Kikwete awataka wazee wa CCM wanyamaze. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete awataka wazee wa CCM wanyamaze.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiranja, Feb 27, 2009.

 1. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2009
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa mujibu wa taarifa ya habari iliyorushwa na kituo cha Star TV na Itv jioni ya leo, wamemwonyesha Rais Kikwete akiwataka wazee wa CCM waliokuwa madarakani wakati wao, wasiwe wanayumbisha utawala wake.

  Amesema kuwa wamekuwa wakikosoa kila anachofanya , wakati hata wao walipokuwa madarakani walishindwa kufanya hayo wanayotaka yafanyike leo na utawala wake.

  Akasema kuwa wamekuwa wakikosoa kila serikali yake inachofanya na kuwataka wajifunze kutoka kwa Kawawa ambaye hajakosoa.

  Aliyasema hayo akiwa Ikulu leo wakati wa sherehe za Kawawa kutimiza miaka 84, pamoja na uzinduzi wa kitabu cha maisha ya Kawawa.

  My take,
  Amechoshwa na kelele za wakina Butiku, Kitine et all ambao siku za karibuni wamekuwa wakosoaji wakubwa wa serikali yake?

  Kuna mpasuko ndani ya CCM ambao umeanza kujitokeza wazi kwa kauli hii?

  Mbona mtandao ulikuwa unakosoa utawala wa Mkapa na haswa Sumaye , mbona waliona kuwa ni sawa?
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hizo ni alama za utawala wa mabavu ngoja tuone mwisho wake ,yaani haambiliki ,aachiwe tu avuruge ama kweli madaraka yana ulevi wake ,lakini dawa ya watu hawa ambao Kikwete amesema mbona wengine walishindwa ni kuondolewa madarakani,Kikwete amedhihirisha kuwa kuna mambo waliopita hawakuweza kuyatekeleza na hivyo asilazimishwe serikali yake kuyatekeleza yaachwe kama yalivyo ,kwa maana ni urithi uliomo ndani ya CCM hivyo si viziri kubadilisha msimamo ni uleule huyu ni mwenzetu sasa hawa wanaoingilia utawala wa Kikwete wanamaana Kikwete si mwenzao ?

  Hawa wote ni samaki kwenye tenga moja la CCM ,ambalo limetoa samaki wa bovu kwa msemo huo wameoza wote ,hivyo dawa ni kuwatema na kuwaondoa kwenye utawala na uongozi wa kuingoza Tanzania.
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hakika nawaambia, wakinyamaza hawa, hata mawe yatapiga kelele
   
 4. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2009
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mr.President anapaswa kujua kuwa kama unaongoza wenzako wakikuonyesha ulipokosea njia sio kuwakemea ila ni kujisahihisha na sio kuwataka wakae kimya hata kama hawaridhiki na uongozi wako.

  Hii ni dalili mbaya kwa nchi kwani wasiopenda kukosolewa ni madikteta , sasa tunampango wa kuelekea huko?
   
 5. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hapa tupo ukurasa mmoja ila hataanza mpaka akianza cheza 2nd half kuanzia 2011. Nawaambia kuwa serikali inayonyamazisha wazalendo "pro bono publico" ipo tayari hata kutumia njia haramu kama ikishindwa njia halali yaani kujisahihisha . Na huu ni mwanzo wa njia haramu, wanasema kauli ya rais ni amri, sasa hawa jamaa wataanza kutishwa na vyombo vya dola
   
  Last edited: Feb 27, 2009
 6. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mtu ambaye hajiamini siku zote anafikiri ukosoaji wa utendaji wake ni:
  1. Personal attack
  2. Chuki binafsi
  3. Kejeli ya nafsi yake
  4. Wanamdharau
  In other words it's all about me, myself and I

  Lakini mtu mwenye hekima anajua ukosaji wowote:
  1. hulenga kumsaidia kujirekebisha na kuboresha utendaji wake
  2. Hujifunza mengi na kuzuia makosa siku za mbele
  3. Mara nyingi haimhusu yeye binafsi bali ni mtazamo wa mkosoaji
  4. huimarisha timu yake nzima

  in other words it is about I, you and US

  Maneno yake JK yameonyesha ya kuwa yeye ni sehemu ya kundi la kwanza pamoja na mawaziri wake woooote!
  Hebu tufanye kweli na tuchague viongozi wa kundi la 2 mwaka 2010...
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Susuviri,
  Sasa nimeelewa kwa nini Kingunge alinukuliwa juzi akisema maslahi ya chama ni muhimu kuliko maslahi ya taifa. Kumbe hawa mindset yao ni moja.
   
