Kikwete awakaribisha Wachina kuwekeza katika kilimo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete awakaribisha Wachina kuwekeza katika kilimo

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jul 29, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Raymond Kaminyoge

  RAIS Jakaya Kikwete ametoa wito kwa Wachina kuja nchini kuwekeza katika kilimo kwa kuwa Tanzania imebahatika kuwa na ardhi yenye rutuba.Alisema sekta binafsi ina mchango mkubwa katika kuleta mageuzi ya kilimo nchini na kwamba wawekezaji wa ndani wakishirikiana na wenzao wa China kilimo kitakuwa na mafanikio makubwa.

  Rais Kikwete alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongamano la kimataifa kuhusu mageuzi ya kilimo kwa maendeleo na kuondoa umaskini Afrika.Katika kongamano hilo lililoandaliwa na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (POPC) kwa kushirikiana na Kituo cha

  Kimataifa cha Kuondoa Umaskini cha China (PRCC), Kikwete alitaja Mikoa ya Iringa, Mbeya Ruvuma, Rukwa na Morogoro kuwa ndiyo yenye mazingira mazuri kwa kilimo.


  Rais Kikwete aliwaambia wajumbe 120 wanaohudhuria kongamano hilo kwamba bila sekta binafsi kuwekeza katika kilimo, vita ya kupambana na umaskini itakuwa ngumu hapa nchi na Afrika kwa ujumla. “Sekta binafsi inaweza kuwekeza katika kilimo cha mashamba makubwa, kuuza vifaa vya kilimo, kutoa mikopo kwa wakulima, utafutaji wa masoko ya mazao na kujenga viwanda vya kuongeza thamani ya mazao,” alisema Kikwete.


  Alisema sekta binafsi ikifanya hayo, Serikali kazi yake itakuwa ni kuimarisha miundombinu kama vile barabara ili kuweka mazingira bora ya kilimo na upatikanaji wa masoko.“Siku za nyuma sekta binafsi haikutumika katika kilimo, lakini hivi sasa tumejipanga kuona kwamba wanakuwa wadau wakubwa,” alisema Kikwete.


  Alisema sababu mojawapo inayokwamisha kilimo hapa nchini ni kutokuwa na vifaa vya kisasa vya kilimo kwa sababu wakulima wengi ni maskini wasiokopesheka na benki.Kikwete aliiomba Serikali ya China kuisaidia Tanzania katika eneo la utafiti wa kilimo ili kupata mazao yenye ubora zaidi na hivyo kuwaletea manufaa wakulima.


  Naye Waziri wa Nchi, Maendeleo na Kuondoa Umaskini wa China, Fan Xiaojian alisema kilimo nchini mwake kilifanikiwa baada ya kuwawezesha wananchi wa vijini kielimu na kiuchumi.Alisema Wachina walifundishwa namna ya kuendesha kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia ambazo waliwezeshwa kuwa nazo huku wakifanya hayo kwa kushirikiana.


  Xiaojian alisema Serikali iliwekeza kwenye tafiti za kilimo kwa kuvipatia vyuo vya kilimo vifaa na fedha za kutosha kufanya shughuli zake.Naye Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dk Philip Mpango alisema lengo la kongamano hilo ni kubadilishana uzoefu

  kati ya China na nchi za Afrika katika maendeleo ya kilimo na upunguzaji wa umaskini.

  Alisema pia ni kuangalia namna nchi za Afrika zinavyoweza kufaidika na maendeleo yaliyopatikana China.Kwa mujibu wa Dk Mpango, mbali

  na wataalamu wa Kichina walioshiriki katika kongamano hilo, nchi nyingine ni Tanzania, Kenya, Zambia, Ghana, Senegal, Siera Leon, Eritrea na Mauritius.

  Lengo la kongamano hilo ni kuchanganua kilimo cha kisasa cha China na kuangalia uwezekano wa ujuzi huo kutumika katika sekta ya kilimo katika nchi za Afrika.Ajenda zinziojadiliwa niu mtazamo mzima wa maendeleo ya kilimo na upunguzaji umaskini na China na Afrika,

  wajibu wa kilimo na teknolojia ya kilimo, tafiti na kuongeza huduma katika kilimo cha kisasa.Kongamano la tatula ushirikiano wa kimaendeleo la upunguzaji wa umaskini
  Kikwete awakaribisha Wachina kuwekeza katika kilimo

   
 2. m

  mr green Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 25
  kwa iyo watz tunarudi utumwani tena?
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tuna chuo cha kilimo, chuo cha Sokoine. Kinafanya kila aina ya utafiti katika kilimo. Kinachohitajika ni kukiwezesha zaidi chuo hicho na wala si kuwakaribisha Wachina eti watusaidie katika utafiti wa kilimo. Lini tutaachana na hizi dhana kwamba wageni ndio wenye uwezo na elimu zaidi yetu?
   
