Kikwete azomewa Bukombe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete azomewa Bukombe!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by PayGod, Sep 28, 2010.

 1. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Habari nilizozipata kutoka wilaya ya BUKOMBE, Shinyanga zinasema kuwa mkutano wa JK wa kampeni, uliofanyika leo hapo Bukombe umevyunjika baada ya wananchi kuanza kumzomea JK na mgombea ubunge.

  Kwanza alianza kupanda mgombea ubunge, ambaye wananchi walianza kumzomea, na baadae ilibidi apande mwenyekiti wa CCM Shinyanga, ambaye alimkaribisha JK, ambaye baada tu ya kuanza kuhutubia wananchi walimwonyesha alama ya CHADEMA, na kuendelea kuzomea, na kusababisha mkutano uvunjike.
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Duh! Mambo sasa ni mbele kwa mbele. Watu hawadanganyiki tena. Wameamua kuleta mabadiliko.
   
 3. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hapo, mida ya saa tano, nilipata ujumbe kutoka kwa rafiki yangu, ambaye ni mfanyakazi wa halmashauri ya bukombe,ambao unasomeka hivi.

  DOGO LEO TUNAYE BABA WA MAFISADI ,KIKWETE, TUMELAZIMISHWA, WAFANYAKAZI WOTE WA HALMASHAURI, TWENDE TUKAMSIKILIZE.


  baadaye, nikamuuliza vipi mmepewa fulana, za ccm, akaniambia ndiyo, ila yeye amekataa, na wenzake wamezivaa
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,231
  Trophy Points: 280
  JK safari hii atakiona cha motoooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
   
 5. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  wagombea ubunge CCM vs CHADEMA ni akina nani?
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,231
  Trophy Points: 280
  Channel Ten kwenye taarifa yao ya habari wasema JK aomba kura lakini wamekaa kimya juu ya ukweli huo wa zomeazomea
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Inanikumbusha ya nyerere '95 pale moshi uwanja wa mashujaa wakati anamnadi mkapa kwa wachaga wa nccr
   
 8. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  astagfilulaha jk
  huyu mkwere ana hali mbaya
   
 9. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Siamini kama ni watanzania wanaoweza kufanya hivyo. Nimezoea kuwaona watanzania wakinyenyekea na kujipendekeza kwa unafiki kwa CCM, lakini kama kweli leo hii wanaweza kufanya hivyo, basi kwa hakika saa ya ukombozi imefika. Mungu ibariki Tanzania.
   
 10. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  ccm ni EMANUEL LUAHULA, NA CHADEMA ni PROF K K KAHINGI, ambaye habari zake zimetolewa kwenye MWANAHALISI la jumatano lililopita, ambaye alikuwa profesa wa kiswahili pale UDSM.
   
 11. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  wera weraaaa .... wera weraaaaaaaaaaaaaaaa ..... ngoma inogile
   
 12. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  wadau, kama, kuna mtu ambaye anandugu yake ambaye yuko, kwenye msafara wa jk, atupe hata picha.
   
 13. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Prof. Kahigi: Tegemeo la Bukombe  Na NdimaraTegambwage - Imechapwa 22 September 2010

  "NENDA upinzani, sisi tutakuunga mkono!" Hiyo ndiyo sauti ya umma iliyomwelekeza Prof. Kulikoyela Kanalwanda Kahigi kuvuka mstari – kutoka CCM kwenda CHADEMA.
  Ni vyama viwili vikubwa vinavyofahamika katika jimbo la Bukombe – Chama cha Demokrasia na Maendeleo na Chama Cha Mapinduzi.
  Yaliyompata Kahigi ndiyo yalimpata Dk. Willibrod Slaa wakati akitafuta ubunge wa Karatu miaka 15 iliyopita kupitia CCM. Jina lake, tena akiwa mshindi kwa mbali, lilitupwa.
  Mafundi ujenzi wa CCM hawakujua kuwa walikuwa wanakataa jiwe muhimu ambalo lingeimarisha mihimili mikuu. Ndivyo ilivyotokea pia kwa Prof. Kahigi.
  Historia imetufunza kukataa kukasirika; kwani kukasirika kunaleta jazba na maamuzi kengeza.
  Tumefunzwa kuchukia na tumezingatia. Ukichukia unachukua hatua. Ndivyo alivyofanya Dk. Slaa ambaye leo hii anachora ramani ya ajenda kuu za uchaguzi mkuu mwaka huu.
  Ndivyo alivyofanya pia Prof. Kahigi wa Bukombe. Hawakuhamaki. Hawakukasirika. Walichukia kilichotendeka. Wakauliza wazee na vijana. Wakashauriwa: "Nenda kule tutakufuata."
  Kahigi alizaliwa Agosti 1950. Katika umri huo tayari amesoma hadi chuo kikuu na kujizolea shahada ya kwanza (1976), shahada ya pili – ya umahiri (1977) na shahada ya udaktari wa falsafa (1988).
  Katika umri huo pia Kahigi amefanya ufundishaji, tathmini na utahini katika vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi.
  "Nimeipenda kazi yangu na kuifanya kwa dhati kwa miaka yote," anasema Kahigi wakati akielezea familia yangu jijini Dar es Salaam juu ya uamuzi wake wa kugombea ubunge.
  Huku akitabasamu aliongeza, "Lakini huku pia kuna kazi, tena nzito, ya kufanya kwa ushirikiano na wananchi ambao wamekuwa chimbuko la ‘raslimali' tunazotumia kufundishia na kuandika vitabu."
  Kahigi ambaye ameandika na kuchapisha zaidi ya vitabu 10 na makala nyingi za kitaaluma katika majarida ya kitaifa na kimataifa, anabeba kauli ya ushirikiano kwa wakazi wa Bukombe. Anasema, "Maendeleo sahihi yanawezekana tukishirikiana."