 8. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sasa waswahili tunaposema akioza mmoja wameoza wote ,ulifikiri ni utani ,unaemuona anakurupuka kuisifu CCM basi muogope kama mwenye marazi ya ukoma ,kuikana CCM inataka moyo wa kujitolea kulitetea Taifa na uelewe kuwa unaweza kukutwa na masaibu mengi sana hata kupoteza uhai si umesikia kauli zao za papo kwa papo ndivyo walivyo lakini wimbi ni kubwa na nakuhakikishieni tukishakuwa kitu kimoja basi hawataweza kuyazuia mageusi ya utawala bora unaoheshimu wengine ,maana unaweza ukawa na utawala bora nchi imetulia lakini huwaheshimu wengine unawafanya blalful ,ndio maana yake Utawala wa CCM unawafanya wengine wote hivyo ,wao ni wababe tu ,kila mmoja ni mkubwa kuliko mwenzake ,kila mmoja anajiona yupo juu ya sheria ,maana hata yule anaebeba kadi basi anajiona anaweza kufanya lolote kwa kuwa tu ana kadi ya CCM au ni mwanachama wa CCM ,wewe ukiendesha baiskeli haina taa polisi atakukamata akikuona ni mwanachama wa CCM atakuachia ,ndio maana yake Nchi imekwisha haribika bado kulipuka tu.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,442
  Trophy Points: 280
  Kikwete awaonya viongozi wastaafu

  Gloria Tesha
  Daily News; Friday,February 27, 2009 @20:30

  Rais Jakaya Kikwete amewaonya viongozi wa serikali wastaafu kuacha kuingilia serikali ya sasa, kwa kutoa kauli ‘vijiweni’ zinazoashiria kuwa serikali yake imeshindwa kiutendaji. Bila kutaja moja kwa moja wahusika, Rais Kikwete alisema viongozi hao wanasahau kuwa wanayoyasema hawakuyafanyia kazi wakati wa uongozi wao.

  Aliwataka viongozi hao kutambua kuwa kipindi chao cha kuwa madarakani kimekwisha na kazi kubwa walionayo ni kutoa ushauri kwa walioko madarakani, badala ya kuwa vikwazo katika juhudi za kuleta maendeleo. Rais alisema hayo Ikulu, Dar es Salaam jana, wakati akitoa hotuba baada ya kuzindua kitabu cha historia ya Rashidi Mfaume Kawawa kiitwacho ‘Simba wa Vita katika Historia ya Tanzania, Rashid Mfaume Kawawa’ kilichoandikwa na Dk. John Magotti.

  Magotti ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kivukoni, Dar es Salaam aliyefanya kazi na Kawawa kwa muda mrefu. Katika hafla hiyo iliyohusisha pia sherehe za kuzaliwa kwa Kawawa aliyetimiza miaka 83 jana, viongozi mbalimbali wastaafu na walioko madarakani walihudhuria.

  Miongoni mwao ni marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, mawaziri wakuu wastaafu, Jaji Joseph Warioba na John Malecela. Wengine ni Spika mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM – Bara), George Kahama, mke wa Baba wa Taifa, Maria Nyerere, Kingunge Ngombale-Mwiru, viongozi wa taasisi za serikali na zisizo za serikali, mashirika ya kimataifa na familia ya Kawawa.

  Rais Kikwete, ambaye alitumia hafla hiyo kuzungumzia viongozi hao wanaoikosoa serikali, alisema viongozi wengine wanakosa kutambua kuwa kila jambo lina wakati wake, hivyo wanajikuta wakitoa ‘kauli za vijiweni’ zinazokwamisha maendeleo.

  “Nakushukuru Mzee Kawawa, kwa kipindi chote cha kupanda na kushuka kwa uongozi wako, hukuwa kama baadhi ya viongozi wanaosahau wajibu wao wa kuwasaidia walioko madarakani na kujikuta wanapiga maneno vijiweni yasiyo mazuri,” alisema Kikwete na kuongeza: “Inashangaza mtu huyo enzi za kuwa madarakani yeye hayo hakuyaona na wala kuyafanya … wewe siku zote umekuwa ukishauri pale unapoona mambo hayaendi sawa na tunakushukuru sana Mzee wetu,” alisema Rais.


