Kikwete azungumza na wazee wa Dar; ajiandaa kwa mgongano na TUCTA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete azungumza na wazee wa Dar; ajiandaa kwa mgongano na TUCTA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngongo, May 3, 2010.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Wanajamvi leo asubuhi nilikuwa natazama TBC1,kulikuwa na tangazo kwamba Rais J Kikwete atazungumza na wazee wa jiji la Dar sijui kama ni leo au kesho.Mara nyingi wazee wa jiji la Dar wamekuwa wakitumiwa na viongozi wakuu wa kisiasa tangu enzi za Mwl J Nyerere kufikisha ujumbe kwa wananchi wote wa Tanzania.

  Nahisi Muungwana safari hii atazungumzia kitisho cha mgomo wa wafanyakazi ambao unaratibiwa na vyama vya wafanyakazi.Mei mosi hakualikwa kama ilivyo desturi ya nchi yetu,Muungwana anakuwa rais wa pili kususiwa na wafanyakazi iliwahi kumtokea Mzee Ruksa kipindi cha urais wake vyama vya wafanyakazi vilimualiaka Baba wa taifa Mwl Nyerere badala ya Mzee Ruksa.

  Vyama vya wafanyakazi kwa mara ya kwanza vimeistukia serekali ya Muungwana kwamba vinawakumbatia wawekezaji na mafisadi na kuwasahau wafanyakazi wa nchi hii ambao historia inadhihirisha walihusika kupigania uhuru wa Tanzania.Nilikuwa nasikiliza risala ya mgeni rasmi kwenye kilele mei mosi kwa kweli ilimtwanga nyundo ya uhakika Muungwana,serekali na chama chake kwa ujumla.Nategemea kusikia porojo za Muungwana leo/kesho katika mkutano wake na wazee wa Jiji la Dar.Wenye data zaidi tafadhali mtuhabarishe.

  ====================
  UPDATES:

  Rais amewashutumu viongozi wa wafanyakazi kuwa ni WANAFIKI na wao ndio wanaoshinikiza mgomo na kusema watakaogoma watakiona cha mtema kuni.

  Kasisitiza hakuna mgomo, vinginevyo virungu vitatembea. Pia kasisitiza mgomo ni batili na kinyume cha sheria.

  Watakaogoma kupoteza nafasi za kazi?

  'Aruhusu' waajiri kuwafungia milango watakaogoma!

  [​IMG]
   
 2. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Bwana weee huyu ni Rais wa kwanza kupatwa na mustakabari huu ule wa mzee ruksa angalau haukuwa kama huuu. Unataka kumtolea record yake mzee wetu Kikwete aa no rais Kijana wetu. Jamaa sasa hivi ana chachawa tu hana pa kushika, wazee watamsikiliza tu ila wangetokea wazee jasiri wamkampa ukweli wake ingekuwa kazi kweli kweli. Harafu wazee wa east africa hawapo waende huko? maana wale lazima wangempa ukweli wake.
   
 3. B

  Bizzly Member

  #3
  May 3, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 70
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  muungwana huyu ataongea leo saa kumi jioni
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Mkuu Mess,

  Unajua Muungwana alijua urais ni kutabasamu na kucheka cheka,anataka kutumia jukwaa dhaifu sana kwasababu anajua hakuna atakae muuliza jinsi alivyoshindwa kuwapeleka mahakamani watuhumiwa wote wa ufisadi [Richmond,Deepgreen,Radar na nk].
   
 5. J

  Jafar JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nadhani ule umati uliojaa ile neshino ya zamani siku ya mei mosi serikali hawakutarajia. Walidhani kwa kuwa Rais ameomba mazungumzo basi watu hawatajaa uwanjani. Picha ni pana zaidi kwa kuwa madai ya TUKTA yanagusa wafanyakazi woooooooote hata waliopo pale Ikulu - kwani kila mfanyakazi ni kweli analipa kodi zaidi ya mfanyabiashara na hela ya kustaafu ni kiduchu na zinatofautiana kati ya PPF, NSSF, LAPF etc.

  Ngoja tuone akicheka na kutabasamu - sitegemei ufumbuzi kupitia hotuba hiyo.
   
 6. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wazee wa Dar? Wapo wale wastaafu wa iliyokuwa jumuiya ya afrika mashariki ambao hawajalipwa mafao yao? Muungwana kweli sijaona jipya atakalo ongea. Mi nimechoka na viongozi wa nchi hii.
   
 7. S

  SHAMTE Member

  #7
  May 3, 2010
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni vizuri tukasikiliza anachoongea
   
 8. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Real Madrid?
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako N-handsome,

  Mkuu bado sijakuelewa hapa ?.
   
 10. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Anazuga tu huyo hajui watu wameshastuka.
   
 11. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hashim Thabit, yes na Picha yake? Lol na Yebo Yebo kutoka China.
   
 12. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sijakuelewa
   
 13. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Duh mbona nazidi kuchanganyikiwa,Wakuu ebu tumtendee haki Muungwana anaweza kuja na majibu ya maana sijui ebu tuwe na subira
  .
   
 14. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  kocha anayetumia komputa kufundishia soka!
   
 15. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mara nyingi sana anapenda kuongea na wazee. INGEKUWA VYEMA ZAIDI KAMA ANGALAU SIKU MOJA AKAONGEA NA VIJANA. MAANA WATANZANIA SI WAZEE PEKEE YAO.
   
 16. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Nadhan ataelezea mafanikio za safari zake za majuu, hamna jipya
   
 17. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Saa kumi jioni sio mbali wakuu tumsubiri tumsikie anachotaka kueleza. Huwezi kujua pengine anajipya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 18. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,190
  Likes Received: 996
  Trophy Points: 280
  Mheshimiwa sii hapa majuzi tuu alisema serikali yake ijayo kama atapata ridhaa itakuwa ya vijana watupu? Sasa inakuwaje tawi lake la mwisho kujiokoa na mgomo wa wafanyakazi anashika wazee badala ya vijana? Nafikiri mh ana akili sana amejua vijaana watampa ukweli wa mambo wakati yeye anachohitaji ni faraja ya kupakwa pafuta kwa mgongo wa chupa.
   
 19. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mi afadhali nikae zangu t gardern bar nipige taska zangu kuliko kumsikiliza maana naweza kupasua tv kwa hasira
   
 20. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ebu kaka niambie ni lini toka Kikwete aanze madaraka ameshakuja na majibu ya maswali? Amewaacha watu kwenye mataa mara kibao. Unakumbuka sakata la zombe kikwetet aliahidi nini kwa wananchi?unajua kumetokea nini mpaka leo. Nadhani watu sio kwamba hawana subira ila jamaa kachemka , subira wamewahi kuwa nazo mara kibao lakini jamaa ha convice hata kidogo. Sasa kaka Ngongo kesho tutakutana hapa jamii forum tuzungumze alichoongea Rais wenu wa Vijana.
   
Loading...