Kikwete awaweka pabaya wakosoaji wa serikali yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete awaweka pabaya wakosoaji wa serikali yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jan 5, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  KAULI ya Rais Jakaya Kikwete ya kusema kuna watu wenye njama ovu za kulivuruga taifa, imetafsiriwa kuwa ni moja ya njia ambazo ametumia kuwakemea baadhi ya watu wa kada mbalimbali ambao katika miezi ya karibuni wamekuwa wakiukosoa uongozi wake

  Rais Kikwete pia aliwataka Watanzania kuwapuuza watu hao, ambao alieleza bayana kuwa ni wanasiasa, viongozi wa taasisi za kijamii "na hasa wa dini" kwa kuwa wataibuka na hoja hizo kwenye uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba, tena kwa nguvu kubwa zaidi.

  Uongozi wa Kikwete umejikuta ukifuatiliwa kwa karibu katika siku za karibuni, na hasa rais mwenyewe ambaye ameelezewa kuwa anasita kufanya maamuzi magumu, huku CCM ikipoteza mwelekeo na kutekwa na matajiri, na ilifikia wakati wakosoaji hao walikishauri chama hicho kisimteue Kikwete kugombea urais kama atashindwa kufanya maamuzi dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi.

  Awali Kikwete alisema kuwa angeshangaa kama watu hao ambao ni pamoja na mawaziri wa zamani Matheo Qares na Mussa Nkangaa, wasingesema hayo na kuahidi kwenda kuandaa majibu. Lakini katika salamu zake za kuaga mwaka na kuukaribisha Mwaka Mpya, rais alidokeza kuwa kuna watu ambao hauli zao zina mwelekeo wa kuvunja amani na mshikamano na kuwataka wananchi kuendelea kuwapuuza watu hao.

  Mwanasiasa mkongwe nchini, Bob Makan alisema kwamba kauli ya Kikwete imewalenga moja kwa moja wanasiasa wanaomkosoa, lakini akasema kwamba inawezekana wanafanya hivyo kwa kumsaidia na siyo kumharibia.

  Alimshauri Rais Kikwete kuwa mvumilivu katika hayo na kuyatumia kama kioo cha kuangalia mapungufu ya serikali yake kwani kuwapuuza itakuwa sawa na mtu kukimbia kivuli chake.

  "Kufanya hivyo ni sawa na kukimbia kivuli chake. Wanasiasa tupo kwa ajili ya kumkosoa na ndio wajibu wetu sidhani kama kuna mtu anayetaka kulivuruga taifa,"alisema Makani ambaye alistaafu uenyekiti wa Chadema.

  Muasisi na mwenyekiti wa kwanza wa Chadema, Edwin Mtei alisema Rais Kikwete asingeweza kuwasema wapinzani kwa sababu wamekuwa mstari wa mbele kumueleza mapungufu ya serikali yake kwa lengo la kujenga.

  Kwa mujibu wa Mtei, Rais Kikwete alilenga zaidi makundi yaliyomo ndani ya CCM kwa kuwa suala la ufisadi limewavuruga hadi wakaanza kunyoosheana vidole wenyewe kwa wenyewe.

  Moja ya kauli zilizowafanya wanasiasa hao kuhisi Rais Kikwete anawashambulia ni pale aliposema: "Taifa letu limeendelea kuwa moja na watu wake wameendelea kuwa wamoja, licha ya kuwepo kwa changamoto za hapa na pale zilizotokana na harakati za vyama vya siasa na kauli za baadhi ya wanasiasa na viongozi wa kijamii na hasa wa dini.

  "Wakati mwingine, matendo na kauli zao zimekuwa na mwelekeo wa kuwagawa Watanzania katika makundi yenye mifarakano na uhasama."

  Katika kuonyesha kwamba matendo na kauli hizo za 'wabaya' wake zimegonga ukuta, Rais Kikwete alisema: "Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza na kuwashukuru kwa dhati Watanzania wenzangu kwa ukomavu wa kisiasa, moyo wao wa uzalendo na busara waliyotumia ya kukataa kuwa wahanga wa njama hizo ovu."

  Rais Kikwete hakuishia hapo, bali aliwasifu Watanzania wengi kuwa upande wake akisema: "Mmechagua kufuata na kufanya mambo yenye maslahi kwa umoja, maendeleo na usalama wa taifa letu.

