Kikwete apokelewa kwa mabango na bendera za upinzani!

Katani A Katani. Alipigwa na polisi hadi kuvunjwa mkono akilazimishwa kusaini matokeo ambayo ni wazi yalibadilishwa.
Du!! Hii kali. Kuna haja ya kuiongeza ripoti hii kwenye ripoti ya Godbless Lema juu ya ukatili unaofanywa na jeshi la Polisi. Ajipe moyo Mungu atamsaidia.

Tutaendelea kuandamana mpaka hii serikali iondoke madarakani.

Kikwete ni mwizi wa kura, assets na fedha za taifa.

Uhakika upo kikwete afiki 2015. Kama uhakika upo mbona hii issue haifanyiwi kazi,je tutaendelea kumlea huyu mwizi wa mali zetu mpaka lini?

Gazeti, lile tukio la mbunge kuvunjwa mkono lilikuwa maarufu sana mkoa mzima lilikuwa linafahamika, hata jinsi ushindi ulivyonyang'anywa ni jambo linalofahamika. Ina maana zile habari hazikutoka kwenye vyombo vya habari? Mbona naona kama kuna watu wanaiona kama habari ngeni kabisa?

Kiukweli nahisi kama ni hadithi vile,maana ni jambo kubwa ambalo lingevuma nchi
nzima,iweje CUF wasimsaidie huyo jamaa kudai haki yake mahakamani?
Waandishi wa habari ni vipi?

leo nimecheka sana....kwenye kipindi cha redio asubuhi ,Zembwela alikuwa anasoma message za wasilikilizaji...mdau mmoja aliandika hivi...... kweli ufisadi umetumaliza..ni bora huyu anayetuongoza angetangualia mbele ya ..... ! zembwela akaipotezea huku mtangazaji mwenzake akiwa anachekacheka! Ni kweli watanzania wamefikia hatua ya kumuombea rais JM Kikwete atangulie mbele ya haki ili madhila yapungue!

Mkuu umenikumbusha mbali sana, ....................Tandahimba nilikuwepo pia nilikuwa msimamizi kituo cha Mihambwe. Sio kwamba Katani Kachakachuliwa bali kanyang'anywa..................... akisisitiza kuwa Rais atamuelewa vipi kama jimbo hilo litaenda kwa Wapinzani? (Huyu mama mkuu wa Wilaya ni yule aliyetimuliwa UWT)

....matokeo kutangazwa jambo la kwanza lilikuwa ni kuwapiga mabomu ya machozi mamia ya wananchi ambao walikuwa wanasubiri kushangilia ushindi huo wa Katani............ walivuruga amani ya Tandahimba kiasi ambacho ilisababisha hata baadhi ya nyumba kuchomwa moto.....................,Pia siwezi kusahau kumtaja Makamba kuwa ndiye aliyekuwa anapiga simu mara kwa mara na kumlazimisha Mama Mwilima KUmtangaza mbunge wa CCM badala ya Yule mshindi!

Je ni kweli Tanzania ni nchi huru? Tunatawaliwa bila ridhaa! Kikwete naye kaiba kura, siyo Raisi halali.

Tunatawaliwa kimabavu.
Mi nipo tayari kutetea UHURU wetu kwa gharama na namna yoyote.

Katani A Katani. Alipigwa na polisi hadi kuvunjwa mkono akilazimishwa kusaini matokeo ambayo ni wazi yalibadilishwa.

Huyo sindie waliomwenyesha akaletwa mpaka muhimbili na hogo na akaongea na vyombo vya habari alikuwa ni kijana mdogo tuu.

Gazeti, lile tukio la mbunge kuvunjwa mkono lilikuwa maarufu sana mkoa mzima lilikuwa linafahamika, hata jinsi ushindi ulivyonyang'anywa ni jambo linalofahamika. Ina maana zile habari hazikutoka kwenye vyombo vya habari? Mbona naona kama kuna watu wanaiona kama habari ngeni kabisa?

aiseee hii habari ni ngeni hata kwangu na nimeshtushwa sana na habari za huyo Katani!!

