Elections 2010 Kikwete awateua Meghji na Nahodha ubunge

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Wabunge watatu (3) kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, kama ilivyorekebishwa na kupewa mamlaka ya kuteua Wabunge 10.

Wabunge walioteuliwa ni Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa na Ndugu Zakia Hamdan Meghji.

Rais atateua wengine waliosalia siku zijazo.

Rais Kikwete ameshawasilisha majina ya wateule hao kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda (Mb) kwa ajili ya hatua zipasazo.

MWISHO
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu.
Dodoma
17 Novemba, 2010
 
Ukistaajabia ya Firauni utayaona ya Kikwete. Hivi huyu Hamdani wa Nini sasa??? Au ndio asilimia 40% ya mtaji wa kuchakachua????? Watu wengine bwana, alafu eti ndio raisi wa Tz!! hakika huyu ni rais wa NEC.

Hongera Nahodha kwa kupoozwa maana najua uliambiwa umpishe mkulu Zenji na natarajia kwa ufupi wa mawazo ya Mkwere utapoozwa zaidi na kale ka tiketi ka ulaji bongo sijui ndo mnaitaga ka uwaziri vile eee!!!
 
Huu ni mwanzo wa kuwafahamu mawaziri wake wateule, ishu hapa ni kujua watapelekwa wizara gani, Mama mkwe wizara ya mali asili na Utalii.
 
Yaani pamoja na kashfa zote zilizomkabili huyo Zakia bado anampa nafasi katika serikali yake! Jamani jamani! Mimi siangalii hayo mengine, maana sio lazima amefikiri kwa misingi ya udini, lakini naona anaendekeza taabu alizokuwa tayari anaziweka kando. Zakia kule Mali Asili Zakia kule Wizara ya Fedha - madudu yale!!!!!!
 
Yaani pamoja na kashfa zote zilizomkabili huyo Zakia bado anampa nafasi katika serikali yake! Jamani jamani! Mimi siangalii hayo mengine, maana sio lazima amefikiri kwa misingi ya udini, lakini naona anaendekeza taabu alizokuwa tayari anaziweka kando. Zakia kule Mali Asili Zakia kule Wizara ya Fedha - madudu yale!!!!!!

Mvinyo wa Zamani na Hata Chupa ya Zamani.
 
Nchi inamaudhi hii!hii katiba lzm ibadilishwe kwnn so many viongozi jamani..mara viti maalum,mara cjui huu upupu gani.unecessary costs!nachukia sana!
 
Hao walochagulia ndo mawaziri watarajiwa.....:)
Ni kweli, hiyo ndio line up ya awali ya mawaziri kutoka Zanzibar, msimsahau Samia Suluhu Hassan ni mbunge na tayari alishaapishwa.
Hao wa leo, wataapishwa kesho kabla rais hajalihutubia Bunge, Baraza jipya kutangazwa Ijumaa saa 4 asubuhi toka viwanja vya Ikulu.

Kwa maneno mengine, wale vigogo wengine wote waliopoteza na waliokuwa wakisubiria huruma ya JK, imekula kwao.
 
Huyo Profesa Makame Mnyaa Mbarawa aligombea jimbo la Mkanyageni akashindwa na Mohamed Habib Mnyaa wa CUF, ambaye jana alijitoa kuwania Unaibu Spika kumpisha mgombea wa CCM, Job Ndugai. Duh, Mnyaa aliyekua Kamati ya Mwakyembe ya Richmond leo anamuunga mkono mgombea wa CCM?!!
 
Nahodha si mjumbe wa baraza la wawakilishi zanzibar? kama ni hivyo, atawezaje kuhudhuria vikao vyote viwili? Naomba mwenye ukweli wa hili atujuze
 
Yaani hapa hakuna ubishi, hawa ndio mawaziri watarajiwa, Jei Kei kafanya makusuidi hapa ili waingie bungeni mapema waapishwe then yeye next week akichagua baraza la mawaziri awaingize.........hii kazi kweli kweli
 
Huyo Profesa Makame Mnyaa Mbarawa aligombea jimbo la Mkanyageni akashindwa na Mohamed Habib Mnyaa wa CUF, ambaye jana alijitoa kuwania Unaibu Spika kumpisha mgombea wa CCM, Job Ndugai. Duh, Mnyaa aliyekua Kamati ya Mwakyembe ya Richmond leo anamuunga mkono mgombea wa CCM?!!

Halisi,

Prof. Mbarawa aligombea kupitia chama kipi huko Mkanyageni? Nataka kujua kama ni CUF na hivyo kuwa matokeo ya muafaka.

Hi ni dalili kutokea Zanzibar hakuna wabunge wa maana wa CCM wanaoweza kuwa mawaziri na hivyo kuanza kuteua.

Pia kwa watu toka Zanzibar lazima tutegemee kwa asilimia karibu 100 watakuwa Waislam hivyo sidhani kama tunahitaji hata kujadili juu ya dini zao.
 
Uteuzi wa JK umezingatia matatizo ya Zanzibar zaidi na wote ni Wazanzibari na kule jamani viongozi ni Waislamu. Hapo ndio maana nafasi 7 ni za bara na hajateua mtu na anaweza kuteua hata mwakani au keshokutwa kabla au wakati wa kutangaza baraza lake
 
Huu ni mwanzo wa kuwafahamu mawaziri wake wateule, ishu hapa ni kujua watapelekwa wizara gani, Mama mkwe wizara ya mali asili na Utalii.

Sielewi mkuu unavyosema Mama mkwe? Naomba unihabarishe nani kamuwowa nani?
 
Mweee JK bana ..sitashangaa nikiona meghji anakuwa waziri wa fedha
 
Tuache udini wana JF au la sivyo tutashindwa kujadili mambo muhimu ya kuendeleza taifa letu. Je unamjua Salim Ahmed Salim ni mwislam lakini CV yake inatufurahisha wote an dunia yote pamoja na kuwa wao Wanzanzibar Hawamtaki. Tusichokitaka hapa ni kuteua mradi kuteua watu ambo ni nonperformers kama huyo prof kafanya nini? Tupe Cv yake basi. Shida kubwa kwa JK ni kuteua ndugu zake kulipa fadhila hii ndiyo hatuitaki KABISAAAAA.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom