Kikwete Atibiwa Muhimbili: Mfano mzuri, for a change! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete Atibiwa Muhimbili: Mfano mzuri, for a change!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dilunga, Aug 29, 2009.

 1. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwa hili Kikwete apongezwe na kuigwa...
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Aug 29, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli nimefurahishwa sana na kitendo hiki cha Rais kuoonyesha kuwa anathamini huduma za afya zitolewazo na taasisi zetu.

  Imekuwa kawaida ya viongozi wetu na familia yao kwenda Ulaya kwa gharama za serikali kwa ajili ya huduma za afya nyingine zikiwa ndogo sana na nyingine zinazoweza kuepukika kwa kubadili life style zao.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Labda alifanya usanii tu,kila siku yuko ulaya halafu kutibiwa atibiwe bongo??????????its called political stunts..........
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Apongezwe kwa kipi?. Alitakiwa baada ya kutibiwa atoe tamko kuwa ni marufuku kwa hela ya serikali kutumika kutibia watu nje ya nchi. Serikali iboreshe huduma za afya zilizopo nchini ili kuvutia watu wa nchi nyingine kuja kutibiwa Tanzania.

  Serikali ingepiga marufuku viongozi kutibiwa nje basi ni dhahiri inge invest kwenye huduma bora za afya nchini. Hiki kitendo alichofanya ni usanii wa kuelekea 2010 election, hawana nia ya kuboresha huduma nchini kwani wao haziwahusu wakiugua tu wanaenda nje ya nchi.
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Aug 29, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..hivi mnategemea JK anaweza kulazwa au kufanyiwa upasuaji Muhimbili, KCMC, Bugando, Ocean Road, au Bombo?

  ..mara alipochaguliwa alitembelea magereza na hospitali ya Muhimbili, sasa naomba mnieleze mabadiliko yaliyotokea.
   
 6. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #6
  Aug 30, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Mkuu JokaKuu umenikuna hapo!

  Halafu hivi JK hajaenda Geneva kwenye mkutano wa Climate Change? Au kaona aibu safari hii katuma wawakilishi?
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,547
  Likes Received: 81,984
  Trophy Points: 280
  Ni usanii tu wa kujiandaa na 2010, hakuna lolote! Akiwa mgonjwa hatathubutu kukanyaga Muhimbili.
   
 8. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  True, true, angeweze kusema anapiga marufuku viongozi kutibiwa nje. Lakini nadhani kuonyesha mfano pia ni njia nyingine tofauti, japo sio robust kama kutoa amri za marufuku. Kikwete hana ethics deep kiasi hicho, au principle za kupiga marufuku matibabu ya nje, lakini, Hostede, nadhani kwa upeo wake amejitahidi. Kwa kuanzia.

  Wenzake labda wataona aibu.
   
 9. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Halafu nyie wadanganyika nani amewaloga?. Kama anatibiwa na huduma zinasimama kwa watanzania WOTE si afadhali aende nje ya nchi?????????? wanakufa wangapi kwa humduma kusimama ili atibiwe yeye pekee yake!!

  Je maisha ya watanzania elfu ni sawa na Rais pekee yake jamani??, labda kwenye vita tu!
   
 10. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Sidhani, Joka Kuu, nadhani hawezi.

  Lakini tulichonacho mbele yetu ndio hicho, ametibiwa Muhimbili. Hayo mengine yote ni imaginations nzuri, kwamba ikiwa hivi itakuwaje, "hivi mnategemea akihitaji upasuaji atatibiwa Bombo" hayo yote tunaweza kuyajibu kabla ya, lakini ni speculations tu. Kwa sasa, kwa alichoonyesha so far, nadhani ni chema.

  Well, hakuna mabadiliko makubwa ya hali za mahospitali, labda (maana anaweza kusema Muhimbili wamejenga vitengo vipya since, kikiwepo cha Moyo kama kimeshamalizika) lakini hiyo ni mada nyingine nadhani. Tunaongelea yeye kukubali kutibiwa katika hali hiyo mbaya, wanakotibiwa wananchi, ni mfano kwa wenzie.

  Hivi high-lifers kama kina Lowassa wanaweza kuvaa miwani ya waganga wa KCMC? Naona JK hapo amejitahidi.
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Aug 30, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  Invisible, Dilunga,

  ..wangetueleza aina ya uchunguzi wa macho aliofanyiwa.

  ..isije ikawa amekwenda kwa shughuli ndogo ya kupima miwani mipya halafu wananchi tunaona ni big deal.

  ..vilevile haijulikani alitumia muda gani hapo Muhimbili, na madaktari wangapi walimhudumia. hiyo inaweza kutusaidia kujua case yake ni serious kiasi gani.

  NB:

  ..hivi ile zahanati ya Ikulu pale karibu na ofisi ya waziri mkuu imefungwa?

  ..vilevile hivi mnaona Muhimbili ni hospitali ndogo hiyo? je, kila mlalahoi[shangazi na mjomba kule kijijini] anaweza kufika hapo?

  ..siku JK akienda kuchomwa "shindano" kwenye zahanati ya Lugoba basi ndiyo nitaona yuko serious na kuondokana na dhana ya kutibiwa nje ya nchi.
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Tupo pamoja...hili la kwenda Muhimbili ni usanii tu 2010 ipo njiani...hizo ni pipi tu! Alikwenda magerezani hakuna kilichoboreshwa, alikwenda bandarini hali ni mbaya zaidi....
   
 13. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Rais angepanga foleni kumuona daktari ndugu? Rais anapanga foleni kwenye traffic barabarani?

  Tusiongee mradi tumeongea tu, hizo hoja sasa hazina mwelekeo. Nchi gani Rais anapanga foleni kupata huduma in the public square? Kumuita mtu Rais, moja ya maana zake na uzito wake ni kwamba tunampa dhamana ya heshima na kumpisha kwenye foleni.

  Halafu hujui, labda alikuwa na appointment na hao madaktari, ndio maana Wananchi wakasogea pembeni.
   
 14. C

  Choveki JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2009
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hofstede; Hata mimi naona kwa hilo apongezwe kwani kama unafuatilia viongozi wetu hata mafua inabidi wapande ndege wakatibiwe ulaya au india. Kama Mkuu wa kaya JK ameonesha kuwa yeye anatibiwa Muhimbili nadhani wengine wote watafuata mkumbo hata kwa shingo upande- si unajua wanavyojua kujipendekeza?

  Si lazima JK atoe tamko rasmi, yeye kuanza kutibiwa Muhimbili ni tamko tosha!- Na viongozi wengi walivyowaoga wa kumwaga unga watakuwa wanafoleni Muhimbili na kwingineko kama KCMC au Bugando!

  Ila, binafsi nahisi watakuwa wanaenda majuu kutibiwa kinyemela, si waziwazi kama ilivyo sasa.

  Once again, pokea tano JK kwa kuonesha mfano mzuri.
   
 15. RADIKALI

  RADIKALI Member

  #15
  Aug 30, 2009
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mchanga wa macho tu huo matibabu mengine yatafanywa mkishamchagua mwakani, ndio atakwenda marekani hapo ni geresha tu politics is a dirty game wahenga eeeehhhh
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Aug 30, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..jamani amekwenda kupimwa miwani. sasa hiyo mnaona ni big deal?

  ..ninavyoelewa mimi Muhimbili ni hospitali ya Rufaa, sasa JK alipata hiyo referal toka hospitali ipi?

  ..isije ikawa hata hicho kitendo chake cha kudamkia Muhimbili kwa ajili ya matibabu ni ukiukwaji wa taratibu.

  ..je, kupima miwani ni matatizo ambayo yanalazimisha aende Muhimbili, badala ya Mzani Mmoja, Mwananyamala, au Temeke?
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Aug 30, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mijitu mingine bwana, sasa akiumwa wakati yupo kazini ulaya, arudi bongo kutibiwa? Mijitu ya Ulaya mingapi ikiumwa hapa kwetu ina tibiwa hapa hapa?

  Mijitu mingine bwana kazi kuponda tu, hata haya haioni?

  JMK kaumwa Tanzania katibiwa Tanzania na for your information anaposafiri kote anafatana na Daktari wake official ambae ni kijana wa ki Tanzania aliebobea kwa tiba tofauti. Na kama yupo nje na kuumwa kwake kutahitaji vipimo au kulazwa Hospitali au uchunguzi wa Daktari bingwa wa tatizo lake, kwa nini asiende hospitali? na ikiwa yupo hapa nchini tumeona mfano, anakwenda hapo hapo panapotibiwa wa Tanzania wengine, hiyo pekee tosha kuwa motisha kwa wanaotowa huduma hapo Muhimbili.

  Hongera JMK kwa yote uyafanyayo, kuna mijitu yenye chuki binafsi hata ufanye nini kwao inakuwa si kitu, tena kila unapofanya zuri na jema wao ndio huzidi kukereka na kutafuta kila hila na mbinu ya kulifanya lionekane si jema, lakini mwisho wa siku, uyafanyayo kwa nchi na wananchi wako tunayaona na yote ni mema na yote yana nia njema kabisa, mwenye macho haambiwi tazama, mwenye masikio haambiwi sikia.
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Aug 30, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Uelewe kuwa JMK katika moja ya privileges zake kama Mkuu wa nchi, ana Daktari wake, na huyu Daktari wa JMK ni mTanzania na ametokea hapo Muhimbili na yeye ndie anaeweza kumpa referal ya kutibiwa panapoonekana anastahili kutibiwa. Si lazima akaanzie Mnazi Mmoja kama utakavyo wewe, after all, he is THE PRESIDENT of The United Republic of Tanzania and he must have his privileges.

  For your information, kitengo cha kupima miwani Muhimbili hakihitaji uwe na referal yoyote.
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Aug 30, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Donge tu!
   
 20. J

  JokaKuu Platinum Member

  #20
  Aug 30, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  Dar Es Salaam,

  ..asante kwa taarifa kwamba kupimwa miwani Muhimbili hakuhitaji referal.

  ..swali langu liko palepale: kwanini hakwenda Hospitali ya Mnazi mmoja,Temeke, au Mwananyamala?

  ..labda JK kwenda hospitali hizo za walalahoi anahitaji referal.

  ..JK kuwa na daktari Mtanzania siyo big deal. hilo lipo kwa viongozi wote wakuu.
   
Loading...