Kikwete awatema mawaziri wakongwe


M

Msharika

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Messages
937
Likes
4
Points
35
M

Msharika

JF-Expert Member
Joined May 15, 2009
937 4 35
RAIS Jakaya Kikwete leo ametangaza baraza jipya la mawaziri.

Katika baraza hilo, Rais Kikwete amewatema baadhi ya mawaziri na manaibu mawaziri ambao wameshika wadhifa huo kwa muda mrefu wakiwamo waliokuwa kwenye awamu za Serikali zilizopita pamoja na alioanza nao katika serikali yake ya awamu ya nne.

Katika baraza la mawaziri jipya alilolitangaza leo, Rais Kikwete aliyekuwa Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, aliyekuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk Maua Daftari, na aliyekuwa Naibu Waziri wa Miundombinu, Ezekiah Chibulunje.

Wengine waliotemwa ni aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msolla, na aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano Mohammed Seif Khatib.

Rais Kikwete pia amemuacha aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Jeremiah Sumari, aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati.

Wengine walioachwa walikuwa mawaziri kwenye baraza lililopita lakini kutokana na ama kushindwa katika kura za maoni wakati wa uchaguzi mkuu au katika uchaguzi wameshindwa kuingia kwenye baraza jipya kwa kuwa si wabunge.

Wanasiasa hao ni pamoja na aliyekuwa waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira),Dk Batilda Burian,aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Sera, Uratibu na Bunge, Philip Marmo , aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Aisha Kigoda, na aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Mwantumu Mahiza .

Wengine ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera , aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha , na aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Magreth Sitta.

Aidha mawaziri wengine waliotemwa ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, aliyekuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk James Wanyancha, na aliyekuwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Diodorus Kamala.


Source: HabariLeo | Kikwete awatema mawaziri wakongwe
 

Forum statistics

Threads 1,235,846
Members 474,742
Posts 29,238,336