Kikwete apunguza maofisa anaosafiri nao nje

Lugha iliyotumika na waziri Membe kwamba Rais "AMERIDHIA" inamaanisha nia ya kupunguza gharama za serikali haikutokana na yeye.
Kama mkuu mwenyewe haoini ulazima wa kupunguza idadi ya watu wanaojipachika kwenye dege lake, hii inafungua pazia jingine la kujua tuna kiongozi "madhubuti" kiasi gani.

Kwenye mafaniikio ya ziara sidhani kama mapesa ya MCC aliyotoa President Bush yanatokana na ziara za Kikwete.

Wao wanasema "MCC forms partnerships with some of the world's poorest countries who are committed to good governance, economic freedom, and investment in their citizens".
Zipo nchi karibu 40 kwenye mpango huu na Tanzania na Morocco ndio zenye mgao mkubwa $ 698.1 million kwa $ 697.5 million.

Mchongo huu wamarekani hawakupi eti kwa vile unawatembelea sana - Waziri aache upuuzi kwenye maswala ya msingi.

MCC selection criteria Selection Criteria | MCC | Washington, DC
 
Itakuwa kawapunguza kwa visasi au wivu? Au yamemkuta yaliyomkuta Moi kwa Ouko alivyokwenda USA kwani inasemekana Ouko alionekana kuwa aliqualify for Presidency na si Moi? Wewe kwa picha kama hii unategemea Obama atasemaje?

Obama-kikwete.jpg

Uomba omba mbaya kweli, Presidaaa wetu amekwenda na orodha ya mahitaji (karatasi ngapi sijui hapo) wakati mtoa posho wala ha-note tunachomuomba.
 
Kwenye hii picha ni kama jk anapata shida kupata maneno ya kiingereza, si huwa ana kibabaisha hapa kwetu,... utoro wa madarasa.
Pia inaonyesha Obama anapata shida kumuelewa!
Teh, teh...
 
hapa hakijapungua kitu chochote. mwacheni ****** wa watu akatalii. ndicho alichokua anagombea. kwani huko aendako kunakua hakuna ulinzi adi aende na maofisa 34. kawa obama kwa umaarufu adi adhuriwe. si ajabu huko anakoendaga hata hakuna anayemfahamu, sasa walinzi mia wa nini. ukute wanaomuona ka raia tu wa uswazi kwa kule.
 
Uomba omba mbaya kweli, Presidaaa wetu amekwenda na orodha ya mahitaji (karatasi ngapi sijui hapo) wakati mtoa posho wala ha-note tunachomuomba.

Kwa hiyo mkuu atakupa atakacho kumbuka tu ?
 
Kabla ya idadi hiyo ya 34 zamamni walikuwa wangapi? Bila ya hiyo takwimu hatuwezi kujua wamewapunguza kwa kiasi gani
Wanamahesabu tutatoa statistical analysis ambayo itaonyesha kwamba wamepungua kwa asilimia gapi? Pia wasisahau kutueleza upunguzwaji wa idadi unaendana na kupugunzwa kwa gharama hizo. Je kiasi gani tuna save?
 
hapa hakijapungua kitu chochote. mwacheni ****** wa watu akatalii. ndicho alichokua anagombea. kwani huko aendako kunakua hakuna ulinzi adi aende na maofisa 34. kawa obama kwa umaarufu adi adhuriwe. si ajabu huko anakoendaga hata hakuna anayemfahamu, sasa walinzi mia wa nini. ukute wanaomuona ka raia tu wa uswazi kwa kule.
Wewe nawe hujui raisi ni tasisi kubwa nchini? Maraisi wote wanastahili ulinzi kama Obama.
 
Itakuwa kawapunguza kwa visasi au wivu? Au yamemkuta yaliyomkuta Moi kwa Ouko alivyokwenda USA kwani inasemekana Ouko alionekana kuwa aliqualify for Presidency na si Moi? Wewe kwa picha kama hii unategemea Obama atasemaje?

Obama-kikwete.jpg
Waamerika watampenda Kikwete kwasababu ni light skin... Wanampenda kweli toka wakati wa George Bush ni Model wa Rais Mwislamu kuongoza Nchi half Christians half Muslims - Everywhere from State Department to the White House... He's a model...
 
Kama anaogopa usalama wake akienda arusha aongozane na jeshi zima.Huko ndio kuna watu wanaoichukia serikali yake zaidi.
 
Wengi wetu tushamuona baada ya miaka mitano ya kwanza na ndo maana hatukumpa jukumu la kuiongoza nchi hii sema basi tu ni NGUMBARU furani ilituingiza mkenge
 
nilishangaa walikuwa wanaonesha ziara ya Malaysia kwenye TV, rais anaomba business card kutoka kwa exhibitor.

Wasaidizi wake wanafanya kazi gani?
 
Kwenye hiyo picha hapo juu naona obama anasikitika kweli hadi kashika kidevu..nahisi anawaza hivi.."Hii ndo Cream ya Tz.?"AMA KWELI TANZANIA WANA RAIS,
 
Hivi ni nchi zipi anazokwenda JK ambako usalama wake ni tete!!? Nchi anazokwenda mara kwa mara walinzi wake JK huwa hawana kazi, kwani ulinzi wote huwa chini ya wanausalama wa nchi husika.Ukiangalia safari zenye misafara mikubwa ni hizo zenye usalama na ulinzi imara. Akienda Sudan au Burudi anaenda na msafara mdogo.Safari za JK inabidi azipunguze mwenyewe, rais gani asiye tulia nchini mwake? Kila kukicha yuko safarini, basi tumwite RAIS MTEMBEZI.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom