Kikwete at Subhash Patel fund raiser ... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete at Subhash Patel fund raiser ...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pundit, Mar 14, 2008.

 1. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Kikwete is still embracing Jeetu Patel, to the extent of gracing his fundraiser despite the recent turn of events.I wonder what message will this send to law enforcement officers who are supposed to go after somebody like Jeetu Patel.

  [​IMG]


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mkewe Mama Slama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na MaendeleoWAMA kwa kuchangia shilingi milioni moja katika mfuko wa elimu wa wilaya ya Bagamoyo wakati wa harambee iliyofanyika katika hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam Ijumaa jioni.Katika Harambee hiyo zaidi ya shilingi milioni tisa zilichangwa.Katikati ni Mwenyekiti wa harambee hiyo Bwana Jeetu Patel.

  Pic and caption from BongoPix
   
  Last edited by a moderator: May 3, 2009
 2. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hivi umaskini gani una nafuu?
  1, Akili?
  2,Pesa?
   
 3. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2008
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Tukumbishe ilikuwa tarehe ngapi maana wengine tulikuwa Tanganyika
   
 4. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Huyo ni SUBHASH PATEL siyo JEETU PATEL!

  Subhash ndiye mwenye makampuni wa M M steel mzaliwa wa bagamoyo wamosoma na kikwete pamoja

  Jeetu Patel ndiye fisadi aliyechota mabilioni benki kuu
   
 5. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #5
  Mar 14, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Haaaa haaaa, hiyo ndiyo CCM bwana. Guys, we should stop whining, treachery and corruption are difficut to break if you are used to them. Let's organise; it is action that will save our country and not our anger and frustration!
   
 6. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Karibu sana
  Pili acha kuwa mwonga, hawa akina Patel tokea lini wakawa wazaliwa wa Bagamoyo bwana? Tafuta njia nyingine ya kutetea haya Mafisadi, sio hii
   
 7. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa nataka kumhukumu Jk hapa,lakini kwa sababu yako Bwana Mdogo naahirisha hadi nipate memba mwingine atupe maelezo ya ku support post yako.Itakuwa vema kama pia tupate picha ya Jeetu Patel ili kuwatofautisha hawa wawili.

  Na kwa huyu anayeuliza juu ya umaskini mbaya zaidi katika akili au pesa itakuwa ime mtouch sana habari hii.Nadhani amepumua baada ya kusoma ufafanuzi wako.
   
 8. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2008
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,612
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  Jamani huyo sio jeetu Patel. Patel wapo wengi sana Tanzania. So, please go back to you facts check
   
 9. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hapa tunapata jibu la umaskini wenye nafuu baina ya pesa na akili.
   
 10. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Ahsanye BabaH

  Mie sina nia ya kutetea mafisadi,wewe inaelekea humjui huyo subhash patel,nilikuwa naelezea huyo jsiyo eetu patel!Ina maana akina patel huwa hawazai humu Tanzania?kila patel ni mzaliwa wa India?
  labda wewe unamjua vizuri tuelezee huyo subhash patel ni nani?
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ila si jambo la kushangaza ata kama angekuwa yeye Tz hii kuna watu wana vichwa vya kuku ie wepesi wa kusahau mambo.

  Ila afadhali sio Jeetu mwenyewe manake tusi lilitaka kunitoka apa kwa maana ingekuwa zarau kwa watz.

  Ebu mwenye data atumwagie asije akawa ukoo mmoja na mbaya wetu Jeetu.
   
 12. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hata nami nilikuwa nataka kuaanza kurusha laana kwa viongozi wote wa serikali, ingekuwa huyu ni jeetu patel.

  jee huyu wa kwenye picha na jeetu wana uhusiano wowote? au imetokezea tu bahati "mbya" kuwa na jina linalofanana?
   
 13. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wanauhusiano wote ni mafisadi, nadhani huyu Subhash Patel ndiye anayemjengea Castel lake Muungwana kule Lugoba!!
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mod tafadhali badili heading hapo, isomeke Kikwete at Subhash Patel fund raiser ...
   
