Kikwete bado ana nafasi ya kujirekebisha, kukubalika, ni suala la kusikiliza na kufanya maamu sahihi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete bado ana nafasi ya kujirekebisha, kukubalika, ni suala la kusikiliza na kufanya maamu sahihi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by zimmerman, Feb 6, 2012.

 1. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Nikiri kwamba mimi ni mmojawapo ya watu wasiofurahishwa na utendaji kazi wa rais Kikwete. Taasisi ya urais ni nafasi kuu sana na nyeti hivyo tunategemea kiongozi wa hiyo taasisi afanye maamuzi sahihi kwa mambo tata; ila rais wetu hajawahi kuonyesha huo uwezo. Mara zote amekuwa mtu wa kutaka kutokuwaudhi marafiki zake, viongozi wenzake au wanachama wenzake hata kama ni waroho tu au mafisadi.

  Lakini kuna dalili kwamba anaanza kubadilika. Japo amechelewa sana, suala la yeye kutokubali kusaini posho za wabunge laki mbili kwa kitako linaweza likawa "turning point" ya utendaji kazi wake na bado kuna miaka 3 mbele ya kurekebisha mambo menginena hivyo akaepusha kuitwa "rais mbovu kupata kutokea katika historia ya Tanzania".

  Kwa suala la posho za wabunge rais Kikwete amefanya maamuzi sahihi. Nimesoma gazeti la Habari Leo kwamba sababu za kununiwa kwake na wabunge wa chama chake ni kwa kuwa hakuwasupport katika hilo hitaji lao la uroho. (Na katika hili niseme Chadema wamefanya vibaya sana kwenye issue ya posho -- ukimwondoa Mbunge Zitto Kabwe -- waliobaki hawana tofauti yoyote na wabunge wa CCM).

  Na wabunge walihitaji hizo posho ili walipie madeni yao waliyokopea benki ili kuhongea wapiga kura wakati wa kampeni za kuchaguliwa, sasa ndo wafanye hivyo kwa matone ya damu ya wavuja damu ya walipa kodi?

  Walipa kodi wenyewe ni akina nani zaidi ya Mwalimu wa shule ya msingi na sekondari anayepata kwa wastani wa laki moja na nusu kwa mwezi? Hawa hawana posho yoyote ile zaidi ya vitumbua au ice-cream wanazopika usiku na kuuza kwa wanafunzi wao saa nne asubuhi kesho yake.

  Rais kafanya jambo sahihi na kwa hili anahitaji kusifiwa. Nilishawahi kusema huko nyuma kwamba simchukii Kikwete kwa sababu zozote binafsi, au dini yake, au kabila lake. Kama alivyowahi kusema Mbowe, Rais Kikwete akifanya jambo sahihi atasifiwa na tutamuenzi -- na kwa suala la posho za wabunge huo ni uamuzi sahihi kwa maslahi ya taifa.
   
Loading...