Kikwete atakiwa kuisafisha CCM -WAZO LA BURE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete atakiwa kuisafisha CCM -WAZO LA BURE

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 14, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,485
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  Kikwete atakiwa kuisafisha CCM [​IMG] [​IMG] [​IMG] Molloimet akerwa na kauli za mzaha za Makamba

  Na Mohamed Hamad, Manyara

  MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya mrisho Kikwete ametakiwa kuchukua maamuzi magumu kukisafisha chama hicho kabla ya matokeo yake kumfika mwaka 2010.

  Rai hiyo imetolewa na kada wa chama hicho wa muda mrefu, Bw. Lepilal Ole-Molloimet alipozungumza na Majira juu ya hali ya kisiasa ndani ya chama hicho na kulaani kauli ya Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba kuwa 'Wanaotaka ang’olewe wasubiri afe'.

  Alisema umefika wakati kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais kikwete kutoa maamuzi magumu ya kukisaidia chama ya kuwanyofoa watu walafi madarakani ambao kazi zao zimefahamika kuwa za maslahi binafsi.

  Ukimya wa mwenyekiti unaendelea kumgharimu katika utawala wake, kwa kuwa hakuna kinachotendeka bali malumbano ya muda mrefu yasiyo na tija kwa wananchi huku yakiachwa mambo ya msingi kwa wananchi.

  Alimtaka mwenyekiti huyo asiwaonee haya kuwanyooshea kidole viongozi waovu kwa kuwa wanaonekana kubinafsisha CCM ambayo ni chama cha wakulima, wafanyakazi.

  Akizungumzia kauli ya Bw. Makamba alisema: “Mimi ni Kada wa CCM wa muda mrefu tumekuwa tukiongozwa na Mwasisisi wa chama hiki, Mwalimu Nyerere. Yeye hakuwa na kauli ya mamna hii hata siku moja, na ndio maana hata leo hii tunaendelea kumuenzi yale yote mazuri aliyoyafanya,” alisema Ole Molloimet.

  Alisema kauli hiyo inaonyesha ni ya kibabe, yenye utovu mkubwa wa nidhamu kisiasa, sio ya wana CCM niya upotoshaji ambayo inaonyesha kuwa chama hicho ni cha watu wachache kwa maslahi yao waliyopo madarakani.

  Alisema CCM hairithishi mtu uongozi na ndio maana kuna demokrasia ambayo inatakiwa kuzingatiwa kwa kauli za Bw. Makamba hazina mafunzo ya kuiga kwa kizazi kijacho.

  Alisema kauli hiyo inakatisha tamaa wanachama wa CCM na kujiona kuwa hawana chao, bali chama ni cha akina Makamba na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi ambao wamekaidi kujiuzulu badala yake wamekuwa ving’ang’anizi.

  “Chama kimekuwa kichaka cha baadhi ya watu kuficha maovu yao ambao wananeemeka wakidhani wananchi hawayafahamu na kujipa moyo kuwa wao ndio wasemaji wakuu kuliko wenye chama.

  “Maamuzi ya chama ni kauli za wanachama wakiongozwa na katiba na si kauli isiyokuwa na maadili kama ya Bw. Mkamba kwa wanachama ambao ni waadilifu na wenye uwezo mkubwa kimaamuzi kuliko yeye,” alisisitiza Ole-Molloimet.

  Akizungumza na Majira jana, Bw. Makamba alisema kauli yake haikuwa na lengo baya, bali alitaka kuwahusia watoto kwenye mahafali kuwa waipende nchi yao kwa kuwa muda wake umeshakwenda.

  Bw. Makamba hivi karibuni alikaririwa akisema 'wanaotaka ang'olewe wasubiri amalize miaka minne iliyosalia kwenye maisha ya binadamu ambayo ni miaka 75, wakati yeye amefikisha 71.

  Kada huyo alitolea mfano malumbano yanayochukuwa muda mrefu yasiyo na tija kwa wananchi ya viongozi kushushuana, kuitana mafisadi, huku wengine wakidaiwa sio wana-CCM.

  “Serikali haiongozwi kiundugu, inaongozwa kwa uadilifu mkubwa baada ya kupata ridhaa kwa wananchi ambao ndio wenye kauli na si walio madarakani kujiamulia na kuwashurutisha wananchi ambao sasa wanajua na majibu yake yataonekana mwaka 2010” alisema Ole-Molloimet.

  Alisema maadili ya uongozi yamekiukwa na hao hao walioko madarakani kwa kuheshimu pesa kuliko utu na hata baadhi ya wanaoingia madarakani hasa wanasiasa, lengo lao ni kuchuma pesa tu.
   
Loading...