Kikwete ataka tatizo la ajira Afrika lipatiwe majibu haraka

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
jk%282%29.jpg



Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Rais Yoweri Museveni wa Uganda huku Katibu Mtendaji wa Kamati ya Kimataifa ya Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) anayemaliza muda wake, Balozi Liberata Mulamula, akitega sikio katika siku ya 2 ya mkutano huo wa viongozi wakuu wa ICGLR mjini Kampala jana.

Rais Jakaya Kikwete, amesema ukosefu wa ajira kwa vijana wa Afrika ni jambo kubwa linalohitaji umakini na kutatuliwa haraka bila ya kucheleweshwa tena na viongozi wa bara hilo.


Amesema uharaka wa kupata majawabu ya tatizo hilo unatokana na ukweli kuwa kila nchi ya Afrika inazalisha jeshi kubwa la vijana wasiokuwa na ajira wanaoingia katika soko la ajira kila mwaka baada ya kumaliza shule.

Alitoa rai hiyo kwa viongozi wenzake wa Afrika jana, alipokuwa anashiriki mjadala kuhusu mada ya ukatili wa

kijinsia katika nchi za eneo la Maziwa Makuu, kwenye siku ya kwanza ya mkutano wa mwaka huu wa wakuu wa nchi wanachama wa eneo hilo.


Kuhusu pendekezo kuwa wakubwa wa ICGLR wajadili tatizo hilo katika kikao kijacho cha wakuu wa nchi hizo katika miaka miwili ijayo mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Rais Kikwete amewaambia wakuu wa nchi na Serikali wenzake:


“Suala hili ni la haraka. Linahitaji mjadala wa kina na makubaliano makini na majawabu sahihi ya jinsi ya kupambana na jeshi la vijana linaloingia katika soko la ajira kutoka shule na vyuoni kila mwaka. Hatuwezi waheshimiwa viongozi kuendelea kusubiri miaka miwili kujadili suala hili sasa.”


kufuatia pandekezo lake, viongozi hao wa ICGLR wamekubaliana kuwaagiza mawaziri wao wanaohusika na ajira na sekta zinazohusiana na ajira kukutana haraka katika muda wa miezi sita ijayo kujadili na kutoa mapendekezo kwa serikali za nchi wanachama wa ICGLR kuhusu namna zinaweza kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na watu wengine.


CHANZO: NIPASHE
 
Anataka tatizo la ajira litatuliwe na nani?! Tatizo la nchi yetu kila mtu analalamika hadi Rais analalamika..tutafika tu ka tumeweza kufika kwa miaka 50 ya uhuru kwa mtindo huu
 
Hizi ba.nge mbichi na viuno anavyokata vinamuwewesesha sn mpaka anaonekana ka zuzu, kwake ni % ngapi ya vijana wenye ajira? Na nikwanini hawana? Sbb za kufungwa kw viwanda vingi Tz ni zipi?
 
Nyumbani kwake Tanzania ajira kitendawili iweje aanze kuzungumzia Africa? Maana lazima hao unaowahamasisha kuongeza nafasi za ajira wajifunze kutoka kwake Tanzania.
 
ajira zipi za kikwete? mshahara 146000 kwa mwezi ndo ajira?
aendelee tu kula maisha...sisi tunajua tutaishi vipi?
kazi kuwalaghai wazee wa dar kwa pilau nk ndo iliyompendeza.
 
Awape mbinu hao viongozi wenziwe jinsi "alivyoshuhulikia" swala la ajira Tanzania! Sijui anapata wapi ujasiri wa kuongelea ajira kwa vijana!
 
our president is handsome jamani wacha auze sura.
kwani hamjui sio kila mvaa suti analalia godoro wengine mkeka
 
Dokta bwana, hotuba zake zinanikooooosha! Ila mi ningeshauri aongeze idadi ya wabunge wa viti maalum ili tupate ajira hiyo tukale ongezeko la posho ya kukabiliana na maisha ya idodomya
 
Back
Top Bottom