Kikwete ashauriwa kuivunja serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete ashauriwa kuivunja serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Korosho, Dec 12, 2008.

 1. K

  Korosho Senior Member

  #1
  Dec 12, 2008
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 132
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kikwete ashauriwa kuivunja serikali


  Mwandishi Wetu

  Disemba 10, 2008

  RAIS Jakaya Kikwete, ameshauriwa kuvunja Serikali ili aunde ya mpito itakayoanzisha mchakato wa kujenga misingi mipya ya mwafaka wa kitaifa.

  Ushauri huo ulitolewa wiki hii na wananchi wa Mwanza waliohudhuria mkutano wa hadhara katika viwanja vya Sahara, mkutano ulioandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Katika mkutano huo ambao msemaji mkuu wake alikuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, wananchi waliokuwapo katika mkutano huo wakiwamo baadhi ya wazee wa Mwanza waligusia mambo kadhaa yanayopaswa kutatuliwa kwa pamoja.

  “Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete atangaze kipindi cha mpito (transition period), aivunje serikali yake na kuunda utawala wa mpito ambao utawezesha kuanza kwa mchakato wa kujenga misingi mipya na ya mwafaka wa kitaifa,” linaeleza tamko la wananchi hao waliloliita Azimio la Mwanza.

  Miongoni mwa mmambo waliyopendekeza kuhusishwa katika mwafaka ni pamoja na Mfumo na muundo wa Muungano, nafasi ya dini katika mfumo wa utawala, Misingi imara ya kusimamia masuala ya kijamii kama haki ya kupata elimu na huduma za afya.

  Tamko lenyewe limeanza kwa kusema:

  Sisi wananchi wa mkoa wa Mwanza tuliokutana hapa jijini Mwanza kwa ajili ya mkutano wa hadhara wa CHADEMA leo tarehe 5 Disemba 2008, na baada ya kupata taarifa ya ziara ya Operesheni Sangara ya viongozi wa CHADEMA kutoka katika majimbo manane ya Mkoa wa Mwanza, wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma Ndugu Kabwe Zuberi Zitto (Mb), tunapenda kuazimia yafuatayo;

  Tunasikitishwa sana na kiwango cha Ufisadi katika Taifa letu na hivyo kulifanya taifa kupoteza rasilimali fedha nyingi ambazo zingeweza kusaidia maendeleo ya wananchi na kutuondoa katika dimbwi la umasikini; Ufisadi ambao sasa umeanza kuleta nyufa katika misingi ya uhai wa taifa letu;

  Kwa kutaja tu baadhi ya mabilioni ya shilingi ambayo yamefujwa kutokana na wizi, ufisadi, mikataba mibovu na ubadhirifu wa rasilimali fedha za Watanzania ni pamoja na;

  Akaunti ya madeni ya nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania 133bn
  Kampuni ya Meremeta na Tangold 155bn
  Kampuni ya Deep Green 10bn
  Mapato ya kikodi kutoka makampuni ya Madini kwa miaka 10 (15% allowance clause kutoka sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004 baada ya marekebisho ya sheria ya fedha 1997) 883bn
  Misamaha ya kodi ya mafuta kwa makampuni ya Madini kuanzia 2005 170bn
  Mkataba wa IPTL (3bn kwa mwezi) 168bn
  Mkataba wa Richmond (wabunge na vyombo vya habari viliokoa) 172bn

  Tunatambua hatua ambazo zimeanza kuchukuliwa kutokana na baadhi ya tuhuma ambazo tumezitaja hapo juu kwa baadhi ya wafanyabiashara na viongozi wa kisiasa kufikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa mujibu wa sheria; Hata hivyo tunahisi na tunasisitiza kuwa hatua hizi haziwezi kumaliza tatizo la rushwa kubwa hapa nchini ama ufisadi kwani hatua za aina hii zimewahi kuchukuliwa huko nyuma na zinawaacha watuhumiwa wengi ambao wana makosa ya aina hiyo hiyo kwa kutokana tu na misingi ya kisheria na kikatiba;
  Kwa mfano, tunakumbusha ya kuwa katika kipindi cha utawala wa Rais Benjamin Mkapa, aliyekuwa Waziri wa Ujenzi na Katibu Mkuu wake wakati wa utawala wa Rais Mwinyi (Nalaila Kiula na Dk. Mlingwa) walifikishwa mahakamani kwa kosa la rushwa wakiwa viongozi wa umma na hatimae wote walisafishwa kimahakama.

  Hii ni dhahiri kwamba hata kesi za sasa zinaweza kuishia katika mazingira ya aina hiyo hiyo. Aidha ikumbukwe kuwa baada ya hatua hiyo, vitendo vya rushwa na ufisadi viliendelea kukithiri katika utawala wa Rais Mkapa.

