Kikwete awapiga mkwara mabalozi uchaguzi 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete awapiga mkwara mabalozi uchaguzi 2010

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GAMBLER, Jan 9, 2010.

 1. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2010
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]Raisi Jakaya Kikwete ambaye amewaonya mabalozi kutothubutu kujihusisha na chama chochote cha siasa wakati wa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwakani[​IMG]Ramadhan Semtawa

  RAIS Jakaya Kikwete jana alitumia hafla ya kukaribisha mwaka 2010 kwa kuwaonya mabalozi kutothubutu kujihusisha na chama chochote cha siasa wakati wa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25.

  Katika hafla ya kawaida ya kusherehekea Mwaka Mpya na mabalozi kutoka nchi mbalimbali, Rais Kikwete alisema kitendo chochote cha mabalozi hao kushabikia chama chochote kitashughulikiwa vema na serikali yake.

  "Tunawashukuru sana nyote ambao mmekuwa mkisaidia mchakato wa programu za uchaguzi chini ya Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)," rais alianza kurusha kombora hilo.

  Kitu ambacho Tanzania isingependa kuona, alisema Rais Kikwete, ni miongoni mwa mabalozi kugeuka kuwa wanachama wa vyama fulani kwa kuvishabikia na kulazimisha kuchagulia Watanzania mtu au chama fulani.

  "Tafadhali jizuieni kufanya hivyo," alionya rais.

  "Mkifanya hivyo mtakuwa mmevuka hatua ya mamlaka yenu na hiyo itakuwa ni ukiukaji wa maadili ya kazi za kidiplomasia."

  Kikwete, ambaye anatarajiwa kugombea urais kwa kipindi kingine cha miaka mitano kupitia CCM, alisisitiza kwamba licha ya heshima kubwa kwa wanadiplomasia hao lakini kitendo hicho kitashughulikiwa kwa nguvu.

  Ni kwa nadra sana mabalozi huingilia siasa za ndani na hasa kwenye uchaguzi, lakini iwapo misingi ya kidemokrasia inakiukwa kwenye uchaguzi au uendeshaji nchi, mabalozi hutoa taarifa kwa nchi zao ambazo huamua kuiweka serikali kwenye hali ngumu kifedha, hasa nchi wahisani ambazo huamua kuzuia fedha zao wanazoahidi kwenye bajeti ya nchi husika.

  Mkuu huyo wa nchi aliongeza kwamba serikali imepanga kuhakikisha uchaguzi huo wa Oktoba unakuwa huru na haki ukitawaliwa na amani na utulivu.

  Kwa mujibu wa rais, hakuna mtu atakosa haki yake ya kupiga kura au kupigiwa kura na kusisitiza kwamba hata uchaguzi wa serikali za mitaa wa Oktoba mwaka jana ulikuwa huru na haki.

  Kuhusu athari za mvua zinazoendelea kunyesha, rais alisema uharibifu wa miundombinu, na hasa madaraja unahitaji Sh6.7 bilioni ambazo serikali inategemea kuzinyofoa kwenye fedha zilizotengwa kwa wizara mbalimbali.

  Balozi Juma Mpango, akizungumza kwa niaba ya ujumbe wa mabalozi nchini, alisema wamekuwa wakiridhishwa kuona Tanzania imekuwa nchi ya amani na utulivu na utekelezaji mzuri wa mwafaka visiwani Zanzibar kati ya CUF na CCM.

  Mpango, ambaye ni kiongozi wa mabalozi nchini, alisema nchi hizo zimekuwa zikifuatilia kwa karibu mazungumzo kati ya katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad na Rais Aman Abeid Karume, hivyo wataendelea kuunga mkono juhudi hizo.

  Kwa mujibu wa mpango, mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini pia wanaridhishwa na hatua zinazochukuliwa na serikali katika kuimarisha utawala bora na kupambana na rushwa. Jana Rais Kikwete aliwaalika mabalozi wote wanaowakilisha nchi zao nchini kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya 2010, hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  [​IMG]
   
 2. S

  SIYAMMOJA New Member

  #2
  Jan 9, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nina suari iwapo zanzibar hawato kuwa na uchaguzi kama mambo ya huko ya navyo onyesha je na sisi huki tanganyika si ndo tushakuwa na serekali yetu baada ya miaka karibu 46 ..!!!
  Nyinyi wenzangu wadau mna onaje ?
   
 3. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #3
  Jan 10, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Balozi wa Marekani,Balozi wa Uingereza,Balozi wa Urusi,Balozi wa China; wakimpigia debe Kikwete,Kikwete atawazuia?
   
 4. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #4
  Jan 10, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Message ya Mwaka Mpya inapaswa kuwa moja tu,kwamba watu tusameheane kwa makosa tuliyofanya katika mwaka uliopita. Kwamba,kama wapo watu ambao unaona mmefarakana katika mwaka uliopita na inabidi mshirikiane tena katika mwaka huu,basi jitihada zifanyike kutibu matatizo yaliyotokea,kufanya marekebisho. Huu ndio wakati wa New Year Resolutions,'Nitawacha kuvuta sigara,Nitafanya mazoezi zaidi,Nitapunguza kula sana,Nitapunguza kunywa pombe,''na mambo mengine mengi ambayo watu wanataka kufanya kujitesa. Haya mambo yote hayana maana.Jambo muhimu ni kuondoa tu fitina,na choko choko katika maisha ya kila siku,na siyo kufikiria jinsi ya kuutesa mwili,kwa sababu matatizo ya ufisadi yasipoondolewa,mwisho wake,hatimaye,itakuwa ni mateso ya mwili,maisha mabaya kwa kila Mtanzania.
  .
   
 5. A

  August JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,510
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Tukiwa na shida iwe njaa, mafuriko nk , tunawakumbuka mabalozi /donors, ikiwa ni hela za kuiba na matumizi mabaya oh! we are independent country tuachie tufanye tunavyo taka, ndege ya raisi tunataka, radar, nyumba ya governor, airport mpya, umeme wa Diesel badala ya Gas nk nk. kuongeza vyeo ili wajomba nao wapate kazi nk nk
   
Loading...