Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 2,204
- 4,692
Dar es Salaam. Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amesema gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu ndiye aliyetoa fursa kwa mitandao ya simu kuanza kutoa huduma za kifedha hapa nchini.
Kikwete aliyasema hayo Aprili 22 nchini Marekani wakati wa majadiliano maalumu ya kumbukizi ya Profesa Ndulu yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha New York (NYU) kupitia jukwaa lake la Africa House.
Profesa Ndulu alikuwa Gavana wa BoT kuanzia mwaka 2008 hadi 2018 alipostaafu. Mtaalamu huyo wa uchumi alifariki Februari 21 mwaka huu jijini Dar es Salaam katika Hospitali ya Kairuki.
Katika hotuba yake aliyoitoa katika majadiliano hayo, Kikwete alisema wakati akiwa Rais, Profesa Ndulu alimpelekea wazo lake la kuanzisha huduma jumuishi za kifedha, akamruhusu, sasa wazo hilo limeleta matokeo makubwa.
Alisema uamuzi wake huo ulisababisha ongezeko la huduma jumuishi za kifedha kwa wananchi kutoka asilimia 16 zilizokuwapo mwaka 2009 hadi asilimia 65 mwaka 2018 alipostaafu kama Gavana wa Benki Kuu.