  Kwa hiyo hofu yetu ni kuwa hatua zinazochukuliwa hivi sasa zinaelekea kuisafisha tu serikali na sio kuvunja misingi ya ufisadi ndani ya mfumo wa utawala wa nchi yetu; Tunataka Taifa letu lirudi kwenye misingi ya umoja, haki, usawa mbele ya sheria na mshikamano wa kitaifa.

  Ufisadi umeanza kubomoa kabisa misingi imara ya Taifa letu. Hivyo, hatua madhubuti zapaswa kuchukuliwa kuhusu ufisadi ili kumaliza kabisa mianya ya ufisadi wa kimfumo ulioshamiri (Institutional corruption);

  Tunajua ya kuwa, kwa mfano, katika ufisadi uliofanyika katika akaunti ya madeni ya Nje (EPA) Benki Kuu ya Tanzania, kampuni moja ya Kagoda Agricultural Limited ilichota takribani 40bn wakati wa kampeni za uchaguzi na tunaamini kuwa fedha hizo zilitumiwa na Chama Cha Mapinduzi kufanyia kampeni zake na kufanikiwa kushinda Urais, Wabunge na Madiwani kwa kishindo.

  Ndio maana serikali imepata kigugumizi kutaja wamiliki wa kampuni ya Kagoda. Vilevile misamaha ya kodi ya mafuta kwa kampuni za madini ilitolewa katikati ya kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na kwa hiyo tuna mashaka kuwa makampuni haya yaliisaidia CCM; Hivyo hivyo kwa fedha kupitia kampuni ya Deep Green.

  Kwa hiyo tunasisitiza kuwa serikali ambayo imeingia madarakani kwa kutumia fedha za kifisadi kamwe haiwezi kusafisha ufisadi; Vilevile chama kilichochukuwa utawala kwa kutumia fedha za ufisadi hakiwezi kudhibiti serikali yake wala kuunda serikali ambayo haitokani na ufisadi.

  Hivyo basi, tunatoa matamko yafuatayo;

  1.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete atangaze kipindi cha mpito (transition period), aivunje serikali yake na kuunda utawala wa mpito ambao utawezesha kuanza kwa mchakato wa kujenga misingi mipya na ya mwafaka wa kitaifa kwa masuala yafuatayo;
  (i) Mfumo na muundo wa Muungano,

  (ii) Nafasi ya dini katika mfumo wa utawala,
  (iii) Misingi imara ya kusimamia masuala ya kijamii kama haki ya kupata elimu, huduma za afya nk.

  2.Kuainisha tunu za Taifa ambazo zitaongoza mienendo ya uongozi wa nchi, vyama vya siasa na jamii kwa ujumla.
  3.Kuandika Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo mbali na matakwa ya tamko namba 1 hapo juu itaweka misingi ya utawala wa maadili ya Taifa na Utaifa, mfumo wa uchaguzi na kuweka sheria mpya ya uchaguzi itakayokidhi misingi ya demokrasia ya vyama vingi na itakayodhibiti matumizi ya fedha katika kampeni.

  4.Iundwe mahakama maalumu (Special Tribunal) kwa sheria ya Bunge itakayofanya kazi ya kupitia masuala yote ya rushwa kubwa kubwa zinazotajwa na zisizotajwa, itakayotoa nafasi kujua ukweli mtupu kuhusu ufisadi na kujenga maridhiano ya Taifa.

  5.Mapendekezo ya Taarifa ya Bomani kuhusu sekta ya madini itekelezwe mara moja ili taifa lianze kunufaika na rasilimali zake za Madini.
  Tunaomba atanzania wa mikoa mingine yote watuunge mkono katika maudhui ya Azimio hili ambalo sisi wananchi wa Mwanza tunaona linaweza kuliokoa Taifa letu na kulirejesha katika misingi ya uanzishwaji wake na waasisi wetu.  Maoni Yangu : Naunga mkono hoja na mapendekezo. Sio siri serikali iliyopo madarakani imeingia kwa misingi ya rushwa hivyo haiwezi kupiga vita rushwa.
  Iundwe serikali ya mpito yenye watu credibal na sisi kama nchi tuanze upya. Tuache kufurahia "sarakasi" zinazoendelea na kamata kamata wakati "wakamatwaji" na "wakamataji" wanajuana kwa vilemba.

  Haina maana kuendelea kupoteza muda na fedha kuhusu uchunguzi wa kampuni kama Kagoda wakati kila kitu kinafahamika. Huu ni unafiki, na kama nchi hatuwezi kusonga mbele. Ni mpaka tutakapoamua kuacha "longolongo" na kuwa watendaji na kuzikabili changamoto kwa jinsi zinavyokuja.
   