  Hakika ni moyo huo na ufahamu huo ndiyo umeliweka taifa letu kuwa moja na lenye amani na utulivu tulionao tangu uhuru wa Tanganyika, mapinduzi ya Zanzibar na baadaye Muungano mpaka leo."

  Hivyo akaendelea kuwasisitizia Watanzania wasirudi nyuma akiwahimiza: "Nawaomba ndugu zangu tushikilie msimamo huo hasa katika mwaka ujao wa uchaguzi ambapo haya yaliyofanywa mwaka huu yanaweza kufanywa maradufu."

  Rais hakumtaja mtu yeyote kwa jina wala kutaja kauli zilizotolewa na 'waovu hao wa taifa’ lakini baadhi ya wachambuzi wa siasa walisema kauli zake ni sehemu ya ahadi yake aliyoitoa uwanja wa ndege aliporejea kutoka ziara ndefu iliyohusisha nchi za Jamaica, Trinidad na Tobago, Cuba na Marekani na kuwaambia waandishi wa habari atajibu shutuma dhidi ya utawala wake zilizotolewa kwenye kongamano la kutimiza miaka 10 tangu kifo cha muasisi wa taifa la Tanzania, Julius Kambarage Nyerere.

  Ingawa kwenye kongamano hilo wajumbe walimlaumu rais pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kushindwa kuwakamata watuhumiwa wa ufisadi, kwenye salamu zake za mwaka mpya, Rais Kikwete aliisifu taasisi hiyo kwa kufanya kazi nzuri ambapo wengi wamefikishwa mahakamani na kuahidi kwamba serikali yake itaendelea kuwa nao bega kwa bega.

  "Nawapongeza sana wenzetu wa Jeshi la Polisi na Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini kwa kazi nzuri waliyoifanya. Nawaomba mwaka 2010 waongeze juhudi maradufu. Mimi naendelea kuwaahidi msaada na ushirikiano wangu na wa serikali," alisema Rais Kikwete kwenye sehemu ya salamu zake za mwaka mpya.

  Kikwete anajivunia rekodi ya serikali yake kuwafikisha mahakamani mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona, na katibu mkuu wa wizara, Grey Mgonja kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka na kuisababishia serikali hasara, pamoja na kesi kadhaa za wizi kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

  Lakini wachambuzi wanaona kuwa kashfa ya EPA inahusisha wanasiasa na wafanyabiashara vigogo wengi ambao hadi sasa hawajafikishwa mahakamani kwa makosa ya kuchota zaidi ya Sh133 bilioni.

  Pia wachambuzi wanaona kuwa rais ameshindwa kuighulikia kikamilifu kashfa ya utoaji zabuni ya ufuaji umeme wa dharura kwa kampuni Richmond Development, kutokana na kutowawajibisha watendaji walio kwenye mamlaka yake ambao walitajwa kwenye ripoti ya kamati teule ya Bunge na maazimio 23 ya chombo hicho cha wananchi.

  Suala la serikali ya Kikwete kutekeleza maazimio hayo limekuwa likipigwa danadana tangu mwaka juzi baada ya serikali kupewa miezi sita kulighulikia.

  Pamoja na Kikwete kutoeleza viongozi wa dini wamefanya uovu gani, lakini mijadala iliyotikisa taifa kutokana na kuwa na udini ni suala la Waislamu kutaka serikali itekeleza ilani ya chama tawala, yaani CCM kwa kuanzisha Mahakama ya Kadhi.

  Pia waraka wa Kanisa Katoliki uliotolewa kama mwongozo kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu ulisababisha mjadala mkubwa kutokana na wanasiasa kudai kuwa unaweza kuchochea tofauti za kidini.

  Waraka huo ulifuatiwa na mwingine uliotolewa na Shura ya Maimamu wa Kiislamu.

  CHANZO: MWANANCHI
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Kikwete akemea wanaotaka kuligawa taifa


  [​IMG]

  WATANZANIA wametakiwa kutowapa nafasi watu wanaotaka kuigawa nchi kwa dini, kabila, rangi, Bara na Visiwani au Unguja na Pemba na wasitoe mwanya kwa wanaotaka kuleta machafuko nchini...
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Ndio maana siku hizi nimeamua kutumia muda wangu mwingi kuwapa kizazi kipya historia yetu na michezo yetu, maana this is incredible kama sio a big joke!

