Kikwete azindua mradi wa Umeme uliojengwa na Kanisa Katoliki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete azindua mradi wa Umeme uliojengwa na Kanisa Katoliki

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Candid Scope, Nov 13, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]


  Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (kushoto) na aliye kulia kwa Mbunge Deo ni ambaye amevaa shati jeupe lenye roman collar ni Askofu wa jimbo katoliki la Njombe, Mhashamu Alfred Maluma, mara baada ya kutua mkao makuu ya tarafa ya Mawengi Ludewa kufungua mradi wa umeme ulioasisiwa na kuendeshwa na Kanisa Katoliki kupitia Parokia ya Madunda.


  [​IMG]  Aliye katikati ya Rais Kikwete na First lady Mama salma, ambaye ana shati jeupe lenye roman collar ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe Mhashamu Alfred Maluma. Ni mchezaji mzuri sana wa mpira wa miguu, na siku za nyuma kabla hajateuliwa Na Pope kuwa Askofu akiwa jimboni Njombe kwa kushirikiana na Padre Chaula mkurugenzi wa vijana, alianzisha timu ya mpira wa miguu kutokana na umoja wa vijana katoliki Njombe (UVIKANJO) timu ambayo ilipanda daraja hadi kucheza Ligi kuu na ilizoeleka kuitwa timu ya Baba Askofu, wakati huo askofu wa jimbo la Njombe alikuwa Askofu mstaafu Raymond Mwanyika. Timu hiyo ilisuasua wakati Mhashamu Alfred Maluma alipohamishiwa Peramiho Songea kuwa Rector (gombera) wa Serminari Kuu Peramiho ambako uteuzi wa kuwa askofu ulimkuta akiwa instructor wa Seminari hiyo baada ya kuhitimu chuo kikuu cha Rome, Italy, alikosoma Dr. Slaa.  RAIS KIKWETE APONGEZA KANISA KWA MRADI WA UMEME ,ATAKA WANANCHI KULIPA BILI KWA WAKATI


  RAIS Jakaya Kikwete amelipongeza kanisa la Romani Katoliki jimbo la Njombekwa kusaidia serikali kutatua tatizo la umeme kwa wakazi wa kijiji cha Mawengiwilaya ya Ludewa huku akiwataka wananchi kuendelea kutunza nyanzo vya maji ilikuwezesha maradi huo wa umeme wa gharana nafuu kwa wananchi kuendeleakusambazwa zaidi katika vijiji vingine vya wilaya ya Ludewa kwa msaada wa kankisa hilo.Akiwahutibia wananchi wa kata ya Mawengi mara baada ya kuzindua mradi wa umeme wa Lumama Electrical Asosoation jana ,Rais Kikwete alisema kuwa hatari ya maradi huu kufa itasababishwa na wananchi wenyewe wa kata hiyo iwapohawatatunza vyanzo vya maji na kusababisha mradi huo ambao unategemea zaidi maji ili kuendeshwa kushindwa kufanya kazi kwa uhakika .


  "Waswahili wanasema hivi kitunze kidumu ,kitunze kikutunze ….sasa nawapongeza mmeanzisha chombo chenu cha kusimamia mradi Lumama …..sasa nawaombeni Lumama iendelee kusitawi ili kuhakikisha mazingirahayaharibiwi na maji yanaendelea kuwepo kwani kama vyanzo vya maji vitaharibiwabasi mradi utakufa….pamoja na kuwa maji haya ni neema ya Mungu ila Mungu ametua maarifa ya kuvitawala vyanzo hivyo ili vidumu zaidi kwa kutumia kanunizinazotawala mazingira ili yaendelee kuwepo" Hivyo aliwataka wananchi kupitia umoja wao wa Lumama kuhakikisha wanatunzavyanzo vya maji kwa kutoharibu ovyo mazingira , kuchangamkia fursa hiyo kwakuingiza umeme katika nyumba zao huku akiwakumbusha kulipa bili kwa wakati . Aidha alisema kuwa serikali kupitia shirika lake la huduma ya umeme vijijiniitaendelea kusaidia mradi huo ili uweze kusonga mbele zaidi na kuwanufaishawananchi wengi .


