema Orio na kutaja vyama vinavyoifuatia CCM kuwa ni Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na TLP.

  Utafiti huo uliofanywa kupata maoni ya watu kuhusu masuala ya jamii, siasa na uchumi, umebaini kuwa rushwa nchini imeongezeka na kwamba maofisa wa Jeshi la Polisi na Idara ya Mahakama, ndio wanaoongoza kwa kuomba na kupokea rushwa.

  “Taasisi za dini, vyombo vya habari, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na Bunge, ndiyo yanayofuatia kwa utaratibu huu,” alisema Orio.


  Source: Mwananchi newspaper.
   
 2. K

  Kachero JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kweli mwendo wenyewe wa uelewa wa wananchi wa Tanzania ndio huu basi kazi kubwa inahitajika ili kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini Tanzania.Mbali na makashfa yote na mambo yote ya ufisadi JK na CCM wana nafasi kubwa ya kushinda kwenye uchaguzu ujao.

  Nini maoni yako.
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  JK anafanya kazi ingawa sio kwa VIGEZO na VIWANGO vya baadhi ya members humu JF ambao siku zote natamani wangeteuliwa au kuchaguliwa kwenye nafasi yoyote ile ya kitaifa ili tuone wao wangefanyaje kazi hizi.
   
 4. K

  Kachero JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KATIBU Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, anapewa nafasi kubwa ya kushinda kiti cha urais visiwani Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani, kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa kampuni ya Synovate.


  Synovate, ambayo zamani ilikuwa ikijulikana kama Steadman Group Tanzania, imesema katika matokeo ya utafiti huo uliofanyika miezi mitatu iliyopita kwa kuwahoji wananchi wa Zanzibar pekee kuhusu urais wa visiwa hivyo, mtu anayeweza kumfuatia Maalim Seif ni aliyewahi kuwa Waziri Kiongozi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Gharib Mohammed Bilal.


  "Watu wanaotarajiwa kumrithi Rais Karume baada ya kustaafu mwaka 2010 ni Maalim Seif anayepewa asilimia 28 na Gharib Mohammed Bilal asilimia 24," alisema meneja msaidizi wa kampuni hiyo, Aggrey Orio.


  Utafiti huo pia umeonyesha kwamba, Waziri Kiongozi wa sasa, Shamsi Vuai Nahodha, amepata asilimia 10 wakati anayeshika nafasi ya nne ni Makamu wa Rais, Dk Mohamed Shein, aliyepata asilimia 2.


  Maalim Seif, ambaye alikuwa waziri kiongozi kabla ya kupata misukosuko iliyomfanya awekwe kizuizini, amekuwa akigombea urais wa visiwa hivyo tangu mwaka 1995 wakati uchaguzi wa vyama vingi uliporejeshwa, lakini amekuwa akishindwa kwa asilimia chache.


  Tofauti hizo ndogo za ushindi ambao umekuwa ukienda kwa mgombea wa CCM, zimekuwa zikisababisha CUF kukataa matokeo na wakati mwingine kusababisha vurugu kama za mwaka 2001 zilizosababisha watu zaidi ya 26 kupoteza maisha.


  Bilal amekuwa akipanda chati katika siasa za Zanzibar na mwaka 2005 alichukua fomu kupambana na rais wa sasa wa Zanzibar, Amani Abeid Karume lakini jina lake likaondolewa kwenye vikao vya juu vya CCM, ambayo ina utamaduni wa kumwachia mshindi wa kiti cha urais kutetea kipindi kingine cha miaka mitano.


  Nahodha na Dk Shein hawatajwi sana kwenye kinyang'anyiro cha urais wa visiwa hivyo ambao huwa na upinzani mkali baina ya CCM na CUF.


  Hata hivyo, katika utafiti huo idadi kubwa ya watu walioulizwa swali kuhusu mtu maarufu baada ya kustaafu kwa Rais Karume, hawakuwa na jibu.


  Utafiti huo wa Synovate unaonyesha kuwa, asilimia 24 ya watu waliohojiwa, hawakuwa na jibu katika swali hilo.


  Kwa kuangalia umaarufu wa viongozi wa kisiasa, utafiti huo uliofanywa nchi nzima ukiwashirikisha watu 2,000, unaonyesha kuwa Rais Jakaya Kikwete anaongoza kwa asilimia 66 akifuatiwa kwa mbali na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ambaye amepata asilimia 11.


