Kikwete apewa ujumbe mzito toka kwa wafuasi wa Nyerere

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
77
WATAKA MAWAZIRI WAACHE KUCHANGANYA URAFIKI NA UTENDAJI


Na Waandishi Wetu

WAZEE na wafuasi mbalimbali wa muasisi wa taifa la Tanzania, hayati Mwalimu Julius Nyerere, wametuma ujumbe mzito kwa serikali ya sasa, wakisema aina ya uongozi anaoutumia Rais Jakaya Kikwete hauwezi kumfikisha alipokusudia katika kulijenga taifa hili.

Wakongwe hao ambao walifanya kazi na Mwalimu enzi ya utawala wake, walisema kwa nyakati tofauti hivi karibuni kwamba, kama Rais Kikwete hatajenga juu misingi mizuri aliyoiacha Mwalimu ya kuwajibika na kuwatumikia wananchi, hawezi kufikia ndoto yake ya maisha bora kwa kila Mtanzania.

Wafuasi hao wa Mwalimu walisema, ili serikali iweze kuondokana na matatizo yanayotokea sasa, inabidi itenganishe kazi na urafiki.

Mzee Hassan Nassor Moyo, aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi wakati wa serikali ya awamu ya kwanza na ya pili, alisema Mwalimu Nyerere alifanikiwa kujenga uwajibikaji katika serikali kwa sababu, kamwe hakutegemea mawaziri wake wawe marafiki zake.

“Mwalimu alikuwa akitegemea mawaziri wake washirikiane naye kufanya kazi za watu kinyume na sasa ambako urafiki umetawala katika kazi,” alisema Mzee Moyo.

Kuhusu sifa za uongozi alizokuwa nazo Mwalimu, Mzee Moyo alieleza kuwa Nyerere alikuwa akijua usimamizi wa kazi na alikuwa akifuatilia kwa karibu sana.

"Alikuwa anajua kusimamia na kufuatilia kwelikweli. Akikupa kazi anakuita na kuuliza ulipofikia. Hali hiyo ilisaidia mawaziri wake kuwa wachapakazi. Walikuwa waaminifu kwa vile yeye mwenyewe (Mwalimu) alikuwa mwaminifu,” alisema Moyo.

Moyo alisema kiongozi huyo alifanya kazi kubwa kuliunganisha taifa lililokuwa limegawanyika kutokana na utawala wa kikoloni na kumfanya awe tofauti na viongozi wengi barani Afrika.

Naye mwanadiplomasia wa Kimataifa, Dk Salim Ahmed Salim ambaye pia alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania wakati wa serikali ya awamu ya kwanza baada ya kufariki dunia Edward Moringe Sokoine, akieleza jinsi anavyomkumbuka Mwalimu Nyerere. Alisema Tanzania imepoteza kiongozi shupavu asiye na ubaguzi.

“Ukweli ni kwamba, Mwalimu alikuwa ni kiongozi shupavu. Ni kiongozi ambaye alikuwa hajali mtu bali utu, alikuwa anathamini zaidi mchango wa mtu bila kujali ametoka wapi… Mwalimu hakuwa na ubaguzi, hivyo alifanikiwa kuifanya nchi yetu kuwa moja,” alifahamisha Dk Salim.

Kuhusu kuanguka kwa Azimio la Arusha ambalo Mwalimu Nyerere aliliasisi, Dk Salim alisema anaamini kuwa misingi ya azimio hilo bado haijafa bali watu wanalipuuzia tu.

“Azimio la Arusha lilikuja kwa wakati fulani na lengo lake lilikuwa ni uwajibikaji katika uongozi. Mtu achague kuwa kiongozi au kujilimbikizia mali. Siyo haramu mtu kuwa tajiri na wala Mwalimu hakupinga mtu kuwa na utajiri. Bali alichopinga ni mtu kutumia uongozi alionao kujitajirisha,” alifafanua mwanadiplomasia huyo.