  Rais alisifu pia hatua ya kiongozi huyo mstaafu kukubali kuandikiwa kitabu cha historia yake, ambayo imebeba historia ya nchi kwa ujumla, kutokana na maudhui yake kuzingatia maisha ya ujana hadi uzee katika harakati za kisiasa, ukombozi wa nchi na utawala bora, ambacho Rais alisema kitasaidia vizazi vya baadaye lakini akakereka na tabia ya Watanzania kutopenda kusoma vitabu.

  “Mzee wangu, ninyi viongozi wenye historia mnapokubali enzi za uhai wenu kuandika yaliyokuwa nchini enzi hizo, inaeleweka kwa uhakika zaidi kuliko mwandishi akiandika kwa mtazamo wake yeye, maana atatulazimisha tuamini maneno yake,” alisema Rais na kuongeza: “Kinachonisikitisha zaidi ni tabia ya Watanzania kutosoma vitabu ‘our people don’t read’, wanasoma vichwa vya habari vya magazeti na wanaridhika kuwa wamesoma mpaka ndani, wanasahau kuwa elimu yote ipo vitabuni, sijui tufanyeje! Labda tuanzishe siku maalumu ya kusoma vitabu pengine itasaidia,” alisema Rais Kikwete.

  Katika hatua nyingine, alimpongeza Kawawa ambaye aliwahi kuwa Makamu wa Pili wa Rais enzi Mwalimu Nyerere akiwa Rais na pia Katibu Mkuu wa kwanza wa CCM, kwa kutimiza miaka 83 na kumwombea aishi zaidi ya miaka 100 ili nchi iendelee kufaidi hekima na ushauri wake. “Sikuombei uishi miaka mingine 83, lakini angalau ufike 100 na kitu hivi, ili wengine tuzidi kupata yaliyomo moyoni mwako kwa maslahi ya Taifa na hapa niseme tu kwamba kutokana na kutekeleza wajibu wako kwa unyenyekevu mkubwa, viongozi wa siasa hawana budi tuige kwako,” alisema Kikwete ambaye alitumia fursa hiyo pia kumpongeza mwandishi wa kitabu, Dk. Magotti.

  Rais aliagiza na kumhakikishia Kawawa kuwa kitabu hicho kitasambaa mitaani, shuleni na katika vyuo na kupewa muda wa kusomwa, ili kupanua wigo wa Watanzania kufahamu historia ya Taifa lao. Kwa upande wake, Kawawa katika hotuba yake aliishukuru CCM kwa kumlea, kwani mafanikio yake yanatokana na malezi ya chama hicho na kuwaonya viongozi kuacha tabia ya kutanguliza maslahi yao mbele na kusahau Taifa.

  “CCM imenilea na Mwalimu Nyerere amenisaidia kufika hapa leo, kamwe msikubali ubinafsi wa viongozi wachache uyumbushe CCM, tukumbuke wosia wa Nyerere (Baba wa Taifa) aliyosema (akanukuu) ‘bila CCM madhubuti, nchi itayumba’, migawanyiko isipewe nafasi miongoni mwenu,” alisema Kawawa. Kawawa, ambaye kitabu hicho kinamzungumzia kama shujaa wa vita dhidi ya Ukoloni na harakati za kuwakomboa wafanyakazi alizozifanya akiwa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi mwaka 1954, alisema uongozi si lelemama, kwani alibahatika mara ya kwanza kukutana na Mwalimu Nyerere wakati huo akiwa Waziri Mkuu mwaka 1956 kupitia vyama vya wafanyakazi.

  “Nilipeleka Sh 500 kama mchango wa shirikisho kumwezesha kuhudhuria mkutano … hiyo ikiwa sehemu ya michango ya nauli na kutoka hapo alinifahamu na siku 45 baada ya Uhuru wa Tanganyika (kabla ya Muungano) alijiuzulu uwaziri mkuu na kunipa mimi hayo madaraka,” alisema akieleza namna alivyoshuka na kupanda katika ulingo wa siasa.

  Aidha, Kawawa aliishukuru familia yake kwa kumwezesha kufanikisha kuandikwa kwa kitabu hicho chenye sura sita na kurasa 127 na kuwataka watoto na wajukuu wazidi kuelewana na kusikilizana bila kuingiliana na kuheshimu mipaka ya kila familia. Akizungumza na gazeti hili, Malecela alipongeza hatua ya kuandikwa kitabu cha kihistoria kuhusu Kawawa, ambaye alisema ni miongoni mwa hazina chache za Taifa na kushauri serikali iweke utaratibu wa kuwapeleka katika mafunzo ya uongozi angalau miezi sita, watu wanaochaguliwa kuwa viongozi ili wapigwe msasa.

