Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,180
- 664
Kikwete, Tanzania wavutia nje
Habari Zinazoshabihiana
Mwaka mmoja madarakani...Rais Kikwete kutoa tathmini leo 21.12.2006 [Soma]
Kikwete, Salma wamkuna mke wa Rais Bush 30.07.2007 [Soma]
Lumbanga awa Balozi Umoja wa Mataifa 02.02.2006 [Soma]
Na Godfrey Lutego, Paris
WAKATI nchini Tanzania baadhi ya watu na hasa wa vyama vya upinzani wakimdhihaki na kumpaka matope Rais Jakaya Kikwete, Wazungu na watu wa mataifa mengine wa Ulaya, Marekani, Afrika na nchi za Pasifiki na Karibeani, wamevutiwa naye na kumwona kama alama ya kiongozi wa Afrika kwa vitendo vyake, mwelekeo na anavyoendeleza heshima ya Tanzania tangu enzi za Mwalimu Julius Nyerere.
Hayo yalibainishwa hapa juzi usiku na watu mbalimbali walioshiriki hafla iliyoandaliwa na Tanzania baada ya mchana Rais Kikwete kuhutubia mkutano wa 36 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwenye makao makuu yake mjini hapa.
Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH), Bw. Theophilus Mlaki na Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, Profesa Peter Msolla ambao taasisi zao ziliandaa hafla hiyo, walisema walikuwa na kazi ya ziada kuwatuliza watu wa nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya waliofurika kwenye moja ya kumbi za UNESCO juzi usiku kwa hafla hiyo fupi, waliokuwa na shauku ya kumwona Rais Kikwete kwa karibu, baada ya kuvutiwa naye na hasa kwa hotuba nzuri aliyoitoa alipohutubia mkutano wa 34 wa UNESCO.
"Sasa tunaweza kupumua. Yaani ilikuwa kazi kuwatuliza watu. Ilibidi tuhangaike kuwauliza wasaidizi wake kama anakuja au la, kwani watu walikuwa na shauku ya kumwona," mmoja wa viongozi wa Wizara ya Elimu, Bw. Oliver Mhaiki aliwambia waandishi wa habari baada ya Rais Kikwete kuingia ukumbini na kufanya watu wachangamke, kila mmoja akisalimiana naye kwa kushikana mikono na kupiga naye picha kuonesha walivyovutiwa naye kutokana na uwezo mkubwa wa uongozi aliouonesha katika Afrika hadi sasa.
Naye Bw. Mlaki alisema Tanzania na Rais wake, imejizolea sifa kubwa zaidi kwa ilivyoandaa mambo yake katika mkutano wa mwaka huu wa UNESCO kiasi cha Wazungu kuona fahari na wengine kutangaza ukumbini pale kuwa nao ni Watanzania mmoja akiwa ni Bw. hubert Gijzen, raia wa Uholanzi ambaye sasa ni Mkurugenzi na Mwakilishi wa UNESCO Jakarta, Indonesia.
Mzungu huyo alisema aliwahi kuishi Tanzania miaka minne ya 90 akifundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Idara ya Fizikia na rafiki zake, Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Profesa Juma Kapuya.
"Nchi ni watu si miti. Tanzania ni nchi bwana. Watu wake wakarimu. Nimetembea nchi nyingi duniani lakini Tanzania ni ya pekee. Watu wake ni wakarimu sana. Niliwahi kuishi Mikocheni. Nitakuja tena Tanzania kesho, " Mzungu huyo aliwaambia waandishi wa habari waliokuwa kwenye ziara ya Rais Kikwete, akiungwa mkono na mwanamke mwingine wa kizungu ambaye ameolewa na Mtanzania.
Mwanamke huyo awali alihangaika kumtafuta Rais Kikwete apige naye picha alipoingia ukumbini na baadaye alisema alivutiwa sana naye mwaka juzi wakati wa kampeni na aliposhinda, alisema alitamani siku moja amwone kwa karibu, hivyo juzi alifurahi.
