Kikwete atua Dar awahoji mawaziri

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,047
Kikwete atua Dar awahoji mawaziri
* Awataka kuelezea mikoa waliyotembelea

* Zitto uso kwa uso na Karamagi uwanja wa ndege

* Wasalimiana kwa kupeana mikono

* Alikuwa kwenye ndege aliyosafiria rais


Na Tausi Mbowe
Mwananchi

RAIS Jakaya Kikwete, jana aliwasili nchini akitokea Marekani na kuwahoji mawaziri waliofika kumpokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akimtaka kila mmoja, kueleza mkoa aliotembelea kuwaeleza wananchi kuhusu utekelezaji wa bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2007/2008.

Rais ambaye alikuwa nchini Marekani kwa ziara ya wiki tatu ambapo pamoja na mambo mengine alihudhuria Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam saa 8:00 mchana jana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates.

Baada ya kuwasili uwanjani hapo, alianza kuwauliza mawaziri hao, mmoja baada ya mwingine ambapo kila mmoja alimjibu kulingana na mkoa aliotembelea.

Baadhi ya mawaziri hao ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge), Dk Batilda Burian, Waziri wa Fedha, Zakhia Meghji, Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Dk Hussein Mwinyi, Naibu Waziri wa Miundombinu, Dk Maua Daftari, Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Omar Yusuf Mzee.

Baada ya mahojiano hayo, alikwenda moja kwa moja kwa wananchi na kuwapungia mkono kabla ya kupanda katika gari lake na kuondoka uwanjani hapo.

Kuanzia wiki iliyopita, baadhi ya mawaziri wako katika ziara kutembelea mikoa mbalimbali nchini kuelezea utekelezaji wa bajeti hiyo.

Mbali na mawaziri hao, viongozi waliofika kumpokea Rais Kikwete, ni Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini, Jenerali, Davis Mwamunyange na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba.

Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abas Kandoro, Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Alhaj Adam Kimbisa pamoja na makada mbalimbali wa CCM.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Kabwe Zitto, alikutana uso kwa uso na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na kusahau tofauti zao kwa muda.

'Mahasimu' hao walikutana jana uwanjani hapo na kusalimiana kwa kupeana mikono.

Katika tukio la jana, Zitto alikutana na Karamagi uwanjani hapo alipokuwa akitokea nchini Kenya alikokwenda kuhudhuria kampeni za mgombea urais, Raila Odinga.

Karamagi alifika uwanjani hapo saa 8:00 mchana kwa ajili ya kumpokea Rais Jakaya Kikwete aliyewasili uwanjani hapo kutoka ziarani nchini Marekani.

Karamagi aliyekuwa na mawaziri wengine na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari katika chumba cha watu mashuhuri (VIP), walipigwa na butwaa baada ya kumuona mbunge huyo akishuka ngazi akitokea katika sehemu ambayo wasafiri mashuhuri hutumia kupita.

Hali hiyo ilifanya karibu ukumbi mzima kukaa kimya kwa sekunde kadhaa kabla ya kuangua kicheko baada ya Zitto ambaye inasadikiwa alisafiri katika ndege moja na Rais Kikwete, kumshika mkono Waziri Karamagi huku waandishi wakichukua picha za tukio hilo. Kitendo hicho kilimshawishi Waziri Karamagi pia kuangua kicheko.

Hata hivyo, mbunge huyo alikaa katika eneo hilo muda mfupi na baadaye aliondoka uwanjani na kuacha maswali mengi yasiyo na majibu kwa viongozi hao waliotaka kujua alikokuwa ametokea na sababu za kufika wakati huo ambao rais aliwasili.

Tukio hilo la kusalimiana limetokea ikiwa ni mara ya kwanza kwa 'mahasimu' hao kukutana tangu Zitto asimamishwe kuhudhuria vikao vya Bunge hadi Januari, mwakani, baada ya kuwasilisha bungeni hoja binafsi kuhusu mkataba wa mradi wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, wilayani Kahama uliosainiwa na waziri huyo jijini London, Uingereza.

Zitto aliwasilisha hoja hiyo akitaka kuundwa Kamati Teule kuchunguza mazingira ya utiaji saini mkataba huo.
 
Kama wauza unga walipewa muda wajisahihishe itakuwa mawaziri.
 
Hivi leo si ndio Muungwana amekutana na mawaziri, alafu inakuwaje tena Muungwana anapanda commercial airline kaG5 ketu kameshakosa vipuri?
 
yaani kupingana kihoja ndio kunawafanya watu wawe mahasimu ? ama kweli kama mie ningekuwa kiongozi basi bila shaka wengi wangekuwa mahasimu wangu !
 
..kwahiyo hawakuchuniana kama ilivyoelezwa awali?

..icadon,hiyo g5 na hiyo misafari ya huyo bwana itakuwa balaa tupu!

..hizo charges zitakavyolundikana,i cannot even imagine!
 
hawakuchuniana, mwanakijiji yupo kwingine na hao waliokuwepo airport ( zitto, karamagi ) wanajua wenyewe yaliyojiri, magazeti yashasema bana walisalimiana kama kawaida, na isingeandikwa hapa kwamba walisalimiana, karamagi angezidi kunuka !
 
muandishi kakosa habari, hoja si nini kikwete kawauliza mawaziri, wananchi tunataka kujua hao wamaziri wamejibu nini? walimuambia kama wanazomewa_?
 
Back
Top Bottom