Elections 2010 Kikwete awateua Meghji na Nahodha ubunge

kumbe yupo na mkwe pia?? unamaanisha mama wa Salma kikwete??:nono:mbona umeniacha hapo kidogo
Huu ni mwanzo wa kuwafahamu mawaziri wake wateule, ishu hapa ni kujua watapelekwa wizara gani, Mama mkwe wizara ya mali asili na Utalii.
 
Ukistaajabia ya Firauni utayaona ya Kikwete. Hivi huyu Hamdani wa Nini sasa??? Au ndio asilimia 40% ya mtaji wa kuchakachua????? Watu wengine bwana, alafu eti ndio raisi wa Tz!! hakika huyu ni rais wa NEC.

Hongera Nahodha kwa kupoozwa maana najua uliambiwa umpishe mkulu Zenji na natarajia kwa ufupi wa mawazo ya Mkwere utapoozwa zaidi na kale ka tiketi ka ulaji bongo sijui ndo mnaitaga ka uwaziri vile eee!!!

ni mkwe wa rais
 
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT'S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Wabunge watatu (3) kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, kama ilivyorekebishwa na kupewa mamlaka ya kuteua Wabunge 10.

Wabunge walioteuliwa ni Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa na Ndugu Zakia Hamdan Meghji.

Rais atateua wengine waliosalia siku zijazo.

Rais Kikwete ameshawasilisha majina ya wateule hao kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda (Mb) kwa ajili ya hatua zipasazo.

MWISHO
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu.
Dodoma
17 Novemba, 2010

Hii ina maana hawa wateulewa watakuwa mawaziri katika serikali ya Muungano. Nilishangaa sana Shein alipomuacha Nahodha bila kumpa uwaziri kule Zanzibar kumbe walikuwa wameshafanya mawasiliona na Kikwete kwamba Nahodha atakuwa waziri kwenye serikali ya muungano. Mama Zakia yeye alipigwa chini baada ya EL kujuuzulu. Huyu mama alikuwa waziri wa fedha wakati wa sakata la EPA. Alishindwa kutoa taarifa sahihi kwa wananchi wakati ule kueleza jinsi hii kashfa ilitokea. Pia alichemsha sana kupandisha kodi ya petroli huku alikujua kwamba kufanya hivyo ni kupandisha bei ya kila kitu nchi na gharama ya maisha kwa ujumla. Sasa anarudi kufanya nini wakati aliprove failure?

Huyu Prof Makame mimi binafsi sina CV yake. Ila nadhani atakuwa ni mtu wa Dr Balal (makamu wa Rais). Hapa Jamaa anampa rafiki yake ulaji tu hakuna cha maana zaidi.
 
Huu ni mwanzo wa kuwafahamu mawaziri wake wateule, ishu hapa ni kujua watapelekwa wizara gani, Mama mkwe wizara ya mali asili na Utalii.
Hehehe mama mkwe! sasa JK atafanya lolote atakalo kwa shinikizo la mafisadi kwani hatarudi tena kwa wananchi kuwajibika after 5 years
 
Mie ninachojiuliza hivi wanataka znz iwe na wabunge wangapi? maana mpaka sasa eneo la watu milioni moja tayari linawakilishwa wabunge wasiopungua 70 kutoka kwenye vyama vyote.

Kwa kweli this is unfair hata kama huu muungano ungekuwa na thamani kiasi gani. Kinachoumiza zaidi watu wanapewa hizo nafasi si kwa vile wanastahili bali ni huruma/kipoozo kwa waliokataliwa na wananchi au kwa kuzuiwa nyazifa flani flani ambazo kimsingi wangestahili kuzipata katika mchakacho huru.

Kwa mtindo huu hii nchi haitafika kokote.

Hivi sasa nasubiri kuona L.Masha nae akirudishwa bungeni kwa kofia ya mkwere.
 
Wana JF nina uhakika katika hizo nafasi saba zilizosalia kati ya hizo kumi za kuteuliwa kati ya wafuatao hawatakosa:
1. L.Masha
2.B.Mramba
3.P.Marmo
4.S.Malechela
5.G.Mongela
6.M.Mbega
7.J.Mungai
8.A.Kandoro
9.S.Mashishanga

Endeleza list hapo chini
 
Prof Makame Mbarawa, Associate Professor at the Department of Mechanical Engineering, Faculty of Engineering and the Built Environment, recently returned to home soil after spending five months on sabbatical leave at the Combustion and Laser Diagnostic Laboratory of the Seoul National University in Korea. In the course of his visit to Korea, he also spent time working at the Combustion Laboratory of the Donkook University, also in Seoul.

Prof Mbarawa's main focus was to examine the effects of various gaseous additives on soot formation in laminar diffusion flames, using a laser light scattering/extinction technique. During his visit, he also read three papers at various international conferences.


Prof Mbarawa said he would like to use the knowledge he gained during the trip and compare it to the current teaching approaches in the Department, and identify and apply best practices. He added that he would also apply the quality of good supervision principles that he observed on postgraduate students.


The Seoul University's Mechanical and Aerospace Department comprises 1 300 students, 600 of whom are involved in postgraduate studies.


He explained that the research group he worked with had consisted of one post- doctorate, six doctorate and five master's students. The group met every week for two hours to discuss problems, find solutions and give feedback on the previous meeting's problems. This "buddy" approach between the students made a lasting impression on him, Prof Mbarawa added.


