Kikwete azungumza na wazee wa Dar; ajiandaa kwa mgongano na TUCTA

Unajua huyu kiongozi anawalinganisha watanzania na uwezo wake mdogo wa kuangalia na kufanya mambo.

Ina maana watu wake hawasomi demographic survey kwamba 44% ya watanzania leo hii ni vijana wa chini ya miaka 35 na wazee hawazidi asilimia 4 ya population yetu? Na kwa kweli wazee hao watakosa hekima kama hawatazungumzia angalau swala la wazee wa iliyokua EAC na maswala ya serikali yake kugeuka kiosk cha wakina Rostam, swala zima la ripoti ya uwezeshaji kwamba uchumi wetu uko chini ya 1% ya watanzania waasia na wageni wachache haiwezi kuelezewa kwa kutuia vigezo vya kwamba tulirithi toka kwa wakoloni hivi hawajui kwamba hiyo ndio sababu iliyowafanya watanzania wagombee uhuru?

Hatukugombea uhuru wa siasa bali wa kiuchumi watu hawasomi historia hata ya nchi yetu? Na pia wamuulize hivi nchi imejiandaaje kutumia nafasi ya mkutano wa world economic forum? ama objective ni kuuza sura kwa kutoa speech ya ufunguzi, nimesoma kituko cha statement ya serikali kwamba itatoa investment opportunities 'crap' hivi kila mtu ni mjinga kiasi hicho jamani? Unajua ni uoga tu lakini Lowasa akichukua form leo hii wengi tutamuunga mkono, tunachotaka sasa ni kumtoa huyu bwana na si CCJ si nani atakaeweza kuuzika katika hili ni Lowasa tu.

Hatuna miaka mingine mitano ya kupoteza kulea ubovu
 
nikiwa graduates school pale UDSM MWAKA 2005, vijana wadogo pale UDSM PLUS WALE WA GRADUATES SCHOOL nililionekana ni kungi la kipekee lililoshabikia Kikwete kumshinda Mark Mwandosya na kisha kutangazwa kuwa mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM, Wasomi wa kada mbalimbali hapa TZ waliwaaminisha wananchi wa TZ kwamba tangu baada ya JK nYERERE nchi imepata mkombozi wa aina yake , mwenye haiba na muonekana sawa wa Julius..

Wa kulaumiwa ni wasomi na wakazi wa mijini kwa kumshabikia rais legelege, rais asieweza kutembea katika maneno yake, rais mpenda makuu, rais anaeshindwa hata kudhibiti familia yake, maana kila mara Ridhwani huchafua hali ya hewa katka chama chao.

Rais asieweza kusimama mbele ya Wafanyakazi maana anaona aibu. kwa hali ya maisha ya leo unamlipa mtu Tsh100,000, kisha unajisifu umemboreshea maslahi yake.
 
nahisi mgomo hautafanikiwa kwa sababu ya woga wa Wafanyakazi katika sekta ya UMMA, HASA wanachama wa TUGHE.... ILA RAAWU,CWT, hawa ni mangangari saaana, wamepita katika mambo mengi. kwahiyo nawatakia kila la heri wafanyakazi wa nnchi hii katika kupigania maslahi yao.
Kikwete(Rais) atawapigia porojo , lakini nyie simamieni maslahi yenu, muoneni debe tupu haliachi kutima.
 
Me sitegemei atazungumza mambo ya msingi zaidi ya kutaka tu simpathy ya wananchi kuhusu mgomo unaotarajiwa kuanzia tarehe 5 kesho kutwa. Me nafikiri viongozi wake serikalini wamekosa uwezo wa kutatua matatizo ya wafanyakazi. Yasemwe yote lakini hili swala la kodi katika mshahara "PAYE" inauma sana na lazima lifanyiwe maamuzi.
 
He is miserable...Huwezi kuwashawishi wananchi waliokata tamaa na uongozi wako kwa MANENO!

Anaenda kuuza sura tu, ili aonekane yupo nchini, na kuwadanganya wenye bongo ndogo kwa kauli zake za jeuri na mitego...Utamsikia tu.."sijui mkutano wa WEF"....HANA JIPYA ATAKALOWEZA KUSEMA!
 
Unajua huyu kiongozi anawalinganisha watanzania na uwezo wake mdogo wa kuangalia na kufanya mambo.

Ina maana watu wake hawasomi demographic survey kwamba 44% ya watanzania leo hii ni vijana wa chini ya miaka 35 na wazee hawazidi asilimia 4 ya population yetu? Na kwa kweli wazee hao watakosa hekima kama hawatazungumzia angalau swala la wazee wa iliyokua EAC na maswala ya serikali yake kugeuka kiosk cha wakina Rostam, swala zima la ripoti ya uwezeshaji kwamba uchumi wetu uko chini ya 1% ya watanzania waasia na wageni wachache haiwezi kuelezewa kwa kutuia vigezo vya kwamba tulirithi toka kwa wakoloni hivi hawajui kwamba hiyo ndio sababu iliyowafanya watanzania wagombee uhuru?

Hatukugombea uhuru wa siasa bali wa kiuchumi watu hawasomi historia hata ya nchi yetu? Na pia wamuulize hivi nchi imejiandaaje kutumia nafasi ya mkutano wa world economic forum? ama objective ni kuuza sura kwa kutoa speech ya ufunguzi, nimesoma kituko cha statement ya serikali kwamba itatoa investment opportunities 'crap' hivi kila mtu ni mjinga kiasi hicho jamani? Unajua ni uoga tu lakini Lowasa akichukua form leo hii wengi tutamuunga mkono, tunachotaka sasa ni kumtoa huyu bwana na si CCJ si nani atakaeweza kuuzika katika hili ni Lowasa tu.

