Kikwete asema Profesa Benno Ndulu ndiye aliyeleta utaratibu wa malipo ya fedha kwa njia ya simu

Wanahangaika sana mkuu wanadhani wote mafala, haya mambo aliyeleta ni Safaricom kampuni ya Waingereza ndugu na Vodacom lakini makazi yao yakiwa jijini Nairobi,ndulu yeye alipitisha tu baada ya kuona kule Kenya hii huduma imesambaa na inafanya kazi na wakati huo huo hapa Tanzania vodacom walikuwa tayari wamejiandaa kuanzisha hii huduma na na walikuwa ndio wanaomba kibali cha kuendesha emoney. Hizi sifa za makusudi hazina mshiko.
Mbna mmeshindwa kutuletea paypal??

Ndulu ansifiwa hapa kwa kua mwepesi kukubali na kupokea mabadiliko yenye tija sio kuanzisha.
 
Kikwete asingeweza kunena maneno haya enzi za Mwendazake kwasababuMwendazaka alikuwa anajua ufisadi alioufanya kwa kushirikiana na Ndulu akiwa Gavana na LikwelIle akiwa Katiba Mkuu hazina.[ ndio maana hakutaka aendelee kuwa Gavana baada ya muda wake; alimuondoa Likwelile hazina]. Among many other things , kama mnakumbuka kulikuwa na forex denominated bond which was floated Mustapha Mkullo akiwa Waziri wa fedha wa Kikwete; fedha zilizopatikana kwenye ile bond mpaka leo haijulikani zilituka kwa mradi gani!! Zitto alijaribu kuuliza bungeni juu ya ile bond akapigwa stop kwa kupewa safari na Rais kwenda kubembea!!

Vasco Dagama amewaumiza watu wengi sana kwa ufisadi wake enzi za utawala wake. Ukichunguza kwa ndani watu kama Rugemalila na Kitilya wameozea gerezani kwa sababu ya dili za Vasco Dagama!! David Mattaka aliingia matatani akiwa ATCL kwasababu ya kutekeleza maagizo ya Vasco Dagama!! Halafu leo anataka kuturudisha kule kule kwa mgongo wa Samia!!!
NI bora Rais fisadi kuliko Rais Katili roho mkononi.
 
Dar es Salaam. Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amesema gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu ndiye aliyetoa fursa kwa mitandao ya simu kuanza kutoa huduma za kifedha hapa nchini.

Kikwete aliyasema hayo Aprili 22 nchini Marekani wakati wa majadiliano maalumu ya kumbukizi ya Profesa Ndulu yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha New York (NYU) kupitia jukwaa lake la Africa House.

Profesa Ndulu alikuwa Gavana wa BoT kuanzia mwaka 2008 hadi 2018 alipostaafu. Mtaalamu huyo wa uchumi alifariki Februari 21 mwaka huu jijini Dar es Salaam katika Hospitali ya Kairuki.

Katika hotuba yake aliyoitoa katika majadiliano hayo, Kikwete alisema wakati akiwa Rais, Profesa Ndulu alimpelekea wazo lake la kuanzisha huduma jumuishi za kifedha, akamruhusu, sasa wazo hilo limeleta matokeo makubwa.

Alisema uamuzi wake huo ulisababisha ongezeko la huduma jumuishi za kifedha kwa wananchi kutoka asilimia 16 zilizokuwapo mwaka 2009 hadi asilimia 65 mwaka 2018 alipostaafu kama Gavana wa Benki Kuu.
Kama laiti marehemu ndiye angekuwa Rais wakati huo, nina hakika asingekubali. Marehemu hakupenda kabisa mtu kuwa na uhuru kwenye masiala ya fedha, biashara na uchumi.
 
kwanini JK hakunena maneno haya enzi za Mwendazake??
muwe mnasoma mada kwanza kabla ya kuandika chochote, hiyo ilikuwa siku ya kumbukizi ya Kifo cha Prof. Beno Ndulu iliyofanyika huko Marekani kwenye chuo kikuu cha New York. Sasa ulitaka aongelee tu huko barabarani bila kuwa na sababu?

Mbona alishawahi kumpa makavu kwenye mazishi ya mzee mkapa kuhusu nchi kufikia uchumi wa kati wa chini? au umeshasahau? au ulitaka kila siku apinge tu hata kama Rais Magufuli anafanya vyema?
 
Kikwete asingeweza kunena maneno haya enzi za Mwendazake kwasababuMwendazaka alikuwa anajua ufisadi alioufanya kwa kushirikiana na Ndulu akiwa Gavana na LikwelIle akiwa Katiba Mkuu hazina.[ ndio maana hakutaka aendelee kuwa Gavana baada ya muda wake; alimuondoa Likwelile hazina]. Among many other things , kama mnakumbuka kulikuwa na forex denominated bond which was floated Mustapha Mkullo akiwa Waziri wa fedha wa Kikwete; fedha zilizopatikana kwenye ile bond mpaka leo haijulikani zilituka kwa mradi gani!! Zitto alijaribu kuuliza bungeni juu ya ile bond akapigwa stop kwa kupewa safari na Rais kwenda kubembea!!