  Mwenyekiti huyo wa Chadema amempiku kwa umaarufu mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba, ambaye katika Uchaguzi Mkuu uliopita alishika nafasi ya pili.

  Prof Lipumba, ambaye atakuwa akigombea urais kwa mara ya tatu iwapo atapitishwa na chama chake, ameshika nafasi ya tatu kwa umaarufu akiwa amepata asilimia tisa, huku mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema akiambulia asilimia moja sawa na mwenyekiti wa UDP, John Cheyo.


  Utafiti huo umebaini kuwa kiwango cha demokrasia nchini kimeongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na Watanzania kujua majimbo yao ya uchaguzi na wawakilishi wao bungeni, huku CCM ikiongoza vyama vingine kwa kufahamika zaidi kwa wananchi.


  "Asilimia 67 wanaifahamu na kuipenda CCM kutokana na sera, uongozi wake na imani kwamba ni chama cha kidemokrasia," alisema Orio na kutaja vyama vinavyoifuatia CCM kuwa ni Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na TLP.


  Utafiti huo uliofanywa kupata maoni ya watu kuhusu masuala ya jamii, siasa na uchumi, umebaini kuwa rushwa nchini imeongezeka na kwamba maofisa wa Jeshi la Polisi na Idara ya Mahakama, ndio wanaoongoza kwa kuomba na kupokea rushwa.

  "Taasisi za dini, vyombo vya habari, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na Bunge, ndiyo yanayofuatia kwa utaratibu huu," alisema Orio.


  Alisema katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, takriban mtu mmoja kati ya watu kumi waliopata huduma kwenye taasisi za serikali ambayo ni sawa na theluthi mbili, walihonga na rushwa ilifikia hadi Sh10,000.


  Alisema utafiti umebaini kuwa asilimia 13 ya wananchi walieleza katika utafiti huo kuwa, hawana imani na Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), kutokana na wizi wa mitihani huku asilimia 12 wakisema kuwa hawana imani na taasisi za fedha kutokana na riba kubwa.


  Taasisi nyingine zilizonyoshewa kidole katika utafiti huo ni vyama vya upinzani, Tume ya Uchaguzi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).


  "Watanzania wengi vijijini wanamuunga mkono Rais Kikwete kuliko mjini, lakini hawajaridhika na jinsi ambavyo serikali inashughulikia mambo mbalimbali," alisema.

  Katika kuangalia masuala ya jinsia katika kinyang'anyiro cha urais, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk Asha Rose Migiro ndiye aliyepewa nafasi kubwa ya kuwa rais akifuatiwa na mbunge wa jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, wakati mwanasiasa mkongwe, Getrude Mongella na Waziri Hawa Ghasia wamepewa nafasi ndogo.


  Watu waliulizwa swali kwamba, "kwa kuangalia wanawake na demokrasia, kama Tanzania ingetakiwa kuwa na rais mwanamke, ni nani kati ya viongozi wa kitaifa anaweza kuchaguliwa kuiongoza Tanzania.


  Asilimia 36 ya walioulizwa walimtaja Migiro, wakati asilimia 20 walimtaja Kilango, asilimia 10 walimtaja Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Margareth Sitta. Mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa, Anna Tibaijuka alipewa asilimia 5, akifuatiwa na Sofia Simba, huku Mongella, Salma Kikwete na Ghasia wakiambulia asilimia 2.


  Katika swali hilo, asilimia 19 ya waliohojiwa, hawakuwa na jibu.
  Asilimia 71 ya watu walioulizwa kama wanawake nchini wana uwakilishi mzuri kwenye uongozi wa kitaifa, walikubali wakati asilimia 25 walikataa na asilimia 12 haikuwa na jibu.
   
 5. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hata sijui anapeta kwa lipi Mungu wangu.Hivi anayepeta ni huyu huyu Kikwete ninayemjua au mwingine.Kama mambo yenyewe ni hivyo, basi hatufiki mbali!

   
 6. b

  bnhai JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Jamani mie nadhani watu wangehoji methodology, sampling nk. Ila kuanza na kukataa tafiti sasa inakuwa kituko. Steadman ni wazuri, mie binafsi nawaamini sijui kama walivyobadili jina na siasa zimeingia.
   