"Wakati wa kampeni nilikuwa naishi kisiwani Mayote na nilikuja Dar es Salaam. Nakumbuka kampeni zilisimama, kwa sababu ya msiba wa mgombea mwenza wa urais wa CHADEMA. Nilipata khanga ya 'Chagua CCM' yenye picha yake lakini sijui iko wapi ningependa nipate nyingine ya CCM. Naipenda CCM," aliwaambia waandishi na kusema ingewezekana, angekuwa mwanachama wa CCM.
Mbali ya Wazungu hao na wengine waliofurahishwa na hotuba ya Rais Kikwete iliyozungumzia mwelekeo wa Tanzania katika elimu na utamaduni na umuhimu na haja ya taasisi za kimataifa kama Umoja wa Mataifa (UN) na mashirika yake kama UNESCO kuzidi kusaidia jitihada za Serikali kuboresha elimu na huduma nyingine za jamii ukiwamo utamaduni, wengine walifurahishwa na jinsi Watanzania walivyokuwa wakicheza muziki wa taarab uliporomoshwa na kikundi cha Daruwesh Sound kinachomilikiwa na msanii wa zamani wa kundi la East Africa Melody, Bw. Mohammed Ahmed Daruwesh, Mzanzibari aliyeweka makazi yake Paris akisema anatafuta maisha huku.
Watu wa mataifa mengine ya Afrika ya Senegali, Mali, Uganda, Kenya, Afrika Kusini wengine wakiwa na bendera za nchi zao, waliujaza ukumbi ambako hafla ya Tanzania ilifanyikia na kuufanya uchangamke zaidi na wengi wakionekana kupiga picha na kuzungumza na Rais Kikwete kwa muda mrefu, kabla hajapiga picha na wasanii wa taarab na kuondoka.
Bw. Mlaki alisema wamekuwa katika mkutano wa UNESCO kama wataalamu wa mambo ya elimu na sayansi na teknolojia yeye na wenzake wa ujumbe wa Tanzania na wamekuwa wakiulizwa sana kuhusu habari za Rais Kikwete na anavyofuata nyayo za Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na kuendelea kusikika na kusikilizwa na mataifa ya nje na kuwa msemaji wa mataifa mengi ya Afrika.
Awali Rais Kikwete aliwashangaa Watanzania wanaoitukana nchi yao kwa kuwaambia Watanzania wanaoishi Roma, Italia, kuwa wasidhani Wazungu huwa wanawaona wana akili nyingi wanapoikandia nchi yao, bali wakiwapa kisogo huwa wanawang'ong'a kwa kuisema vibaya nchi yao wakati wao, Wazungu wanaiona ni nzuri na wanalilia kuja kuiona.
Aliwaambia Watanzania kuwa wale wanaowaambia Wazungu nchi zao za Afrika ni mbaya wanajitukanisha, kwani Wazungu hao hao baadaye huja kuzungumza na viongozi wa Serikali zao na kuzipa misaada, jambo linaloonesha kuwa wanawaheshimu na kuwaona kuwa nchi yao na uongozi wake unafaa.
Rais Kikwete alisema, Watanzania walioko nje ya nchi hawana budi kuipenda nchi yao na kuisaidia ipige hatua zaidi za maendeleo kwa kuleta wawekezaji, kampuni na asasi kuwekezea katika miradi mbalimbali ambayo wao wanaweza kuwa wabia na Serikali itawasaidia
Rais Kikwete jana jioni alitarajiwa kuzungumza na watanzania wanaoishi Ufaransa na leo anatarajiwa kurejea nyumbani.
Wakati huo huo, Rais Jakaya Kikwete amemteua Bw. Michael Mwanda, kuwa Katibu Mkuu Ikulu.
Uteuzi huo kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Bw. Phillemon Luhanjo kwa vyombo vya habari jana, unajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bibi Rose Lugembe, ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.
Taarifa hiyo ilisema uteuzi huo wa Bw. Mwanda ambaye kabla alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu unaanza rasmi leo.
http://www.dailynews-tsn.com/habarileo/index.php