Vasco Dagama amewaumiza watu wengi sana kwa ufisadi wake enzi za utawala wake. Ukichunguza kwa ndani watu kama Rugemalila na Kitilya wameozea gerezani kwa sababu ya dili za Vasco Dagama!! David Mattaka aliingia matatani akiwa ATCL kwasababu ya kutekeleza maagizo ya Vasco Dagama!! Halafu leo anataka kuturudisha kule kule kwa mgongo wa Samia!!!
pumba dot com.
 
Dar es Salaam. Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amesema gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu ndiye aliyetoa fursa kwa mitandao ya simu kuanza kutoa huduma za kifedha hapa nchini.

Kikwete aliyasema hayo Aprili 22 nchini Marekani wakati wa majadiliano maalumu ya kumbukizi ya Profesa Ndulu yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha New York (NYU) kupitia jukwaa lake la Africa House.

Profesa Ndulu alikuwa Gavana wa BoT kuanzia mwaka 2008 hadi 2018 alipostaafu. Mtaalamu huyo wa uchumi alifariki Februari 21 mwaka huu jijini Dar es Salaam katika Hospitali ya Kairuki.

Katika hotuba yake aliyoitoa katika majadiliano hayo, Kikwete alisema wakati akiwa Rais, Profesa Ndulu alimpelekea wazo lake la kuanzisha huduma jumuishi za kifedha, akamruhusu, sasa wazo hilo limeleta matokeo makubwa.

Alisema uamuzi wake huo ulisababisha ongezeko la huduma jumuishi za kifedha kwa wananchi kutoka asilimia 16 zilizokuwapo mwaka 2009 hadi asilimia 65 mwaka 2018 alipostaafu kama Gavana wa Benki Kuu.
Halafu wanatokea sukumagang wanasema nchi iliibiwa sana, shenzi kabisa.
 
Mnaosema hio miamala tumeiga hatujakataa. Kikwete kasema huyo professor ndio kaja na wazo la hio miamala kufanyika hapa nchini... So kwa upande wetu ye ndio kaanzisha hio miamala hapa nchini... Lazima tumpe sifa hio na mambo mengi yanafanyika kwingine hapa hayafanyiki kwa hio akija mtu kuyaleta hapa lazima tumpe heshima hio.....
 
Chumba na sebule masaki kwa mwezi sh.

Mkuu wasomi wazuri wa sayansi huwa wengi hawana social skills ndo hata magu alikuwa na kauli za ajabu haimaanishi alikuwa hawezi kazi.
Muhongo ndo aliyeleta na kuandika mradi wa rea unaenda hadi vijiji vilivyokosa umeme toka uhuru .na alikuwa na speed kali sana .muhongo alileta wawekezaji ambao ni kampuni zenye uzoefu wa kazi hiyo zinazoaminiwa kukopa mabenki mtwara hadi nyumba zilianza fulika wafanyakazi wazungu na uchumi wa gesi ulianza nukia viwanja havikushikika.
Ni ukweli utajiri wote wa moo akiuza hadi chupi hawezi shika hata kitalu kimoja .walichochukia matajiri watanzania walitaka wadalalie walete makampuni kwa cha juu muhongo alikaza waje wenye technolojia tuwape vitaru wawekeze bila vikwazo vya madalali
Kwanini asingelishauli serikali itunge sheria kuwa kila mwekezaji akija kuwekeza lazima ashilikiane na mzawa?Alafu akashauli serikali iwawezeshe mtaji wazawa, Maana hata hao wawekaji wanaokuja huku wanawezeshwa na serikali zao.Muongo ni msomi mwenye majivuno akuna alichosaidia serikali kwenye secta ya madini,labda udalali tu wa kuuza vitalu vya gesi kwa wachina
 
Kitaru kimoja ni dollar usd bil moja sawa na hela yoooote mara mbili inayokusanywa na serikali kwa mwezi kulipa mishahara madawa wafanyakazi etc wazawa washirikishweje aliweka huduma kama chakula usafiri etc vndo vitoke kwa wazawawatanzania ni masikini wanauwezo wa bviwanda vya maji kaka .huo ndo ukweli
 
Mkuu JK kaulizwa swali kuhusiana na Prof Beno Ndulu juu ya utendaji na mafanikio yake wakati akiwa Gavana wa BOT. Kwakuwa yeye ndiye aliyemteua wakati huo. Sasa ulitaka amwambie muuliza swali akamuulize Mama Samia kwakuwa yeye ndiye Rais kwa sasa??
Kuna watu awamu hii ya sita wameamua kuishi na vinyongo na chuki nyingi, sababu haswa ni kifo cha JPM kama vile Samia au JK ndio wahusika wakuu. Ushahidi wa ubaya wanaoudhania wakiombwa wauweke wazi hawawezi lakini wameamua kuishi kwa unyonge na mateso ya moyo.
 
Back
Top Bottom