Kikwete 'awapakazia' viongozi wa dini biashara ya madawa ya kulevya

hapa ndipo makanisa yanapokuwa na nguvu. ccm ikitishwa kidogo na makanisa yanakuwa taharuki. mbona huwa kimya kwa waislam?
Kwasababu hawaumiumi maneno banaaaaa, penye kweli tunataka kweli isemwe si ulete mipasho, tatizo lenu huwa mnasalimiana kwa mapozi mkimaliza hapo mnaanza kutetana kwenye maulidi...nawajua sana nyie, haya igeni mfano sasa hapo!!! They are true leaders.
 
Mbona matamko ya bakwata huwa hayajibiwi wala kushughulikiwa?Mhhh ccm inakumbatia makanisa sana!
 
JK ajifunze kusoma kilicho andikwa, na sio kutamka anavojisikia!!!!!!!!!! Hicho ni kimeo kwake
 
hivi huyo jk ana taarifa na hiyo taarifa ya kibanga?

nchi hii bana... kama unajua utachemka kwenye maongezi yako bora ukaandika then ukasoma kila kitu kama kilivyoandikwa.. tunatofautiana uwezo wa kuongea jamani
 
Kama hii kweli ni taarifa kutoka ikulu basi tuna kazi!!!!!!!!! Du haya mambo mengine bora kuongea tu kuliko kuyaweka kimaaandishi!!!!!!!
 
kwahiyo waislam wanahitaji kusemewa na Wakristo ? Acha kutudhalisha .
Hajawadhalilisha kasema ukweli Mpwa, si unaona hata mambo yenu mnavyokurupuka, haya kasema ukweli wewe unasema kwadhalilisha, usiwe hivyo, ukiambiwa ukweli utasaidia kuku-reshape
 
Was it necessary kwa Rais kwenda kuongelea hayo mapungufu kwenye sherehe za kisimikwa Askofu?. Au ni mwendelezo wa semina elekezi? Sina shaka hata kidogo kwamba viongozi wa dini ni binadamu na kwa hiyo wana mapungufu kama binadamu wengine. Pia viongozi wa dini hawako juu ya sheria. Sasa hii tabia ya kusutana inatoka wapi wakati kama nchi tuna taratibu na kanuni za kukabiliana na 'mapungufu' au makosa ndani ya jamii yetu?

Pia reaction ya kauli ya Kikwete siyo ni kwa sababu ya kauli yake ya Mbinga - ila ni kutokana na mlolongo au tabia ya Raisi 'kulalamika' na 'kuvizia' wale anawaona ni kero. Hivi kama hakualikwa Mbinga angeendelea kukaa kimya? Na kazi ya Rais ni nini? Hivi aliapa kufanya nini? Na kauli kama ya huyu mwandishi wake (Premji) kwamba "anayejishuku ajisalimishe mwenyewe" ni udhaifu mkubwa! Kwamba mwizi, muuwaji, mbakaji na muhalifu yeyote akijishuku basi ajisalimishe mwenyewe? wapi? Kwa ni tunawalipa polisi? au kazi ya polisi ni kuwakamata Mbowe na Magdalena Sakaya?

Kila kukicha kuna kila dalali ya Kikwete to be the worst president ever to hold office in Tanzania. Very devisive individual and shockingly disingenuous!
 
Si vema kutufanya wengine hatuchambui mambo, Hebu chukua tena muda wako usome hii ili angalau uone umejikwaa wapi katika uchambuzi wako;

haya karibu;
Rais Jakaya Kikwete, ametangaza kuwa ataunda chombo maalum cha kupambana na ongezeko kubwa la tatizo kubwa la biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Aidha, Rais Kikwete amewaomba viongozi wa dini na taasisi za dini nchini kusaidiana na Serikali katika kupambana na tatizo hilo lenye madhara makubwa kwa jamii, na hasa miongoni mwa vijana ambao wanaunda asilimia 60 hadi 80 ya Watanzania wanaotumia dawa za kulevya ambazo zinaharibu mwili na akili ya mtumiaji.


Vile vile, Rais amesema kuwa wakati ni kweli kuwa mikoa yote ya Tanzania inakabiliwa na tatizo hilo, lakini ni mikoa saba inayoongoza kwa kuwa na tatizo kubwa zaidi ikiwa ni Dar es Salaam, Mwanza, Mjini Magharibi – Zanzibar, Arusha, Tanga, Mbeya na Dodoma.

Rais Kikwete alitangaza kusudio lake la kuunda chombo maalum cha kupambana na dawa za kulevya jana wakati wa sherehe za kusimikwa kwa Askofu Mteule Albert Jella Randa wa Kanisa la Mennonite, Tanzania, kuwa Askofu wa Dayosisi ya Mwanza ambako alikuwa mgeni.


Sherehe hizo zilifanyika kwenye makao ya Dayosisi hiyo Nyakato, mjini Mwanza.


Akihutubia mamia ya waumini wa Kanisa hilo pamoja na wananchi wengine waliohudhuria sherehe hizo, Rais Kikwete amewaomba viongozi wa dini, madhehebu ya dini mbali mbali nchini kuongeza juhudi za kupambana na biashara na matumizi ya dawa za kulevya.


Akisema kuwa pamoja na kwamba matunda ya juhudi za Serikali katika kupambana na tatizo hilo yameanza kuonekana bado kazi iliyoko mbele ya jamii ya Tanzania ni "kubwa sana".


"Mwaka jana, 2010, watu 12,119 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Katika kipindi hicho, dawa za kulevya zilizokamatwa ni heroine kilo 190 na gramu 780, cocaine kilo 65, morphine kilo 11, bangi kilo 279,520 na mirungi kilo 10,317. Takwimu zinaonyesha kuwa mkoani Mwanza tatizo linakua kwa kasi sana," amesema Rais Kikwete na kuongeza:


"Dawa za kulevya zina madhara makubwa kwa watumiaji na kwa jamii. Kwa watumiaji hatima yake ni mtu kuharibikiwa kimwili na kiakili. Watu huwa mazezeta na hivyo kushindwa kutokuwa na manufaa kwa jamii. Hii ni hasara kwa familia, jamii na taifa. Bahati mbaya sana waathirika wengi ni vijana. Tafiti zilizopo zinaonyesha kwamba asilimia 60-80 ya watu wanaotumia dawa hizo ni vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 30, alisema."


Aliongeza: "Hii ni hasara kubwa kwani vijana ndio nguvukazi ya leo na kesho. Ndiyo roho ya taifa na warithi wa familia, jamii na taifa. Wakiharibikiwa taifa letu litaangamia. Tusikubali. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kulichukia tatizo hili na kulikemea kwa nguvu zake zote ili kuokoa taifa letu. Nawaomba viongozi wa dini kushirikiana na Serikali na watu wote wenye mapenzi wa nchi yetu kupambana mpaka tufanikiwe kudhibiti na hatimaye kulitokomeza tatizo hili."


Sherehe za leo za kusimikwa Askofu Randa (50) kuwa Askofu wa Kanisa Mennonite, Jimbo la Mwanza, pia zilihudhuriwa na mamia kwa mamia ya waumini wa Kanisa hilo na wananchi wengine.


Kwenye sherehe hizo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT), Mhashamu Severin Watson Mang'ana amemkabidhi askofu huyo mpya nguvu kuu ishara za mamlaka na madaraka ya uaskofu ikiwamo Biblia, Katiba ya KMT, Cheti cha Uaskofu na vitabu vya taratibu ya kuendesha ibada za Kanisa hilo na nyimbo.

Kanisa la Mennonite lililoanzishwa duniani mwaka 525 na Mchungaji Menno Simon mjini Zurich, Uswisi, liliingia nchini miaka 77 iliyopita mwaka 1934 na liko katika maeneo yote ya Tanzania isipokuwa Zanzibar, Ruvuma na Pwani. Kanisa hilo lina makao yake mkoani Mara.

Source: Maganga One.: VIONGOZI WA DINI NA TAASISI SAIDIENI SERIKALI KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA - JAKAYA KIKWETE
watu wengine mnataka tuwatukane tupewe bun tumesema aliyowahusisha viongozi wa dini na madawa ya kulevya ni ile ya MBINGA achana na ya Mwanza mkuu! Hiyo uliyoiweka ni ya mwanza tafuta aliyosema mbinga! Mbona mnataka kupotosha habari!
 
Ndugu wana JF msikubali kuingia mkenge kirahisi hivyo hiyo si taarifa ya ikulu tunataka kopi halisi ambayo ni official na yenye nembo ya ikulu.Nyaraka hii si halali ni utumbo small thinkers
 
Kikwete asikwepe WAJIBU!
MAjbu haya si ya Kikwete, ni majibu ya mtu mwingine (Labda Premy Kibanga!).
Mh KIkwete, kauli ilitoka Mdomoni kwako, MAaskofu wanataka ufafanuzi wa kauli yako kutoka katika Kinywa chako.
 