Hatuna miaka mingine mitano ya kupoteza kulea ubovu

Ndugu yangu Nimeipenda hii!!!! Lowasa kwakweli yupo Juu I like the guy coz yeye ni mtu wa VITENDO hizi ni siasa...Unajua wanajamii wenzangu mimi kitu ninachoamini Kama kweli Muheshimiwa huyu alishiriki kwenye dhambi ya Ufisadi kwanini hashitakiwii??? mbona wengine walishitakiwa mimi naamini Ndugu yetu Lowasa ni mtu safi na ni Kiongozi bora.....

Nakuunga mkono kwa asilimia zote bila ubishi...
 
Hakuna jipya atakaloongea zaidi ya kwenda kujichekelesha mbele ya wazee!
 
Anakwenda kuzungumza na wazee wa Dar au wazee wa CCM walioko Dar, kwa ninavyo fahamu na kwa kumbukumbu zangu za mikutano yake kama hii ( maana sio mara ya kwanza) ukumbi utajazwa na masharti na fulana a CCM! so tusitegemee kitu hapa, watakachofanya hao wazee ni kupiga makofi kwa kila atakalosema!
 
Sasa anataka kuwatumia wazee ili wafikishe ujumbe kwa wafanyakazi wasigome? Nataka wagome kazi na uchaguzi ujao wagome pia!!!! Kama kweli wafanyakazi mmechoshwa na hali ngumu na ahadi hewa toka kwa serikali mlioichagua kupitia chaguzi za sunami, sasa iweje msigome kuwachagua mwaka huu ili iwe fundisho?? Tafadhali muwe serious msije mkatishiwa nyau mkarudisha majeshi!! Fanyeni kweli. Kodi inaumiza mno, tena nafikiri hii ya wafanyakazi ndiyo inayopokelewa TRA wakati kodi nyingi zinaishia mifukoni mwa wachache.
 
Ndugu yangu Nimeipenda hii!!!! Lowasa kwakweli yupo Juu I like the guy coz yeye ni mtu wa VITENDO hizi ni siasa...Unajua wanajamii wenzangu mimi kitu ninachoamini Kama kweli Muheshimiwa huyu alishiriki kwenye dhambi ya Ufisadi kwanini hashitakiwii??? mbona wengine walishitakiwa mimi naamini Ndugu yetu Lowasa ni mtu safi na ni Kiongozi bora.....Nakuunga mkono kwa asilimia zote bila ubishi...

ahahah wazee msijekuwa ni ma agent wa lowasa ndo mmeanza debe humu, anyway mi 2005 baada ya huyu jamaa kushinda kura za maoni nilisita i mean moyo ulikuwa mzito lakini by then hakuna alosikia wala kuambiwa kuhsu jamaa, alikuwa juu kiufupi ila matendo yake yamejionyesha..leo hii ni mambumbu tuu au wale wanaonufaika na madudu yake ndo wasio ona jamaa hafai, lowasa alitolewa kafara nahisi, sina ushahidi wa uhakika but spidi yake ilimtisha mzee akaona mmmhhh mshkaji anakuja kasi ngoja nimzime...kwa mtazamo wangu tu!
 
Wazee wa DSM ni watu gani?

Atazunguza si na wazee wa DSM kama inavyodaiwa bali ni viongozi wa kada mbalimbali katika chama chake. Huu ni uzoefu wa siku zote. Hivyo ni bora wangetangaza kuwa kutakuwa na mkutano wa viongozi wa chama katika mkoa wa dsm.

Cha msingi ni watu kumdharau na kuendelea na mipango ya mgomo.

Ukombozi wako hautaletwa na raisi, wala waziri, wala mbune wako, wala mwajiri wako, bali wewe mwenyewe. Pigania haki yako sasa na wakati uliokubalika kwa ukombozi wako ni huu
 
maana Kikwete kashindwa hata kutatua mogoro wa wafanya kazi East AFRIKA , mgogoro huu unamtia aibu kubwa, leo anaenda kuongea na wababu ambao baadhi ya wababu wanatesekea maslahi yao miongo na miongo.
 
ABRAHAM LINCOLN:
Labor is prior to, and independent of, capital. Capital is only the fruit of labor, and could never have existed if Labor had not first existed. Labor is superior to capital, and deserves much the higher consideration.

MARTIN LUTHER KING, JR.:
In our glorious fight for civil rights, we must guard against being fooled by false slogans, as 'right-to-work.' It provides no 'rights' and no 'works.' Its purpose is to destroy labor unions and the freedom of collective bargaining... We demand this fraud be stopped.
 
Mkutano wa wazee wa Dar na Rais unafanyika diamond jubile,nimetune TBC1 wanatangaza moja kwa moja.Walioko maeneo ya mkutano tafadhali mtujuze zaidi
 
Hakuna jipya atakaloongea zaidi ya kwenda kujichekelesha mbele ya wazee!

Just right, nothing new, Atawashukuru wazee kwa kuja, baadaye mvua hizi na matumaini ya umeme, sheria ya uchaguzi na jinsi walivyomchomekea vifungu bila kujua, halafu mkutano wa world economic forum ( mgeni njoo mwenyeji apone) hahahahhaaahahha, halafu mei mosi na TUCTA asanteni kwa kunisikiliza. Any updates???????
 
Hivi hawa wazee ulipwa 'sitting allowance' na vigezo vipi vinatumika kuwaalika. Pia nafikiri wengi wa wazee walikuwa wanachama wa TANU na baadaye CCM. Ukienda Ikulu pale reception ndio utaona wazee wenyewe - wamechoka!
 
Hivi kikwete tangu aingie madarakani amesha fanya nini cha kuonekana??
 
Muungwana kaanza porojo zake anaanza kuusifia mkutano unaotegemewa kufanyika Dar.
 
Back
Top Bottom