Je ni kweli Tanzania ni nchi huru? Tunatawaliwa bila ridhaa!
Kikwete naye kaiba kura, siyo Raisi halali. Tunatawaliwa kimabavu.
Mi nipo tayari kutetea UHURU wetu kwa gharama na namna yoyote

Wengi wetu tupo tayari serikali isije ikadhani kuwa sie ni mambumbu sana maandamano hayo sio yaaanzishwe na CHAMA chochote cha Siasa bali vyama vya haki za binadamu kama nchi nyingine zilivyo fanya hapo serikali inakuwa haina nguvu tena.

Kama serikali inataka kwenda rekebisha sheria ya maandamano ujue wameisha ona hali halisi ya upepo inavyokwenda na sasa wanataka kujihami kulazimisha kututawala watakavyo wao hatutokubali hilo Mfano mzuri IGUNGA Live hadi Aljazeera itafika ngoje mwone, JK hana pa kutokea yeye aendelee na safari za nje na kutafuta mahali pa kukimbilia. a.k.a Hifadhi ya Kisiasa

namuona LIVE TBC yupo Dodoma kwenye ufunguzi wacnane nane! Mpeni V kubwa na bendera za cdm atambue yeye ni rais wa wezi wa kura!!!

namuona LIVE TBC yupo Dodoma kwenye ufunguzi wa nane nane! Mpeni V kubwa na bendera za cdm atambue yeye ni rais wa wezi wa kura!!!

Mkono mtupu haulambwi, alikuwa amebeba nini kwa ajili ya kuwapa wananchi, au alikuwa amebeba tabasamu la kishindo kama kawaida yake, bora wamepunga bendera za wapambanaji, excellent.!

Kiukweli nahisi kama ni hadithi vile,maana ni jambo kubwa ambalo lingevuma nchi
nzima,iweje CUF wasimsaidie huyo jamaa kudai haki yake mahakamani?
Waandishi wa habari ni vipi?

Mkuu ni kweli mimi ni mzawa wa Tandahimba, kwa suala la vyama vya siasa kuna tatizo watu wa kusini hawapati support ya kitaifa. Na CUF taifa haikumsaidia Katani vya kutosha. Ukiangalia kwa undani kwenye vyama vyote CUF, NCCR, CHADEMA na hata CCM.

Bado kuna mentality ile ile ya kwamba huko kusini ni kwa mwisho tangu enzi hizo. Nakuhakikishia wapinzani wangewekeza ipasavyo majimbo yote yangekuwa yao kwa sababu kuna mambo mengi tu yanawachukiza wananchi lakini hawana kwa kwenda wasomi wetu wachache wote ni ccm na wana fursa huko.

Unakumbuka Mbunge Hayati Nandonde (RIP) alifikia uamuzi wa kutaka tujitenge tena enzi hizo kukiwa na chama kimoja jamaa wakaanza kumwita eti mtani wa Bunge. Chadema ilianza kupata nguvu tandahimba 1995 na 2000 haikupata suport kutoka juu. na cuf iliibuka kwa vile tu kuna mstaafu mmoja alijitoa mhanga.

Kwa taarifa yako ni kwamba tangu Mheshimiwa Nandonde (RIP) aongoze kwa miaka 10 hakuna mbunge aliyewahi shika mihula 2 na huyu Juma Njwayo alianza kuwachakachua hata wenzake kwa hiyo hakuwa na sababu ya kushinda hata kidogo.

Katani A Katani. Alipigwa na polisi hadi kuvunjwa mkono akilazimishwa kusaini matokeo ambayo ni wazi yalibadilishwa.

Kumbe siasa sasa si kuwa na ngozi ngumu tu,.ni l na ngozi n

Kiukweli nahisi kama ni hadithi vile,maana ni jambo kubwa ambalo lingevuma nchi
nzima,iweje CUF wasimsaidie huyo jamaa kudai haki yake mahakamani?
Waandishi wa habari ni vipi?
Yaani ukitaka kujua juu ya hili la kuvunjwa mkono huna haja ya kuzunguka mitaani nenda tu pale hospitali ya Wilaya Tandahimba uulize maana hospitali ilikuwa inafurika mpaka wauguzi na madaktrari waliingiwa na hofu!