 7. K

  Kachero JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninapata shida na timing ya huu utafiti wakati huu ambapo kuna watu lukuki ambao hawaridhiki na utendaji wa Kikwete sa Serikali yake.Inawezekana kabisa haya majibu yanatolewa wakati huu ili kukidhi haja ya kisiasa zaidi.

  Tanzania lolote linawezekana kwa kweli, sasa hata wakiiba kura watasema hata watafiti wamethibitisha kuwa CCM na Kikwete bado wanapendwa na watanzania walio wengi.Huu ni usanii wa kisiasa.
   
 8. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu ni vizuri ukiwa unatoa mifano ya kazi alizofanya JK, kuliko kusema tu kuwa anafanya kazi. Ukiuliza kuhusu Mkapa, pamoja na ufisadi wake wa kujiuzia Kiwira, kusimamia EPA na kukalia kimya Radar,ndege etc....stil kuna mengi tunayoweza kutaja kuhusu kazi aliyofanya Mkapa. Angalia TRA, angalia Mkukuta, mkurabita,MMEM, memkwa na nyingine nyingi, hara barabara ambazo JK ssasa hivi anasuasua kuzijenga yote ni mipango ya awamu ya Mkapa.

  Ni kweli kuna vigezo ambavyo tungependa JK avioneshe wakati wa utawala wake. Lazima aoneshe strong thinking capacity kama aliyoonesha Mkapa, ni lazima awe innovative kama Mkapa, lazima awe na uwezo wa kusimamia sheria za Taifa kama Mkapa, lazima awe na thinking capacity, judgement, reasoning na leadership capability zaidi ya alioyoonesha Mkapa. Tatizo ni kuwa JK hana vyote hivyo ndio maana uongozi wa Chama na Serikali unakuwa kama mzito kwake, na ndio maana nchi inayumba.
  Hakuna la maana ambalo JK leo anaweza kusimama mbele ya watanzania na kusema nimefanya hili nichagueni tena. Huwezi kusema eti kutoa ambulance kwa kijiji ni utendaji mzuri, hizi ni cheap politics huwezi kusema eti nimeteua wanawake wengi kwenye nyadhifa za serikali, hii sio kigezo cha utendaji au efficiency ya mkuu wa nchi. We need prosperity, security and improvement in social welfare.

  Tukiwa na siasa za Kijiweni hatutaenda popote
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huu utafiti una ualakini.
  Mlitegemea watasema umaarufu wa JK umeshuka wawe matatizoni thubutu.
   
 10. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #10
  Aug 11, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Hapa ndipo tunalambishwa spins. Njia nzuri ya kupinga utafiti ni kufanya utafiti mwingine. Hawa hata wakikupa methodology yao bado hutakuwa na hoja za kisayansi za kuwapinga. Tuache kabisa hii mentality ya kulalama na badala yake tufanye vitu.

  Lakini ukweli ni kwamba utafiti huu umeonyesha kuwa mwaka mmoja kabla ya uchaguzi tayari Kikwete ameporomoka sana (alichaguliwa kwa 80%) Kwamba uchaguzi ungeitishwa sku ile waliojaza madodoso angepata 66% tayari ni ushindi kwetu kwa wale tunaotaka mabadiliko ya kisiasa katika nchi. Asilimia 66 ni chini ya 'two third'!

  Huu utafiti ni wa June 9 - 17, kabla ya mjadala wa bajeti kuwa mkali, kabla ya hoja za ujenzi wa mabarabara, kabla ya hoja za Kiwira na Richmond Bungeni (hoja ambazo zimeichanganya serikali sana). Utafiti mwingine ukifanywa leo JK anaweza kufika kati ya 55 na 60%.

  Tatizo kubwa la Tanzania ni kwamba tuna vyombo vichache sana ambavyo vinafanya tafiti. Kama tungekuwa na asasi kama 4 hivi zinafanya tatifi nyakati tofauti tungeweza kulinganisha matokeo yao. Hata vyama vya sasa vyenyewe havifanyi 'internal polls' kujua 'perceptions' za wapiga kura na wana nchi kwa ujumla kuhusu vyama na kuhusu sera za vyama (kama kuna tofauti ya kisera ya vyama). Hii ndio changamoto tuliyonayo badala ya kukaa na kusema, aaah hawa wamenunuliwa hawa! Tutoke huko, tuwapinge kwa njia zao hizo hizo. Twende tukawaulize watu na tupate mawazo yao kwa njia hizo hizo.