Kazi hii ya kupambana na madawa ya kulevya haimhusu Rais peke yake inamhusu kila Mtanzania, popote alipo katika nafasi yake na viongozi wa dini wananafasi kubwa sana kwa sababu wao wanasikilizwa, wanatoa ushauri na wanategemewa kuwa na maelekezo yanayompendeza Mungu]


Sasa kama rais tayari anajua majina kwa nini asimalize game?
ikiwa atawaacha maaskofu washiriki wa hii biashara na hapa anakiri wanainfluence kwa jamii vipi wakiwaharibu mamia na mamia ya watanzania kwa kofia ya uaskofu?
Atutajie aache kuzunguka zunguka mh.Rais
 
Nilikua na mpango wa kuchumbia mke wa pili toka kwenye familia hii ila nazidi kuogopa sana, naona kama vile wanamatatizo hapa juu hapa karibu na macho na pua....
 
Haya maneno ndivyo tulivyoyapata kupitia vyombo vya habari? Au kikwete anategemea wote tulikuwa Mbinga? Vipi yale majina ya vigogo wa madawa hayo aliyosema anayo ameyadondoshea wapi? Au alikuwa anatafuta sifa za kijinga tu?!
 
majib hayaridhishi, tunasubiri atutajie majina ya hao watumishi, hatutaki bla bla hapa! Kama ana majina ayataje ili arahisishe kazi ya kuwakamata.

Sweety, njoo mie kwangu ntakupa majibu yanayo ridhisha na ntakutajia majina yote pole pole Sweety wangu !
 
Askofu Mokiwa ame kurupuka na ku overact kwa statment aliyoitoa JK kule Mbinga. Tatizo letu kubwa ni kufanya uchambuzi wa mambo pasipo kuwa na taarifa za uhakika.

Nimeisikiliza ile hotuba tena kupitia radio WAPO na ku transcribe Alichokisema JK ni hiki "

Siku hizi kila siku kuna watu wanaokamatwa kwa kujihusisha na dawa za kulevya. Inaashiria kuimarika kwa vyombo vyetu vya usalama. Lakini, inasikitisha sana kuona kuwa biashara hiyo sasa inawavutia hata baadhi ya watumishi wa Mungu. Huku sasa tunakoelekea kwa kweli ni kubaya sana. Nawaomba mtoe uzito unaOstahili kwa tatizo hili. Viongozi wa dini mnasikilizwa. Nawaomba kemeeni, onyeni na elimisheni jamii juu ya madhara ya dawa za kulevya. Waelimisheni vijana ambao ndiyo walengwa wakuu, waepuke na waache kujihusisha na biashara na matumizi ya dawa za kulevya.

Hiyo text haiongelei JK kasema maaskofu wanauza dawa....imesema baadhi ya WATUMISHI wa mungu. Katika orodha hiyo yawezekana kuwa wapo wachungaji, mashehe na watendaji wengine.

Rais hakurupuki kusema mambo yasiyokuwepo. Hadhara ile haikuwa mahala pa kutaja majina....sio utamaduni kwenye mahubiri ya kanisani mtu kutaja majina.....mbona hata huyo askofu Mokiwa kila siku anahubiri kanisani na kukemea ufisadi, lakini hataji majina ya mafisadi? Je kwa kutokutaja majina ya mafisadi anaowakemea kila mara, ndio maana yake mafisadi hawapo?

Ukweli ni kwamba watumishi wa mungu sio MALAIKA, ni binadamu kama binadamu wengine wote....na wao hupotoka kama binadamu wengine wote.....ndio maana Mwenzi Mungu akaweka provision ya KUTUBU! Ndio maana kila jumapili.....wachungaji wanaongoza sala ya TOBA......THEY ARE NOT EXEMPTED kwenye sala ile ya TOBA......