Huyo sindie waliomwenyesha akaletwa mpaka muhimbili na hogo na akaongea na vyombo vya habari alikuwa ni kijana mdogo tuu

Ndiyo huyo na hata mkuu wa Wilaya alikuwa anaongea wazi kuwa hatuwezi kumpa Ubunge kijana mdogo kama huyu pia aliwahi kumuita hata yeye mwenyewe na kumuahidi kuwa atapewa nafasi fulani na muheshimiwa Rais iwapo atakubali kusaini!

Mkuu ni kweli mimi ni mzawa wa Tandahimba, kwa suala la vyama vya siasa kuna tatizo watu wa kusini hawapati support ya kitaifa. Na CUF taifa haikumsaidia Katani vya kutosha. Ukiangalia kwa undani kwenye vyama vyote CUF, NCCR, CHADEMA na hata CCM. Bado kuna mentality ile ile ya kwamba huko kusini ni kwa mwisho tangu enzi hizo. Nakuhakikishia wapinzani wangewekeza ipasavyo majimbo yote yangekuwa yao kwa sababu kuna mambo mengi tu yanawachukiza wananchi lakini hawana kwa kwenda wasomi wetu wachache wote ni ccm na wana fursa huko. Unakumbuka Mbunge Hayati Nandonde (RIP) alifikia uamuzi wa kutaka tujitenge tena enzi hizo kukiwa na chama kimoja jamaa wakaanza kumwita eti mtani wa Bunge. Chadema ilianza kupata nguvu tandahimba 1995 na 2000 haikupata suport kutoka juu. na cuf iliibuka kwa vile tu kuna mstaafu mmoja alijitoa mhanga.

Kwa taarifa yako ni kwamba tangu Mheshimiwa Nandonde (RIP) aongoze kwa miaka 10 hakuna mbunge aliyewahi shika mihula 2 na huyu Juma Njwayo alianza kuwachakachua hata wenzake kwa hiyo hakuwa na sababu ya kushinda hata kidogo.

Nashukuru kwa sapoti mkuu nafikiri kwa sasa ni bora kuitumia Jf kuleta matukio muhimu kwa kuwaletea hata picha pale itakapolazimika. Kuna vijana pale kitama walikimbia na kuishi porini kufuatia uvamizi wa polisi ambao walitanda eneo lote la Kitama.

Ni Tukio ambalo hatujalisikia kwenye chomboi chochote cha habari, Mbaya zaidi ni kitendo cha polisi kuzunguka mitaani na kupiga mabomu ya machozi hata sehemu ambayo kulikuwa na watoto tu!

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Rais wa Tanzania J.M. Kikwete alijikuta anapata wakati mgumu pale alipokuwa anakatisha katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Tandahimba. Mheshimiwa huyo alijikuta akipita kwa kasi katika baadhi ya vijiji bila kusimama na wala kupunga mkono kama ilivyo kawaida baada ya kukuta mabango ambayo wananchi walikuwa wanadai kurudishwa kwa mbunge wao aliyechakachuliwa. "TUNAMTAKA MBUNGE WETU ALIYECHAKACHULIWA", "HATUMTAKI NDONDOCHA WENU MLIETUWEKEA" "TUNATAKA KESI YA KATANI IISHE" Hivyo ndivyo yalivyosomeka baadhi ya mabango huku bendera za upinzani zikipamba bara bara za vijiji hivyo.

Bendera za vyama nilizobahatika kuziona ni CUF, CHADEMA, NCCR na TLP. Kikwete alipita maeneo hayo kwa lengo la kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura lakini hakufanya hivyo kutokana na mapokezi hayo ya aina yake!

walisahau kusema hatumtaki nchi kuongozwa na ndondocha

hiyo ni Tandahimba bado Dar, Arusha, Mwanza na nchi nzima, aibu sanaaaaa. Kama ni mimi najiuzulu kuonesha nina akili ya kuelewa wanachi wanataka nini

Kama uhakika upo mbona hii issue haifanyiwi kazi,je tutaendelea kumlea huyu mwizi wa mali zetu mpaka lini?

bora uumie kimya kimya nakumbuka yale ya Raiafulani kupigwa ban maisha kwa uchochezi..

Back
Top Bottom