  Dk. Magotti, ambaye alitumia miaka mitatu kuandaa na kuandika kitabu hicho, alimshukuru Kawawa kukubali historia yake iandikwe na kusema kuwa aliguswa kuandika kutokana na nafasi ya Kawawa katika Uhuru wa nchi na ustawi wa maendeleo ya Taifa pamoja na kufanya naye kazi kwa muda mrefu. Siku za hivi karibuni baadhi ya viongozi wastaafu wamekuwa wakiibuka ghafla na kuzungumza na waandishi wa habari, wakidai kuwa Serikali ya sasa imeshindwa na haina mwelekeo.

  Baadhi yao ni wale waliokuwa na nafasi nzuri enzi zao tangu awamu ya kwanza, tena wakiwa karibu na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na wengine walikuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri. Miongoni mwa wazungumzaji hao ni pamoja na Joseph Butiku, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere na mbunge wa zamani wa Makete, Hassy Kitine, ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa.

  Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, Dar es Salaam, Kitine alisema Taifa linakabiliwa na tatizo la uongozi, ambalo halijawahi kutokea katika historia ya nchi. Akasema nchi imekuwa ikiendeshwa kienyeji, kwa sababu ya kuporomoka kwa maadili ya uongozi.“Hali tuliyofikia si nzuri, tena niseme ni mbaya sana. Kuna kuporomoka kwa kiasi kikubwa kwa maadili ya uongozi. Na hii nawaambia, nchi haijawahi kuwa katika hali mbaya huko nyuma kama ilivyo sasa. Kwa hali tuliyofikia ni ngumu kurekebisha maadili ya uongozi.

  “Tatizo kubwa ni viongozi kukosa uadilifu. Kwanza ni ya viongozi wenyewe, pili ni wito, tatu ni utaifa. Haya ndiyo yalikuwapo wakati wa Mwalimu,” alikaririwa Dk. Kitine na vyombo vya habari. Alidai uteuzi mbaya wa viongozi hususan wa mawaziri, umechangia kupatikana kwa viongozi wasio waadilifu, wengi wao wakijihusisha na vitendo vya rushwa.
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hizi hadithi za alifu ulelaulela haziishi ,ila mpka utawala huu mbovu utakapo ondolewa madarakani kwa njia sahihi kabisa ya kura , tunataka mabadiliko ya katiba ,mabadiliko ya tume ya uchaguzi mabadiko ya mahakama ,mabadiliko ya nguvu alizokuwa nazo Raisi ,tunataka viongozi wasiwe juu ya sheria ,hizo longolongo za kutoingiliwa zimejibanza katika mambo makuu hayo ndio maana Mheshimiwa Kikwete ameweza kutoa kauli yake hiyo au naweza kusema CCM imeweza kutoa kauli hiyo ya kutoingiliwa ,wanao ikosoa serikali hawaikosoi kama wao ni wananchama bali wanaikosoa kama wao ni wananchi wa kawaida ambao baada ya kukaa uraiani wamelionja joto ya jiwe na kuona kuna nini huku uraiani kuna tabu na shida zake,ukiwa huko juu na ndani ya utawala mengi huyaoni yanakupita na tabu ya kuyaondoa na kuyadai pia inakuwa mbinde hivyo system nzima inahitaji mabadiliko ili asiwepo asieweza kukosolewa au kufikishwa kwenye mkondo wa sheria pindipo akichezea jukumu alilopewa.

  Mabadiliko makubwa yanahitajika Tanzania ili kiongozi asione anaingiliwa ,kutokufanyika kwa mabadiliko hayo ndiko kunakomfanya CCM chini ya kikwete na utawala wake waone wamevamiwa katika kuiongoza Tanzania ,kwani sivyo ilivyokuwa wakati wa Chama kimoja ukisema ndio au hapana kunakuwa hamna tofauti ,ndio ni kwa mtawala na hapana ispokuwa mtawala ,hivyo wananchi wanakuwa wafuataji tu wanakoongozwa ndio huko huko hakuna kuhoji ?

  Nchi inahitaji mabadiliko tena haraka sana ,tuweke pembeni kelele za mafisadi na kuishukia serikali na kuilazimisha kufanywe mabadilko ya haraka kuhusiana na katiba na mambo mingine muhimu ,ili miaka ijayo kusiwe na kiburi kwa walioko madarakani na kwafanya wananchi kama watumwa wao.
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,200
  Trophy Points: 280
  Kwamba Kikwete anaweza kwa bashasha zote kutamka maneno haya yasiyoyumkinika siyo tu inatisha na kutaka kutapisha, bali pia inatuonyesha jinsi gani mawazo ya kimangimeza na kisultani yalivyomkaa Kikwete.

