Kikwete azungumza na wazee wa Dar; ajiandaa kwa mgongano na TUCTA

Namsikiliza JK amezungumzia mkutano wa WEF. Sasa anazungumzia tishio la mgomo wa TUCTA. Ameibeza kauli ta TUCTA kuwa serikali haiwajali wafanyakazi na kuwa serikali yake sio sikivu "TUCTA ni waongo!.
 
JK atishia virungu kwa wagomaji na kusisitiza mazungumzo baada ya mgomo watazungumza wakiwa tayari na manundu.
JK awahakikishia Watanzania hakuna mgomo. Mazungumzo yanaendelea
 
Ndiyo ataongeza mishahara ila si kwa maneno.Naomba umpe maswali yafuatayo

1.kipindi cha maswali kikifika muulize itakuwa shiling ngapi?

2.Bajeti ilishamalizika..Hizo pesa zainatoka wapi?

3.Alikuwa wapi kusema haya kabla ya siku ya wafanyakazi?

4.Anajua wafanyakazi wanataka mabadiliko gani?

Cha kusikitika watu wanaweza kuwa wanampigia makofi kabisa..sijui tumelogwa?

online hatuwezi kupata?
 
PASCO ...asante kwa update, unajua JK anaijua fika nguvu na uoga wa wafanyakazi wa Tanzania, ingekua ni SA hasingeweza kubeza chama cha wafanyakazi...ipo kanuni moja inasema kuwa kwenye rate kubwa ya Unemployment ndipo mahali kwenye Unyonyaji mkubwa dhidi ya wafanyakazi na ndipo pahala penye nguvu ndogo ya vyama vya wafanyakazi.....

Sasa TZ hiyo kanuni inaaply plus historical background yetu ndio kabisa mapambano dhidi ya wanyonyaji ni jambo gumu.
 
Muungwana kaanza porojo zake anaanza kuusifia mkutano unaotegemewa kufanyika Dar.

Kama nilivyotarajia hii lazima ni ajenda, mkutano huu hauwasidii wazee, vijana watoto, wanawake wala mtanzania yoyote it is a non starter. watakaofaidi waliopeleka magari yao yakodishwe na mengine yatakaa hapo mpaka mkutano utapokwisha yatakuwa hayajatumika. Afadhali mwalimu wakati wa group of 77 alinunua benz kibao akaweka serikalini na zikawa zinakodishwa na kutokana na mkutano huo ndo tupata hotel 77 ambayo watanzania tumeinywa tayari
 
Amewaita viongozi wa TUCTA ni wanafiki wa ajabu. Amesema mazungumzo yanaendeleo vizuri, yako mambo yamekamilika na mengine yanaendelea kuzungumzwa hivyo hakuna tishio la mgomo.
 
Amewaita viongozi wa TUCTA ni wanafiki wa ajabu. Amesema mazungumzo yanaendeleo vizuri, yako mambo yamekamilika na mengine yanaendelea kuzungumzwa hivyo hakuna tishio la mgomo.

Si angeenda uwanja wa taifa kusema hayo??????
 
Amewaita viongozi wa TUCTA ni wanafiki wa ajabu. Amesema mazungumzo yanaendeleo vizuri, yako mambo yamekamilika na mengine yanaendelea kuzungumzwa hivyo hakuna tishio la mgomo.
 
Hotuba nimeanza kuisikiliza kati lakini naona topic muhimu anayozungumzia ni mugomo wa Wafanyakazi (watumishi, waajiliwa) kama ulivyotangazwa na TUCTA.

Sijui itaishia wapi lakini naona hapo alipo nimeshangaa. Kwanza ni choice ya audience yake, 'wazee wa Dar es Salaam' Kama ni wazee kwa maana ya siku zote naona kama siyo watumishi wa Serikali. Muenendo naona anatoa hotuba kwa washabiki (nilitegemea hili) maana wanashangilia hata bila sababu.

Baya ambalo sikutegemea, ni jinsi alivyoahidi kwamba wakigoma na kuandamana, watapigwa na polisi. Huyu ni Rais na naamini anafahamu nguvu ya maneno yake, Sijui ni kwa nini anaelekeza tendo kama hilo. Anazidi kusema Polisi watawaumiza. Kakumbusha uwezo wa polisi kuua kama ilivyowahi kutokea huko nyuma.

Ok, vyovyote itakavyokuwa ktk hotuba hii, binafsi sifahamu ni kwa nini hotuba za viongozi wetu hazitofautiani na zile za Mugabe. Tusubiri anakoishia.
 
Namsikiliza mkuu wa nchi anaongea na wazee sasa hivi...hotuba kwa kweli inanisikitisha sana, imejaa mipasho, mipasho ya kila aina...

Ni jambo la kusikitisha sana kuona mkuu wa nchi anatoa mipasho, anawasuta na kuwashushua wakuu wa TUCTA
 
huyu mzee analiitafuta sana mei day ajinadi kwa watanzania lakini ameikosa, hapa naona anajikosha kwa wazee, ngoja nao wanuulize hela zao za east africa
 
mi mwenyewe namsikiliza lakini mpaka sasa sijaelewa anawaeleza hawa wazee kitu gani, hivi hawa wazee wanahusiana na tucta? au ndio meseji senti
 
Back
Top Bottom