 4. N

  Nonda JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Hili ulilolisema hapa hata huyo waziri wa China amelisema hilo hilo au niseme amewaambia washiriki kuwa serikali ziwezeshe vyuo vya kilimo na wananchi.
  "Fan Xiaojian alisema kilimo nchini mwake kilifanikiwa baada ya kuwawezesha wananchi wa vijini kielimu na kiuchumi.Alisema Wachina walifundishwa namna ya kuendesha kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia ambazo waliwezeshwa kuwa nazo huku wakifanya hayo kwa kushirikiana.

  Xiaojian alisema Serikali iliwekeza kwenye tafiti za kilimo kwa kuvipatia vyuo vya kilimo vifaa na fedha za kutosha kufanya shughuli zake."

  Sasa lililobaki ni serikali na watendaji wake kuacha usanii na wathibitishe kwa vitendo.

  Hata hivyo sio mbaya kutafuta urafiki na China kuliko US na NATO ambao wao nyimbo yao ni vita dhidi ya ugaidi, pirates, vita, IMF, mazoezi ya kijeshi...bla..bla.
   
 5. C

  Chris B. Daniel Member

  #5
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 31, 2012
  Messages: 66
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watakuja kulima, yes, wameka vizuri kwenye kilimo lakini hatutaki kutugundulia mazao mapya like ile mboga yao ya chainizi-mboga mbaya kuliko hata shetani.
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  wanakuja kulima mazao feki hao!
   
 7. M

  Malila JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Bora wakilima mazao feki,lakini watakapo mkimbiza babu yako kule kijijini kwenu ndio utajua ubaya wa hawa wakulima wa kigeni. Kumbuka hawachukui eka mbili, wanachukua na visima,mito,njia za wanyama na kila kitu.
   
 8. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ujumbe wa serikali ya China ulianza kufuatilia suala hili tangia mwaka jana. Moja ya matakwa yao ni wapatiwe ardhi ili walime kwa kushirikiana na wakulima wadogowadogo wa hapa nchini. Walifanya survey ya maeneo mbalimbali kabla ya kuanza kudemand ardhi. Suala hili lilishindikana kwa kuwa Katibu mkuu wa kilimo alilisukumia katika uongozi wa juu watoe maamuzi. Ingawa waliahidi kutoa ushirikiano kwa kuendeleza rasilimali watu na mengine kama wadau walivyotaja lakini serikali yetu ilisita ktk suala la ardhi. Utapenda kufahamu kuwa China inahitaji chakula cha kutosha kwa ajili ya kulisha watu wake hivyo wanatafuta vyanzo vya chakula kutoka sehemu nyingine.
   
 9. k

  kimario joseph New Member

  #9
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hawa wachina wamemshauri vizur sana anatakiwa awazeshe wakulima walioko vijijin sio kuomba wageni waje kumsaidia kulima. huwezi amini rais ana promote kuuza ardhi yetu hivhiv ili badae tuanze kupigwa risas kma wanavyopigwa ndugu zetu waishio maeneo ya mgodin yaan wachimbaji wadogowadogo.hv nani aliwambia atuwezi kuchimba wenyewe mpaka achimbe mzungu
   
 10. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  wacha nijionee, yangu macho kama nipo hai.
   
 11. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Waje tu kama sie Watanzania hatujui kulima, mimi nadhani hii ni mbinu mpya ya kuwamilikisha wageni ardhi yetu kwa dhana eti ya uwekezaji wakati ni ubabaishaji wa hali ya juu.Nimesharudi kwetu Chala - Namanyere nakuambia sitakubali ardhi ya babu zangu ichezewe kiajabu ajabu kama ni kulima wafipa tunaongoza kwa kilimo labda wakabinafsishe huko huko Pwani
   
 12. HUGO CHAVES

  HUGO CHAVES JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 1,852
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  matarajio ya vijana wengi kupata ajira yamekwisha ,vijana jiandaeni na virungu kuchunga mashamba ya wawekezaji.hakuna jinsi ,biashara za machinga nyingi zilipata mtikisiko wa uchumi ,wafugaji wa kuku , wakulima,mama ntilie na wengine wengi wanahitaji jitihada binafsi za serikali kutoa stimulus package kuinua hali zao ,
   
Loading...