akashube
JF-Expert Member
- Dec 24, 2009
- 401
- 23
Kamati kuu ya CCM inayomaliza muda wake mwaka 2012 imeacha 'legacy' ya kukumbatia ufisadi na kukigawa chama cha mapinduzi. Kati ya wananchi wa Tanzania na Mafisadi kamati kuu ya CCM imechagua Mafisadi kwa kumtwangilia mbali mheshimiwa Samwel Sita na kufagia ndoto zake za kumalizia kazi aliyoianza ya kuendesha bunge kwa 'speed and standards', kazi ambayo imekubalika sana kwa wananchi.
Hivi sasa Samwel Sita ndiye kiongozi bora kuliko kiongozi yeyote wa CCM kwa kuwa kuna 'legacy' ameacha kwa wananchi wa Tanzania. Sita ataendelea kukumbukwa na watanzania kwa karne nyingi zijazo.
SUALA ZITO
Leo hii mchana huu, mheshimiwa Anne Makinda atataja jina la waziri mkuu ambalo ndilo litakalothibitisha kama Kikwete ana mkono wake kwenye kuunga mkono mafisadi au la.
Endapo Mizengo Pinda atarudi, basi hii inaonyesha Kikwete anataka kujitwalia yeye sura ya kuogofya na kuula mkate wote peke yake maana huyu Pinda ni mtu asiye na jipya. Anafanya kazi ya uwaziri mkuu kama bado yuko 'secret service'. Anasubiri amri na hana jambo lake jipya, japo ni muadilifu.
Endapo atatuletea E. Lowasa au mwanamtandao yeyote hii itaonyesha kuwa Jakaya ameamua kulipa fadhila kwa waliomsaidia kuchakachua matokeo.
Akichagua mwanamke, itaonyesha kabisa Jakaya anataka kukumbukwa kama mnafiki aliyeamua kujianika waziwazi maana ingekuwa vema kama angewaachia wanawake kiti cha urais ili tujue kwamba kweli amekusudia...badala ya kuomba yeye amalizie muda wake, ila wengine wapishe jinsia nyingine.
SWALI
Jakaya Kikwete, unataka kukumbukwa kwa lipi na watanzania. Waziri mkuu utakayemteua ndiye atakaye kubeba au kukubomoa na kubomoa CCM kabisa.
USHAURI
Wape mapenzi watanzania, mtu ambaye wamempima wakaona anajali maslahi ya watanzania kuliko maslahi ya CCM, ufisadi au upuuzi. Mtu asiyeogopa mafisadi, tupe Sokoine mwingine. Kwa hili Jakaya Kikwete hata baada ya urais wako utatembea kifua mbele.