  Ukweli kwamba rais wetu ameweza kutoa maneno yanayopingana na falsafa ya uhuru wa kujieleza unaonyesha jinsi gani Kikwete na CCM wasivyo kuwa na heshima kwa demokrasia.

  Kama Kikwete anaweza kuwaambia wazee wa CCM wenye taadhima kubwa maneno haya, je vijana wasio na bango la CCM wala majina atawafanyaje?

  Kwa muda mrefu ninaona jinsi gani rais Kikwete anavyolewa madaraka kibabe na kukosa kiasi, kujisetiri, uerevu wa mahusiano ya jumuiya na kuonyesha utupu wake katika matamshi anayotoa.

  Kama anasema hivi katika matamshi wazi, sijui huko ndani ya vikao anatukanaje!
   
 12. C

  Chuma JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Binafsi namuunga Mkono Kikwete kwa hili...Hawa wastaafu wakae kimya, kwani wakati wao uozo ulikuwepo hawakufanya lolote...na wao walikuwa mstari wa mbele ktk ufisadi.

  Kama wapo serious kushauri sio kukaa vijiweni na kuropoka, wao wana access na watu ambao wapo ktk government na pia wana uwezo kuomba kukutana na Rais face to face kuliko kukaa na waandishi na kujifanya wasafi. na huo kwa sura ya Nje unaaonekana mpinzani badala ya kuwa unataka kushauri. Wadau lazima tujue kila mmoja na nafasi yake, Hawa wastaafu wanataka kujifanya Nyerere wakati wa Mzee Mwinyi...

  na Tena JK katumia kauli njema, otherwise ni kuwatia Adabu!!!
   
 13. J

  JokaKuu Platinum Member

  #13
  Feb 27, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,146
  Trophy Points: 280
  ..kuna kitabu kingine kinachohusu maisha ya MZEE RASHIDI KAWAWA kimeandikwa na mwandishi ABEID SAKARA.
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Waandike vitabu wakati Chama chao kimeshakaa pembeni ,kuandika vitabu huu si wakati wake, zaidi ni kutaka kujikosha tu,halafu hii nchi hivi sasa iko katika mfumo wa vyama vingi Kawawa ni CCM ,itawezekanaje kitabu chake kipelekwe kwenye mashule ya serikali kama wanataka wasome wapeleke kwenye matawi yao ya CCM waweke kwenye libraru zao na sio kwenye vyombo vya serikali ,maana hata raisi akiondoka basi hata zile picha zake za kwenye ukuta nazo huondolewa ,ila sijui zinapelekwa wapi ,maana za wingine zinakuwa hata kuuzika haziuziki.

  Mambo haya ya kusema vitabu vienezwe kwenye mashule ni kutaka kuturudisha kwenye colonization ya CCM , fedha ya kueneza vitabu hivyo serikali hii itazipata lakini kuwapatia vitabu vya elimu wanafunzi inashindwa na kusababisha kitabu kimoja kusomwa na watu wa nne kwenye deski moja ,tunaelekea wapi ?
   
 15. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2009
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 80
  kuna usemi usemao " nyani mzee kakwepa mishale mingi".sasa nyani mzee akimwambia nyani kijana njia hii si nzuri,usipite huko naye akagoma kushauriwa kwa kujifanya mjuaji basi mwacheni akadungwe na hiyo mishale.asiye sikia la mkuu ..... Ila yote katika yote ni vizuri kupokea ushauri wa wazee then uchuje na kufanyia kazi yale yaliyo mazuri.sio kuwakemea. hapa tukisema ni utovu wa nidhamu je????????
   