By the way ukirejea kwenye historia ya dini...... Yesu Mara kadhaaa ame point out kwamba Mafarisayo na viongozi wa dini hawatendi yale wanayohubiri...soma kitabu cha MATHEW 23:
Matthew 23

A Warning Against Hypocrisy

1 Then Jesus said to the crowds and to his disciples: 2 "The teachers of the law and the Pharisees sit in Moses' seat. 3 So you must be careful to do everything they tell you. But do not do what they do, for they do not practice what they preach. 4 They tie up heavy, cumbersome loads and put them on other people's shoulders, but they themselves are not willing to lift a finger to move them.
5 "Everything they do is done for people to see: They make their phylacteries[a] wide and the tassels on their garments long; 6 they love the place of honor at banquets and the most important seats in the synagogues; 7 they love to be greeted with respect in the marketplaces and to be called ‘Rabbi' by others.

8 "But you are not to be called ‘Rabbi,' for you have one Teacher, and you are all brothers. 9 And do not call anyone on earth ‘father,' for you have one Father, and he is in heaven. 10 Nor are you to be called instructors, for you have one Instructor, the Messiah. 11 The greatest among you will be your servant. 12 For those who exalt themselves will be humbled, and those who humble themselves will be exalted"

Ukiendelea kusoma hawa viongozi wamekuwa warned 7 times.....Matthew 23 - Passage Lookup - New International Version - BibleGateway.com

Hivyo, Mokiwa hana haja ya kuja juu na kutoa ultimatum. Alichotakiwa kufanya ni kuwahubiria watumishi wa kanisa lake kwamba endapo wao ni sehemu ya wanaojishughulisha na biashara hiyo, basi waache.....kwani ni kinyume na mafundisho ya Mungu.

Lakini tukirudi nyuma....hili suala la kashfa dhidi ya baadhi ya watumishi wa "Mungu" si geni...huko Bolivia Mchungaji mmoja mashuhuri, alikamatwa na kilo 240 za cocaine soma taarifa yake hapo kwenye website:
Pastor Caught Got 240 Kgs Cocaine

A priest of the Aymara Indians, who gave his blessing to the President of Bolivia Evo Morales during his inauguration ceremony four years ago, was arrested for having 240 kilograms of cocaine.

Anti-narcotics police found a cocaine laboratory in the vicarage was named Valentin Mejillones. Besides the pastor, children, and a pair of Colombian citizens were also arrested. Raw cocaine is appraised at a value of about 240,000 U.S. dollars.

The priest says he was framed by the Colombian people. Bolivian Vice President Alvaro Garcia said Morales did not choose it as the pastor who took the presidential oath of office four years ago.

Morales, who is also from Aymara Indian and former farmer of cocaine, was sworn in as the first president to come from local indigenous people. Pastors should preach, not the narcotic involved directly or indirectly.

Similar story imetokea marekani pia....angalia Corapi accuser promised to ‘destroy' priest after being fired: claim | LifeSiteNews.com

Hata hapa kwetu,wapo wachungaji kadhaaa waliofungwa kwa makosa mbalimbali....likiwemo kosa la kubaka......kumbukeni story iliyowahi kuripotiwa hata hapa jamvini juu ya mchungaji wa KKKT kufungwa miaka 30 kwa kubaka: https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/69196-mchungaji-afungwa-miaka-30-jela-kwa-kubaka.html
Hivi mtu mwenye propensity ya kubaka, atashindwa kuuza madawa ya kulevya, akipata opportunity?

ALL IN ALL mimi nadhani badala ya kukurupuka na jazba.....tuli address tatizo kubwa la madawa lililo mbele yetu....soooote ni wadau kwani athari za madawa ni kwa watoto wetu, kaka zetu, ndugu zetu, dada zetu, marafiki zetu na taifa letu kwa ujumla......

so who are u kutafsiri aliyoongea mwingine? we unajuaje alichomaanisha yeye?
watu bana au nawe uko kwenye payrol fulani humu?
 
Sasa kama rais tayari anajua majina kwa nini asimalize game?
ikiwa atawaacha maaskofu washiriki wa hii biashara na hapa anakiri wanainfluence kwa jamii vipi wakiwaharibu mamia na mamia ya watanzania kwa kofia ya uaskofu?
Atutajie aache kuzunguka zunguka mh.Rais
mimi nilifikiri taarifa hii ndio ingebeba kabisa hayo majina ya hao viongozi wa dini ili amalize mchezo kama kweli yeye ni Raisi...si wapo taja sasa...mbona Askofu mmoja walimkamata Airport na kumchunguza hawakukuta kitu? Labda yeye ndio kachukua taarifa hizi ambazo zina zaidi ya miaka kumi sasa....
 
Back
Top Bottom