 2. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2008
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Imekaa vizuri sana kwa kusema lakini nafikiri hii itakuwa Ndoto za Mchana. Hata Binadamu hakuna anayekubali KUWA MUME MWENZA
   
 3. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2008
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Dini zisiwekwe kabisa kwenye mfumo wa utawala; constitution iendane na priorities zetu kama waTanzania. dini ziachiliwe mbali na waumini wenyewe.
   
 4. K

  Korosho Senior Member

  #4
  Dec 12, 2008
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 132
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ili upone ugonjwa ni LAZIMA upate matibabu, upende usipende, hata kama matibabu hayo yatahusisha kunywa dawa chungu au sindano kali sana.

  Ili tusonge mbele, ni LAZIMA tufanye mapinduzi ya kifikra na vitendo....

  Nchi zote kubwa hazikufika hapo zilipo bila kupitia vipindi vigumu kabisa katika historia za nchi zao. Ni katika kupitia michakato hiyo ndipo viwango (standards) ziliwekwa ili watu wote wazifuate.

  Ni kutokana na demokrasia ya hali ya juu, nchi kama Marekani, Gavana wa Illinois ameshitakiwa kwa "intention" ya kutaka rushwa, au rais anaweza kuwa impeached for undue personal behaviour.

  Sisi hapa kwetu, vitendo vimeshafanyika, na ushahidi upo.......

  Kila siku wahalifu wa kawaida wanauwawa bila kufikishwa mahakamani lakini "wale wengine" wanapewa escort in air conditioned SUVs.......Tunataka tufike mahali tuchinjane ndio tujue maana?

  Ili tujenge jamii ya kistaarabu yenye kufuata misingi ya haki (kama ambayo TZ siku zote tunajigamba), ni lazima tuone accountability of the highest order and this has to start from the very top....Jamaa aachie ngazi. Full stop.
   
 5. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #5
  Dec 12, 2008
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Nakubaliana na azimio la Mwanza,kwa masharti ya dini iachwe kama ilivyo yaani isihusishe na mambo ya siasa/serikali;tatizo ninaloona hapa siku zote sisi watanzania huwa hatupendi kuwa wakweli!Ukiwa mkweli unaonekana mbaya,sasa basi kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla ni wazo zuri na linastahili kutekelezwa haraka iwezekanavyo.
  Tofauti na hivyo itakuwa mazingaombwe na kuendelea kuwa Taifa ombaomba.
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Dec 12, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ndoto za Abunuasi za kutaka kujenga gorofa hewani. Labda jeshi liamua kufanya vitu vyake kitu ambacho nacho ni hekaya vilevile (riwaya simulizi).
   
 7. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #7
  Dec 13, 2008
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Zitto,
  Tanzania hatuna matatizo na dini; ila tuna matatizo ya law enforcement na ethics. Wewe pigania tu ethics, na kuheshim sheria. Tutavunja serikali, tutatunga sheria nyingine, bado the backbone is who will enforce and respect those laws? If the man at the top is a law breaker what do you expect? Ethics! Do we have ethics? The IGP slept with a house servant, and had a child born, he ran away and wanted to corrupt the judiciary! We have to start from our own values, ethics and respect of law; we ahave to distinguish our own from the animals!
   
 8. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #8
  Dec 13, 2008
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  The government of Tanzania has no codes of conduct. .......??????. Ni kam shamba la bibi.
   
 9. Baba Sangara

  Baba Sangara JF-Expert Member

  #9
  Dec 13, 2008
  Joined: Dec 16, 2007
  Messages: 244
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Compared to many other African Presidents, JK has achieved a lot without upsetting the balance of power in the country. Zitto should give him credit for getting "change" into gear.. We are at least now hearing about "ufisadi". ask yourselves honestly, did you even hear of scandals of such magnitude when Mwinyi or Mkapa were leading the nation? NO
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Dec 13, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Baba Sangara History is whats decides whats going on and NOT just simply a leader...A leader will just encounter whats going on in regard to upsetting the balance of power.....Ni utawala wa viongozi aliwaowachaguwa kumsaidia kutuletea maendeleo kwa kuzisimamia vizuri rasilimali za Taifa ndio vigezo vitakavyo tumika wakati wa ku decide how popular the Government is amongst the people.
  Nasema ni history kwasababu uliposema kuhusu awamu mbili zilizopita pia utaona kuna still struggle of power kutokana na kupigiana panga mali za Taifa na sasa mwelekeo huo unaonekana kutopendwa na wananchi kiasi cha kuhatarisha usalama wa Taifa letu changa...Kusikia scandals za such magnitude pia ni same...History...Na transtition ya ubinafsishajianaji wa mali za Taifa na uuzwaji wake....Hili limepelekea wananchi wengi kujiona kama hawako HURU ndani ya Taifa lao TAJIRI.
   