  Changamoto kubwa tuliyonayo hivi sana Tanzania ni kuwa na libunge lenye wabunge wengi wa chama kimoja (soma CCM). Asilimia 86 ya wabunge ni wa CCM. Hii maana yake ni kuwa nchi siyo ya mfumo wa vyama vingi, ni ya mfumo wa chama kimoja hodhi (Single Party Dominance). Hata hivyo, wananchi 69% ndio waliwapigia kura wabunge wa CCM katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Tatizo ni nini? Mfumo wetu wa uchaguzi hauonyeshi kiukweli NIA ya mwananchi mpiga kura na matokeo yake wananchi 69% wanapigia kura wabunge wa CCM lakini CCM inapata 86% ya viti Bungeni. Changamoto hii tutaimaliza iwapo tu watu wengi zaidi watajitokeza kugombea Ubunge kupitia vyama vya upinzani. Tukipata wagombea wazuri wenye nafasi nzuri za kushinda na kuinyima CCM two-third majority Bungeni tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana katika ujenzi wa demokrasia nchini.

  Mimi binafsi ninakaribisha kwa mikono miwili matokeo haya ya utafiti wa kampuni hii. Ninawataka waendelee kufanya utafiti zaidi na mara kwa mara na pia kujikita katika nini haswa matakwa ya raia kutoka kwa viongozi wao.

  Iwapo mwaka 2005 JK alipata 80% ya kura lakini wabunge wake wakapata 69% tu, 2010 JK akipata 66% ya kura ni wazi wabunge wa CCM hawatafika 55%................ Hii maana yake ni kuwa vyama vya upinzani vitapata nguvu zaidi ndani ya Bunge na kufanya mabadiliko makubwa.

  Matokeo haya ya utafiti mimi naona yanatupa nguvu ya kufanya kazi zaidi, kuangalia tunapokosea na kuparekebisha na kuunda sera zinazokonga nyoyo za raia ili kuwaondoa kabisa madarakani CCM na mafisadi wao.

  I personally welcome the poll results.
   
 11. K

  Kwayu JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2009
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hayo matokeo huenda yakawa ni ya kupikwa tunapoelekea uchaguzi mkuu mwakani kujaribu kuwaaminisha wadanganyika kuwa Kikwete bado yuko. UKWELI NI KWAMBA AMEFULIA.Mkitaka ukweli nendeni mkawaulize wafanyabiashara kariakoo, waalimu, wastaafu wa E.A.C na wanafunzi vyuo vikuu.
   
 12. K

  Kachero JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sawa Mkuu nakubaliana na mawazo yako lakini tukumbuke kuwa nguvu kubwa ya CCM inapatikana vijijini ambako CCM inaaminika zaidi ya vyama vya upinzani.Hata utafiti tunaouzungumzia sasa unaonyesha hivyo.

  Labda cha kujiuliza nini kifanyike ili wananchi wa vijijini waweze kukubali kuwa vyama kama Chadema,NCCR,CUF na vingine vinaweza pia kuaminika kupewa uongozi wa nchi.Hapa kwa mtazamo wangu ndiko kwenye changamoto.

  Kwa kuwa mjini uelewa wa wananchi ni mkubwa hiyo haiwapi shida sana Chadema kuuza sera zake na kukubalika.Lakini huko vijijini hata hii mijadala ya hivi karibuni bungeni hawakuiona na wala hawana habari na nini kilitokea.As long as wananchi wengi wa vijijini bado wana associate CCM na Mwalimu Nyerere Mungu amrehemu huko aliko,hawabadili mawazo.

  Sasa je mikakati iko ya kuweka nguvu kubwa zaidi vijijini ili kuleta mabadiliko ya demokrasia yanayokusudiwa.Kwani hata hiyo idadi kubwa ya wabunge wa upinzani tunayoitaka kama mkakati wa kuwaelimisha watanzania walioko vijijini hautakuwepo idadi hiyo ya wabunge wa upinzani bungeni bado itakuwa ndoto tu.

