Kikwete ateua Majaji Mahakama ya Rufaa

Mfumwa

JF-Expert Member
Aug 29, 2008
1,456
42
*Rais Kikwete ateua Majaji Mahakama
ya Rufaa
----
RAIS Jakaya Kikwete amewateua Jaji Salum Abdallah Legho Massati na Jaji William Steven Mandia kuwa majaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania.
Uteuzi wa majaji hao umeanza rasmi tangu Desemba 18,mwaka huu. Kabla ya uteuzi huu Jaji Massati alikuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Jaji Mandia alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi Dar es Salaam.Uteuzi wa majaji hao wawili umeifanya sasa Mahakama ya Rufani kuwa na majaji 16.

Source: Food For Thought
 
wajitahidi kupunguza rufaa na haswa za mauaji na wizi kutumia silaha maana ndio wamejaza sana magereza yetu....hongereni sana ila tunaomba mkaongeze ufanisi....
 
Masati kumpeleka rufaa ni kuipunguza kasi ya uongozi mahakama kuu, jamaa tangu ameingia pale kama jk aliipa sura yenye tumaini mahakama kuu, ni hardworking na msikivu kwa haki za wafanyakazi na umma

big up jmk na hongera mbuyi massati
 
Mkuu FDR,Jr,
Nadhani mkwere kafanya jambo jema.
Masati kupelekwa mahakama ya rufaa ni kupanda cheo kwasababu ya uchapaji kazi.Mlitaka Masati abaki mahakama kuu mpaka lini.
 
Kwa kumpandisha Mandia mkwere sasa naona anaanza kutumia uwezo kama kigezo cha kuwateua na kuwapandisha vyeo wachapakazi. Nadhani akiendelea namna hii mwaka ujao, ataanza kujitengenezea legacy ya kutukuka.
 
Mkuu FDR,Jr,
Nadhani mkwere kafanya jambo jema.
Masati kupelekwa mahakama ya rufaa ni kupanda cheo kwasababu ya uchapaji kazi.Mlitaka Masati abaki mahakama kuu mpaka lini.

Ni kweli jamaa ni mchapa kazi long time tangu akiwa wakili wa kujitegemea hadi kuteuliwa kuwa jaji wa mahakama kuu.
Na amekuwa akiendesha kesi kwa haraka na kwa umakini mkubwa.
Inasemekana pia ni mtu wa karibu sana na state, toka enzi za chenkapa sijui kama hilo lina influence yeye kupanda vyeo haraka haraka!!
BTW nami ninamtakia kila la kheri katika majukumu yake mahakama ya rufaa.
 
Hatuna majaji wa kutosha,

Hatuna wataalam wa kutosha

hatuna wataala wa kuangali na kuandika mikataba

hatuna viongozi walio bora!

yaani upuuuzi mtupu ,inakuwaje nchii inakuwa na majajai wazee,watu kama Jaji Makame ni watu amabo wanatakiwa kupumzika ila ndiyo kila siku wanapewa vyeo tu!
 
*Rais Kikwete ateua Majaji Mahakama
ya Rufaa
----
RAIS Jakaya Kikwete amewateua Jaji Salum Abdallah Legho Massati na Jaji William Steven Mandia kuwa majaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania.
Uteuzi wa majaji hao umeanza rasmi tangu Desemba 18,mwaka huu. Kabla ya uteuzi huu Jaji Massati alikuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Jaji Mandia alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi Dar es Salaam.Uteuzi wa majaji hao wawili umeifanya sasa Mahakama ya Rufani kuwa na majaji 16.

Source: Food For Thought

Hivi Jaji Kiondozi ni mdogo kicheo kwa jaji yoyote wa rufaa? Haya maakubwa tena. Ina maana marupurupu ya jaji wa rufaa yako juu kwa jaji kiongozi? Huko rufaa sasa wako wangapi?
 
Hivi Jaji Kiondozi ni mdogo kicheo kwa jaji yoyote wa rufaa? Haya maakubwa tena. Ina maana marupurupu ya jaji wa rufaa yako juu kwa jaji kiongozi? Huko rufaa sasa wako wangapi?[/QUOTE]

mkuu wamefikia 18 according to mtoa habari,au hujamsoma vizuri mfumwa???
hebu cheki nae tena.
 
...yaani upuuuzi mtupu, inakuwaje nchii inakuwa na majajai wazee, watu kama Jaji Makame ni watu amabo wanatakiwa kupumzika ila ndiyo kila siku wanapewa vyeo tu!
Mkuu, hizi ndio athari za zama za ruksa ambazo wengi waliona kisomo hakina maana na kugeukia "mission-town". Ukiangalia kwa makini utaona sekta nyingi sana zina gepu za watumishi; kuna generation ambayo mchango wake umekuwa mdogo ktk kutoa watumishi na wataalam, hivyo kufanya waajiriwa wengi kuwa wazee sana na vijana wa miaka ya 75 kwenda juu.

Hakuna haja ya kunyooshea mtu kidole lakini yapasa kuwa fundisho ili hali hiyo isirudie tena. Yapasa kutoa elimu kwa watu wetu na sio kumwaga mabilioni bila kuzingatia kama mlengwa ana elimu ya kuizalisha au la. Kosa kama hilo linaweza kuchangia watu kutoona umuhimu wa shule kwa kudhania njia za mkato za mafanikio.
 
Mkuu FDR,Jr,
Nadhani mkwere kafanya jambo jema.
Masati kupelekwa mahakama ya rufaa ni kupanda cheo kwasababu ya uchapaji kazi.Mlitaka Masati abaki mahakama kuu mpaka lini.

Big Up! to Muungwana
 
Angalau sekta ya haki imekumbukwa. Tatizo la upungufu wa wanasheria competants ni kubwa kwa Tanzania and lets hope litamalizika miaka ya hivi karibuni baada ya kuwepo kwa School of Law ambayo sasa wahitimu wa sheria vyuo vikuu, wanakuwa mawakili moja kwa moja. Tungechelewa kidogo tuu, mawakili wa Kenya wangevamia Tanzania baada ya kusainiwa kwa Free Labour Migration kwa nchi za EAC.
 
Back
Top Bottom