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  Dec 13, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu you nailed it mpaka Ikulu, heshima mbele sana, lakini haya ya Zitto na kuvunja serikali yamepitwa na wakati sasa rais amevunja mno cabinet toka ashike power, cha muhimu abadilishe mawaziri wawili au watatu tusonge mbele.

  - Otherwise, kwa kwwli ninakubali hoja yako ya msingi kwamba huyu rais amejitahidi sana, kuliko marais wote waliopita, mimi ni mshabiki mkubwa sana wa the respect kwa rule of Law na kila siku ninaota hivyo kuwa ipo siku tutafikia huko yaani Tanzania, ninaamini behind hiki kipengele ndio kuna matatizo yetu yote kitaifa yalikolala, hatuheshimu sheria na hatujui sheria, taifa lisilokuwa na sheria, haliwezi kuheshimu haki za wananchi, na Mungu yuko very open na blunt on hilo kwamba hawezi lisaidia taifa la namna hiyo yaani kama letu.
   
 12. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #12
  Dec 13, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Wht exactly that is supposed to justify?

  There is a right and a wrong way of upsetting the balance of power...!

  We can not capitalise n not upsetting the balance while there is a lot to be done which can lead to some kind of initial tabulance but finaly bring the nation to where it should be... to the power of people.
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Dec 13, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Wale wanaodai "Bila ku upsett balance of power" Na wakati tumeshaambiwa kuwa kuna mafisadi ambao ukiwashughulikia wata upset balance of power...Mafisadi ambao bado ni very powerfull...Then naona kama mazingaombwe flani hivi tukianza kujipongeza mapema hii....Yani Baba Sangara anasema tumpe JK sifa kwasababu at least tunaweza kusikia kuhusu "ufisadi" tofauti na vipindi vya Mwinyi na Mkapa...Kwangu still hayo ni mazingaombwe tu....Kwasababu sasa wananchi hawataki kusikia tu...Wanataka kuona ACTION.
   
 14. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #14
  Dec 13, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu Mushi siku zote ni vyema kukubali ukweli na kutoa credit where it is due tena on time, rais amejitahidi so far as far as vita vya ufisadi is concerned, ingawa sio kwa speed tunayoitaka wengi hapa JF.
   
 15. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #15
  Dec 13, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Ni kweli amejitahidi so far...Ila Baba Sangara yeye kasema tufurahi kwasababu at least tunasikia kuhusu ufisadi tofauti na awamu mbili zilizopita..
  Mkuu FMES sasa ni KAGODA AGRICULTURE...Nakubali tunampa 5 Mh Rais kwa speed yake ya kinyonga..Lakini ngoma bado mbichi sana kusema ukweli kwasababu kuna maswali mengine magumu sana ambayo watashindwa kuyajibu ama wataya ignore ama kutumia mbinu zisizofaa ka anavyofanya Chiligati na Makamba....Sasa matokeo yake ni kama Huko Mara na kabla ya hapo ilikuwa walimu,wanafunzi na wazee.
  Balance of power anayoizungumzia Baba Sangara ambayo kwa maoni yake ni kuwa iko preserved na huku mafisadi wakishugulikiwa to me ni too early to conclude.
  yani isiwe kama eti tayari haki imeshapatikana...Isije ikwa theatrical.
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Dec 13, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu Mushi siku hizi ninazimia sana na vitu vyako, maana viko pointed, clear na very sharp, hapa tupo ukurasa mmoja.
   
 17. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #17
  Dec 13, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kama Chadema wanategemea CCM wawasikilize then wamebugi step!
   
 18. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #18
  Dec 13, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Je ccm inaweza kuwasikiliza wananchi bila kuwasikiliza CHADEMA? Je wananchi kwa ccm ni wanachama wake takriban milioni peke yake? Ama CHADEMA wanataka ccm wawasikilize kivipi?
  Je unaweza kufafanua zaidi?
   
 19. Baba Sangara

  Baba Sangara JF-Expert Member

  #19
  Dec 13, 2008
  Joined: Dec 16, 2007
  Messages: 244
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  If you don't mind civil war.. go on mate, rock the boat hard enough and you'll have Cote d'Ivoire in TZ... In view of "power to the people".... where do we have this? US? hmmm UK?.... Germany?... Am lost..
   
 20. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #20
  Dec 13, 2008
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  FEMES
  "hatuheshimu sheria na hatujui sheria, taifa lisilokuwa na sheria, haliwezi kuheshimu haki za wananchi, na Mungu yuko very open na blunt on hilo kwamba hawezi lisaidia taifa la namna hiyo yaani kama letu"
  BRAVO INCUMBENT FMES, YOU TOUCHED my heart! Tell me why; please maybe we are missing something because this looks as a core of our problem. We must do something on this!
   
Loading...