  - Baada ya Mtandao wake kuwatisha sana wajumbe wa NEC na CC kwenye uchaguzi wa rais 2005 kwamba rais lazima awe Musilamu, leo wamegeuka na kuwa champions wa kukataa udini? Wamesahau ile article ya Sumaye, kwamba CCM wamekula nyama ya mtu akisema wazi jinsi udini ulivyotumiwa na walioko madarakani sasa hivi kule Chimwanga na hasa kumchafua Salim? Leo maji yamewafika shingoni kwa kushindwa kuongoza ndio wamejua kuhusu ubaya wa ukabila na udini ahhh this is a joke!

  - Ati kuna wanaotaka kuleta machafuko, masikini ya Mungu eti haelewi kwamba ni uongozi wake mbovu ndio unataka kutuletea machafuko, yale yale badala ya kujibu hoja ni kwa nini majambazi kama Lowassa na Rostam, na kina Ndulu yanaruhusiwa kuwa huru badala ya Segerea, yeye anatafuta scapegoat na hizi ngonjera?

  - Garademiti ngoja nirudi kwenye michezo na historia ya siasa yetu, enough! Mr. President do us a big favor resign utaona wananchi na taifa litakayokuwa na amani ni uongozi wako dhaifu ndio unatuletea matatizo hili taifa!

  Respect.

  FMEs!
   
 4. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Lakini si ndio ao hao wanaomuunga mkono? Anataka kulikata tawi la mti alilolikalia?

  Leka
   
 5. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Hawezi, mwoga sana!
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Ulishawahi kuona wapi ufalme unaosimama kwenye mihimili ya uongo? Mwisho wa siku uongo ikiwa ndio nguzo za utawala basi ni kuanguka kwa utawala huo.
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kweli leo naona mkuu FMES unekereka... Kama mbwai, mbwai au siyo?

  Watanzania wote tujiulize, toka lini tofali la barafu likajenga nyumba???
   
 8. Insurgent

  Insurgent JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 469
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hakuna mbaguzi kama Malecela. Huyu ni mtu ambaye aliwahi kuongea maneno ya kibaguzi dhidi ya Watanzania wengine ndani ya vikao vya Chama na Serikali.
   
 9. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Maneno gani? kwani mimi sio mjumbe wa hivyo vikao na hivyo ukinielewesha naweza kukuamini ,ila ukiishia hapo ntalazimika kuyapuuza maneno yako.
   
 10. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Wananchi wa Tanzania 70% ni bendera fuata upepo, Rais ni Jakaya Kiwkete sio Malecela alishastaafu longtime ago, kama ni mbaguzi wananchi wa Mtera watasema jinsi anavyowabagua, otherwise inathibitisha maneno ya Kikwete ya 70% na kufuata tu bila kujua substance!

  - Inafurahisha sana hasa kutoka kwa Great Thinker Bwa! ha! ah!

  Respect.


  FMEs!
   
 11. Insurgent

  Insurgent JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 469
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Great thinker like Nyerere hakukosea kumuita muhuni. Ataficha makucha yake ya ubaguzi sasa lakini rekodi za maneno yake ya kibaguzi zipo. Hii ni sababu iliyofanya aanguke 2005.

  Great thinker (to be?) historia ipo haiwezi kubadilishwa na maneno.
   
 12. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Bwana/Bibi au Ndugu Insurgent

  Tuletee maneno ya kibaguzi alosema Malecela.
  Kinyume na hapo, umekosa mashiko, period.
   
 13. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Kumuita waziri wako wa nje muhuni inajisema wazi kuhusu tabia zako wewe mwenyewe Nyerere, unless aliyeambiwa ni mmoja wa wale 70% anaosema Kikwete ndio inakwua tofauti! Bwa! ha! ha!

  - Alishastaafu longtime ago, ila wka vile ni mawazo yale yale ya 70%, ndio maana ni lazima kuendelea kulilia tulioambiwa ya kufuata upepo bila kufikiri for ourselves, samahani kuna tunaofikiri wenyewe maana sasa tuko huru!

  - Tatizo katika siasa sio kuanguka ila umeaangukia wapi, ukikosa urais ukaangukia umakamu wa CCM taifa bado unakubalika na busara za siasa kwamba ni mwanasiasa wa kweli, sio kama wale 80% waliomchagua Rais anayewaburuza sasa as if hawakumchagua! punguza nguvu katika hoja, badala yake weka hoja yenye nguvu!

  I mean ungetegemea uwe unalia kuhusu uongozi mbovu wa sasa lakini wewe unalilia walioshindwa urais, inaonyesha uwezo wako mkuu wa kufikiri unapoanzia na kuishia, pole sana!

  Respect.


  FMEs!
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  hakuna aliyesema maneno yana badilisha historia ila inaelekea wewe umekuja na agenda yako. Ishu hapa ni kuhusu JK. Kama una ishu ya Malecela anzishia thread yake. Sasa unataka watu wasitaje makosa ya JK kisha kuna mtu mwingine kafanya makosa hayo hayo? Au ndiyo yale yote mwizi akiiba hautaki akamatwe mpaka wezi waliomtangulia washikwe? be serious mkuu.
   
 15. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Inasemekana kuwa maamuzi hasa ya uteuzi katika nyadhifa mbalimbali Serikalini mara nyingi yanategemea 'ushauri' wa EL na RA.
  Hawa ndio vinara wa Serikali hii.

  As long as JK is in power, they are untouchables.
  Very irritating, very annoying, very sad.

  Get rid of JK, you'll get rid of EL and RA.

  Or better, let's send them to CHINA to face grand corruption charges!!!


  Grrrrrrr!!!!!!!
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Exactly hii yako mkuu ndio tunaita Great Thinking!

  Respect.


  FMEs!
   
 17. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #17
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mkuu Insurgent inawezekana kuna mengi wayajua chini ya uvungu ambayo wengine hatuwezi kuinama na kufika huko.Sasa do us a favor please mkuu utujuze aliyoyatamka Malecela kwenye vikao ambayo yalikuwa ni ya kibaguzi/kidini.

  Nilichosikia mimi ni kuwa kutokuelewana kwa Nyerere na Malecela kulianza pale wabunge wa G55 walipokomalia hoja ya serikali ya Tanganyika wakati Malecela akiwa waziri mkuu.Nyerere alimwita muhuni kwa madai kuwa alikuwa hamshauri vizuri Rais(Mwinyi),yeye na Kolimba.Sasa haya ni maoni ya Nyerere na si lazima wote tuyakubali kwavile kayasema Nyerere,isitoshe katika jambo la Muungano ambalo wote tunajua jinsi ulivyokuwa na hitilafu nyingi.

  Hoja nyingine kuwa alibadili dini na kuchukua hela za waarabu katika kampeni yake ya Urais 1995 sidhani kama ina mashiko sana.
   
 18. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Malecela anahusika vipi na hii thread, kwa nini msifungue inayomuhusu na mtuambie hao G55 walikuwa wanatumwa na nani hasa? Mbona hawakukamatwa na wakati sio siri walichokuwa wanakifanya ni uhaini?

  - Eti kwa sababu Chenney alimshauri vibaya Bush, kuhusu vita na Iraq basi Chenney anakuwa mhuni? Bwa! ha! ha! sometimes vinachekesha kweli

  - Sasa kwa kushindwa na siasa yake ya ujamaa aliyojishauri mwenyewe Mwalimu anakuwaje na hizi standards alizoziweka mwenyewe I mean anakuwa muhuni au what?

  - Bwa! ha! ha! inachekesha kweli kuambiwa bila kufikiri wenyewe! yaani ya 70%! kufuata tu upepo!

  Respect.


  FMEs!
   
 19. P

  PELE JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 229
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Msanii tu huyu! Yeye anataka kuona dhambi za wenzake tu ambazo si dhambi maana wanasema kweli kabisa kuhusu utendaji wake mbovu lakini dhambi zake za kushindwa kupambana na mafisadi na matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi hayaoni. Nakuunga mkono kabisa kwamba huyu anastahili kujiuzulu haraka sana.
   
 20. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Mkuu wacha tupige angle zote haina noma wala nini.Malecela alishamu endorse Kikwete ni sawa na kusema wanaopinga 2nd term ya Kikwete wanapingana na Malecela pia kwahiyo ni walewale tu.
  Na siyo siri Mwalimu alimwita Malecela muhuni.Sasa alikuwa na maana gani hatujui,labda angekuwa hai mwenyewe alifafanue hili ila sababu yake ipo.
   
Loading...