  Rais Kikwete pia aliwahakikishia wananchi na wahisani hao kuwa serikaliimeendelea kutoa mchango wake katika mradi huo na itaendelea kuaunga mkonojitihada za kanisa hilo na wahisani wake kwa kusaidia fedha zaidi kwa awamu ya pili ili kuwezesha mradi huo kujitanua zaidi. Alisema kuwa hadi sasa makao makuu ya wilaya ya Ludewa kuna umeme wa Genereta ila bado mkakati wa serikali ni kuiunganisha wilaya hiyo ya Ludewa na umeme wa uhakika wa Gridi ya Taifa ambapo kazi hiyo kubwa mchakato wakeunaandaliwa. Pia alisema kuwa mkakati mwingine wa serikali ni kupeleka umeme wa gridi yaTaifa wenye uwezo wa KW 232 kutoka Makambako wilaya ya Njombe kuelekeaSongea mkoni Ruvuma na kuwa umeme huo utapoonza madaba ili kufikia KW 11na baada ya hapo wananchi wa vijiji vya Ndolela ,Mkongobaki, Shauri moyo ,Mavanga , Mndindi ,Lugarawa ,Mbwila,Mkiu ,Mlangali na Luana . Alisema kuwa wananchi wa kata hiyo ya Mawengi mbali ya kuwa na mradi huo wa umeme wa Lumama bado serikali ipo katika mchakato wa kupitisha umeme wa gridi ya Taifa utakaotokea katika kituo cha Madaba na kupitishwa katika maeneo yao kwenda makao makuu ya wilaya.


  Rais Kikwete kabla ya kufika katika kijiji hicho alizuiwa na wananchi wa kijiji cha Mlangali kata ya Mlangali ambao waliziba barabara na kulazimika kusimama kuwasikiliza na kujibu madai yao mbali mbali likiwemo na kuchelewa kufika kwa gari la wagonjwa ambao alipata kuwaahidi wakati wa kampeni ,tatizo la soko la Mahindi kusimama na kero ya maji ambapo aliwahakikishia kuwa malalamiko hayo yatafanyiwa kazi na majibu ya madai yao atampa mbunge wao Deo Filikunjombe iliawafikishie. "kwanza niwashukuru sana wananchi wa Ludewa kwa kukichagua chama cha mapinduzi (CCM) na kumpitisha mbunge wenu Deo Filikunjombe bila kupingwa ….sasa nawahakikishieni madai yenu yatafanyiwa kazi na kuhusu soko la mahindi wiki ijaya fedha za kununua mahindi zitakuja hapa"


  Kuhusu liganga na Mchuchuma Ludewa ,Rais Kikwete alisema kuwa sasa umefikawakati wa kuanza kutekeleza mradi huo kwa kampuni kutoka nchi ya China ambaokuanzia wiki ijayo wawekezaji hao watafika na kuanza kutekeleza mradi huo na ajira 8000 hivyo kuwataka vijana kuacha kuhoji juu ya maisha bora na badala yake kwenda kuomba kazi . Hata hivyo alisema barabara ya lami ya uhakika na Reli kwa ajili ya kupitisha makaa ya mawe na chuma kutoka wilaya ya Ludewa na kwenda kuyauza nchi za nje mkakati wake kuanza kuandaliwa . Alisema kuwa kila jambo lina wakati wake na kuwa sasa ni zamu ya wilaya ya Ludewa kubadilika kimaendeleo .  Awali mbunge wa jimbo hilo la Ludewa alimweleza Rais Kikwete kuwa pamoja naTaifa linasherekea miaka 50 ya Uhuru ila wakazi wa wilaya ya Ludewa wao baada ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika mwaka huu chini ya utawala wa RaisKikweye ndio wanapata uhuru wao baada ya kuwa na uhakika wa barabara ya lami na kuanza kuchimbwa kwa mradi wa Lingana na mchuchuma.

  Kwa upande wake meneja wa mradi wa umeme wa Lumama Alice Michelazziakisoma taarifa ya mradi huo mbele ya Rais Kikwete alisema kuwa mradi huo ulianza toka mwaka 1998 kwa kufanyiwa utafiti uliogharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 8.900. Hata hivyo alisema kuwa shughuli za mradi kwa sasa ni kujenga mtambo wa kuzalisha umeme wa kiasi cha KW 150 ambao tayari umekamilika mwaka 2010 nakuwa kanisa Katoliki jimbo la Njombe linatekeleza mradi huo kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la ACRA.

  Aliwataja wahisani wengine kuwa ni wizara ya mambo ya nje ya Italia,mkoa wa Lombaridia-Ilaty,Itervita,Foranzione Cariplo na umoja wa nchi za Ulaya
   
 2. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Wengine wanazalisha umeme, wengine wanataka kadhi.
   
 3. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  baada ya wananchi kuziba barabara ndiyo statement kama hizi zinatoka...! barabara isingezibwa??
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Hongera Kanisa Katoliki lakini tusifanye hii issue ni ya kidini ndugu zangu...

