Kikwete awalinda Mawaziri - Asisitiza waachwe, UPEPO HUU UTAPITA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete awalinda Mawaziri - Asisitiza waachwe, UPEPO HUU UTAPITA!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 22, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  WAKATI taarifa ya Kamati ya wabunge wa CCM chini ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, juzi iliridhia mawaziri wote wanaokabiliwa na tuhuma za ubadhirifu kwenye wizara zao wajiuzulu, jana Rais Jakaya Kikwete aliwasili nchini akitokea Brazil akiwa na msimamo tofauti.

  Taarifa zinasema kumekuwa na mazungumzo baina ya Rais Kikwete na Pinda yaliyolenga kunusuru serikali yao lakini walitofautiana kuhusu hatua inayopaswa kuchukuliwa dhidi ya mawaziri waliotakiwa kujiuzulu.

  Msimamo wa Pinda inadaiwa kuwa anataka mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma waondoke ili kuleta uwajibikaji serikalini, lakini Rais Kikwete amesema mawaziri hao waachwe waendelee na kazi zao, kwa kuwa suala hili ni la upepo tu, liachwe litapita.


  Tanzania Daima Jumapili limeelezwa kuwa rais anakataa shinikizo hilo kwa madai serikali haipaswi kuyumbishwa yumbishwa.


  Miongoni mwa mawaziri wanaopaswa kuondoka ni Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo; Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Cyril Chami na naibu wake, Lazaro Nyalandu; Waziri wa Tawala wa Mikoa na Serikali za Mitaa, George Mkuchika na naibu wake, Aggrey Mwanri; Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda na naibu wake, Lucy Nkya na Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu.


  Wengine ni Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige.


  Habari zinasema Rais Kikwete na Pinda walitofautiana juu ya hatua dhidi ya mawaziri hao, hivyo kuwafanya baadhi ya mawaziri kutamba mitaani kuwa hawang'oki madarakani kwa sababu tayari bosi wao ameonyesha kutounga mkono tuhuma zinazoelekezwa kwao na wabunge wa upinzani na CCM.


  Habari hizi zinasema pia kwamba Pinda amekuwa hafurahishwi na msimamo wa ‘bosi' wake, hasa katika kushindwa kutoa uamuzi mgumu.


  Zinadai kuwa rais amekuwa na tabia ya kuacha upepo uchukue nafasi yake wakati Pinda anataka baadhi ya watu wawajibike bila kujali nyadhifa zao au ukaribu na kiongozi mkuu wa nchi ili kurejesha imani ya serikali kwa wananchi.


  Pinda inadaiwa amekuwa akitaka maamuzi magumu yafanyike, kwakuwa yeye ndiye anayesulubiwa na maswali pamoja na hoja za wabunge wawapo bungeni.


  Baadhi ya wabunge waliozungumza na Tanzania Daima Jumapili, wameweka wazi kuwa kama Rais Kikwete ataamua kuwalinda na kuwatetea mawaziri wake basi watawaondoa kwa mkakati tofauti utakaomlazimisha rais kukubaliana na hoja za wabunge.


  Baadhi ya wajumbe waliozungumza na gazeti hili waliweka wazi hatua hiyo inahitaji muda na mipango madhubuti na wao wapo tayari kufanya hivyo, kwani nchi inazidi kudidimia kwenye umaskini huku watu wake wakikosa huduma muhimu za kijamii.


  Walisema kwa muda mrefu wamekuwa wakiwalalamikia watendaji wa serikali na chama tawala lakini rais amekuwa mgumu wa kuyashughulikia matatizo hayo.


  Wanasema rais ndiye kikwazo kikubwa cha maendeleo ya chama chao na serikali, hasa kwa kuwateua mawaziri, wakurugenzi na maofisa wengine bila kuangalia uwezo wao wa kiutendaji.


  "Kaka kwenye Bunge la Februari kuna mbunge alitoa kauli kuwa kama tunaona mambo hayaendi serikalini tupige kura ya kutokuwa na imani na rais, watu walimshambulia. Sasa tunaona umuhimu wa kauli yake ile," alisema mbunge mmoja.


  Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa makada wa CCM wameanza kuingiwa na hofu ya kubomoka kwa chama chao hasa baada ya makada wenzao kuanza kujiunga na vyama vya upinzani.


  Wanasema wakati makada wa chama hicho wakiendelea kukihama uongozi wa CCM hauonekani kuchukua hatua zinazostahiki dhidi ya viongozi wanaochangia wananchi wakose imani na chama tawala.


  Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, aliweka wazi kuwa wabunge wa CCM ni lazima wakemee ubadhirifu kwakuwa Tanzania si mali ya CCM.


  Mbunge huyo alikwenda mbali kwa kumtaja Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo, kuwa ni mwizi, mwongo na mbadhirifu wa mali za umma.


  Mawaziri wasuasua kuwasilisha barua

  Hadi jana Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema hajapokea barua ya kujiuzulu kutoka kwa waziri yeyote huku akiweka wazi kuwa kesho atatoa taarifa kamili juu ya jambo hilo.

  Juzi vyombo vya habari vilipata taarifa kutoka kwenye kikao cha wabunge wa CCM kuwa baada ya wabunge kuzituhumu baadhi ya wizara kukithiri kwa ubadhirifu mawaziri wake wameamua kujiuzulu.


  Taarifa hizo zilidokeza kuwa mawaziri hao walishinikizwa kuachia nyadhifa zao ili kukinusuru chama na serikali dhidi ya hasira za wananchi wanaokerwa na ufisadi.


  Chami atoboa siri

  Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, amejitetea kuwa wizara yake haimlindi Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Charles Ekelege, kama alivyotuhumiwa na baadhi ya wabunge.

  Alisema amesononeshwa na taarifa ya ukaguzi wa CAG juu ya TBS iliyotolewa kwa waheshimiwa wabunge bila yeye mwenyewe au wizara kupewa nakala kwa kipindi cha wiki nzima.


  Alisema kuwa baada ya kusikia kuwa waheshimiwa wabunge wengi wanayo taarifa hiyo na hata naibu wake kukiri bungeni kwamba taarifa imetoka wakati yeye hana nakala, alikwenda kwa Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashillilah na kuiomba nakala ya taarifa hiyo.


  Alibainisha kuwa baada ya kufanya ufuatiliaji katika ofisi ya CAG ilikiri kuigawa kwa wabunge na kusahau kuipeleka kwa wizara hiyo ambayo ndiyo inayohusika.


  "Hapa wasomaji wapime wenyewe. Inawezekanaje taarifa ya CAG iliyoandikwa kutokana na takwimu zilizotolewa na wizara yangu, iwafikie wabunge huku wizara yangu itakayotakiwa kuifanyia kazi taarifa yenyewe haipewi nakala, eti kwa kughafilika?


  "Ni ukweli ofisi ya CAG walighafilikiwa, au jambo hili limesukwa ili kuniaibisha mimi mbele ya Watanzania, rais aliyeniteua na hasa wapiga kura wangu wa Moshi Vijijini?" alihoji.


  Nundu ajitetea

  Naye Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, alisema tuhuma dhidi yake zilizoelekezwa na baadhi ya wabunge, hazina ukweli na zimelenga kumchafua.

  Alisema kilichoelezwa na Kamati ya Miundombinu ni uongo na uzushi, kwani nyaraka walizozitumia kuorodhesha tuhuma dhidi yake si halali.


  Kuhusu kuingilia utendaji wa Mamlaka ya Bandari kwa masilahi binafsi, alisema si kweli, akaongeza kuwa kinachomponza ni kuipinga kampuni inayotetewa na menejimenti isipewe zabuni ya kufanya upembuzi yakinifu peke yake na kwenda kukopa na baadaye iruhusiwe kujenga gati namba 13 na 14.


  "Wanasema namtaka mwekezaji ambaye makubaliano yanaonyesha atamiliki gati hilo kwa miaka 45. Nachelea kusema ni uongo na uzushi," alisema Nundu.


  Mkuchika apata kigugumizi

  Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika, alipoulizwa juu ya suala hilo alishindwa kukubali wala kukataa iwapo ataandika barua ya kujiuzulu. Alimtaka mwandishi amuulize Katibu wa Kamati ya Uongozi

  Chanzo: Tanzania Daima
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hakuna CHANGE - Mambo vilevile, ulaji palepale...
   
 3. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAKATI taarifa ya Kamati ya wabunge wa CCM chini ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, juzi iliridhia mawaziri wote wanaokabiliwa na tuhuma za ubadhirifu kwenye wizara zao wajiuzulu, jana Rais Jakaya Kikwete aliwasili nchini akitokea Brazil akiwa na msimamo tofauti.


  Taarifa zinasema kumekuwa na mazungumzo baina ya Rais Kikwete na Pinda yaliyolenga kunusuru serikali yao lakini walitofautiana kuhusu hatua inayopaswa kuchukuliwa dhidi ya mawaziri waliotakiwa kujiuzulu.

