Kikwete asema tofauti zakwamisha Afrika moja

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,029
Achana na hizi alinacha JK! Serikali moja ya Afrika Mashariki nanga inapaa tutaweza Serikali moja ya Afrika nzima kweli!? :confused:
Cha muhimu ni kuwa na currency moja kwa Afrika nzima na ushirikiano wa karibu kiuchumi kama ule wa EU.


Kikwete asema tofauti zakwamisha Afrika moja
Claud Gwandu, Arusha
Daily News; Friday,May 23, 2008 @00:03

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Kikwete amesema nchi za Afrika zina utashi wa kuwa na serikali moja lakini zinatofautiana katika masuala machache ambayo yanaweza kutatuliwa.

Akifungua mkutano wa siku mbili wa marais na viongozi wa nchi 12 za Afrika zinazounda Kamati ya Kushughulikia Serikali Moja ya Afrika mjini hapa jana, Rais Kikwete alisema tofauti hizo zipo katika muundo na muda wa kuanzishwa kwa serikali hiyo.

"Kimsingi nchi za Afrika zina azma ya kutimiza mchakato wa kuwa na serikali moja ulioanza tangu miaka ya 1960 na dalili zinaonyesha kuwa tunaweza kutimiza nia ya kuwa na serikali moja katika muda mfupi ujao," alisema.

Alisema ili kutimiza lengo hilo, AU imekuwa ikiunda kamati mbalimbali za kutafuta maoni ya wadau kama vile azimio la Accra ambako walikubaliana kuunda kamati itakayopitia muundo wa AU na vyombo vyake kwa nia ya kuimarisha utendaji wake katika kuelekea serikali moja.

Kamati hiyo iliyokuwa chini ya mchumi maarufu, Profesa Adedeji Adebayo wa Nigeria iliwasilisha mapendekezo 159 kwa mawaziri wa nchi za nje wa umoja huo waliokutana mjini hapa mapema mwezi huu.

Awali, Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU,Dk. Jean Ping alisema mapendekezo ya mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje yaligusia masuala muhimu katika kuelekea katika umoja kama vile kuwaelimisha zaidi wananchi wa Afrika juu ya AU na kuangalia vyanzo zaidi vya mapato kwa umoja huo.

Alisema mawaziri hao walitoa mapendekezo yaliyoweka msingi wa kuanzishwa kwa serikali moja ya Afrika katika misingi inayokubalika katika bara hilo masikini zaidi duniani ingawa lina rasilimali nyingi za asili.

Mkutano huo unaomalizika leo utapitia mapendekezo ya mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje na kuandaa mapendekezo yake yatakayopelekwa katika kikao cha wakuu wa nchi wanachama wa AU kitakachofanyika nchini Misri Julai, mwaka huu.

Hata hivyo, kati ya marais 12 wanaounda Kamati hiyo, ni watano tu waliohudhuria mkutano wa jana huku wengine saba wakiwakilishwa na mawaziri wao wa Mambo ya Nchi za Nje.

Marais waliohudhuria mkutano ni Yoweri Museveni wa Uganda,Thabo Mbeki wa Afrika Kusini,Umaru Yaar'dua wa Nigeria,Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zanawi na mwenyeji wao, Rais Kikwete.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu,Salva Rweyemamu alipoulizwa juu ya marais wengi kushindwa kuhudhuria mkutano huo, alisema kuwa mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wanawakilisha marais wao hivyo wana mamlaka ya kutoa uamuzi.

Marais walioshindwa kuhudhuria mkutano huo ni Muamar Gaddafi wa Libya, John Kuffour wa Ghana, Abdoulaye Wade wa Senegal, Paul Biya wa Cameroun, Omar Bongo wa Gabon, Hosni Mubarak wa Misri na Ian Khama wa Botswana.
 
Kabla hatujafikiria kuunda serikali moja ya Afrika kutatuletea mafanikio kwanza tutafute mifano ya serikali mojamoja za Afrika zilizofanikiwa.
Si sahihi kuamini kuwa kwa vile tunaishi kwenye bara moja basi interest zetu zinafanana kiasi cha kuhitaji serikali moja.
Let us revolutionise the use of our own resourses before trying to benefit from other nation´s resourses or offering others a legal pass to use ours.
 
Nadhani tungefikiria kujenga bara bara nchi nzima , maji safi , umeme na national id kabla ya kufikiria umoja wa afrika . Tuungane ili tuweze kufanya nini ? kuuza samaki au ?
 
Hujajenga choo unataka kununua gari. Mwalim alishasema hilo, shona suti kutokana na ukubwa wa kitambaa chako.

JK au Ze Comedy kweli koboko yao, badala ya kuwaza utadumisha vipi muungano wa Unguja na Pemba unaleta hadithi zako za kuunganisha Africa.
 
Back
Top Bottom