  Kazi bado naiona pevu ya kushawishi watanzania asilimia 80 wenye uwezo wa kupiga kura wapige kuwa huku wakiwa na ufahamu wa dhamani ya kura zao,hapo ndipo tutakapoweza kutegemea kuwa na bunge lenye wabunge wengi wa upinzani na hapo nakubaliana na wewe kuwa ndio mwanzo mzuri wa kuleta mabadiliko ya dhati Tanzania.Kinyume na hapo CCM itaendelea kuongoza kwa muda mrefu.
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ndo maana mimi nasema huu utafiti ni wakupikwa tu tunaweza sema wamefanyia kwenye maeneo ya ccm unategemea nini>?
   
 14. Makalangilo

  Makalangilo Senior Member

  #14
  Aug 11, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Utafiti umefanyika na matokeo ya utafiti ndiyo hayo.Sasa lawama za nini?Naamini CCM bado ina nguvu kubwa katika nchi hii na naamini kuwa JK ni maarufu kuliko wanasiasa wengine.Naamini kuwa Seif shariff huko Zanzibar ni maarufu kuliko wanasiasa wengine.Huu ni ukweli na inauma sana.

  La kufanya ni kwa vyama kama Chadema na CUF kufanya kazi kubwa ya kuwafikia wananchi huko vijijini.
   
 15. W

  WildCard JF-Expert Member

  #15
  Aug 11, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Zitto,
  Kwenye tafiti za kisiasa 66% bado ni kubwa mno na hasa ikizingatiwa kwamba ni kama watu 2000 tu waliohojiwa. Sidhani kama ni sahihi kuilinganisha na ile 80% ya kura alizopata 2005.
  Vyama vya Upinzani mna kazi kubwa mno ya kufanya ikiwemo kupunguza umaarufu wenu wenyewe na kuuelekeza kwenye vyama vyenu, agenda ya ufisadi imebamizwa mno. Inatosha. Tafuteni viongozi "tutakaowakubali".
   
 16. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #16
  Aug 11, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Hamtukubali?........................ Tatizo kwa vyama ni sisi viongozi?
   
 17. W

  WildCard JF-Expert Member

  #17
  Aug 11, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Tatizo kwa sasa ni ninyi VIONGOZI. Hakuna mbadala wa JK kwa sasa. Jipangeni upya. Kule Uingereza Conservatives wamehangaika sana kumpata mbadala wa Tony Blair. Sasa wamempata Cameron na watachukua uongozi wa Nchi hata kama uchaguzi ungeitishwa leo!
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Aug 11, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu mnakubalika sana tena mno jana nilikuwa na shangazi yangu mzee sana ana miaka 76 tulikuwa tuna angalia medani za siasa Star TV shangazi akaulizwa unapenda chama gani shangazi alijibu sasa tunataka chama kipya cha zamani hapana. Kwa hiyo mkuu elewa kabisa huku mtaani watu wanawaunga mkono sana cha kufanya mpiganie Tume huru ya uchaguzi la sivyo mtakuwa mnacho fanya sawa sawa na hakuna maana tume iliyopo ni ya CCM.
   
 19. Komamanga

  Komamanga JF-Expert Member

  #19
  Aug 11, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kweli kabisa yaani natoa support kwa hoja ya Wildcard tatizo la vyama vyetu vya upinzani ni uongozi wa juu kwanini tusiwe tunakubali kuwapa nafasi watu wapya na mkajipanga vizuri. Au hivi vyama ni kama kampuni ya mtu binafsi kwa maana faida lazima iende kwa mwenye kampuni kwanza?
   
 20. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #20
  Aug 11, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Poll inonyesha 66% JK akiwa mbele, sawa lakini hii ni wake-up call kwa CCM kwani ameteremka ukilinganisha na 80% ya 2005.

  Wapinzani Msijipe moyo, wapiga debe wa chama tawala wakiingia vijijini na kuanza kampeni ya kimyakimya mwakani hali itakuwa tofauti. Nakumbuka ilifanyika poll kama hii kwa mkapa mwaka 1999 na alionekana kushuka sana lakini uchaguzi wa mwaka 2000 akashinda kwa 70%
   
Loading...