 15. T

  TechMaro Senior Member

  #15
  Mar 14, 2008
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Na Mwandishi Maalum
  Date: 14 March 2008

  RAIS Jakaya Kikwete juzi usiku aliwaongoza wadau wa elimu na wafanyabiashara katika kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 882 ya sekondari mpya zinazotarajiwa kujengwa mkoani Dar es Salaam kupunguza uhaba wa shule.


  Katika chakula cha usiku kilichoandaliwa katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski na Mwenyekiti wa Kamati ya Kuchangisha fedha hizo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro, zaidi ya Sh milioni 600 zilichangwa.


  Uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ulianza Septemba 21, mwaka huu na hadi kufikia juzi mchana Sh bilioni 6.7 zilikuwa zimekusanywa kupitia kwa Kandoro. Sh bilioni 10 zinahitajika.


  Katika chakula hicho cha usiku, wafanyabiashara na wadau mbalimbali walichangia fedha taslimu, ahadi, hundi na ahadi za kujenga madarasa au kununua madawati kwa ajili ya shule zitakazojengwa.
  Mfanyabiashara maarufu nchini, Azim Dewji aliongoza harambee ya kujenga madarasa kati yake na wafanyabiashara wenzake na kuahidi kujenga madarasa 10 yenye thamani ya karibu Sh milioni 100.


  Rais Kikwete alichangia Sh milioni tatu, Mkuu wa Majeshi Davis Mwamunyange alichangia Sh milioni 57, Shubash Patel Sh milioni 100 na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano (TCRA) Sh milioni 15.


  Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Margaret Sitta alisema nia ya kuongeza madarasa inatokana na uchungu wa kuona watoto wengi wanafaulu Dar es Salaam, lakini wanakosa shule za sekondari za kujiunga.


  Alitoa mfano mwaka 2005 kati ya wanafunzi 17,000 waliofaulu, ni 4,143 tu ndiyo walikwenda sekondari na kwa mwaka jana kati ya wanafunzi 21,974 waliofaulu ni 4,771 tu walikwenda sekondari waliobaki wote hawajulikani walikwenda wapi na wanafanya nini sasa.


  Source: Radio Free Africa,
  http://www.radiofreeafrica.co.tz/Ujenzi%20wa%20sekondari%20Dar%20wafikisha%20bilioni%206.7.html
   
 16. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Oops kumbe ile habari siku zile za hekalu kujengwa ni valid ? Maana watu waliipinga sana leo naona inakuwa kweli .Haya tuendelee .Mke wa Rais kajaa ma gold kila mahali Watanzania wanakufa njaa Pemba .
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu wa majeshi alichangia milion 57 ? Za kwake ama toka jeshini ? Vipi hali ya wanajeshi wetu kuanzia uniform hadi mlo na familia zao ?
   
 18. Tulamanya

  Tulamanya Senior Member

  #18
  Mar 14, 2008
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Techmaro,

  Asante sana kwa kuleta hiyo habari hapa! Cause watu wengine walisha anza kutuletea udaku bila kuwa na facts muhimu! I like that!
   
 19. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu wa Majeshi anatoa milioni 57, pesa za jeshi huku wanajeshi wake wako hoi?

  Haya ni matumizi mabaya sana ya pesa za umma. Kwenye michango watoe pesa zao za mfukoni na sio pesa ambazo zimetengwa na budget kwa kazi zingine.

  Kinachofanyika sasa ni kuhamisha toka huku na kupeleka kwingine.
   
 20. Tulamanya

  Tulamanya Senior Member

  #20
  Mar 14, 2008
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtz,
  Hizi ni pesa ambazo mabosi wa vitengo hutengewa kwa ajili ya CSR so hata kama asingechangia huko angezipeleka sehemu nyingine au kuzirudisha wizarani (note bado miezi mitatu) fedha zote zilizo bakia inatakiwa zirudishwe hazina!

  Cha msingi ni kujiuliza, uchangiaji wa madarasa was the only best priority ya huyu mkuu?
   
Loading...