  Msimamo wa Pinda inadaiwa kuwa anataka mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma waondoke ili kuleta uwajibikaji serikalini, lakini Rais Kikwete amesema mawaziri hao waachwe waendelee na kazi zao, kwa kuwa suala hili ni la upepo tu, liachwe litapita.

  kwa taarifa zaidi bofya hapa
  JK AWALINDA MAWAZIRI WAKE.....ADAI KUWA SUALA HILO NI UPEPO WA KISIASA TU NA HIVYO LITAPITAGUMZO LA JIJI
   
 4. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAKATI taarifa ya Kamati ya wabunge wa CCM chini ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, juzi iliridhia mawaziri wote wanaokabiliwa na tuhuma za ubadhirifu kwenye wizara zao wajiuzulu, jana Rais Jakaya Kikwete aliwasili nchini akitokea Brazil akiwa na msimamo tofauti.


  Taarifa zinasema kumekuwa na mazungumzo baina ya Rais Kikwete na Pinda yaliyolenga kunusuru serikali yao lakini walitofautiana kuhusu hatua inayopaswa kuchukuliwa dhidi ya mawaziri waliotakiwa kujiuzulu.

  Msimamo wa Pinda inadaiwa kuwa anataka mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma waondoke ili kuleta uwajibikaji serikalini, lakini Rais Kikwete amesema mawaziri hao waachwe waendelee na kazi zao, kwa kuwa suala hili ni la upepo tu, liachwe litapita.


  Taarifa zinasema kuwa rais anakataa shinikizo hilo kwa madai serikali haipaswi kuyumbishwa yumbishwa.


  kwa habari zaidi bofya hapa
  JK AWALINDA MAWAZIRI WAKE.....ADAI KUWA SUALA HILO NI UPEPO WA KISIASA TU NA HIVYO LITAPITAGUMZO LA JIJI
   
 5. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAKATI taarifa ya Kamati ya wabunge wa CCM chini ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, juzi iliridhia mawaziri wote wanaokabiliwa na tuhuma za ubadhirifu kwenye wizara zao wajiuzulu, jana Rais Jakaya Kikwete aliwasili nchini akitokea Brazil akiwa na msimamo tofauti.


  Taarifa zinasema kumekuwa na mazungumzo baina ya Rais Kikwete na Pinda yaliyolenga kunusuru serikali yao lakini walitofautiana kuhusu hatua inayopaswa kuchukuliwa dhidi ya mawaziri waliotakiwa kujiuzulu.

  Msimamo wa Pinda inadaiwa kuwa anataka mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma waondoke ili kuleta uwajibikaji serikalini, lakini Rais Kikwete amesema mawaziri hao waachwe waendelee na kazi zao, kwa kuwa suala hili ni la upepo tu, liachwe litapita.


  Taarifa zinasema kuwa rais anakataa shinikizo hilo kwa madai serikali haipaswi kuyumbishwa yumbishwa.


  kwa habari zaidi bofya hapa
  ​
  JK AWALINDA MAWAZIRI WAKE.....ADAI KUWA SUALA HILO NI UPEPO WA KISIASA TU NA HIVYO LITAPITAGUMZO LA JIJI
   
 6. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Sasa naanza kuamini kuwa JK anataka Pinda atolewe ili amuweke Migiro in preparation for a presidency marathon in 2015!
   
 7. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Huyu Rahisi ni mpuuzi wa mwaka, kazi tunayo jamani, na mwaka wake wa mwisho anampango wa fungulia mbwa wale.
   
 8. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  The way the cookie crumbles in Tanzania.....
   
 9. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #9
  Apr 22, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Niliweka bandiko humu kuwa anayetakiwa kuwajibishwa ni JK na sio Pinda. Watu wakaniona pimbi. Sasa hapo mwenye afadhali nani kati ya hawa wawili? Tunataka mabadiliko halafu tunamuogopa mwenye nyumba? M4C ya kweli ni kuanza maandamano nchi nzima kuelekea ikulu moja kwa moja.
   
 10. rweyy

  rweyy Senior Member

  #10
  Apr 22, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  wabaki tu ili mambo yaendelee kuwa magumu ili 2015 iwe kazi laisi kuitoa ccm madalakani.mi napenda sana jk anavyochukulia mambo kilaisi laisi hajui kama anawapa cdm nafasi hongera jk kazi nzuri hiyo.
   
 11. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ndio kawaida ya jamaa, never serious hata siku moja.

  The so called chagua la Mungu.
   
