Kikwete awaambia UVCCM 'msitutishe'; ahoji walikopata fedha

sasa nimeamiani kweli WASSIRA choka mbaya kifikra

Yeye ndiye aliye kaa na UVCCM na kuwashauri la kufanya leo tena anakuwa mstari wa mbele kuwa shambulia dah hii kali


Unategemea nini? Na kama walimwamini basi nao ni vilaza sana. Alichofanya yeye ni kuwaingiza mkenge halafu awakaange kama alivyofanya kisha yeye aendelee kupeta.
 
Kaazi kweli kweli,magamba hawavuani wamekimbilia kwa vigamba vinavyochipukia kwa kasi-UVCCM,kazi jimalizeni muwezavyo tumewachoka kweli
 
Hao UVCCM wameyataka badala ya kusimamia misingi ya chama chao wanaweka maslahi mbele na kutumiwa na haohao wanasiasa ambao leo wanawadhihaki...hata hivyo bora uvunjwe naamini zaidi ya asilimia kubwa ya viongozi wa Uvccm hawajui chama chao kimejengwa katika misingi gani!
 
Rais Kikwete amenukuliwa na mtoa taarifa wetu akisema: "Mnataka kututisha, msitutishe hata kidogo maana nasikia kwamba mnataka kwenda Chadema, nendeni hata kesho, au mnasubiri tuuvunje ndiyo muondoke!"

Kadhalika Rais alinukuliwa akihoji vijana hao walikopata fedha zinazowawezesha kukaa hapa kwa muda wote huku akiwakumbusha kwamba CCM hakiwezi kuyumba ikiwa kitawatimua kwani kimewahi kufanya hivyo kwa viongozi wa ngazi za juu.

Pamoja na hali hiyo, viongozi wengi wa UVCCM wa mikoa na wilaya mbalimbali nchini bado wapo Dodoma na baadhi yao walisema huenda wakatoa tamko baada ya kikao cha NEC kumalizika.
Sioni kama CDM panawafaa hawa. NCCR inaweza kuwa sehemu muafaka kwao wakiamua kuondoka.
 
Well done JK.... sometimes hawa watoto hawajui huyo anayewatumia ana nia gani nao

ukimaliza kikao waite wagonjwa wako wote kwenye mawizara mkubaliane namna ya ku-transition kazi zao wakati wana ugua, kwani wengine wameanza kukwamisha mambo na kusema siri walizonazo pia wanaogopa
 
CCM inawawia vigumu kufanya maamuzi kutokana na kutokuwa consistent katika kutoa maamuzi yao; hawafuati kanuni na taratibu walizojiwekea ama sivyo wasingekuwa wanapata haya matatizo.

CCM huangalia sura za wahusika na sio makosa yaliyotendeka na hicho ndicho kikwazo kikubwa cha kufanya maamuzi ya busara. Double standard application to decision making Mkweree ameipeleka mpaka serikalini sasa na ndio maana utaona mtu kama Mattaka anashitakiwa mahakamani kwa kutumia ofisi vibaya lakini Jairo aliefanya makosa makubwa zaidi hapelekwi kizimbani kwa makosa aliyoyafanya kwa sababu tu ya kulindwa !!

Mwalimu Nyerere alijitahidi sana kuwafundisha hawa nunda mpaka kwa mifano hai lakini hawakumuelewa; alipotoa ule mfano wa mtoa rushwa na mpokea rushwa kuwa wote walikuwa ni 'MAJI YA NYANJA" maana yake ilikuwa hukumu hutolewa kutokana na kosa [ kanuni na taratibu] na sio sura ya mkosaji!!
 
sijawahi kuona kiongozi wa juu wa ccm aliyewahi kutimuliwa.

unaumri gani kwani ? Wajumbe wa cc aboud jumbe na seif sharrif hamad ambapo mmoja alikuwa rais wa zanzibar na mwingine aliwahi kuwa waziri kiongozi lakini kutimuliwa kwao kulitokea kwa nyakati tofauti
 
unaumri gani kwani ? Wajumbe wa cc aboud jumbe na seif sharrif hamad ambapo mmoja alikuwa rais wa zanzibar na mwingine aliwahi kuwa waziri kiongozi lakini kutimuliwa kwao kulitokea kwa nyakati tofauti

BigMan,
Ile ilikuwa CCM nyingine tofauti kabisa na hii tuijuayo leo. Kilichobaki ni majina kufanana tu.
 
Haramu siku zote huzaa haramu, wala jk asitegemee haramu kuzaa halali, kama wao wanatumia njia haramu kupata uongozi na mali kwa njia
 
Haramu siku zote huzaa haramu, wala jk asitegemee haramu kuzaa halali, kama wao wanatumia njia haramu kupata uongozi na mali kwa njia za kifisadi walitegemea nini kutoka kwa watoto wao, ama kweli nyani haoni kundule na ukusitaajabu ya jk utayaona ya uvccm
 
Pochi ya EL mngemtimua ndipo mngekiona cha moto kutoka kwa hiyo mitoto yenu mnayoirithisha sera yenu kuu ya UFISADI. Time will tell Unabii umeishashuka MENE MENE TEKELI NA PERESI CCM!!
 
Wanabodi.
Kuna tetesi kuwa umoja wa vijana wa ccm UVCCM wanapanga mkakati wa
kuhamia CHADEMA.
Hii habari ni kubwa sana lakini haipewi kipaumbele sana na magazeti ya Tanzania.
Je kuna ukweli wowote wa hili.
 
Mwenyekiti mwenyewe ni gamba, na tayari alishawatuliza magamba wenzie kuwa hakuna kitakachoharibika. Sasa wewe unashangilia nini hapo!!!!!!!!!
Ccm wanatuchezea picha utadhani ni kina ray na kanumba wanaigiza? Ccm to hell!
 
Ze habari ze utamu sanaaa,baada ya 6 jana kupuliziwa bange tunaomba mtujuze nani tena kapewa poda ama ile mukitu mafuta ga betri ya gari kwenye mumaji ga gilasi bwana..
 
Sidhani kama CCM itasalimika kwani wameupotosha umma wananchi hawana imani nayo tena cha kuwashauri hawa CCM nikuakikisha wanatekeleza hazima yayo ndo watarudisha imani kwa wananchi, Kikwete acha ubabaishaji fanya kazi fanya maamuzi huo ndo uongozi bora.
 
Eti Jk anatuzuga kwa kushangaa vljigamba vidogo uvccm wamepata wapi hela? Hawajaenda dodoma kwa bahati mbaya meeeen! Wapo kimkakati, wale ni safina ya kumbeba EL kuelekea urais 2015. Ccm yametimia!
 
Kama nikweli basi hawa jamaa wakaribishwe chadema ila, wasipewe uongozi maana hawana utii na adabu kwahiyo wanaweza kuhmishia vurugu hiyo ya ccm huku chadema na kuvuruga upinzani kama shibuda nawengine ambao wametoka ccm.Kama wakija wapewe mafunzo kwanza wajue itikadi ya chadema arafu wakubali kuwa wanaachana na ufisadi Amina.
 
Kaazi kweli kweli,magamba hawavuani wamekimbilia kwa vigamba vinavyochipukia kwa kasi-UVCCM,kazi jimalizeni muwezavyo tumewachoka kweli

Mpaka sasa hivi mwanasiasa aliyewasumbua watu vichwa vyao ni mmoja tu JOHN SHIBUDA kumfukuza hawawezi yaani wanajuta walomchukua wa nini
 
Back
Top Bottom