Changamoto nyingine ilitolewa na Waziri Mkuu mwingine wa zamani, Jaji Joseph Warioba ambaye alisema: “Mwalimu Nyerere alikuwa na uwezo mkubwa wa kufikia makubaliano juu ya jambo na uamuzi ukitolewa unakuwa ni wa vingozi wote. Kwa hivyo suala la uwajibikaji wa pamoja uliwezekana kwa sababu ya uwezo wa kiongozi wa juu wa kuwaweka watu pamoja na kuwa na kauli moja”.

Jaji Warioba alisema tofauti kubwa ya uongozi wa awamu ya kwanza na awamu zilizofuatia ni ile dhamira ya kutumikia umma.

“Mimi nafikiri kwa wakati ule kulikuwa na dhamira ya kutumikia umma. Sasa hivi siasa hizi zimekuwa za ubinafsi mno, yaani ule mkazo wa kutumikia umma umepungua,” alisema Jaji Warioba.

Naye Mzee Rashid Kawawa, maarufu kama Simba wa Vita, aliyemrithi Nyerere Uwaziri Mkuu wa Tanzania mwaka 1966, alisema wakati wao uongozi haukuwa lelemama kwa sababu viongozi wa juu walikuwa wakali sana na kwamba walisisitiza uwajibikaji na kuweka maslahi ya taifa mbele.

“Sisi tulikuwa wakali, ndiyo maana kwenye ahadi 10 za mwana TANU tulisema, ‘rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa’. Hatukuvumilia mtu anayechukua rushwa,” alisema Mzee Kawawa.

Naye Mzee Peter Kisumo aliyewahi kuwa Waziri wa Tawala za Mikoa, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ndani ya CCM enzi za Mwalimu alisema enzi zao kiongozi mbovu alikuwa havumiliwi ilikuwa lazima wamjadili na kumwajibisha.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema anamkumbuka muasisi wa Taifa hili, Julius Nyerere kwa kuongoza taifa kwa uadilifu tofauti na sasa ambapo viongozi wengi wanakiuka miko ya maadili ya uongozi.

"Uadilifu ni silaha inayowezesha kutunza raslimali za nchi, lakini kutokana na kwamba sasa hakuna uadilifu rasilimali zetu zimeanza kutoweka," alisema.

Naye Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alimtaka Rais Kikwete kuongeza kuandaa kuwa na mjadala kuhusu mwelekeo wa taifa, kuliko kusubiri nchi ikumbwe na umwagaji damu kama uliotokea visiwani Zanzibar mwaka 2001 na kusisitiza kwamba, muda wa kuyatekeleza kwa vitendo maneno yaliyozungumzwa na Mwalimu Nyerere umewadia.

Mbatia alisema tabia ya baadhi ya viongozi kuwa wabinafsi na kujiona wao wana haki kuliko watu wengine kutalipeleka taifa katika hatua mbaya.

“Hivi sasa mwitikio wa wananchi katika upigaji kura umeshuka kwa kiwango kikubwa kutokana na ubinafsi wa baadhi ya viongozi. Hivi sasa Tanzania kuna pengo kubwa sana kati ya walionacho na wasionacho,” alisema Mbatia na kuongeza:

“Nyerere alisisitiza suala la utu wa mwanadamu katika maslahi yake binafsi, hivyo suluhu ya nchi hii ni kila mtu kuwa na utu na huo ndiyo utakuwa utekelezaji wa yale aliyoyasema Mwalimu.”

Naye Mwenyekiti chama cha United Democratic (UDP), John Cheyo alisema umoja wa kitaifa ulioachwa na Mwalimu Nyerere umeendelea kutoweka kila kukicha.