  Ni Tanzania kila mtu ana haki, yeah wanataka Kadhi lakini rais kasema hapana;

  Tufurahie huu Umeme utanufaisha wote hautajali Dini, Rangi, Kabila...
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Nov 13, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  RUZUKU - Kwa kodi za wananchi lakini! halafu watalipishwa bill za umeme.
   
 6. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #6
  Nov 13, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,074
  Likes Received: 7,562
  Trophy Points: 280
  You are a Great thinker bt unfortunately biased, it hurts to see this happening to a person with with vision and mind quality of your standards.
  Oh God!! What a loss!!!
   
 7. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #7
  Nov 13, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkuu umeisoma makala yote? Sasa unataka watumie umeme bure huo mradi utajiendeshaje?
  Jamani kwenye pongezi tutoeni pongezi...tuache tofauti zetu za kidini!
   
 8. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #8
  Nov 13, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,424
  Likes Received: 3,786
  Trophy Points: 280
  Huko ni kutafuta justification ya kushindwa kwenu. Mtabaki hivyo hivyo wakati wenzenu tunajenga mabenki yetu, mahospitali, mashule na vituo vya kuzalisha umeme... Kumbuka kuna cha Peramiho kule Songea
   
 9. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #9
  Nov 13, 2011
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Wengine wanataka mahakama badala ya kuhimiza watu waache makosa (dhambi) ili mahakama zifutwe maana nyingi zake hata hazitendi haki kwa kuwa zinaendeshwa binadam wale wale wenye mapungufu yale yale labda hata zaidi kuliko wanaowahukumu, ipo siku wataomba na gereza sasa kazi ya dini sijui itakuwa ipi naya serikali sijui itakuwa ipi. Wengine wanashusha maendeleo tu kama mvua mara chuo kukuu, leo mradi wa umeme kesho utasikia chuo cha ufundi stadi yaani ni full developee... yaani mpaka raha! Hongereni sana
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Nov 13, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkandara nawe umeanza kudonoa donoa hehehe haya mzee mwenzangu sikutegemea hili lakini kanyaga mafuta twende kaka .
   
 11. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #11
  Nov 13, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,973
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Brother Mkandara, don't let yourself down, please!
   
 12. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #12
  Nov 13, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280

  Uwe unasoma japo kidogo, haidhuru, check hapo chini.

   
 13. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #13
  Nov 13, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Kumbe suala la umeme likiachiwa sekta binafsi inawezekana...
   
 14. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #14
  Nov 13, 2011
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Everything is possible, haya yangewezekana siku nyingi na mengine mengi yangekuwa yamefanywa kama ukiritimba wa Tanesco ungeachwa zamani. Hata hivyo serikali yenyewe ina mipango mingi sana ya maana wamekalia maana kila kitu kikishafanyika watafisadi nini au wapi?
   
 15. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #15
  Nov 13, 2011
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kudos... Haya yanawezekana kama wawekezaji binafsi ambao kweli wanaijali jamii watafanya KWELI! Naomba na wamekezaji wengine waige mfano huu na wamwage umeme kila sehemu ili tuondokane na giza na vishawishi vingine vya richmond na dowans na 2....
   
 16. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #16
  Nov 13, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  kikwete bana wale wananchi wasingemsimamisha wasingepata uhakika wa soko la mahindi yao halafu kuna mahali ameongea kuhusu kutana huu mradi wa umeme lakini hata siku moja hiki kitu hakijawahi kuongelewa .....yaani ana usanii kweli huyu jamaa
   
 17. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #17
  Nov 13, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
   
 18. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #18
  Nov 13, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  [​IMG]

  Rais Kikwete akimshukuru Meneja wa Mradi wa Umeme wa Lumama Bi Alice Michelezi wa taasisi ya Acra baada ya kupokea risala yake aliyoitoa kwa Kiswahili fasaha na kumfurahisha kila mtu.
   
 19. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #19
  Nov 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Serikali yake IMELALA!
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Nov 13, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ndio makosa yanayofanywa kiutawala sasa iwe mfumokristu ama nini lakini swala la UMEME kuendeshwa na jumuiya za kiimani huoni kama serikali ina dini?.. mimi naomba mtu aje hapa anambie hasa maana ya kusema serikali haina dini ikiwa leo Umeme ambao serikali ina wizara yake wanashirikiana na kanisa kufungua nguvu hizo, tena akiwaagiza wananchi walipe bill za umeme huo mapema.
  Nipeni maana ya neno hili -Serikali haina dini - MAANA TU, halafu tuendelee..
   
Loading...