 12. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  The voters in Tanzania can not be predicted so easily...
   
 13. DGMCHILO

  DGMCHILO Member

  #13
  Apr 22, 2012
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Huyu rais vipi?
  JK NYERERE alisema kweli huyu ni mtoto
  sasa ni kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais
   
 14. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mh. Pinda,
  Pole sana na Hongera kwa uadilifu na umakini wako. Tumeanza kuelewa kuwa kumbe kazi yako ni ngumu mno na ndio maana huwazi kuendelea nayo. Kama kweli Mh. Rais amekataa mawaziri wasijiuzulu na tayari ulishawaweka sawa kwa sababu ya moyo wako wa uwajibikaji hii ni mbaya sana.
  Kwa kuwa mheshimiwa raisi hatawahi kugombea nafasi nyingine yoyote baada ya 2015 basi madhara yake kisiasa ni historia yake tu ataiacha vibaya. Kwa upande wako historia yako imekuwa nzuri hadi sasa. Ila ukweli kwa hili nakushauri ujiuzulu kama kweli mawaziri wako wametiwa moyo na Rais kutokuondoka.

  Vyombo vya habari viliandika na kwa kuwa haikukanushwa wananchi wote wanaamini ni ukweli ulisimamia
  mawaziri wako wakaandika barua za kujiuzulu. Hilo lilikuwa ni heshima kwako. kwao, na kwa chama na serikali yetu.

  Sasa kama kuna mabadiliko hii nifedheha kwako, kwa chama, mawaziri na kwa serikali yako.
  Kila mtu anaamini kutokana na uzito wa hoja basi walijiuzulu.

  Japo bado sijaamini kama raisi kweli atakubali kuwaambia wasijiuzulu, lakini kwa kuwa limetajwa nimeona nikutie moyo mapema usikute kweli imetokea.
  Kama imetokea basi nakushauri wewe ujiuzulu na wala usijali watakaosema umetishwa na hoja ya wabunge hilo lisikusumbue. Huwezi kuendelea kufanya kazi katika mazingira haya ya wewe kutokuwa na uwezo wa kutumia utashi, uwezo, dhamira na moyo wako katika kusimamia mambo.
  Jiuzulu sio kwa kushindwa bali kwa kuilinda heshima yako. NAKUSIHI KAMA KWELI HAWAJAJIUZULU MAWAZIRI BASI JIUZULU MWENYEWE. Pia wabunge wa CCM onyesheni heshima kwa nchi yenu juu ya mambo mazito kama ufisadi unaotesa nchi hii.
   
 15. b

  buzz Member

  #15
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Huku ni kulidharau bunge na wananchi pia. Sasa sote kwa pamoja ni kumwadhibu jk kwa kutokuwa na imani naye pia. So stupid!
   
 16. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Nineipitia hiyo habari kama ni kweli bora wananchi tuandamane kumtoa raisi.Raisi anaewatetea wala rushwa/wezi/wahujumu uchumi hatufai hata kidogo,tukisema kuwa alishirikiana na hao mawaziri anaowatetea sasa hivi tutakuwa tunakosea?Jakaya anajianini nini hasa?
   
 17. I

  Imurumunyungu Senior Member

  #17
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JK ni janga la taifa.Kwa hali aliyonayo huyu vasco da gama ni kwamba kwa sasa hafai kuwa hata barozi wa nyumba kumi.Hivi ni kwa nini tunaendelea kumvumilia huyu mtarii wa kikwere.Natoa angalizo kwa ukoo wa KIKWETE kutokujitokeza mtu yeyote kutoka ndani ya ukoo huo akiomba uongozi wowote ndani ya TZ mpaka baada ya miaka 200.Huo ukoo unafaa kuwa wa mabaharia na siyo ungozi.
   
 18. DGMCHILO

  DGMCHILO Member

  #18
  Apr 22, 2012
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Sasa naamini hata LOWASSA aliponzwa na huyu rais
  PINDA linda heshima yako utatolewa kafara kama LOWASSA
  sasa tumegundua ni nani anaharibu nchi hii
   
 19. gmosha48

  gmosha48 JF-Expert Member

  #19
  Apr 22, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 498
  Trophy Points: 180
  Hakyanani, tutafungwa 10 -0 sababu kocha wetu ni mwoga kufanya mabadiliko!
   
 20. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ndiyo maana huwa tunameona Lowasa kuwa ni mwanaume na mkweli juu ya maamuzi yake juu ya kujiuzulu. Ulegelege wa namna hii mwenye busara hawezi kuuhimili.
   
Loading...