“Mwalimu alikuwa mtu mwema sana, hakika tutamkumbuka kwa mambo mema aliyoyafanya hasa suala hili ya kujenga umoja wa kitanifa ambalo hivi sasa viongozi wetu wameendelea kulichafua,” alisema Cheyo.
Alisema nguvu ya umoja wa kitaifa ikishamiri katika nchi fulani, viashiria vya kiuchumi huonekana dhahiri kwani masuala ya ufisadi, maadili mabaya ya uongozi yanakosa nafasi kwa viongozi wenye nia ya kutafuta umoja wa kitaifa.
 
Hii thread inahitaji ku`editiwa sehemu kibao!Lakini kimsingi, nakubaliana na wote waliotoa maoni yao hapo ndani juu ya mwelekeo na hatima ya nchi yetu!Ninachukia sana ninapowaona viongozi wa sasa hivi wanapotamka maneno "KUMUENZI MWALIMU" wakati wana uhakika they dont dare do a peanut of what they utter!...Wajinga!
 
kuedit wapi pakajimmy
Kwa ujumla muheshimiwa anatakiwa abadilishe system yake ya uongozi taifa linakoelekea siko kabisa
 
Wanafurahisha sana hawa wazee only if they mean what they say!Lakini mbona huyu JK haelekei kusikia neno?Ni kwasababu hata yeye ni mmoja wa mafisadi?Anajua kwamba Mwosha huoshwa? labda ndo maana ameweka pamba masikioni!
 
Mimi nashangaa sana kuona kuwa viongozi wanasema tu, Nilikuwa nasoma kitabi cha Mwalimu cha Developments juu ya speech zake za wakti ule ndio unaweza kusema kuwa yeye alikuwa ana maono mengi
 
kuedit wapi pakajimmy
Kwa ujumla muheshimiwa anatakiwa abadilishe system yake ya uongozi taifa linakoelekea siko kabisa

nchi mbona inaelekea sehemu safi sana..mambo yatakuwa safi very soon.jamani Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana kbla ya 2010...nyie ngojeni mtaona tu mambo yatakuwa safi sasa hivi
 
Longolongo za waafrika aziishi. Kama mlikuwa mnalitumikia umma mbona mlituacha tunavaa viroba, kaunguza.
 
Wafuasi wa nyerere what?? hivi nyerere ni "aina fulani ya dini" yenye wafuasi...blah blah hizo...nyerere huyu huyu tuliyekuwa tanafanya foleni hata ya kununua wembe...upuuzi mtupu.
 
Nyerere hakuwa na sifa wanazompatia, eti aliwajibisha watu!! Mashirika yauma yalikufa nahuku anaendelea kuwapatia post za juu zaidi waaribifu, wakina Kawawa wasioelewa wanchofanya walikaa madarakani miaka yote!! Huu ulikua niurafiki na upendeleo wa wazi.

Mwinyi ndie aliewawajibisha wazembe na neneo uwajibikaji liltokea wakati wake. Acheni kkumsifia Nyerere mambasiyokua anayaweza kuyafanya

Nyerere ziara zake wakuu wa mikoa walimpandikizia memea vemeo kumuonyesha eti wanawajibika nae Nyerere alilijua hilo hakuweza kumwajibisha mtu.

Magari ya mashirika walitumika kuwapeleka watoto wa mabosi shuleni.

Wahindi waliifilisi nchi wakati wake.

Tusikubali kuburuzwa na watu wanaotoa misifa kwa mtu asie staili, Nyerere alikua mkali unapompinga sio kwenye ufisadi
 
Nyerere hakuwa na sifa wanazompatia, eti aliwajibisha watu!! Mashirika yauma yalikufa nahuku anaendelea kuwapatia post za juu zaidi waaribifu, wakina Kawawa wasioelewa wanchofanya walikaa madarakani miaka yote!! Huu ulikua niurafiki na upendeleo wa wazi.

