Kikwete ateua makatibu tawala watano

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
BAADA ya kukamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri na kuliapisha hivi karibuni, Rais Jakaya Kikwete ameendelea kupanga safu zake za watendaji katika ngazi mbalimbali baada ya ushindi wa Uchaguzi Mkuu.

Rais Kikwete ametangaza makatibu tawala wa mikoa mitano.

Uteuzi huo kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, unatokana na kustaafu kwa baadhi ya makatibu hao na wengine kushika nafasi za juu serikalini.

Kutokana na uteuzi huo, inatarajiwa pia Rais Kikwete atapangua safu za wakuu wa mikoa na wilaya, hasa baada yao kujitosa katika ubunge na kushinda na wengine kuteuliwa kuwa mawaziri.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), makatibu tawala walioteuliwa ni kwa mikoa ya Arusha, Kagera, Morogoro, Singida, Tanga na Tabora.

Iliwataja walioteuliwa ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Tamisemi, Evelyne Itanisa anayekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha kuchukua nafasi ya Nuru Millao aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Pia aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi Maadili Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Idara ya Maadili, Nassor Mnambila naye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, kuchukua nafasi ya Maria Bilia aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Mwingine ni aliyekuwa Katibu Tawala Msaidizi Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora, Liana Hassan anayekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Singida kuchukua nafasi ya Godfrey Ngaleya anayestaafu utumishi wa umma.

Aidha, Rais Kikwete amemteua aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mgeni Buruani kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro kuchukua nafasi ya Hussein Katanga ambaye aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.

Halikadhalika aliyekuwa Katibu wa Waziri Mkuu, Benedict ole Kuyan ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga kuchukua nafasi ya Paul Chikira ambaye amestaafu utumishi wa umma.

Uteuzi huo pia umempandisha cheo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, Kudra Mwinyimvua kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora anayechukua nafasi ya Theresia Mmbando ambaye amehamishiwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mmbando anahamishiwa Dar es Salaam kuchukua nafasi ya Assumpta Ndimbo ambaye anastaafu utumishi wa umma. Taarifa hiyo ilisema uteuzi huo ulianza rasmi Novemba 2, mwaka huu.
 
Mmmh, huyu Hussein Katanga hakuwahi kuwa hapa Dar es Salaam, manispaa ya Kinondoni akaondoka baada ya kupata kashfa?, enzi za RC Kandoro au Makamba nadhani. Sikumbuki ni kashfa gani though.
 
Ok,ni swala la mda acha mda ufanye maamuzi juu ya mambo yetu

mlio teuliwa hongereni cha muhimu ni kaziiiii,hatutakuwa na huruma juu yenu kwa kuto kuzingatia utawala bora.tupo nyuma yenu

mapinduziiiiii daimaaaa
 
Hongereni mlioteuliwa, kinachotakiwa sasa ni kuchapa kazi ili muoneshe tofauti iliyokuwepo.Naona wengi wa
o ni vijana tupu,cha muhimu wanatakiwa ku perform na waondokane na mawazo mgando ya watangulizi wao
o waliokuwa wagumu kubadlika na kuwa kikwazo kwa maendeleo kama vile Ngaleya aliyekuwa singida, Asu
mpta ndimbo wa hapa DSM na yule Chikira wa kule Tanga.
 
QUOTE=Nyambala:Hivi mna habari hao ndiyo wasimamizi wa uchaguzi?

Wasimamizi wa uchaguzi ni wakurugenzi wa halmashauri a.k.a District Executive Directors (DEDs). Hawa makatibu tawala wa mikoa uitwa Regional Administrative Secretary (DAS),na si wasimamizi wa uchaguzi.
 
QUOTE=Nyambala:Hivi mna habari hao ndiyo wasimamizi wa uchaguzi?

Wasimamizi wa uchaguzi ni wakurugenzi wa halmashauri a.k.a District Executive Directors (DEDs). Hawa makatibu tawala wa mikoa uitwa Regional Administrative Secretary (DAS),na si wasimamizi wa uchaguzi.

Unamaanisha RAS na sio DAS!!!
 
ndiyo wale kikiwete aliowaambia kuwa wakikosa nafasi kuna nafasi za bure kibao kwa hiyo wasihame.................WAMEPATA ZAWADI YA KIKWETE
 
Back
Top Bottom