  Anaonyesha nia hiyo katika shairi lake la Mei – Juni 2005:
  Wimbo wangu, sasa toka, leo kifupi eleza:
  Shakawa ziloifika, wilaya zikaimeza
  Watu wakahamanika, kwa shida za kuumiza
  Kote wakazongomeka, utu wakaupoteza.
  Mwambieje wanati, wenye uchungu wa dhati
  Waiache atiati, waendeshe harakati
  Umoja wauzatiti, kwa kiapo na kwa hati
  Wainuke wasiketi, wajihami madhubuti.
  Niwelezeje lukuki, wafikwao uonezi
  Kwamba jambo lilobaki, ni kutenda ukombozi
  Ni kwa dhati kudiriki, kuupindua uozi
  Madhalimu kuwadhiki, na kuleta MAGEUZI.


  Ni ndoto ya masafa? Ni dhamira? Ni utashi ndani ya kauli? Namfahamu Kulikoyela Kanalwanda Kahigi. Hutenda asemacho. Hufanana na kauli yake. Aweza kufanana pia na wananchi wa Bukombe au jinsi anavyotaka wawe kupitia utetezi wake.
  Miaka ile nilipokuwa sekondari, wanafunzi waliokuwa wakiapa kuwa wakienda chuo kikuu watasomea sheria, wengi walikuwa na historia ya wao, wazazi au nduzu zao kunyang'anywa au kunyimwa haki. Walitaka kuwa watetezi na walinzi wa haki.

  Kahigi anataka kuwa mtetezi wa wananchi katika mazingira ambamo anaona hawana mtetezi:

  Wengi wamekuwa wezi, utajiri kuwania
  Mbinu zao ziko wazi, kwa hakika twazijua
  Fedha za sera azizi, kwa hila hujichotea
  Na hutumia ghawazi, kuhonga kila njia.


  "Nataka niwe karibu na wananchi. Tushirikiane. Inawezekana." Haya ndiyo maneno aliyokuwa akisema Kahigi mara kwa mara wakati tukipata chakula cha mchana alipokuja kueleza familia yangu kile alichodhamiria, wiki mbili zilizopita.
  Bali anasikitikia sana CCM. Anasema hata wananchi wa Bukombe wanajua sasa kuwa chama hicho ni hatari ya kuepuka kwani "kilipora ushindi wao."
  "Nilishiriki mchakato wa kura za maoni CCM. Niliongoza kwa ushindi wa kura za vituoni," anaeleza Kahingi na kuongeza kuwa wahusika walichelewesha kutangaza matokeo (toka Agosti 1 hadi 4) na hatimaye kutangaza mbunge anayemaliza muda wake, Emmanuel Luhahula kuwa ndiye mshindi.
  Kahigi anasema akisimama na vyama vingine walishinikiza kurudia hesabu vituoni na kugundua kuwa Luhahula alikuwa na "kura hewa" kutoka matawi ya kata za Uyovu na Iyogelo ya Zamani. Bado CCM wilaya walimpitisha waliyetaka.
  Pingamizi la Kahigi wilayani lilitupwa. Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Siasa, hata hivyo, walibaki upande wake. Kamati ya siasa mkoa ilijadili pia na kukubali kuwa mshindi ni Kahigi.
  Kahigi anasimulia Kamati Kuu iliyokaa mjini Dodoma, ilivyompitisha lakini Halmashauri Kuu "ikapindua" uamuzi wa Kamati Kuu na ule wa wanachama na kumtangaza Luhahuka kuwa mgombea.
  Kwa kauli yake, "Safari ya kugeuka ilikuwa imeanza. Sababu ilikuwa wazi. Haki za namna mbili zilikuwa zimebakwa: Haki ya mopigakura kumchagua mtu anayemtaka na haki ya mgombea kuchaguliwa na watu wanaomtaka. Baada ya uamuzi kufanyika hapakuwa na kurudi nyuma."
  Profesa Kahigi siyo mgeni katika minyukano. Sisi tuliomwona katika uchanga wake na kufuatilia vitabu, makala, mashairi na mihadhara yake darasani, yeye ni mkondo usiozimwa – ama utavunja vizuizi au utatafuta upenyo mpya.
  Haongei sana lakini kauli yake inapenya. Ana tabia ya kudadisi mkubwa kwa mdogo na kirafiki. Kwa njia hii hukusanya lililoko nyoyoni mwa wengi.
  Makazi ya Prof. Kahigi – pale Kabuhima, Uyovu – ndiko chemchemi ya taarifa za kampeni. Kutoka hapa, siyo tu wanachama na viongozi wa Chadema, bali hata wanachama wa vyama vingine na wale wa CCM, wanapokea na kusambaza ujumbe wa anayeweza kuwa mbunge mpya kesho.
  Prof. Kahigi amekuwa mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM); Mkuu wa Idara ya Kiswahili, Mwenyekiti Mradi wa Vitabu vya Watoto Tanzania, Mhariri Mkuu wa majarida ya UTAFITI na KIOO CHA LUGHA; mhariri mkuu wa Umoja wa Waandishi wa Vitabu Tanzania na Mradi wa Lugha za Tanzania.
  Huyu ni mwandishi wa vitabu vipatavyo 10 vingi vikiwa vya fasishi na vinatumika katika shule na vyuo.
  Moja ya kazi za heshima ambayo haiwezi kufutika haraka ni kuwa Msimamizi na Mratibu wa Mradi wa Kimataifa wa kutafsiri kwa Kiswahili, progamu za kampyuta (Microsoft: Office and Windows).
  Hii ni kazi ya ukombozi iliyorahisisha matumizi ya kompyuta kwa wasiojua vema lugha nyingine isipokuwa Kiswahili.
  Mbali na UDSM, Kahigi amefanya ufundishaji, tathmini na utahini Chuo Kikuu Huria (Tanzania), Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Mt. Agustine, Mwanza.
  Vyuo vikuu vya nje ni pamoja na Michigan na Kalamazoo (Marekani), Leiden (Uholanzi), INALCO (Ufaransa); vyuo vikuu vya Moi, Nairobi na Kenyatta (Kenya) na Makerere (Uganda).
  Prof. Kahigi anasema, "Ndugu yangu, siendi kubahatisha. Nimesimama na walionita kugombe na walioniambia hama tutakufuata. Tunafanya kazi. Kama upepo hautabadilika, ushindi ni wetu." anasema kwa tabasamu.
   
 14. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Watu wamechoka CCM hawaamini kuwa mwisho wao umefika ya Zambia Malawi Kenya mwaka huu yanatokea Tanzania.
   
 15. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  :becky::becky:
   
 16. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  DAh yani raha tupu jamani, nilikuwa Tanesco Msaasni jana nafuatilia mita ya LUKU pale, Hata wafanyakazi wa Tanesco wameshajichokea wote wanailaani sana CCM, walikuwa wanapiga story za Halima Mdee alivyomwaga data kweye mkutano wa chadema kule Mezi beach na watu wakaahidi wakija CCm lazima wazomewe kwa sana tuuu.
   
 17. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jimbo la prof kahigi hilo, nilidhani yuko meatu. Hapo walie tu hawana chao. Chademaaaaaaaa!!!
   
 18. M

  MLEKWA Senior Member

  #18
  Sep 28, 2010
  Joined: Aug 18, 2007
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  LABDA tuanze kufanya utafiti wa Msajili w vyama vya siasa wa kuwa Upinzani utapata viti mia moja mwaka huu lets see if Opposition scoop 27 seats in Zanzibar and how many in Mainland.
  Bukombe, Kigoma mjini, jimbo la Zitto, Ndesamburo, Ubungo, may be one more for Kibaha Chadema), one more Mbeya , two More Arusha . Moshi TLP or Chadema and chadema two seats in Bukoba
  Tarime two seats. Bariadi area one seat. Kusini two seats lets put this list together so we can see the ppower of opposition in Tanzania
   
 19. E

  Eddie JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2010
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimeyapenda mashairi ya "Prof" Kahigi, he is good in that area
   
 20. M

  Msharika JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ee mungu utende kama maombi ya wana wako yalivyo. Tumeonewa sana bwana, wevi wameiba mali zetu watanzania, nawe ulimwahidi nabii habakuki kuwa utamlinda kama mboni ya jicho lako kwa kuwa anatenda yaliyo mema toka kwako.
  Amen.
   
Loading...