Mwinyi ndie aliewawajibisha wazembe na neneo uwajibikaji liltokea wakati wake. Acheni kkumsifia Nyerere mambasiyokua anayaweza kuyafanya

Nyerere ziara zake wakuu wa mikoa walimpandikizia memea vemeo kumuonyesha eti wanawajibika nae Nyerere alilijua hilo hakuweza kumwajibisha mtu.

Magari ya mashirika walitumika kuwapeleka watoto wa mabosi shuleni.

Wahindi waliifilisi nchi wakati wake.

Tusikubali kuburuzwa na watu wanaotoa misifa kwa mtu asie staili, Nyerere alikua mkali unapompinga sio kwenye ufisadi
Nyerere is a total failure...afadhali ametuondokea ..bomu lile
 
Kila mtu siku hizi ni mfuasi wa Nyerere na tena mimi nasema kuwa ngoja ifike mwakani utaona ndio mambo haya yanazidi zaidi
 
Ili tuendelee tunahita watu,ardhi,siasa safi za Mwalimu Nyerere,na ungozi bora wa Rais Kikwete.
Haya ndiyo maoni yangu,na siyaelekezi kwa fisadi yoyote in particular,like a laser beam,isipokuwa yanaelekezwa kwa Watanzania wote,waelewe umuhimu wa kuwa na siasa safi na uongozi bora.
Kwa sababu sasa ni wakati wa kufikiria mshikamano wa Kitaifa.
 
Hawa wanaopeleka ujumbe kwa Kikwete inabidi sasa wawe wakweli wa nafsi zao. Viongozi wa kidini, Viongozi wa zamani ambao waliwahi kushika nyadhifa mbali mbali Serikalini au TANU/CCM ambao wanaona nchi inaenda mrama na kusema ukweli kwamba Tanzania haina uongozi thabiti ndiyo maana nchi inalegalega waache kuzungukazunguka na kumwambia ukweli Kikwete kwamba kwa tathmini yao ta Kikwete kuwa madarakani tangu alipochaguliwa uongozi wa nchi umemshinda na kuna mifano chungu nzima ya hili, nchi inayumba, CCM inayumba na sasa kuna vikundi vinavyopingana tena hadharani (Kikwete anadai na kujidanganya kwamba CCM hakuna mpasuko! ) na wageni wanazidi kupora rasilimali zetu wakati Watanzania hatufaidiki na utajiri wetu huo.

Wakati umefika sasa wa kumwambia ukweli Kikwete kwamba Uongozi wa Tanzania umemshinda hata kama Rais atayechagulia 2010 atatoka CCM basi awe ni mwingine na siyo Kikwete na yeye wamuombe kwamba asigombee tena 2010 ili kunusuru nchi yetu katika matatizo makubwa siku za usoni kutokana na uongozi wake dhaifu. Mambo ya kuoneana haya tuyaweke pembeni ili kuinusuru nchi. Kikwete kawakumbatia mafisadi, hili siyo siri na ndiyo sababu kubwa anashindwa kupambana na ufisadi kama ambavyo Watanzania wengi tungependa.
 
Kina "Lord Resistance Army" utawaona wanavyomkumbatia ukoma wao

Na baadaye wakimaliza kumkumbatia ukoma wao, wanavaa suicide bombs na kujiua eti kwa vile watapatiwa vimwana baada ya kufa.

Ukisikia kuishiwa ndiko huku
 
Na baadaye wakimaliza kumkumbatia ukoma wao, wanavaa suicide bombs na kujiua eti kwa vile watapatiwa vimwana baada ya kufa.

Ukisikia kuishiwa ndiko huku
Baada ya kukumbatia ukoma wataenda kuombewa na sala inaongozwa askofu shoga!
 
Na baadaye wakimaliza kumkumbatia ukoma wao, wanavaa suicide bombs na kujiua eti kwa vile watapatiwa vimwana baada ya kufa.

Ukisikia kuishiwa ndiko huku


Mwafrika acheni hizi huu ugomvi wenu na Tumain unapoteza mwelekeo wa mada
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom