Kikwete asibweteke

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Date::10/10/2008
CUF: Kikwete asibweteke kama Musharraf
Salim Said na Edson Kamukara
Mwananchi

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimemtaka Rais Jakaya Kikwete asibweteke na sifa anazomwagiwa na mataifa ya Magharibi na mashirika ya kimataifa,na badala yake atafute mbinu za kuwaridhisha Watanzania ambao walimchagua.

Tahadhari hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kuhitimisha maandamano ya chama hicho ya kuishinikiza serikali kufikisha mahakamani watuhumiwa wa ufisadi.

Seif, waziri kiongozi wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), alisema sifa ambazo Rais Kikwete anazipata nje hazitamsaidia kitu iwapo Watanzania hawaridhiki na utendaji wake katika serikali anayoiongoza.

"Kikwete amebweteka sana na sifa za nje," alisema kiongozi huyo kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya watu baada ya maandamano yaliyoanzia makao makuu ya CUF yaliyo Buguruni.

"Nchi inayumba kutokana na tabia ya Rais kusafiri mara kwa mara kutafuta sifa kutoka kwa mataifa ya nje huku akikosa muda mzuri wa kuwatumikia wananchi wake waliomuweka madarakani.

"Rais Perves Musharraf wa Pakistan alikuwa anasifika na kukubalika katika mataifa yote ya magharibi na mashirika ya kimataifa, lakini baada ya wananchi wake kuamua, aliondoka madarakani kwa nguvu ya umma na shinikizo la washirika hao.

"Mimi nakuomba sana Rais Kikwete, kwa sababu wewe ni rafiki yangu mkubwa, kwamba japokuwa una sifa nzuri sana katika mataifa hayo, usibweteke na sifa hizo. Watendee wema wananchi na kwa leo Watanzania wanachotaka ni kuwafikisha mahakamani na kuwataja hadharani mafisadi wote."

Rais Kikwete amekuwa akilalamikiwa tangu alipotangaza nafuu kwa mafisadi waliochota Sh133 bilioni kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) alipowataka warejeshe fedha hizo ifikapo Oktoba 31, na iwapo watashindwa wafikishwe mahakamani Novemba mosi.

Pamoja na kutoa nafuu hiyo kwa mafisadi hao, Shirikisho la Kimataifa la Fedha (IMF) lilisema hivi karibuni kuwa linaridhika na hatua zilizokwishachukuliwa na serikali katika kushughulikia kashfa hiyo, kauli ambayo pia imekaririwa na Benki ya Dunia, Marekani na baadhi ya nchi wahisani.

Lakini katibu huyo wa CUF alisema mataifa na mashirika hayo ya kimagharibi hayana urafiki wa kudumu kwa kuwa hayachelewi kumgeuka mtu wakati yanapoona kwamba hayana maslahi naye tena.

Naye Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Profesa Ibrahim Lipumba alisema chanzo cha matatizo na majanga yanayotokea nchini ni ufisadi.

Alisema ufisadi ni adui wa umma na kwamba umeleta mmomonyoko wa maadili baina ya watumishi, jambo ambalo linasababisha kutokea majanga na matatizo mbalimbali nchini.

Prof Lipumba alirejea kauli yake juu ya vifo vya watoto 19 vilivyotokea katika sherehe za sikukuu ya Idd el Fitri mkoani Tabora kwamba vimesababishwa na ufisadi wa serikali ya CCM, ambayo alisema imeuza maeneo yote ya wazi yaliyowekwa maalumu kwa ajili ya michezo ya watoto.

"Maeneo ya wazi yote yameuzwa mkoani Tabora na kujengwa majengo mbalimbali, maofisi na magereji na watoto wanakosa mahali pa kusherehekea Idd mpaka wanaingizwa ndani ya ukumbi wa klabu ya usiku ya starehe (night club) ambao si salama," alisema Prof Lipumba.

Alisema maisha ya Watanzania yamekuwa magumu mno na kwamba ameshuhudia akina mama wanapanga msululu kununua utumbo, vichwa na miguu ya kuku kwa ajili ya chakula.

Naye mwenyekiti wa sekretarieti ya vijana, Mohammed Babu alimtaka Rais Kikwete kushughulikia mambo matano kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

"Tunataka Rais Jakaya kwanza aondoshe migogoro na migomo kwa wafanyakazi wa sekta mbalimbali za umma, aondoe mfumko wa bei ya bidhaa muhimu, mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar, katiba mpya na aunde tume huru ya uchaguzi," alidai Babu.
 
Date::10/10/2008
CUF: Kikwete asibweteke kama Musharraf
Salim Said na Edson Kamukara
Mwananchi

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimemtaka Rais Jakaya Kikwete asibweteke na sifa anazomwagiwa na mataifa ya Magharibi na mashirika ya kimataifa,na badala yake atafute mbinu za kuwaridhisha Watanzania ambao walimchagua.

Tahadhari hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kuhitimisha maandamano ya chama hicho ya kuishinikiza serikali kufikisha mahakamani watuhumiwa wa ufisadi.

Seif, waziri kiongozi wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), "


Tuweke rekodi sawa. Seif siye Waziri Kiongozi wa kwanza wa SMZ. Waziri Kiongozi wa kwanza ni Mheshimiwa Ramadhan Haji Faki.
 
Back
Top Bottom