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  Feb 28, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  JokaKuu,
  Nimeshangaa hichi kitabu cha Maggoti ni kurasa 127 tu baada ya kukiandika miaka mitatu. Ningependa kukiona hicho cha Abeid Sakara, kama unajua jinsi ya kukipata tafadhali ni PM
   
 17. O

  Ogah JF-Expert Member

  #17
  Feb 28, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Ni vema kuwa na kumbukumbu hizi....tena tukizipata wakati hawa wazee watu angali hai....Kudos kwa waandishi
   
 18. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #18
  Feb 28, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  kikwete asitumie vitisho kunyamazisha wazee kukosoa utawala wake. Kubwa wanachosema hapa ni kukosa uadilifu kwa viongozi wa umma. sasa anataka kuwanyamazisha kwa nini? wazee hawa walivyokuwa madarakani walishatimiza wajibu wao kwa kuwa waadilifu, kuheshimu mali za umma, kuweka mbele maslahi ya umma badala ya maslahi binafsi, waliheshimu wananchi, na kulinda rasilimali za taifa kwa manufaa ya umma. leo hii wanapoona nchi inafanywa kama shamba la bibi inawauma sana, hawawezi kuvumilia kuona rasilimali kama madini, samaki, mashirika ya umma, misitu na ardhi ya wananchi ikitumiwa kwa maslahi ya viongozi wachache. Viongozi wakuteuliwa kienyeji kama EL, wakuu kama kina Mnali, na yule mama wa Iringa vinapoteza Morali ya wazalendo kuongeza juhudi za kufanya kazi kwa maslahi ya taifa. Vijana wakikosoa utendaji wa CCM, waliomo ndani ya CCM wananyamazishwa kwa kutishwa. Waliomo nje ya CCM wanaambiwa watakufa na kuiacha CCM ( Refer Chiligati to Zitto). Sasa na Kikwete unanyamazisha wazee. Akina nani waseme? Sasa wasemaji wakuu wawe Rostam, Lowassa, Masha, Karamagi, Chenge, ( a.k.a wavuruga nchi) si ndio?
   
 19. c

  care4all Senior Member

  #19
  Feb 28, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kikwete kakemea tu lakini nyerere alikuwa anawaweka vizuizini watu wa aina hiyo, kuna wanasiasa wengine hata huduriki kuua wanasiasa wenzao kwa sababu kama hizo....kifupi siasa ni mchezo mchafu.

  Nawaona CCM ni kama mlevi anayetembea huku akiyumba, upinzani ni kama mlevi anayeendelea kunywa akiwa amekaa akimnyooshea CCM kidole na kumwambia "mlevi wewe huwezi hata tembea", huenda yule mlevi aliyekaa akasimama na kuondoka mwendo mdundo ama akaanguka kabisa....kuna kuramba dume au garasa hapo.Binafsi sina imani na wote mpaka watakapo badirika. Vyama vyote vina migogoro na mingi inatokana na masilahi binafsi wala siyo taifa, waongo wengi, wezi wa kuaminiwa wamekimbilia kwenye siasa....mpinzani na mpiganaji wa kweli wa taifa hili ni mwananchi mwenyewe. ukibahatika kupata uongozi unaoruhusu mtu ku express mawazo yake hata kwa 10% basi itumie nafasi hiyo ipasavyo kama wanakupa nafasi basi lalamika sana , andamana, goma, tishia kunyima kura na wewe mwenyewe jitume juu ya maisha yako. Lakini usiweke rehani future yako kwa wanasiasa hasa hawa wakibongo utakufa masikini wewe na kizazi chako. Alipita JKN, AHM, BWM atapita JK na atakuja unayemtaka wewe lakini utabakia kama ulivyo ama hata kuwa masikini zaidi ya ulivyo sasa kama hupo makini. Achana na biashara ya kununua bata kwenye viroba itakula kwako ndugu.
   
 20. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #20
  Feb 28, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mie najua hawezi kumnyamazisha Mzee/Bibi yetu anayemumuna-yaani bubu anayependelea kusema?

  Hii inadhihirisha makundi yaliyomo!

  Ya wazee, Ya Sistemu, Ya A, Ya B, Ya C, na sie tunaokuja, A+ CCM, tuna A nyingi na kupenda sisiemu lakini hatupendi siasa za Ubaguzi, za sistemu, za falsafa, za Upendeleo, za Mafisadi, za Kisiasa-Kisasi, na Makundi mengi tu ya Kisiasa za kwetu!

  Toka lini wazee wananyamazishwa? Hii culture tunayoifuata...mhh:(

  Mie nilijaribu(usiniulize)!:D:mad:


  Tunaweza kwenda na wakati, siasa mbadala-hii haimanishi tukumbatie hayo juu kama majalada/vijalada!

  Tunaweza kuwa na yote hapo juu na kuwa Watanzania, Wanasiasa wa karne ya ishirini na ishirini na moja-Historia itanena- Lakini hatuwezi/siwezi kukaa na kukubali kuona ubaguzi wa kisiasa na wa kijamii unaonyemelea nyika zetu!
  Tutafika...!
   
  Last edited: Feb 28, 2009
Loading...