Kikwete azungumza na wazee wa Dar; ajiandaa kwa mgongano na TUCTA

Politics is a dirty game...sasa kama ma professor wote wame kimbilia kwenye siasa na kujitahidi kuwa kamua walala hoi tusio na elimu...tusi shangae kusikia kauli hizo za ajabu...kwani wakosoaji ndio haohao wako kwenye game....kilicho baki hewala bwana...au la 2010 be history to them!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Redet/shehe yahaya ndio wamempa kichwa mkwere, haya ila namkumbuka kk wa zambia kama aliangushwa na hawa mbayumbayu?kwa imani yake atapata tuu
 
Hata kama atapata ushindi lakini uwe mwembamba kabisa! Mambo ya ushindi wa tsunami iwe ni ndoto! Wafanyakazi mpo? Kwenye kupiga kura HAKUNA KUTISHIWA NYAU, FANYENI KWELI OCTOBER!
 
HII ni moja kati ya kauli alizozitoa Rais Kikwete wakati wa hotuba yake aliyoitoa juzi jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wazee kjatika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Rais alitoa kauli hiyo baada ya kuonekana kukerwa na viongozi wa Tucta wanaoandaa mgomo nchi nzima.

" Mgomo huo una lengo la kuongezewa mshahara tu au kuna lingine? Alihoji rais, mimi naona mnataka kuninyima kura zenu, basi kama mmepanga hivyo mninyime tu, wengine watanipa" alisema Rais

"Mana sitaki kuwaongopea kuwa tutalipa kima hicho kama mnataka kugoma na mshahara huo kama hatutawapa basi, ninyimeni kura zenu wengine watanipigia" alisema

Pia aliwasihi wafanyakazi hao atakayegoma atakuwa amejifukuzisha kazi na kukosa haki yake ya msingi katika miaka yake aliyoitumika serikali.

Pia alisema kwa yeyote eatakayefika kazini na akae na asiendlee na kazi pia atakuwa amejifukuzisha mwenyewe na hakutakuwa na msamaha na atakayethubutu kuandamana sheria itafata mkondo wake.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4437294&&Cat=1

Mengine yapo kama:-
Muhimu ni:-
1.Punguzo la kodi kwenye salary za watumishi.
2.Mafao yanayotolewa na mifuko ya pensheni kuwa madogo na kuchukua muda mwingi kulipwa

Mengineyo ni:-
3.Tumechoka na mifumuko ya mabei ya bidhaa muhimu kama mafuta ya kuendeshea magari, vyakula nk na huduma duni kwa jamii.
4.Mafisadi wanaimaliza nchi yetu, hatuwataki na wachukuiwe hatua kali.
 
HII ni moja kati ya kauli alizozitoa Rais Kikwete wakati wa hotuba yake aliyoitoa juzi jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wazee kjatika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Rais alitoa kauli hiyo baada ya kuonekana kukerwa na viongozi wa Tucta wanaoandaa mgomo nchi nzima.

“ Mgomo huo una lengo la kuongezewa mshahara tu au kuna lingine? Alihoji rais, mimi naona mnataka kuninyima kura zenu, basi kama mmepanga hivyo mninyime tu, wengine watanipa” alisema Rais

“Mana sitaki kuwaongopea kuwa tutalipa kima hicho kama mnataka kugoma na mshahara huo kama hatutawapa basi, ninyimeni kura zenu wengine watanipigia” alisema

Pia aliwasihi wafanyakazi hao atakayegoma atakuwa amejifukuzisha kazi na kukosa haki yake ya msingi katika miaka yake aliyoitumika serikali.

Pia alisema kwa yeyote eatakayefika kazini na akae na asiendlee na kazi pia atakuwa amejifukuzisha mwenyewe na hakutakuwa na msamaha na atakayethubutu kuandamana sheria itafata mkondo wake.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4437294&&Cat=1

Mengine yapo kama:-
Muhimu ni:-
1.Punguzo la kodi kwenye salary za watumishi.
2.Mafao yanayotolewa na mifuko ya pensheni kuwa madogo na kuchukua muda mwingi kulipwa

Mengineyo ni:-
3.Tumechoka na mifumuko ya mabei ya bidhaa muhimu kama mafuta ya kuendeshea magari, vyakula nk na huduma duni kwa jamii.
4.Mafisadi wanaimaliza nchi yetu, hatuwataki na wachukuiwe hatua kali.
 
Kikwete akirudia kama Raisi Tanzania kunako OKTOBA mwaka huu basi watanzania TUMELAANIWA.hakuna maelezo mengine tena zaidi ya hayo.i see no future for this guy,if Nyerere said this i would atleast feel for him,maana he was leading by example.HUYU MKWERE yeye anaishi kama US president na waliomzunguka halafu yeye anataka watanania waishi kama wako kuzimu.Naamini wafanyakazi wa Tanzania 350,000 wana multiplier effect ya 10,hence tunaongelea wafanyakazi na ndugu,marafiki wasiopungua milioni 3!!sasa hawa wakiungana basi kikwete sio rasi wa nchi hii,

HAKUNA SABABU ya kuwa na stable president terms isiyowasikiliza na kuwahudumia wananchi wake,kumbukeni israel etc wana very unstable president terms and they are doing just fine.

KURA YANGU NA YA WATU 30 Wanaonitegemea kikwete huna tena!!mwanzoni ulikuwa huna kura yangu sasa nna moja tu la kuwaambia wanaonitegemea,either no more trips to my office,home for misaada isiyokwisha or do not vote for this guy.simple as that.
 
spottheoddoneout.jpg
 
Unajua sisi wananchi tunapenda sana kukurupuka bila kuangalia matatizo ambayo yatajitokeza wakati wa kufanya migomo, simlaumu kikwete na pia siwalaumu wananchi na wafanya kazi

ninacho taka kusema je Wafanya kazi hawa wa selikali walikuwa wamesha chunguza pato la nchi? je wote ni wazalendo wa kununua bidhaa Halisi zenye nembo ya TBS, kwasababu ukinunua bidhaa iliyo thibitishwa na TBS unaichangia selikali asilimia fulani kwahiyo unakuwa umelipa kodi na hivyo kuiongezea selikali yako kipato.

Baada ya hapo unajiuliza performance yako katika kazi ni nzuri? hapo ndipo kuna kimbembe, kwani ni dhahili kuwa offisi z\a selikali zote ni zembe na wafanyakazi wake ni wazembe hawapendi kujishughulisha wakiwa kazini, hii inasababisha pato la selikali kuwa ni la chni.. kwani unapochelewesha project za selikali kinachofuata ni nini?
 
Kikwete alishasema hataki kura za wafanyakazi, hii ikiwemo na watoto wa wafanyakazi ambao wanasongwa na ukata wa mishahara midogo na kodi kubwa huku 'wawekezaji wakisamehew' pia wafanyakazi wakichangia mifuko ya pensioni na mwisho wake kulipwa mafao duni huku mifuko hii ikiwa ni kisima cha serikali kuchota pesa kibao kwa matumizi yao binafsi.

Uchaguzi huu mfanyakazi atakayempa kura huyu bwana sipendi kusikia akiwaambia watoto wake maisha magumu, badala yake ningependa ajililie mwenyewe na nafsi yake. sasa hivi tunatumia masaa 3-5 kwa siku kutafuta magari na kusafiri has kwa wakazi wa Dar, mimi hata kwenye daladala huwa nawaambia haya ndo maisha bora kwa kila mtanzania.

Nasema hivi, umefika wakati tujililie wenyewe na wala siyo kuwalilia wana-siasa, maana bila kura yetu wasingeweza kuwa madarakani na pia kutuibia, tumependa

Hotuba ya rais kwa TUCTA na wafanyakazi kwa ujumla ingekuwa imetolewa kwenye nchi za watu makini kesho yake nchi isingekalika, watu wangetoka barabarani ili alete hao wafanyakazi bora wanaolipwa vizuri - POLISI- ili wapige watu ngeu kama wale wakata miwa wa Kilombero, hotuba mbovu yenye 'mktadha' mbovu. Hao polisi najua wao si wafanyakazi na pia hulipwa vizuri.

Hotuba gani imetawaliwa na hadhira isiyosoma wala kuwa na mtoto mfanyakazi, hadhira unayoita kuongea nayo itajulisha wewe mwenyewe ukoje!! 'hao wazee wa Dar' kimsingi ingekuwa enzi za Mwenye Heri Kambarage wangeshangilia 'wape wape haoo!! angewaambia 'SHUT UP' rais wa nchi hawezi kuongea mambo anayofikiri ni ya mstakabali wa nchi na mtu mwingine akashangilia wape wape vidonge haoooo! hadhira ya wahuni ndo tegemea haya.

JK Kaboa, hataki kura ya wafanyakazi, ukijipendekeza mpe, yeye hataki unajikomba tu

PIGA CHINI JK OCTOBER 31
 
vijana akilizao zina chaji kulingana na upepo wa maelezo ya mtu na mtu, sasa anaogopa Challanges we unafikiri halijui hilo?
 
Kazi kweli kweli.... sijui kama tunarudi kusoma mijadala hii na kulinganisha na kinachoendelea sasa
 
Kazi kweli kweli.... sijui kama tunarudi kusoma mijadala hii na kulinganisha na kinachoendelea sasa

Heshima kwako Halisi,

Mkuu unajua Muungwana anadhani watu wote ni wajinga na hawana kumbukumbu ya maneno yake ya kejeli ya kutisha/dharau dhidi ya wafanyakazi wa Tanzania amabo wamekuwa hawana njia yoyote ya kukwepa kulipa mzigo mkubwa wa kodi PAYE kama wafanyabishara walivyo na nafasi kubwa ya kukwepa kulipa kodi.
 
Back
Top Bottom