"I was amazed by the Korean people's dedication, culture and way of work. A typical workday during the week starts between 09:00 and 10:00 and lasts until 22:00. On Saturdays, the workday is up to 14:00.


He admitted that it was tricky to become accustomed to the chopsticks and highly spiced Korean dishes, but once he had adapted, he even enjoyed kimchi, a traditional Korean dish of fermented vegetables (mainly cabbage) seasoned with chili peppers and salt.
 
nawapa hongera sana waliochaguliwa... rais ameona umuhimu wao ... subirini kwanza amalizie.. waliobaki
 
Sasa nyie mi nashindwa kuelewa. Ungeteuliwa wewe sawa lakini mwingine maneni mengi . Tunachotakiwa kusema ni tusubiri tuone serikali yake na mafanikio na sio mti manyongo.
 
Halisi,

Prof. Mbarawa aligombea kupitia chama kipi huko Mkanyageni? Nataka kujua kama ni CUF na hivyo kuwa matokeo ya muafaka.

Hi ni dalili kutokea Zanzibar hakuna wabunge wa maana wa CCM wanaoweza kuwa mawaziri na hivyo kuanza kuteua.

Pia kwa watu toka Zanzibar lazima tutegemee kwa asilimia karibu 100 watakuwa Waislam hivyo sidhani kama tunahitaji hata kujadili juu ya dini zao.

Prof makame aligombea kupitia CCM mkanyageni. According to various websites. Prof Makeme ni Full professor of mechanical engineering. Anaonekana kuwa ni very strong professor in energy. Amefanya very strong publications kwenye strong databases kama sciencedirect.com (elsevier) pia kwenye other databases kama springer na nyinginezo. Ukijaribu kum-google utaona kazi zake nyingi.

Nafikiri hapa mkwere hajakosea sana. Ngoja tuone atatusaidiaje huko bungeni. Labda wanataka awe waziri.
 
nauliza tena kumbe hii JF ni wakatoliki(VIRISTO) kama CHADEMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!!????????
NI suali tu musiichakachue hii reply.
 
Prof makame aligombea kupitia CCM mkanyageni. According to various websites. Prof Makeme ni Full professor of mechanical engineering. Anaonekana kuwa ni very strong professor in energy. Amefanya very strong publications kwenye strong databases kama sciencedirect.com (elsevier) pia kwenye other databases kama springer na nyinginezo. Ukijaribu kum-google utaona kazi zake nyingi.

Nafikiri hapa mkwere hajakosea sana. Ngoja tuone atatusaidiaje huko bungeni. Labda wanataka awe waziri.
inavyoonekana kuna uwezekano wa Wizara ya Nishati na madini ikagawanywa ili huyu Prof. Apewe wizara ya Nishati ili kulinda siri za mafuta yaliyoko Zenji, wameona wakimuacha atapiga kelele nyingi kwani awa na data za kutosha. CCM nawaaminia
 
This is the manifestation of mediocrity of the man so called "the president of Tanzania". Hajui hata nia ya hicho kifungu kinachompa madaraka hayo. Ni imani yangu kuwa waliweka kifungu hicho ili kama rais anaona kuna mtu mwenye ujuzi wa kufanya mambo muhimu serikalini lakini hakupata nafasi ya kuwa mbunge ateuliwe ili aweze kufanya mambo hayo. Badala ya huyu mkwele kutafuta professionals kuwapa nafasi hizo anamteua mama mkwe kwanza. masihala haya jamani. Kuna haja ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye, lakini ni nani atamfunga paka kengere??
 
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Wabunge watatu (3) kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, kama ilivyorekebishwa na kupewa mamlaka ya kuteua Wabunge 10.

Wabunge walioteuliwa ni Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa na Ndugu Zakia Hamdan Meghji.

Rais atateua wengine waliosalia siku zijazo.

Rais Kikwete ameshawasilisha majina ya wateule hao kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda (Mb) kwa ajili ya hatua zipasazo.

MWISHO
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu.
Dodoma
17 Novemba, 2010


Kuna haja ya kutaja sababu za kuwateua, si kutaja tu kuwa wameteuliwa. Ni vizuri pia tukiangalia harufu ya urafiki na udini kwenye teuzi hizi, na ni vizuri tukijua kama zinafanyika kwa manufaa ya Taifa, Chama au dini.
 
nauliza tena kumbe hii JF ni wakatoliki(VIRISTO) kama CHADEMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!!????????
NI suali tu musiichakachue hii reply.

Hii website ni kwa ajili ya watu wote wenye maoni ya wazi kwa kuzingatia katiba ya nchi. hivyo katika jamvi hili kila mtu anafanya maamuzi nini au kitu gani anataka au yuko interested nacho kujadili, kama wewe utapenda dini wenzio watakuwepo, kama utaamua kujadili ujinga ujinga wenzio pia wapo, kama utaamua kujadili mambo ya kifisadi wenzio wapo, ukiamua kujadili mambo ya maendeleo wenzio pia wamo, ukiamua kujadili maisha ya watu wenzio pia wamo. kwa kifupi humu ndani kila kitu kinajadiliwa, fanya uamuzi unataka kujadili nini na kujifunza nini, yasiyokuhusu achana nao.
 
Back
Top Bottom